Serikali imeongeza kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma kutoka shilingi 370,000 hadi shilingi 500,000, likiwa ni ongezeko la asilimia 35.
Ongezeko hilo limetangazwa na Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani Kitaifa mkoani Singida
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akitoa zawadi kwa wafanyakazi hodari katika sherehe ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi ambapo Kitaifa zimefanyika katika uwanja wa Bombadia Mkoani Singida tarehe 01 Mei, 2025.
“Ninayo furaha ya kuwatangazia kwamba katika kuzidi kuleta ustawi wa wafanyakazi mwaka huu Serikali itaongeza kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa Umma kwa asilimia 35.1″, amesema Rais Samia na kuongeza kuwa
“Nyongeza hiyo itaanza kutumika mwezi Julai 2025…huku ngazi zingine za mshahara nazo zikipanda kwa viwango vizuri kadiri ya namna bajeti itakavyoruhusu”.
Rais Samia ameongeza kuwa kwa upande wa sekta binafsi Bodi ya Kima cha Chini ya Mishahara inaendelea kufanya mapitio ili kuboresha mishahara ya wafanyakazi wa sekta binafsi.
Reply
image quote pre code