Studio za Mwanamuziki wa Kitanzania, Elias Barnabas Inyasi maarufu kama Barnaba Classic, zimeteketea kwa moto
Studio za Mwanamuziki wa Kitanzania, Elias Barnabas Inyasi maarufu kama Barnaba Classic, zimeteketea kwa moto usiku wa kuamkia Juni 1, 2026 maeneo ya Mwananyamala Jijini Dar es salaam.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Barnaba amechapisha video zinazoonyesha tukio hilo la ajali ya moto, kisha akaweka ujumbe usemao:
“Uchungu mkubwa sana ninaoupata kutoa taarifa kwamba studio zangu za (High Table Sound Entertainment Company Ltd: @hightablesound @hightablefilm) zimeungua moto usiku huu ulioanza saa 2:30 kamili, nilitoka kwenye shoo yangu ya Malkia wa Nguvu Arusha na baada ya kufika nilipitia ofisini kwangu na kusalimia, kisha nikaenda nyumbani kwa takribani dakika 15. Nikiwa huko ndipo nilipopigiwa simu kuwa kuna moto unawaka”
“Mungu wangu wa mbinguni, nakushukuru kwa hili, naamini unanipitisha kwenye njia sahihi daima, nimetoka kufanya renovation wiki mbili zilizopita kwa gharama kubwa na muziki ndiyo kazi yangu, sehemu hii inategemewa na Vijana wengi, moyo wangu unaumia, nimelia sana kwa uchungu na nimepoteza nguvu kabisa”
“Nasikitika kusema HQ yetu imekuwa majivu, asante Mungu kwa baraka zote ambazo nimezipokea na nitaanza upya, najua kazi yetu ni ngumu, lakini maisha yanatufundisha na nimepokea hili kama funzo.”



Post a Comment