Showing posts with label Elimu na Ushauri. Show all posts
Showing posts with label Elimu na Ushauri. Show all posts

Kitandani kuna mamilioni ya bakteria, fangasi, wadudu na virusiAfyaclass Forum •

Kitandani kuna mamilioni ya bakteria, fangasi, wadudu na virusi

Fahamu kwamba kitanda chako kinaweza kuwa na mamilioni ya bakteria, fangasi, wadudu na virusi. Ingawa Kila mmoja wetu anadhani kitanda chake ni mahali pazuri sana pa kukaa, ndyo ni Sahihi lakini je unajua pia unaweza kupata vimelea wengi wa magonjwa kitandani?

 Kitandani kuna joto ambalo linaweza kutengeneza mazingira mazuri kwa Vimelea wa magonjwa kukua, pamejaa jasho, mate, chembechembe za ngozi zilizokufa na ndio chakula kwa ajili ya vimelea hao.

Mfano, vijidudu vidogo sana vinavyoishi kwenye vumbi. Tunamwaga seli za ngozi milioni 500 kwa siku, vijidudu hivyo hula seli hizo. Kwa bahati mbaya, vidudu hivyo na mabaki yake (kinyesi) vinaweza kusababisha mzio, pumu pamoja na tatizo la ukurutu.

Mashuka ya kitanda ni kimbilio la bakteria pia. Mwaka 2013, watafiti katika Taasisi ya Pasteur de Lille huko Ufaransa walichunguza mashuka ya kitanda cha hospitali na kugundua yamejaa bakteria wa Staphylococcus, ambao hupatikana zaidi kwenye ngozi ya binadamu.

Ingawa spishi nyingi za staphylococcus hazina madhara, lakini baadhi, kama vile S. aureus, wanaweza kusababisha maambukizi ya ngozi, chunusi na hata nimonia kwa wagonjwa walio na kinga dhaifu.

"Watu hubeba bakteria wengi katika ngozi zao," anasema Manal Mohammed, mwanabiolojia wa Chuo Kikuu cha Westminster nchini Uingereza.

"Ingawa bakteria hawa kwa kawaida hawana madhara, ila wanaweza kusababisha ugonjwa mbaya ikiwa wataingia mwilini kupitia majeraha ya wazi, ambayo ni ya kawaida hospitalini," anasema Manal.

Vitanda vya hospitali

Mwaka 2018, wanasayansi katika Chuo Kikuu cha Ibadan nchini Nigeria walipata bakteria wa E. koli katika mashuka ya kitanda cha hospitali ambayo hayajafuliwa, pamoja na bakteria wengine wa pathogenic wanaojulikana kusababisha maambukizi ya njia ya mkojo, nimonia, kuhara, homa ya uti wa mgongo na sumu katika damu.

Mwaka 2022, watafiti walikusanya sampuli kutoka kwenye vyumba vya wagonjwa waliolazwa hospitalini kwa ugonjwa wa mpox. Waligundua kuwa kitendo cha kubadilisha shuka la kitanda hutoa chembe za virusi kwenye hewa.

Mwaka 2018, mfanyakazi wa afya wa Uingereza inaaminika alipata ugonjwa huo baada ya kuambukizwa virusi wakati akibadilisha mashuka ya kitanda cha mgonjwa.

"Mashuka ya hospitalini huoshwa kwenye maji makali ya moto, ambayo huua bakteria wengi," anasema David Denning, profesa wa magonjwa ya kuambukiza katika Chuo Kikuu cha Manchester nchini Uingereza.

Isipokuwa bakteria wa C. difficile, ambaye husababisha kuhara, hasa kwa watu wazee. Kuosha kunaweza kuharibu nusu ya bakteria C. difficile, lakini seli za bakteria hao ni vigumu kufa. Hata hivyo, viwango vya maambukizi ya C. difficile vimepungua nchini Uingereza.

