Showing posts with label Jukwaa la Uchumi na Biashara. Show all posts
Showing posts with label Jukwaa la Uchumi na Biashara. Show all posts

Serikali imeongeza kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa ummaAfyaclass Forum •

Serikali imeongeza kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma kutoka shilingi 370,000 hadi shilingi 500,000, likiwa ni ongezeko la asilimia 35.

Ongezeko hilo limetangazwa na Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani Kitaifa mkoani Singida



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akitoa zawadi kwa wafanyakazi hodari katika sherehe ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi ambapo Kitaifa zimefanyika katika uwanja wa Bombadia Mkoani Singida tarehe 01 Mei, 2025.

“Ninayo furaha ya kuwatangazia kwamba katika kuzidi kuleta ustawi wa wafanyakazi mwaka huu Serikali itaongeza kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa Umma kwa asilimia 35.1″, amesema Rais Samia na kuongeza kuwa

“Nyongeza hiyo itaanza kutumika mwezi Julai 2025…huku ngazi zingine za mshahara nazo zikipanda kwa viwango vizuri kadiri ya namna bajeti itakavyoruhusu”.

Rais Samia ameongeza kuwa kwa upande wa sekta binafsi Bodi ya Kima cha Chini ya Mishahara inaendelea kufanya mapitio ili kuboresha mishahara ya wafanyakazi wa sekta binafsi.

0 Comment

Hawa ndiyo mabilionea weusi duniani 2025Afyaclass Forum •

Hawa ndiyo mabilionea weusi duniani 2025








Jarida la forbes limetoa orodha yake ya mabilionea.

Kwa jumla mabilionea 3,028 waliorodheshwa katika orodha hiyo mwaka huu inayojumlisha utajiri wao kufikia trilioni $16.1.

Katika orodha hiyo ya mabilionea kuna watu 23 weusi walio na historia ya kutoka Afrika.

Jumla ya fedha za mabilionea hao 23 kutoka sekta za fedha, Kawi na teknolojia ni $96.2.

Ifuatayo ni orodha ya mabilionea weusi duniani.

1. Aliko Dangote

Thamani halisi: $23.9 bilioni

Chanzo cha Utajiri: Simenti na sukari

Nchi: Nigeria

Ni mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Dangote Group na alianza mchakato wa kujenga kiwanda kikubwa zaidi cha mafuta na gesi barani Afrika mwaka wa 2013.

Baada ya miaka 11, uwekezaji wa dola bilioni 23 na maumivu ya kichwa, kiwanda cha kutengeneza mafuta cha Dangote hatimaye kimeanza kufanya kazi mapema 2024, na kusaidia kuongeza utajiri wa Dangote kwa dola bilioni 10.5 baada ya orodha ya mwaka jana.

2. David Steward

Thamani halisi: $ 11.4 bilioni

Chanzo cha Utajiri: Mtoa huduma wa IT

Nchi: Marekani

Ndiye Mmarekani mweusi tajiri zaidi ambaye ni mwanzilishi mwenza wa kampuni kubwa ya World Wide Technology inayotoa suluhu ya masuala ya Teknolojia ambayo wateja wake wakuu ni makampuni ya Citi na Verizon, tangu 1990.

Anahudumu kama mwenyekiti wa kampuni binafsi, ambayo sasa ina wafanyakazi karibu 10,000 na inazalisha dola bilioni 20 katika mapato ya kila mwaka.

3. Robert F. Smith

Thamani halisi: $ 10.8 bilioni

Chanzo cha Utajiri: Mfanyabiashara wa kibinafsi

Nchi: Marekani

Smith alipata dola bilioni 100 (mali chini ya usimamizi) Vista Equity Partners, kampuni kubwa zaidi ya hisa inayomilikiwa na Weusi nchini Marekani, kwa mwaka wa 2000.

Kampuni hiyo bado ipo imara, na imeajiri takriban iwafanyakazi zaidi ya 700 na inalenga kuwekeza katika makampuni ya programu pekee.

4. Alexander Karp

Thamani halisi: $ 10.8 bilioni

Chanzo cha Utajiri: Kampuni za kibinafsi

Nchi: Marekani

Karp ni mwanzilishi mwenza na afisa mkuu mtendakazi wa kampuni ya teknolojia ya Palantir Technologies pamoja na kampuni za data.

Wateja wake ni pamoja na FBI, Idara ya Ulinzi na vitengo vingine vya serikali ya Marekani.

5. Mike Adenuga

Thamani halisi: $ 6.8 bilioni

Chanzo cha Utajiri: Telecom, mafuta

Nchi: Nigeria

Adenuga alijipatia kiasi cha dola milioni moja akiwa na umri wa miaka 26 kama mfanyabiashara wa bidhaa.

