Showing posts with label Malaria. Show all posts
Showing posts with label Malaria. Show all posts

Asilimia 60 ya vifo Maniema nchini DRC husababishwa na MalariaAfyaclass Forum •

Asilimia 60 ya vifo Maniema nchini DRC husababishwa na Malaria



Jimbo la Maniema nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, hatimaye nalo limechukua hatua ya kukabiliana na Malaria kwa kujumuisha chanjo dhidi ya ugonjwa huo kwenye ratiba ya chanjo kwa watoto.

Hii inafuatia tangazo la shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO, kanda ya Afrika la tarehe 31 mwezi Oktoba mwaka jana wa 2024 ya kwamba DRC imeanza kutumia chanjo dhidi ya Malaria, R21 kwenye mpango wa kitaifa wa chanjo, na hivyo kuongeza mbinu muhimu kwenye zile zilizoko za kudhibiti malaria.

Asilimia 60 ya vifo Maniema husababishwa na Malaria

Kwa mujibu wa Radio Okapi ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini DRC, MOUSCO, hatua hiyo imefanyika kwenye mji mkuu wa jimbo la Maniema, Kindu siku ya Jumanne ya Agosti 19.

Kwa mujibu wa Idara ya Afya ya jimbo la Maniema, malaria ndiyo chanzo cha asilimia 60 ya vifo na magonjwa jimboni humo na kwamba watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 na wanawake wajawazito ndio wahanga wakuu wa ugonjwa huu, hali inayohalalisha uharaka wa kuanzishwa kwa chanjo hii.

Walengwa na utekelezaji

Chanjo hii itatolewa kwa watoto wenye umri wa kuanzia miezi 6 hadi miezi 23, katika maeneo yote ya afya ya jimbo la Maniema ikiwa ni sehemu ya mkakati madhubuti wa kinga, unaolenga kupunguza mzigo wa ugonjwa huu katika jamii zilizo hatarini zaidi.

Kupitia mpango huu, Maniema inalenga kupunguza vifo vinavyotokana na malaria na kuimarisha uimara wa mfumo wake wa afya.

Mafanikio ya kampeni hii yatategemea ushirikiano wa familia na utekelezaji bora wa timu za afya katika maeneo ya huduma.

0 Comment

Dalili za malaria sugu na Tiba yake,Fahamu zaidi hapaAfyaclass Forum •

Dalili za malaria sugu na Tiba yake,Fahamu zaidi hapa

Katika Makala hii tumechambua zaidi kuhusu Dalili za malaria sugu na Tiba yake,Fahamu zaidi hapa.

malaria sugu

Malaria Sugu au Chronic malaria ni pale ambapo ugonjwa wa Malaria umekuwa wa muda mrefu ambapo kwa kitaalam tunasema ni "long-term malarial infection" 

Kumbuka: Tofauti ya Malaria Sugu(chronic Malaria) na malaria ya muda mfupi(acute Malaria) ni kwenye Swala la muda tu wa mashambulizi,madhara yake pamoja na matibabu yake,

ambapo Malaria Sugu ni tatizo la muda mrefu,lakini acute malaria;mgonjwa huugua malaria baada ya muda mfupi hupona kabsa na kurudi kwenye hali yake ya kawaida pasipo maambukizi tena.

Hivo basi,Malaria Sugu na Malaria yakawaida ya muda mfupi,vyote husababishwa na vilemelea sawa,dalili sawa n.k

CHANZO CHA UGONJWA WA MALARIA SUGU

Malaria Sugu ni ugonjwa ambao husababishwa na vimelea vya magonjwa viitwavyo Plasmodium, vimelea ambavyo huendelea kufanya mashambulizi kwa muda mrefu ndani ya mwili wako.

Vimelea hivi vya Plasmodium vinavyosababisha Malaria Sugu(chronic Malaria) vipo vya aina mbali mbali kama vile;

  • Plasmodium vivax,
  • plasmodium malariae,
  • plasmodium falciparum,
  • plasmodium ovale

Vimelea hivi huenezwa na mbu jike aina ya anofelesi (anopheles). Lakini watu wengi huelewa kwamba malaria husababishwa na mbu. Mbu huyu husaidia katika usambazaji tuu wa vimelea husika.

Dalili za Malaria Sugu

DALILI ZA MALARIA SUGU NI PAMOJA NA KUPATA DALILI HIZI MARA KWA MARA NDANI YA MUDA MREFU;

1. Joto la mwili la mgonjwa kuwa juu au mgonjwa kuwa na homa

2. Mgonjwa kuhisi kichefuchefu pamoja na kutapika

3. Mgonjwa kupata maumivu makali ya kichwa

4. Mgonjwa kuhisi hali ya kizunguzungu kikali

5. Hamu ya kula au appetite ya chakula kupotea

6. Wakati mwingine mgonjwa kutoa jasho sana

7. Mgonjwa kuwa na dalili zote za kuchanganyikiwa au kuweweseka sana wakati malaria ikiwa kali

•Soma zaidi hapa,Kuhusu dalili za ugonjwa wa Malaria

VIPIMO VYA MALARIA SUGU

Moja ya vipimo ambavyo hutumika kupima ugonjwa wa Malaria Sugu ni pamoja na kipimo cha Damu kwa kutumia kifaa kinachoitwa MRDT,hadubini n.k.

Malaria Sugu,endapo Ugonjwa wa Malaria haujatibiwa huweza kusababisha madhara zaidi mwilini ikiwemo;

  • Kusababisha tatizo la kuvimba kwa bandama,kwa kitaalam hujulikana kama hyper-reactive malarial splenomegaly (HMS),
  • Matatizo kama vile; Kuchanganyikiwa,
  • Na hata Mtu kupoteza Maisha kabsa.

