Showing posts with label Habari Mchanganyiko. Show all posts
Showing posts with label Habari Mchanganyiko. Show all posts

Tanzania yashinda kwenye tuzo za Utalii DunianiAfyaclass Forum •

Tanzania imeendelea kushikilia nafasi yake ya kimataifa kama “Nchi Inayoongoza Duniani kwa Utalii wa Safari” katika Hafla ya Fainali za World Travell Awads 2025.

Tanzania imeendelea kushikilia nafasi yake ya kimataifa kama “Nchi Inayoongoza Duniani kwa Utalii wa Safari” katika Hafla ya Fainali za World Travell Awads 2025.

Tanzania imeendelea kushikilia nafasi yake ya kimataifa kama “Nchi Inayoongoza Duniani kwa Utalii wa Safari” katika Hafla ya Fainali za World Travell Awads 2025.

Tanzania imetunukiwa taji hili adhimu katika Sekta ya utalii duniani wakati wa Hafla ya 32 ya World Travel Awards (WTA 2025), iliyofanyika katika Ukumbi wa Exhibition World Center nchini Bahrain jana Desemba 6, 2025.

Tuzo za WTA, zinazotajwa kama “Tuzo za Oscars za utalii duniani” kutokana na hadhi yake kubwa katika Sekta, Tuzo hizi zimewaleta pamoja zaidi ya washiriki 500 wakiwemo viongozi wa Serikali na wadau wa utalii.

Tanzania  imeshinda Tuzo nne miongoni mwao ni Kisiwa mashuhuri cha Zanzibar (Spice Islands) kushinda Tuzo ya World MICE Awards 2025 kama “Eneo Bora Afrika kwa Mikutano na Matukio ya Kitaasisi.”

Halkadhalika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, imetangazwa kuwa “Hifadhi Bora ya Taifa Duniani 2025” katika tuzo hizo za WTA.

Aidha, Tanzania imepata tuzo mbili zaidi katika kundi la Sekta Binafsi, ikiwemo “Kampuni Bora ya Safari za Puto Duniani,” iliyotwaliwa na kampuni ya Serengeti Balloon Safaris.

Tuzo nyingine imekwenda kwenye Kisiwa bora cha Mapumziko  Duniani na Jumaira Thanda Resort katika Kisiwa cha Mafia nchini Tanzania imeibuka mshindi katika kipengele hicho.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hizo za WTA, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, amesema tuzo hizo ni uthibitisho wa kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Tanzania pamoja na sekta binafsi katika kukuza utalii endelevu na kuimarisha uhifadhi nchini.

Tanzania, ambayo imeshinda tuzo  kwa mwaka wa pili mfululizo, inatarajiwa kuwa mwenyeji wa hafla ya fainali ya World Travel Awards itakayofanyika Desemba 2026.

0 Comment

Bei Mpya za Mafuta Mwezi Disemba, 2025 zatangazwa na EWURAAfyaclass Forum •

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kupungua kwa bei za mafuta nchini, hatua inayotokana na kushuka kwa gharama za uagizaji mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam kwa wastani wa 2.4% kwa petroli na 3.6% kwa mafuta ya taa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa tarehe 3 Desemba 2025 na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Mwainyekule, bei mpya za rejareja zimeanza kutumika rasmi Desemba.

Mabadiliko ya Bei za Mafuta

Petroli

• Dar es Salaam: Punguzo la Sh 2.38 – bei mpya Sh 2,610.10

• Tanga: Punguzo la Sh 2.26 – bei mpya Sh 2,616.13

• Mtwara: Punguzo la Sh 2.45 – bei mpya Sh 2,616.24


Dizeli

• Dar es Salaam: Sh 2,639.54

• Tanga: Sh 2,648.86

• Mtwara: Sh 2,654.32


Mafuta ya taa

• Dar es Salaam: Punguzo kubwa la Sh 120.48 – bei mpya Sh 2,513.87

• Tanga na Mtwara: Hakuna mabadiliko ya bei kutoka mwezi uliopita.


EWURA Yasisitiza Uzingatiaji wa Sheria kwa Vituo vya Mafuta

EWURA imewakumbusha wafanyabiashara wa mafuta kuhakikisha wanatoa stakabadhi za mauzo zinazobainisha:

  • Jina la kituo
  • Tarehe ya ununuzi
  • Aina ya mafuta
  • Bei kwa kila lita

Stakabadhi hizi ni muhimu kama uthibitisho endapo kutatokea changamoto kuhusu huduma iliyotolewa.

Kadhalika, vituo vyote vya mafuta vimetakiwa kuchapisha bei za bidhaa kwenye mabango yanayoonekana wazi, yakionyesha bei halisi, punguzo na vivutio vingine vya kibiashara.

EWURA imeonya kuwa ni kosa kisheria kutoweka bango la bei katika eneo la kituo, na kwamba adhabu kali zitatolewa kwa yeyote atakayekiuka masharti hayo.








0 Comment

Papa Leo alisema ni kashfa kwamba Wakristo bilioni 2.6 duniani hawana umoja thabitiAfyaclass Forum •

Katika sherehe za maadhimisho ya miaka 1,700 ya baraza kuu la Kanisa lenye makasisi wakuu kutoka nchi zikiwemo Uturuki, Misri, Syria na Israel, zilizoandaliwa mjini Iznik ambao awali ulijulikana kama Nicaea, Papa Leo alisema ni kashfa kwamba Wakristo bilioni 2.6 duniani hawana umoja thabiti.

Kiongozi huyo wa kanisa Katoliki pia amesema kwasasa, ubinadamu wote ulioathirika kwa vurugu na mizozo unataka maridhiano na upatanisho.

Pia amesema lazima watu wapinge matumizi ya dini kuhalalisha vita, vurugu ama mfumo wowote wa kiitikadi na kuongeza kusema njia za kufuata ni mazungumzo na ushirikiano.

0 Comment

Waziri Mahmoud Thabit Kombo akutana na Mabalozi wa nchi mbali mbaliAfyaclass Forum •

Waziri Mahmoud Thabit Kombo akutana na Mabalozi wa nchi mbali mbali

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo leo katika kikao na Waandishi wa Habari, ameeleza kuwa amekutana na Wanadiplomasia wanaowakilisha Mataifa yao na Taasisi za kimataifa hapa Nchini wakiwemo Mabalozi wa Nchi mbalimbali na kuwaeleza kuhusu hali ya Tanzania kwa sasa.

Mazungumzo hayo yamefanyika hii leo Novemba 28, 2025 ambapo katika taarifa yake, Balozi Kombo amewahakikishia Mabalozi hao kuhusu dhamira ya Tanzania ya kuendeleza ushirikiano na Nchi pamoja na Taasisi wanazowakilisha.

Waziri Kombo amesisitiza kuwa Tanzania imepitia kipindi kigumu ambacho hakijawahi kutokea katika historia yake ambapo kwa sasa Taifa linaingia katika hatua ya kujenga upya, kuimarisha umoja, udugu na mshikamano wa kitaifa na kwamba Serikali ya Tanzania itahakikisha inafanya tathmini ya kina na kuchukua hatua muhimu zikiwemo majadiliano, uwajibikaji na kuimarisha Taasisi ili kuzuia kilichotokea kisitokee tena.

0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD