Nini kimesimama mbele yako kama Goliath?, Muangalie Daudi Jinsi ambavyo alimshinda Goliath,
Hakumjia kwa nguvu zake mwenyewe,si kwa nguvu wala si kwa uzoefu wa Vita, maana angekuja kwa Vitu hivi asingemshinda Goliath;Mtu wa Vita,Hodari Mkubwa,
bali yeye alimjia kwa Jina la BWANA wa Majeshi akamshinda..
Hata wewe,hicho kilichosimama mbele yako haijalishi kina ukubwa kama wa Goliath, Kikabili kwa jina la BWANA wa Majeshi,Kitaanguka chini na wewe Utaendelea mbele KATIKA JINA LA YESU".
Mstari huu ukukumbushe; TUNASHINDA:"Warumi 8:37 Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda".



Post a Comment