Bila shaka, kuna uwezekano mkubwa wa kupata bakteria wa pathogenic katika kitanda cha hospitali ambapo mgonjwa amelala kuliko katika kitanda cha mtu mwenye afya.

Vitanda vya Nyumbani

Mwaka 2013, kampuni ya vitanda ya Marekani ya Amerisleep ilichukua sampuli kutoka katika foronya ambayo haikuwa imeoshwa kwa wiki moja. IIikuwa na takribani bakteria milioni tatu kwa kila nchi ya mraba - takribani mara 17,000 zaidi ya bakteria waliopo kwenye sinki la choo.

Mwaka 2006, Denning na wenzake walikusanya mito sita kutoka kwa marafiki na familia. Mito hiyo ilikuwa ikitumika mara kwa mara na ilikuwa na umri wa kati ya miezi 18 na miaka 20. Mito yote ilikuwa na fangasi, hasa aina ya Aspergillus fumigatus - ambao hupatikana kwa wingi kwenye udongo.

"Unazungumza mabilioni au matrilioni ya chembe za fangasi kwenye kila mto," anasema Denning.

"Chanzo cha kupatikana fangasi wengi ni kwa sababu wengi wetu tunatokwa na jasho usiku. Pia sote tuna wadudu wa vumbi vitandani mwetu, na kinyesi cha wadudu hao hutoa chakula kwa fangasi. Na kisha jioni mto hupata joto kwa sababu kichwa chako hulala hapo, kwa hivyo kuna unyevu, kuna chakula, na kuna joto.”

Kwa kuwa wengi wetu huwa hatuoshi mito yetu, fangasi huishi katika hali ya utulivu na wanaweza kuishi kwa miaka. Hata kama utaosha foronya, fangasi wanaweza kuishi katika halijoto ya hadi nyuzi joto 50C (122F), na kwa vyovyote vile kuosha mito au foronya kunaweza kuifanya iwe na unyevu zaidi, na hivyo kuruhusu kukua zaidi.

0 Comment

Usipime presha baada ya kunywa vinywaji kama vile Pombe, vinywaji venye Caffeine, KahawaAfyaclass Forum •

Usifanye Mambo haya wakati wa Upimaji presha;

1. Usipime presha baada ya kunywa vinywaji kama vile Pombe, vinywaji venye Caffeine, Kahawa n.k

2. Usipime presha kama umevuta sigara dakika 30 zilizopita

3. Usipime presha kama ndyo umetoka kufanya mazoezi,kukimbia,kutembea n.k, pumzika kidogo kabla ya kuanza kupima presha

4. Wataalam wa afya hushauri hata kama ulikuwa hufanyi kazi yoyote,unashauriwa kutulia angalau kwa dakika 5-10 kabla ya kuanza kupima presha yako

5. Hakikisha unakaa vizuri kwenye kiti,huku miguu hujaikunja(maarufu kama kukunja Nne),kaa kawaida tu,huku ukinyoosha mkono wako ambao upo upande wa Moyo kwa ajili ya kuanza vipimo

8. Hakikisha miguu yako miwili imegusa chini au imekanyaga chini ya Floor wakati unapima presha

9. Usijifunge cuff ya kupimia presha juu ya shati,hakikisha mkono unakuwa wazi na kipimo kinagusa ngozi ya mwili wako

10. Pia hakikisha unafunga cuff kwenye Msuli wa mkono na sio chini ya kiwiko cha mkono au karibia na viganja vya mkono

11. Hakikisha mpira wa kipimo chako unaangalia kwa juu na sio nyuma ya mkono wako

12. Pia unashauriwa Usiongee wakati wa kupima presha yako

Usipime presha baada ya kunywa vinywaji kama vile Pombe, vinywaji venye
Caffeine, Kahawa
0 Comment

Kwa Mujibu wa Shirika la Afya Duniani(WHO); Afya yako inategemea Vitu hiviAfyaclass Forum •

