Sabalenka Afunguka Baada ya Kuporomoka French Open: “Nilitaka Kuacha Tenisi”
Mchezaji namba moja duniani wa tenisi ya wanawake amesema amepitia kipindi kigumu kiakili hadi kufikia hatua ya kufikiria kuachana kabisa na mchezo wa tenisi baada ya kushindwa katika mechi ya robo fainali ya French Open.
Sabalenka alipoteza kwa seti 3-6, 7-5, 6-0 katika mchezo uliochezwa Juni 3, 2026. Kilichoshangaza wengi ni jinsi alivyopoteza mwelekeo wa mchezo baada ya kuwa karibu sana na ushindi, akiwa amebakiza pointi mbili tu kufuzu hatua inayofuata.
Katika seti ya mwisho, Sabalenka aliporomoka kabisa na kupoteza michezo 10 mfululizo, jambo ambalo amesema halijawahi kumtokea kwa muda mrefu katika maisha yake ya tenisi.
“Nilikuwa sina mawazo wala hisia zozote. Kwa wakati huo nilihisi kama nataka kuacha tenisi kabisa. Lakini nitachukua muda kutafakari na kurejea nikiwa imara zaidi,” alisema.
Wakati wa mechi hiyo, pia alionyesha hasira baada ya kupiga mpira kwa nguvu kufuatia kosa la huduma ya kwanza (first serve), ambapo mpira huo ulielekea kwa waamuzi na watoto wa kuokota mipira kabla ya kutua kwenye eneo la watazamaji. Baadaye aliomba radhi kwa kitendo hicho.
Mchezaji huyo wa Belarus amesema changamoto yake kubwa imekuwa kushindwa kudhibiti hisia katika baadhi ya mechi muhimu, jambo ambalo limechangia matokeo yasiyoridhisha.
Licha ya maumivu ya kushindwa, anaamini atajifunza kutokana na tukio hilo na kurejea akiwa bora zaidi siku zijazo.
Ikumbukwe pia,Katika fainali ya French Open mwaka uliopita dhidi ya Diana Shnaider, aliongoza kwa michezo mingi mapema kabla ya kupoteza mwelekeo na hatimaye kufungwa katika seti tatu.
Kushindwa huku kumeibua mjadala kuhusu umuhimu wa afya ya akili kwa wanamichezo wa kiwango cha juu, hasa wanapokabiliwa na presha kubwa katika mashindano makubwa duniani.



Post a Comment