Head

Usile Vitu Hivi Ukiwa Hedhi

Wanawake wengi hujiuliza kama kuna vyakula vinavyopaswa kuepukwa wakati wa hedhi kutokana na maumivu ya tumbo, kuvimba mwili, uchovu au mabadiliko ya hisia wanayopata kipindi hiki, Wengine wanaambiwa wasitumie majani mengi ya chai,wengine hivi.... Ingawa hakuna sheria kali inayokataza chakula fulani kabisa, wataalamu wa afya wanashauri kupunguza baadhi ya vyakula ambavyo vinaweza kuongeza usumbufu wakati wa siku za hedhi.

1. Vyakula vyenye chumvi nyingi

Chipsi, vyakula vya makopo, nyama zilizokaushwa na snacks zenye chumvi nyingi zinaweza kusababisha mwili kuhifadhi maji zaidi. Hii huongeza hali ya kutakuna kwa tumbo na kufanya Mwanamke apate maumivu zaidi.

2. Vyakula vya mafuta mengi

Fast food kama burger, kuku wa kukaanga na vyakula vyenye mafuta mengi vinaweza kuongeza uchochezi mwilini na kufanya maumivu ya hedhi kuwa makali zaidi kwa baadhi ya wanawake.

3. Sukari kupita kiasi

Kula pipi nyingi, soda au keki nyingi kunaweza kuongeza mabadiliko ya hisia na kufanya kiwango cha nguvu mwilini kupanda na kushuka haraka. Wengine hupata uchovu au hasira zaidi baada ya kutumia sukari nyingi wakati wa hedhi.

4. Kafeini nyingi

Kahawa nyingi, energy drinks na baadhi ya soda zinaweza kuongeza hali ya msongo, kukosa usingizi na wakati mwingine kufanya maumivu ya tumbo kuwa makali zaidi. Kwa baadhi ya wanawake, kafeini pia huongeza maumivu ya kichwa wakati wa hedhi.

5. Pombe

Pombe inaweza kuchochea zaidi upungufu wa maji mwilini na kufanya uchovu au maumivu ya kichwa kuwa makali zaidi. Pia inaweza kuathiri usingizi na hisia.

6. Vyakula vinavyosababisha gesi tumboni

Maharage mengi, Kabichi na soda nyingi vinaweza kuongeza hali ya kujaa gesi tumboni kwa baadhi ya watu, jambo linaloweza kuongeza usumbufu wakati wa hedhi.

Kumbuka; Ikiwa maumivu ya hedhi ni makali sana, hedhi ni nyingi kupita kawaida au kuna dalili zisizo za kawaida, ni muhimu kumuona daktari kwa uchunguzi zaidi.

#Reply

#5Replies