Showing posts with label Kipengele kipya cha ChatGPT. Show all posts
Showing posts with label Kipengele kipya cha ChatGPT. Show all posts

Bosi wa Google aonya kwamba hakuna kampuni ambayo haitaathirika ikiwa AI itapata angukoAfyaclass Forum •

Bosi wa Google aonya kwamba hakuna kampuni ambayo haitaathirika ikiwa AI itapata anguko

Mkuu wa kampuni mama ya Google, Alphabet, ameonya kwamba hakuna kampuni itakayoepuka matokeo mabaya ikiwa sekta ya akili bandia inayokua kwa kasi itapata anguko kubwa.

Katika mahojiano na BBC, Sundar Pichai alikiri kwamba "kutokuwa na mantiki" kumechochea ongezeko la uwekezaji wa AI, ambalo limesababisha ongezeko kubwa la soko la teknolojia mwaka huu. Lakini kutokana na hofu inayoongezeka kwamba ukuaji wa AI unaweza kuwa usio endelevu, masoko ya hisa ya kimataifa yameona kupungua kwa kasi katika miezi ya hivi karibuni.

Alipoulizwa kama Google yenyewe inaweza kuathiriwa ikiwa kiputo cha AI kitapasuka, Pichai alijibu: "Nadhani hakuna kampuni itakayokuwa na kinga, ikiwa ni pamoja na sisi."

Mahojiano hayo yalishughulikia wasiwasi wa muda mrefu kuhusu akili bandia, ikiwa ni pamoja na usahihi, uhamisho wa kazi, ongezeko la mahitaji ya nishati na athari kwa ahadi za hali ya hewa.  Pichai alisisitiza matumizi "makubwa" ya nishati yanayohitajika ili kuwezesha mifumo ya AI, akibainisha kuwa AI ilichangia asilimia 1.5 ya matumizi ya umeme duniani mwaka jana, kulingana na Shirika la Nishati la Kimataifa.

0 Comment

Sasa ChatGPT kufikiri kwa niaba ya MtumiajiAfyaclass Forum •

Kampuni ya OpenAI imetangaza kuzindua kipengele kipya katika akili mnemba yake ya ChatGPT kitakachomruhusu Roboti huyo kufanya baadhi ya majukumu ikiwemo kufikiri kwa niaba ya Mtumiaji ikiwa ni sehemu ya mapinduzi ya mtandao ambapo Watumiaji badala ya kuhama program kupata na kutafuta taarifa kwa mikono, atategemea Mawakala wa AI kufanya kila kitu.



Kipengele hicho kipya cha ChatGPT ambacho kimepewa jina la Wakala “Agent Mode” kitaanza kufanya kazi hivi karibuni na kitakwenda kuongeza ushindani katika Makampuni ya kiteknolojia hususani Google na OpenAI ambazo zote zinatengeneza akili mnemba ambayo ina lengo la kutoa usaidizi.

Aidha kwa mujibu wa OpenAI, kipengele hicho cha Wakala kwa sasa kitaiwezesha akili mnemba ya ChatGPT kufikiri na kutekeleza majukumu kwa kutumia mfumo wake wa kidigitali wa kompyuta (virtual computer) ambayo itaiwezesha kufanya mambo magumu kwa mafano Mtumiaji akiitaka imwangalizie kalenda na kumwambia matukio yajayo pamoja na kuiambia ikusaidie kutaja viungo vitakavyotumika kwa aina ya chakula itaweza kufanya hivyo.

Aidha katika video ya maelezo OpenAI Mtumiaji mmoja aliiambia ChatGPT iweze kumwandalia na kumshauri aina ya mavazi ya kuvaa kwa ajili ya harusi na kutaka impe mapendekezo ya nguo tano tofauti kama vile kanisani, hotelini na ukumbini na ilifanya hivyo ambapo kwa mujibu wa OpenAI kipengele hicho kipya kitapatkana kwa wale ambao watalipia kuanzia ChatGPT Pro, Plus au Team Plan.

Aidha ChatGPT imesema kipengele hicho kipya kimekuja na hatari katika kupambana na taarifa za faragha za Watumiaji wake ambapo kampuni hiyo imeendelea kuonya kuwa watumiaji wake wasitoe taarifa zao za muhimu na za faragha kwa akili mnemba hiyo ambapo pia wamesema kuwa haitaweza kufanya kazi na kufikia sehemu kama Baruapepe ambazo zitahitaji uangalizi wa mtuniaji mwenyewe pamoja na kazi hatarishi kama vile kazi za kibenki.

0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Forum Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Forum ASANTE.
UNDERSTOOD