Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na mafuriko makubwa yaliyoyakumba
Taarifa hiyo imetolewa na maafisa wa jimbo hilo wakati juhudi za uokoaji zikiendelea, huku makumi ya wasichana wakiwa bado hawajulikani walipo.Kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa na Shirika la Habari la AFP kutoka kwa maafisa wa maeneo husika, kaunti ya Kerr ndiyo iliyoathirika zaidi, ikiripoti vifo 43.
Kaunti ya Travis imethibitisha vifo vinne, Burnet watu wawili, na mtu mmoja amefariki katika kaunti ya Tom Green. Kufuatia hali hiyo, Gavana wa Texas Greg Abbott ametangaza rasmi hali ya maafa, akilitaja tukio hilo kuwa "janga lisilo la kawaida.”
Rais wa Marekani Donald Trump naye, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, amesema yeye na mkewe Melania wamekuwa wakiwaombea familia zote zilizoathirika na mkasa huo mkubwa.
REPLY HAPA
image quote pre code