Sasa ChatGPT kufikiri kwa niaba ya Mtumiaji

Sasa ChatGPT kufikiri kwa niaba ya Mtumiaji

#1

Kampuni ya OpenAI imetangaza kuzindua kipengele kipya katika akili mnemba yake ya ChatGPT kitakachomruhusu Roboti huyo kufanya baadhi ya majukumu ikiwemo kufikiri kwa niaba ya Mtumiaji ikiwa ni sehemu ya mapinduzi ya mtandao ambapo Watumiaji badala ya kuhama program kupata na kutafuta taarifa kwa mikono, atategemea Mawakala wa AI kufanya kila kitu.



Kipengele hicho kipya cha ChatGPT ambacho kimepewa jina la Wakala “Agent Mode” kitaanza kufanya kazi hivi karibuni na kitakwenda kuongeza ushindani katika Makampuni ya kiteknolojia hususani Google na OpenAI ambazo zote zinatengeneza akili mnemba ambayo ina lengo la kutoa usaidizi.

Aidha kwa mujibu wa OpenAI, kipengele hicho cha Wakala kwa sasa kitaiwezesha akili mnemba ya ChatGPT kufikiri na kutekeleza majukumu kwa kutumia mfumo wake wa kidigitali wa kompyuta (virtual computer) ambayo itaiwezesha kufanya mambo magumu kwa mafano Mtumiaji akiitaka imwangalizie kalenda na kumwambia matukio yajayo pamoja na kuiambia ikusaidie kutaja viungo vitakavyotumika kwa aina ya chakula itaweza kufanya hivyo.

Aidha katika video ya maelezo OpenAI Mtumiaji mmoja aliiambia ChatGPT iweze kumwandalia na kumshauri aina ya mavazi ya kuvaa kwa ajili ya harusi na kutaka impe mapendekezo ya nguo tano tofauti kama vile kanisani, hotelini na ukumbini na ilifanya hivyo ambapo kwa mujibu wa OpenAI kipengele hicho kipya kitapatkana kwa wale ambao watalipia kuanzia ChatGPT Pro, Plus au Team Plan.

Aidha ChatGPT imesema kipengele hicho kipya kimekuja na hatari katika kupambana na taarifa za faragha za Watumiaji wake ambapo kampuni hiyo imeendelea kuonya kuwa watumiaji wake wasitoe taarifa zao za muhimu na za faragha kwa akili mnemba hiyo ambapo pia wamesema kuwa haitaweza kufanya kazi na kufikia sehemu kama Baruapepe ambazo zitahitaji uangalizi wa mtuniaji mwenyewe pamoja na kazi hatarishi kama vile kazi za kibenki.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code