Asilimia 60 ya vifo Maniema nchini DRC husababishwa na Malaria

Asilimia 60 ya vifo Maniema nchini DRC husababishwa na Malaria

#1

Asilimia 60 ya vifo Maniema nchini DRC husababishwa na Malaria



Jimbo la Maniema nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, hatimaye nalo limechukua hatua ya kukabiliana na Malaria kwa kujumuisha chanjo dhidi ya ugonjwa huo kwenye ratiba ya chanjo kwa watoto.

Hii inafuatia tangazo la shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO, kanda ya Afrika la tarehe 31 mwezi Oktoba mwaka jana wa 2024 ya kwamba DRC imeanza kutumia chanjo dhidi ya Malaria, R21 kwenye mpango wa kitaifa wa chanjo, na hivyo kuongeza mbinu muhimu kwenye zile zilizoko za kudhibiti malaria.

Asilimia 60 ya vifo Maniema husababishwa na Malaria

Kwa mujibu wa Radio Okapi ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini DRC, MOUSCO, hatua hiyo imefanyika kwenye mji mkuu wa jimbo la Maniema, Kindu siku ya Jumanne ya Agosti 19.

Kwa mujibu wa Idara ya Afya ya jimbo la Maniema, malaria ndiyo chanzo cha asilimia 60 ya vifo na magonjwa jimboni humo na kwamba watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 na wanawake wajawazito ndio wahanga wakuu wa ugonjwa huu, hali inayohalalisha uharaka wa kuanzishwa kwa chanjo hii.

Walengwa na utekelezaji

Chanjo hii itatolewa kwa watoto wenye umri wa kuanzia miezi 6 hadi miezi 23, katika maeneo yote ya afya ya jimbo la Maniema ikiwa ni sehemu ya mkakati madhubuti wa kinga, unaolenga kupunguza mzigo wa ugonjwa huu katika jamii zilizo hatarini zaidi.

Kupitia mpango huu, Maniema inalenga kupunguza vifo vinavyotokana na malaria na kuimarisha uimara wa mfumo wake wa afya.

Mafanikio ya kampeni hii yatategemea ushirikiano wa familia na utekelezaji bora wa timu za afya katika maeneo ya huduma.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code