Sasa ni mmoja ya watu tajiri Afrika kutokana na kampuni ya mtandao wa simu za rununu, Globacom, na kampuni ya kuchimba mafuta, Conoil.

6. Abdulsamad Rabiu

Thamani halisi: $5.1 bilioni

Chanzo cha Utajiri: Simenti, sukari

Nchi: Nigeria

Abdulsamad Rabiu ndiye mwanzilishi wa kampuni ya BUA Group, muungano wa Nigeria unaofanya kazi katika uzalishaji wa saruji, kusafisha sukari na mali isiyohamishika.

Alianzisha kampuni hiyo 1988 na bado anahudumu kama mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji.

Kupitia wakfu wake wa, Abdul Samad Rabiu , anasaidia katika miradi ya elimu, afya na maendeleo ya kijamii kote barani Afrika.

7. Michael Jordan

Thamani halisi: $3.5 bilioni

Chanzo cha Utajiri: Charlotte Hornets, ridhaa

Nchi: Marekani

Wachezaji wengi walio na viwango vya juu zaidi ni kama mchezaji bora wa mpira wa vikapu wa wakati wote, Jordan alishinda mataji sita ya NBA akiwa na klabu ya Chicago Bulls.

Wakati huo alikuwa akijipatia jumla ya $90 milioni, mbali na zaidi ya $2.4 bilioni (pretax) kutoka kwa washirika wa makampuni kama Nike, Hanes na Gatorade.

Mwaka wa 2023, Jordan aliuza hisa nyingi za klabu ya Charlotte Hornets kwa mkataba wa thamani ya $3 bilioni wa shirika la mpira wa vikapu nchini Marekani NBA.

Hii leo Jordan ni mmoja kati ya Wamarekani weusi wanne tu katika orodha ya Forbes 400 ya watu matajiri zaidi duniani.

8. Patrice Motsepe

Thamani halisi: $3 bilioni

Chanzo cha Utajiri: Madini

Nchi: Afrika Kusini

Motsepe ni mwanzilishi na mwenyekiti wa African Rainbow Minerals, kampuni ya madini inayoendesha shughuli zake Afrika Kusini na Malaysia.

Mwaka 2008, alikuwa Mwafrika wa kwanza katika orodha ya Mabilionea Duniani.

8. Oprah Winfrey

Thamani halisi: $3 bilioni

Chanzo cha Utajiri: Vipindi vya televisheni

Nchi: Marekani

Kipindi chake maarufu cha mazungumzo kiliendeshwa kwa miaka 25, hadi 2011, ambapo aliwekeza tena faida kutoka kwa programu na filamu kama vile The Colour Purple na Selma katika vyombo vya habari na biashara.

Mwaka 2011, alizindua kituo cha kebo cha OWN na kuuza hisa zake nyingi kwa Warner Bros. Discovery mnamo 2020.

10. Jay-Z

Thamani halisi: $2.5 bilioni

Chanzo cha Utajiri: Muziki

Nchi: Marekani

Mmoja wa wanamuziki wakubwa wa hip-hop wa muda wote, Jay-Z alishinda tuzo za Grammys 25 na nikaanzisha biashara nyingi, ikiwa ni pamoja na chapa ya mitindo ya Rocawear (iliyouzwa kwa $204 milioni mwaka wa 2007) na kampuni ya pombe D'Usse na Armand de Brignac.

Mwaka 2019 alikuwa bilionea wa kwanza wa hip-hop.

14. Rihanna

Thamani halisi: $ 1.4 bilioni

Chanzo cha Utajiri: Muziki, vipodozi

Nchi: Barbados

Alizaliwa kwa jina Robyn Fenty kutoka Barbados—Rihanna jina lake la kati—amekuwa bilionea kutokana na kampuni yake ya vipodozi, Fenty Beauty, ambayo anamiliki pamoja na kampuni ya kifahari ya LVMH.

18. LeBron James

Thamani halisi: $ 1.3 bilioni

Chanzo cha Utajiri: Mpira wa Kikapu

Nchi: Marekani

Mwaka 2022, Lebron James alikua mchezaji wa kwanza wa mpira wa vikapu kuwa bilionea, baada ya kupata zaidi ya $ 900 milioni (pretax) kutokana na ridhaa na ubia wa biashara.

James ni mchezaji wa NBA All-Star mara 21, bingwa mara nne wa NBA, na MVP mara nne wa NBA.

0 Comment

Jumla ya noti za Zamani 22 zaondolewa na kutotambulika tena kuanzia LeoAfyaclass Forum •



Jumla ya noti za Zamani 22 zaondolewa na kutotambulika tena kuanzia Leo

Jumla ya noti za zamani 22 zitatolewa katika mizunguko na kutotambulika kama fedha halali za Tanzania ikiwa wamiliki wake hawatakamilisha mchakato wa kuzibadilisha leo.