MATIBABU YA UGONJWA WA MALARIA

Mgonjwa wa malaria hutibiwa baada ya kufanyiwa vipimo kwa kutumia dawa mbali mbali kama vile; ALU au mseto, Malaffin, Quinine N.K

FAQs: Maswali ambayo huulizwa mara kwa mara

Je, Malaria Sugu husababishwa na nini?

Malaria Sugu ni ugonjwa ambao husababishwa na vimelea vya magonjwa viitwavyo Plasmodium, vimelea ambavyo huendelea kufanya mashambulizi kwa muda mrefu ndani ya mwili wako.

Vimelea hivi vya Plasmodium vinavyosababisha Malaria Sugu(chronic Malaria) vipo vya aina mbali mbali kama vile;

  • Plasmodium vivax,
  • plasmodium malariae,
  • plasmodium falciparum,
  • plasmodium ovale

Vimelea hivi huenezwa na mbu jike aina ya anofelesi (anopheles). Lakini watu wengi huelewa kwamba malaria husababishwa na mbu. Mbu huyu husaidia katika usambazaji tuu wa vimelea husika.

Hitimisho

Ni muhimu sana kufahamu kuhusu dalili za Ugonjwa wa Malaria ikiwemo Malaria Sugu,ili kuhakikisha unafanya vipimo na kupata tiba mapema zaidi kabla ya kupata madhara zaidi,

DALILI ZA MALARIA SUGU NI PAMOJA NA KUPATA DALILI HIZI MARA KWA MARA NDANI YA MUDA MREFU;

1. Joto la mwili la mgonjwa kuwa juu au mgonjwa kuwa na homa

2. Mgonjwa kuhisi kichefuchefu pamoja na kutapika

3. Mgonjwa kupata maumivu makali ya kichwa

4. Mgonjwa kuhisi hali ya kizunguzungu kikali

5. Hamu ya kula au appetite ya chakula kupotea

6. Wakati mwingine mgonjwa kutoa jasho sana

7. Mgonjwa kuwa na dalili zote za kuchanganyikiwa au kuweweseka sana wakati malaria ikiwa kali

Ukiona dalili kama hizi,hakikisha unawahi hospitalini kwa ajili ya Vipimo pamoja na Matibabu.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comment

Malaria kutokomezwa 2030, Fedha zachangwa na Wadau wa AfyaAfyaclass Forum •

BILIONI 37.7 KUSAIDIA KUTOKOMEZA MALARIA 2030

Na. WAF – Dodoma

Mchango kutoka kwa wadau wa mfuko wa Afya wa pamoja ikiwemo nchi ya Uswisi, Denmark, Ireland, Korea Kusini, UNFPA, UNICEF, pamoja na Benki ya Dunia kupitia awamu ya ufadhili wa moja kwa moja wa Kituo cha Afya (DHFF), (2021-2025) wamechangia kiasi cha Tshs: Bilioni 37.7 ili kusaidia kutokomeza Malaria nchini ifikapo mwaka 2030.

Waziri @ummymwalimu amesema hayo wakati wa kikao na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot kilichofanyika leo Aprili 8, 2024 katika ofisi za Wizara ya Afya Mkoani Dodoma ambapo kwa pamoja wamejadiliana masuala mbalimbali yenye manufaa kwa pande zote Mbili katika  ushirikiano unaoendelea.

“Kwa niaba ya Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, tunashukuru kupitia kwako Mhe. Balozi kwa msaada wa Serikali ya Uswisi na ahadi zako ambazo umezitoa katika kusaidia Sekta ya Afya kupitia michango mbalimbali ya ruzuku.” Ametoa shukran hizo Waziri Ummy

Amesema, lengo la jumla la mradi ni kuchangia kutokomeza Malaria ifikapo mwaka 2030 kupitia ushirikishwaji wa wadau wa Kitaifa, baina ya kisekta na kikanda kwa kushawishi mijadala ya sera za Kimataifa na miongozo ya kiufundi kwa kushirikishana desturi za Kitanzania.

“Mradi huu unawanufaisha Watanzania (Bara na Zanzibar) wanaokabiliwa na changamoto kubwa ya ugonjwa wa Malaria hasa wale wa vijijini na wale walio katika makundi hatarishi zaidi (wajawazito na watoto, watu binafsi wanaoishi katika mazingira hatarishi)”. Amesema Waziri Ummy

Waziri Ummy ameiomba Serikali ya Uswizi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kutokomeza magonjwa ya ngono ikiwa ni pamoja na VVU, mimba zisizotarajiwa, ndoa za utotoni, ukatili wa kijinsia pamoja na kusaidia wahudumu wa Afya ngazi ya jamii (CHWs) ambao wana jukumu katika kutoa huduma muhimu za Afya kwa Jamii.

Kwa upande wake, Balozi wa Uswizi nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot amesema Serikali ya Uswizi itaendelea na dhamira yake ya kuisaidia Sekta ya Afya nchini Tanzania ili kudumusha umoja uliopo baina ya nchi hizo Mbili.

“Serikali ya Uswizi itachangia kwa pamoja na Serikali ya Ujerumani kwa lengo la kuendeleza umoja wetu kwa kutoa msaada wa kiufundi kwa njia ya kujenga uwezo kwa taasisi zilizopewa mamlaka na uidhinishaji wa Bima ya Afya kwa Wote (UHI).” Amesema Balozi Chassot

Malaria kutokomezwa 2030, Fedha zachangwa na Wadau wa Afya
0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD