Ajali hiyo imetokea leo Jumamosi Juni 28,2025 ikihusisha basi la abiria kampuni ya Chanel One lililokuwa likitokea Moshi kwenda Tanga na Toyota coaster lilikuwa likitokea Same kwenda Moshi.
Same. Wakati shughuli ya uokoaji na uondoshaji wa miili ikiendelea katika eneo ambalo ajali ya basi la abiria la kampuni ya Chanel One na basi dogo aina ya Toyota Coaster yaliyogongana uso kwa uso na kuwaka moto, watu 36 wamethibitishwa kupoteza maisha huku 23 wakijeruhiwa.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi ambaye yupo eneo la tukio usiku huu amethibitisha huku akisema ni taarifa za awali.
"Miili iliyotolewa eneo la tukio mpaka sasa ni 36 na majeruhi 23 ambao wamekimbizwa hospitali na bado zoezi linaendelea,"amasema Kamanda Mkomagi
Hata hivyo, taarifa kutoka eneo la tukio ni kwamba abiria waliokuwa wamepanda coaster kuja Moshi mjini walikuwa wakienda kwenye sherehe ya harusi ambayo inafanyika katika ukumbi wa Kuringe hall, ambao upo Moshi mjini.
REPLY HAPA
image quote pre code