Wanafunzi wa FORM 3 waliwasha moto GODORO,Moto ukawaka,Shule Ikaungua

Waziri wa Elimu Julius Ogamba ametoa taarifa mpya kuhusu moto wa kusikitisha uliotokea Utumishi Girls Academy huko Gilgil, Nakuru County  

Wanafunzi 16 wamepoteza maisha  huku wengine 79 wakijeruhiwa  na saba kati yao bado wamelazwa hospitalini 

Moto huo sasa umethibitishwa kuwa wa makusudi na wanafunzi wanane kwa sasa wako chini ya uchunguzi 

Inadaiwa walimu wawili  walikuwa wamepewa taarifa na baadhi ya wanafunzi wa Form 3 kuhusu mipango ya vurugu lakini hawakuchukua hatua stahiki kuzuia shambulizi hilo la moto 

 Hatua zilizochukuliwa hadi sasa na Wizara ya Elimu:

1.Bodi ya Usimamizi wa shule imevunjwa rasmi 

Mkuu wa shule pamoja na walimu walioshindwa kuchukua hatua watachukuliwa hatua za kinidhamu na TSC 

2.Uchunguzi zaidi bado unaendelea huku maafisa wa DCI wakirekodi taarifa na kuchunguza ushahidi 

3.Maafisa wa DCI wamewakamata wasichana wanane wa Utumishi Girls Senior Secondary School kufuatia mkasa wa moto ulioua wanafunzi 16 siku ya Alhamisi, tarehe 28 Mei 2026 

Timu za forensic zinaendelea kuchunguza namna moto ulivyoenea , kemikali zilizotumika, mifumo ya umeme  pamoja na picha za CCTV 

Walionusurika wanadai baadhi ya wanafunzi wa kidato cha tatu waliwasha godoro moto kwa makusudi  ndani ya bweni la Meline Waithera huku mlango mkuu na emergency exit  zikidaiwa kufungwa kutoka ndani, jambo lililowanasa waathiriwa. Post Via kwa Mdau wetu....

...See more

Reply

Discussions