Showing posts with label MafurikoTexas. Show all posts
Showing posts with label MafurikoTexas. Show all posts

Idadi ya waliokufa kutokana na mafuriko ya Texas yafikia 50Afyaclass Forum •

Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na mafuriko makubwa yaliyoyakumba 



Taarifa hiyo imetolewa na maafisa wa jimbo hilo wakati juhudi za uokoaji zikiendelea, huku makumi ya wasichana wakiwa bado hawajulikani walipo.Kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa na Shirika la Habari la AFP kutoka kwa maafisa wa maeneo husika, kaunti ya Kerr ndiyo iliyoathirika zaidi, ikiripoti vifo 43. 

Kaunti ya Travis imethibitisha vifo vinne, Burnet watu wawili, na mtu mmoja amefariki katika kaunti ya Tom Green. Kufuatia hali hiyo, Gavana wa Texas Greg Abbott ametangaza rasmi hali ya maafa, akilitaja tukio hilo kuwa "janga lisilo la kawaida.” 

Rais wa Marekani Donald Trump naye, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, amesema yeye na mkewe Melania wamekuwa wakiwaombea familia zote zilizoathirika na mkasa huo mkubwa.

0 Comment

Mafuriko Texas yaua takribani watu 24,Vikosi vya Uokoaji vinaendelea kutafuta wengineAfyaclass Forum •

Vikosi vya uokoaji vinaendelea kuwatafuta wasichana wasiopungua 20 waliopotea kutoka kambi ya watoto ya sherehe za majira ya joto pembeni ya mto.



Hii baada ya mvua kubwa kusababisha mafuriko ya ghafla na kuua watu wasiopungua 24 eneo la kusini-kati jimbo la Texas, Marekani.

Kwa mujibu wa afisa wa polisi wa eneo hilo, Larry Leitha, vifo hivyo vilithibitishwa Ijumaa jioni, huku juhudi za kuwaokoa wakazi waliokwama zikiendelea.

Leitha ameongeza kusema kuwa takriban watu wengine 25 hawajulikani walipo wakiwemo wasichana waliokuwa wakihudhuria kambi ya Camp Mystic, yenye watoto wapatao 750, kando ya Mto Guadalupe.

Inaarifiwa kuwa maji yaliongezeka katika mto huo kwa futi 26 ndani ya dakika 45 tu kutokana na mvua kubwa iliyonyesha usiku kucha.

Rais wa Marekani Donald Trump ametuma salamu za rambi rambi akisema ni jambo la kushutua na operesheni za uokoaji zinaendelea.

0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD