Showing posts with label Ajali ya barabarani. Show all posts
Showing posts with label Ajali ya barabarani. Show all posts

RAIS Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kufuatia ajali iliyotokea SameAfyaclass Forum •

 DAR ES SALAAM;RAIS Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kufuatia ajali iliyotokea jana Same mkoani Kilimanjaro, huku akiwataka madereva waendelee kuzingatia kwa umakini mkubwa sheria za usalama barabarani.

"Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya ndugu zetu 37 na majeruhi 30 kutokana na ajali ya barabarani iliyotokea jana jioni eneo la Sabasaba, Barabara Kuu ya Moshi - Tanga, Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, kwa magari mawili kugongana na kuungua moto.

"Ninawaombea kwa Mwenyezi Mungu marehemu wote wapumzike kwa amani, na majeruhi wote wapone kwa haraka. Ninatoa salamu za pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mheshimiwa Nurdin Babu, familia zote za wafiwa, ndugu, jamaa na marafiki. Mwenyezi Mungu awape faraja na nguvu katika kipindi hiki kigumu.

“Kama ambavyo nilieleza Juni 27 katika hotuba yangu ya kuhitimisha shughuli za Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ajali za barabarani zimeendelea kugharimu maisha ya wapendwa wetu. Ninawasisitiza madereva kuendelea kuzingatia kwa umakini mkubwa sheria za usalama barabarani, na Jeshi la Polisi kuendelea kusimamia kikamilifu sheria hizo," ameandika Rais Samia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii.

0 Comment

TANZIA: Watu 36 wafariki dunia kwa ajali wilayani Same,Magari yawaka motoAfyaclass Forum •

Ajali hiyo  imetokea leo Jumamosi  Juni 28,2025  ikihusisha basi la abiria kampuni ya Chanel One lililokuwa likitokea Moshi kwenda Tanga na Toyota coaster lilikuwa likitokea Same kwenda Moshi.



Same. Wakati shughuli ya uokoaji na uondoshaji wa miili ikiendelea katika eneo ambalo ajali ya basi la abiria la kampuni ya Chanel One na basi dogo aina ya Toyota Coaster yaliyogongana uso kwa uso na kuwaka  moto, watu 36 wamethibitishwa kupoteza maisha huku 23 wakijeruhiwa.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi ambaye yupo eneo la tukio usiku huu amethibitisha huku akisema ni taarifa za awali.

"Miili iliyotolewa eneo la tukio mpaka sasa ni  36 na majeruhi 23 ambao wamekimbizwa hospitali na bado zoezi linaendelea,"amasema Kamanda Mkomagi 

Hata hivyo, taarifa kutoka eneo la tukio ni kwamba abiria waliokuwa wamepanda coaster kuja  Moshi mjini walikuwa wakienda kwenye sherehe ya harusi ambayo inafanyika katika ukumbi wa Kuringe hall, ambao upo Moshi mjini.



0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Forum Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Forum ASANTE.
UNDERSTOOD