Tahadhari ya Tsunami Yatolewa nchini Ufilipino
Mji wa mwambao wa Santos uliopo kusini mwa Ufilipino umeshuhudia uharibifu wa awali pamoja na kukatika kwa huduma ya umeme kufuatia tahadhari ya tsunami iliyotolewa katika eneo la Pasifiki.
Mamlaka za Ufilipino zimewataka wakazi wa maeneo ya pwani kuondoka mara moja na kuelekea sehemu za juu na zenye miinuko ili kujikinga na uwezekano wa mawimbi makubwa ya bahari.
Rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos Jr. ameziagiza taasisi zote za serikali kuingia kazini haraka ili kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na janga hilo.
Kituo cha Tahadhari ya Tsunami katika Bahari ya Pasifiki kimesema kuna uwezekano wa mawimbi ya hadi mita 3 kupiga maeneo ya pwani ya Ufilipino, hali inayoongeza hofu kwa wakazi wa ukanda huo.
Wakati huo huo, nchi kadhaa katika eneo la Indo-Pasifiki zikiwemo Indonesia, Malaysia, Taiwan, Japan, Papua New Guinea na Guam zimewaonya wananchi wake kuchukua tahadhari na kufuatilia maelekezo ya mamlaka za uokoaji kutokana na hatari ya tsunami.


Post a Comment