Showing posts with label Ajali ya gari. Show all posts
Showing posts with label Ajali ya gari. Show all posts

Mganga Mfawidhi wa Wilaya ya Arusha, Saidi Salimu, amepata ajali ya gariAfyaclass Forum •

Mganga Mfawidhi wa Wilaya ya Arusha, Saidi Salimu, amepata ajali ya gari

Mganga Mfawidhi wa Wilaya ya Arusha, Saidi Salimu, amepata ajali ya gari akiwa na gari yake ndogo aina ya Benz lenye namba za usajili T782 EHP katika Barabara ya East Africa, maeneo ya Karavati, baada ya kugongwa na lori aina ya Fuso lenye namba za usajili T224 BRS ambalo lilipata hitilafu ya breki.

Kwa mujibu wa mashuhuda, mganga huyo aliokolewa akiwa amevunjika miguu yote miwili baada ya kubanwa ndani ya gari, na mara moja alikimbizwa katika Kituo cha Afya Murieti kwa matibabu.



0 Comment

Diogo Jota amefariki dunia kwa AjaliAfyaclass Forum •

MADRID, Hispania: MSHAMBULIAJI wa mabingwa wa Ligi Kuu England, Diogo Jota amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika ajali ya gari akiwa na umri wa miaka 28.



Idara ya Ulinzi wa Kiraia ya Hispania imesema pia ndugu wa Jota, Andre Silva amefariki katika ajali hiyo iliyotokea katika Valladolid uliopo Jimbo la Zamora.

Mshambuliaji wa Liverpool, Diogo Jota, amefariki dunia katika ajali ya gari akiwa na umri wa miaka 28.

Jota alifunga ndoa na mchumba wake wa muda mrefu, Rute Cardoso, ambaye wana watoto watatu pamoja, mwezi uliopita tu.

Ndugu yake, Andre Silva, ambaye ni mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ureno, pia alifariki katika ajali hiyo ambayo ilitokea katika jimbo la Zamora, nchini Hispania.

Silva, mwenye umri wa miaka 26, alikuwa pia mchezaji wa kandanda wa kulipwa katika klabu ya daraja la pili ya Ureno, Penafiel.

0 Comment

TANZIA: Watu 36 wafariki dunia kwa ajali wilayani Same,Magari yawaka motoAfyaclass Forum •

Ajali hiyo  imetokea leo Jumamosi  Juni 28,2025  ikihusisha basi la abiria kampuni ya Chanel One lililokuwa likitokea Moshi kwenda Tanga na Toyota coaster lilikuwa likitokea Same kwenda Moshi.



Same. Wakati shughuli ya uokoaji na uondoshaji wa miili ikiendelea katika eneo ambalo ajali ya basi la abiria la kampuni ya Chanel One na basi dogo aina ya Toyota Coaster yaliyogongana uso kwa uso na kuwaka  moto, watu 36 wamethibitishwa kupoteza maisha huku 23 wakijeruhiwa.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi ambaye yupo eneo la tukio usiku huu amethibitisha huku akisema ni taarifa za awali.

"Miili iliyotolewa eneo la tukio mpaka sasa ni  36 na majeruhi 23 ambao wamekimbizwa hospitali na bado zoezi linaendelea,"amasema Kamanda Mkomagi 

Hata hivyo, taarifa kutoka eneo la tukio ni kwamba abiria waliokuwa wamepanda coaster kuja  Moshi mjini walikuwa wakienda kwenye sherehe ya harusi ambayo inafanyika katika ukumbi wa Kuringe hall, ambao upo Moshi mjini.



0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Forum Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Forum ASANTE.
UNDERSTOOD