Oktoba 26, 2024 Benki Kuu ya Tanzania (BoT) iliutaarifu umma juu ya matoleo ya fedha hizo yaliyotakiwa kubadilishwa kuanzia Januari 6, 2025 hadi leo Aprili 5 ambayo ni pamoja na ya mwaka 1985 hadi mwaka 2003 pamoja na baadhi ya mwaka 2010.

Noti hizo za zamani zitakazositishiwa matumizi ni za shilingi ishirini (20), mia mbili (200), mia tano (500), elfu moja (1,000), elfu mbili (2,000), elfu tano (5,000) na elfu kumi (10,000) kwa matoleo ya mwaka 1985 hadi mwaka 2003.

Nyingine ni noti ya shilingi mia tano (500) iliyotolewa mwaka 2010 zenye sifa zilizoainishwa kwenye Tangazo la Serikali Na. 858 la tarehe 11 Oktoba 2024.

Kufuatia tangazo hilo BoT imewatoa.hofu baadhi ya Watanzania wanaoshindwa kutofautisha noti za Sh5,000 na Sh 10,000 zinazotolewa kwenye mizunguko na zile ambazo bado zinatumika na kubainisha kuwa zitakazondolewa ni toleo la mwaka 2003.

“Noti za Shilingi 10,000 na 5,000 ambazo ni toleo la 2010 na marejeo yake zinaendelea kutumika na hivyo hazihusiki kwenye zoezi hili la ubadilishwaji linaloendelea…

…Noti hizo zina makundi ya sahihi za Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki Kuu ambazo ni kati ya Mh. Saada Mkuya na Prof. Benno Ndulu, Mh. Mustafa Mkulo na Prof. Benno Ndulu, Dkt. Philip Mpango na Prof. Florens Luoga Pamoja na Dkt. Mwigulu Nchemba na Gavana Emmanuel Tutuba.,”imesema taarifa ya BoT iliyotolewa Aprili 4,2025.

Hii itakuwa mara ya tano kwa BoT kuondoa noti za zamani katika mzunguko wa sarafu. Mara ya kwanza zoezi hilo lilifanyika mwaka 1977 kwa noti ya Shilingi 100 iliyochapishwa kuanzia 1966 hadi 1977. Pia iliendesha zoezi hilo tena mwaka 1979 kwa kuondoa uhalali wa noti ya Shilingi 10 na Shilingi 20 zilizochapishwa kati ya mwaka 1966.

Mwaka 1980, BoT iliondoa katika mzunguko noti ya Shilingi 5 na Shilingi 20 zilizochapishwa kati ya 1966 hadi 1979.Zoezi la nne lilifanyika mwaka 1995 ambapo noti ya Shilingi 50 na Shilingi 100 zilizochapishwa kati ya mwaka 1979 hadi 1995 ziliondolewa katika mzunguko.


0 Comment

BoT yatoa Ufafanuzi,Noti zenye saini za viongozi hawa haziondolewiAfyaclass Forum •

BoT yatoa Ufafanuzi,Noti zenye saini za viongozi hawa haziondolewi



BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), imesema noti za Sh. 10,000 na 5,000 ambazo ni toleo la 2010 na marejeo yake zinaendelea kutumika na hivyo hazihusiki kwenye zoezi hili la ubadilishwaji linaloendelea.

“Noti hizo zina makundi ya saini za Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki Kuu ambazo ni kati ya Saada Mkuya na Prof. Benno Ndulu, Mustafa Mkulo na Prof. Benno Ndulu, Dk. Philip Mpango na Prof. Florens Luoga pamoja na Dk. Mwigulu Nchemba na Gavana Emmanuel Tutuba. 

Noti hizo ni kama zinavyoonekana hapa chini.



Noti Kwa mujibu wa taraifa kwa umma zoezi la kubadilisha noti hizo lilianza rasmi Janauri 06, 2025 na litafikia ukomo Aprili 05, 2025 kama ilivyoainishwa kupitia tangazo la Serikali namba 857 na 858 la Oktoba 11, 2024. 

BoT imelazimika kufafanua zaidi kuhusiana na noti za Sh. 10,000 na 5,000 toleo la 2003 zinazopaswa kuondolewa kwenye mzunguko zinazofananishwa na noti za thamani hiyo toleo la 2010 zinazoendelea kutumika.

“Noti hizo za mwaka 2003 ambazo zinaondolewa kwenye mzunguko na kukoma kutumika kuanzia Aprili 06, 2025,”Imefafanua taarifa hiyo.”
Noti zinazoondolewa.



0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Forum Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Forum ASANTE.
UNDERSTOOD