 

Kwa Mujibu wa Shirika la Afya Duniani(WHO); Afya yako inategemea Vitu hivi;

–  Mazingira Mazuri ya kufanya kazi

– Kuwa Huru na Ubaguzi

– Elimu

– Mazingira Salama na yenye afya

– Kula Vizuri au kula chakula chenye afya(Healthly diet)

– Makazi mazuri au yenye Ubora

– Kupata huduma bora za Afya

– Kuwa na maji Safi na Salama ya kunywa

– Kuwa na hewa Safi n.k

WHO inasema; Afya imejumuishwa kama haki ya binadamu katika katiba za nchi 140, lakini bado mabilioni ya watu wananyimwa haki hii ya kimsingi kiutendaji. Ni wakati wa kuchukua hatua ili kuziba pengo hili.

#AfyaKwaWote #AfyaYanguHakiYangu

Credits; WHO

Photos Source: WHO

Editor,Reviewer: @afyaclass

Kwa Mujibu wa Shirika la Afya Duniani(WHO); Afya yako inategemea Vitu
hivi
0 Comment

Watu wenye ugonjwa wa moyo wanapaswa kupunguza ulaji wa sodiamuAfyaclass Forum •

Watu wenye ugonjwa wa moyo wanapaswa kupunguza ulaji wa sodiamu.

Taasisi ya Moyo ya nchini Marekani “The American Heart Association (AHA)” inapendekeza watu wazima ambao hawana au hawajulikani kuwa wako katika hatari ya kupata ugonjwa wa moyo wasitumie zaidi ya 2,300 mg ya sodiamu kwa siku. Hii ni sawa na kijiko kimoja cha chumvi.

Mtu wa kawaida aliye na ugonjwa wa moyo katika utafiti huu alizidi matumizi ya kiwango hicho kwa karibu miligramu 1,000.

Utafiti ulitumia data kutoka kwa washiriki 3,170 katika utafiti wa NHANEST  wa Kituo cha Kudhibiti Magonjwa. Sampuli hizi zilijumuisha wanaume na wanawake walio na umri wa zaidi ya miaka 20 na utambuzi wa ugonjwa wa moyo na mishipa ya damu yaani cardiovascular disease diagnosis.

Kati ya kundi hili, wengi walikuwa na umri wa miaka 65 au zaidi, walikuwa wazungu, na walikuwa na kiwango cha elimu cha chini ya wahitimu wa shule ya upili. Walikuwa Wanaume, ambao walichukua zaidi ya nusu ya masomo (56.4%), walikuwa na shida ya Uzito Mkubwa(overweight) na wastani wa ulaji wa kalori 1,862 kwa siku.

Ingawa ulaji mwingi wa sodiamu mara nyingi Watu wengi huchukulia  kama matokeo ya kutokula mlo wa kutosha au Mlo kamili swala ambalo hutokea Zaidi kwa watu wenye kipato cha Chini, utafiti huu hubadilisha nadharia hiyo,

Kundi lililokuwa na ulaji mkubwa wa sodiamu walikuwa watu wenye kipato cha Juu na wenye shahada ya chuo kikuu au zaidi.

Waandishi wa utafiti wanapendekeza kwamba watu walio na viwango vya juu vya elimu na mapato wangeweza kuwa bora katika kuripoti na kudhibiti ulaji wao wa sodiamu kila Siku kuliko wengine, ila haikuwa hivo,hii imechangia matokeo kuwa ya kushangaza Zaidi.

Nini kinatokea kwenye moyo ikiwa unatumia sodiamu nyingi?

Jina la kemikali kwenye chumvi ya mezani ni Sodium chloride(Nacl). Sodiamu ni madini ya asili, ambayo ni muhimu kwa afya ya binadamu kwa kiasi kidogo.

