Tahadhari ya ujio wa tetemeko yatangazwa Japan baada ya kuondoa onyo la Tsunami
Maafisa nchini Japani wameonya kuhusu tetemeko la ardhi "kubwa" linalotarajiwa katika wiki ijayo baada ya tetemeko la ukubwa wa richa 7.7 kutokea pwani ya kaskazini-mashariki, na kusababisha amri ya kuhama na maonyo ya mawimbi ya tsunami ya mita 3 (futi 10).
Maelfu ya watu waliamuriwa kuondoka katika maeneo ya pwani kwenda kwenye maeneo ya juu baada ya tetemeko hilo katika karibu na mkoa wa Iwate, kilomita 530 (maili 330) kaskazini mwa mji mkuu Tokyo.
Mawimbi makubwa zaidi ya tsunami yalikuwa na urefu wa sentimita 80. Onyo la ujio wa Tsunami liliondolewa saa chache baada ya tetemeko hilo Jumatatu.
Lakini shirika la hali ya hewa la Japan limeonya kwamba matetemeko "yanayosababisha tetemeko kubwa zaidi" yanaweza kutokea katika wiki ijayo, na kusababisha mawimbi makubwa zaidi.
Mamlaka ilisema kuna uwezekano wa kutokea tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa richa 8.0 au zaidi kuliko wakati wa kawaida.
Japan ina kumbukumbu za tetemeko kubwa la ardhi lililotokea mwaka 2011 lililosababisha tsunami iliyogharimu maisha ya zaidi ya watu 18,000 na kusababisha kuyeyuka kwa kinu cha nyuklia cha Fukushima. Via BCC.





