Mwamuzi Omar Artan azawadiwa Million 260 na Mfanyabiashara wa Somalia
Mfanyabiashara mmoja raia wa Somalia amemzawadia mwamuzi Omar Artan (kulia) kiasi cha Dola100,000, wastani wa Sh260 milioni, kama fidia ya kipato anachotarajiwa kukikosa baada ya kukataliwa kuingia nchini Marekani, ambako alikuwa amepangwa kuchezesha mechi za Kombe la Dunia.
Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, waamuzi wa mechi za Kombe la Dunia hulipwa kati ya Dola50,000 na Dola75,000 kwa mashindano hayo, kiwango ambacho Artan huenda akakikosa kutokana na kushindwa kupata kibali cha kuingia Marekani.



Post a Comment