Idadi ya waliofariki katika mafuriko Indonesia yapita 500

Idadi ya waliofariki katika mafuriko Indonesia yapita 500

#1

Idadi ya waliofariki katika mafuriko yaliyoikumba Indonesia wiki jana sasa imeongezeka hadi zaidi ya 500, huku waokoaji wakiendelea kujitahidi kufika maeneo yaliyoathirika.

Mafuriko hayo, ambayo yalisababishwa na kimbunga kilichotokea kwenye Mlango Bahari wa Malacca, yamekumba majimbo matatu na kuathiri takriban watu milioni 1.4, kulingana na shirika la maafa la serikali.

Watu wengine 500 hawajulikani walipo, huku maelfu ya wengine wakijeruhiwa.

Indonesia ni sehemu moja tu ya Asia ambayo imekumbwa na mvua kubwa na dhoruba katika siku za hivi majuzi, huku Thailand, Malaysia, na Sri Lanka pia zikiripoti vifo.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code