“Sodiamu husaidia kusawazisha maji katika mwili wako,” alielezea daktari wa magonjwa ya moyo Jayne Morgan, MD, mkurugenzi wa kimatibabu katika Shirika la Afya la Piedmont huko Atlanta, GA. “Inasaidia hata utendakazi mzuri wa misuli na mishipa.” (Dk. Morgan hakuhusika katika utafiti huo.)

“Kuna msemo Unasema, ‘Mahali sodiamu huenda, maji hufuata,'” aliiambia Medical News Today.

“Hii ndiyo sababu chumvi huongeza kiasi cha damu katika miili yenu. Madhara ya hili ni kuongezeka kwa shinikizo la damu(presha). Kuongezeka kwa shinikizo la damu basi hulazimisha moyo wako kufanya kazi kwa bidii zaidi, ambayo hatimaye inakuweka katika hatari ya kupata ugonjwa wa moyo,” Dk. Morgan alisema.

Dk. Morgan alibainisha kuwa sodiamu iliyozidi kwa muda mrefu imekuwa ikihusishwa na Tatizo la ugumu wa mishipa ya damu au kwa kitaalam atherossteosis.

SOURCES:Rejea Link;

– Taasisi ya Moyo ya nchini Marekani “The American Heart Association (AHA)”

Medical News Today Cited articles from“The American Heart Association (AHA)”

– Utafiti wa NHANEST

– Daktari wa magonjwa ya moyo Jayne Morgan, MD, mkurugenzi wa kimatibabu katika Shirika la Afya la Piedmont huko Atlanta, GA.

– Creator,Editor,Reviewer; Dr.Ombeni Mkumbwa, @afyaclass

Watu wenye ugonjwa wa moyo wanapaswa kupunguza ulaji wa sodiamu
0 Comment

Jinsi tunavyoweza kupambana na ugonjwa wa ukimwiAfyaclass Forum •

Jinsi tunavyoweza kupambana na ugonjwa wa ukimwi

Kupambana na ugonjwa wa UKIMWI ni juhudi inayohitaji ushirikiano wa jamii nzima, kutoka kwa watu binafsi hadi serikali za kitaifa na mashirika ya kimataifa.

Kujikinga na maambukizi ya UKIMWI (HIV) ni muhimu kwa afya ya mtu binafsi na jamii kwa ujumla. Hapa kuna njia za msingi za kujikinga na HIV:

1. Tumia Kondomu kwa Usahihi

Kutumia Kondomu za latex wakati wa tendo zinaweza kupunguza sana hatari ya maambukizi ya HIV na magonjwa mengine ya zinaa.

Hakikisha pia unajua Matumizi sahihi ya kondomu, hii huweza kusaidia kupunguza maambukizi ya VVU.

>>Hizi hapa ni njia Sahihi za Matumizi ya kondomu

2. Punguza Idadi ya wapenzi,kuwa na Mpenzi mmoja

Kuwa na mpenzi mmoja hupunguza hatari ya kuambukizwa HIV. Kuwa katika uhusiano wa kipekee na mtu ambaye hajaambukizwa HIV pia ni njia nzuri ya kujikinga.

3. Pima afya yako na ya mwenzako kabla ya Tendo

Kupima HIV na Mpenzi wako kabla ya kujihusisha na ngono ni hatua muhimu. Kujua hali yako na ya mwenzako kunaweza kusaidia katika kuchukua hatua za tahadhari.

4. Tumia PrEP na PEP

PrEP (Prophylaxis Kabla ya kuwa kwenye mazngira hatarishi): Ni dawa inayochukuliwa kila siku na watu ambao hawana HIV lakini wako kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa. Inaweza kupunguza hatari ya maambukizi ya HIV kwa njia ya ngono kwa zaidi ya 90%.

PEP (Prophylaxis Baada ya Kuwa kwenye hatari): Ni dawa inayoweza kuchukuliwa ndani ya masaa 72 baada ya kuwa kwenye mazingira ya kuambukizwa virusi vya HIV kuzuia maambukizi. Ni muhimu kuanza PEP haraka iwezekanavyo baada ya kufichuliwa kuwa kwenye mazingira ya kupata HIV.

