Ummy Mwalimu ateuliwa kuwa Mshauri wa Rais anayeshughulikia masuala ya Afya na Ustawi wa Jamii, Mama na Mtoto. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Ummy Ally Mwalimu kuwa Mshauri wa Rais anayeshughulikia masuala ya Afya na Ustawi wa Jamii, Mama na Mtoto. Taarifa hiyo imetolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, kupitia Mkurugenzi wake Shaaban Kissu, ikieleza kuwa uteuzi huo umeanza kutumika rasmi kuanzia tarehe ya kutangazwa kwake.

Reply

Discussions