>>Soma Zaidi hapa kuhusu

5. Epuka Kushiriki au kushare vitu vya ncha kali kama Sindano na mtu mwingine

Kwa watumiaji wa dawa za kulevya na wengine pia, ushiriki wa sindano, syringes, au vifaa vingine vya ncha kali kama nyembe,pin, n.k huongeza hatari ya kupata maambukizi ya VVU kwa kiwango kikubwa.

6. Matibabu kwa Wajawazito

Wanawake wajawazito wenye HIV wanaweza kupunguza hatari ya kuambukiza virusi kwa watoto wao kwa kuchukua na kutumia dawa za antiretroviral (ARVs) wakati wa ujauzito kwa Usahihi.

7. Jitunze Afya Yako kwa Ujumla

Kuwa na magonjwa mengine ya zinaa kunaweza kuongeza hatari ya kupata HIV. Kupata matibabu kwa magonjwa yoyote ya zinaa na kujitunza afya yako ya kinga ni muhimu.

8. Fahamu Vizuri Dalili za Ukimwi kwa Mtu

>>Soma hapa kwa kina Dalili za Ukimwi kwa Ujumla

>> Fahamu hapa dalili za Ukimwi kwa ngozi

Kwa kuchukua tahadhari hizi, mtu anaweza kupunguza sana hatari ya kuambukizwa HIV. Ni muhimu kukumbuka kwamba kujilinda na kulinda wengine ni jukumu la kila mtu katika jamii.

Hapa kuna njia kadhaa za msingi za kupambana na ugonjwa huu:

1. Elimu na Uelewa

Kutoa elimu sahihi na kamili kuhusu jinsi UKIMWI unavyoenea na jinsi ya kujikinga.

Kubomoa imani potofu na stigmatization inayohusiana na HIV/AIDS. Hivi vinaweza kusaidia kupunguza maambukizi.

2. Kupunguza Maambukizi

Kutumia kondomu kila wakati na kwa usahihi wakati wa kujihusisha na ngono ili kupunguza maambukizi ya HIV.

Kuhimiza uaminifu na kupunguza idadi ya washirika wa kimapenzi.

Kuhimiza na kurahisisha upimaji wa HIV na kushiriki hali ya HIV kwa uwazi na washirika wa kimapenzi. Hivi pia husaidia kupunguza maambukizi na kuongeza watu kuchukua tahadhari Zaidi.

3. Matibabu

Kutoa dawa za kurefusha maisha (ARVs) kwa watu wanaoishi na HIV/AIDS.

Kutumia dawa za kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT) wakati wa ujauzito na kujifungua. n.k

4. Utafiti na Ubunifu

Kuendelea kufanya utafiti wa chanjo za HIV na tiba mpya.

Kukuza njia mpya za kuzuia maambukizi, kama vile dawa za kuzuia kabla ya kufichua (PrEP) na baada ya kufichua (PEP).

5. Sera na Ufadhili

Kuunda sera zinazounga mkono upatikanaji wa huduma za afya na matibabu kwa wote, bila ubaguzi.

Kuongeza ufadhili wa kitaifa na kimataifa kwa programu za kuzuia, matibabu, na utafiti wa HIV/AIDS.

6. Kujenga Jamii bora

Kusaidia na kuimarisha jamii za watu wanaoishi na HIV/AIDS.

Kuhimiza ushiriki wa jamii katika kupanga na kutekeleza mikakati ya kuzuia na matibabu ya HIV.

Kwa kuchukua hatua hizi, tunaweza kupunguza maambukizi mapya ya HIV, kutoa msaada kwa wale walioathirika, na hatimaye kumaliza janga la UKIMWI.

Jinsi tunavyoweza kupambana na ugonjwa wa ukimwi
0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD