Showing posts with label Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA). Show all posts
Showing posts with label Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA). Show all posts

TMA yatoa tahadhari mvua kubwa mikoa 19 LeoAfyaclass Forum •

Mvua hizo zinatarajiwa kunyesha Leo Jumapili, Desemba 28, 2025.

Zinaweza kusababisha mafuriko, maporomoko ya udongo na usumbufu wa shughuli za kiuchumi na kijamii. 

Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imewataka wananchi kuchukua tahadhari ya kujikinga na madhara ya mvua kubwa inayotarajia kunyesha katika mikoa 19 nchini ikiwemo Dar es Salaam. 

TMA imesema mvua hizo zinatarajiwa kunyesha kesho Jumapili, Desemba 28, 2025, na huenda zikasababisha madhara mbalimbali ikiwamo mafuriko, maporomoko ya udongo na usumbufu wa shughuli za kiuchumi na kijamii. 

Taarifa ya TMA iliyotolewa leo Desemba 27, 2025 imeeleza kuwa mvua hiyo itanyesha katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Kigoma, Katavi, Singida, Dodoma, Rukwa, Songwe, Mbeya na Iringa.

Mikoa mingine ni Njombe, Morogoro, Ruvuma, Tanga, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara na Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia.

Wananchi wanaoishi katika maeneo tajwa, hususan walioko mabondeni na maeneo hatarishi, kuchukua tahadhari za mapema ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua hizo.

TMA imewasisitiza wananchi kuendelea kufuatilia taarifa na utabiri wa hali ya hewa unaotolewa mara kwa mara ili kupata taarifa sahihi na za wakati.

0 Comment

Hali ya Joto Kali nchini TMA yatoa TaarifaAfyaclass Forum •

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa kuhusu kuongezeka kwa viwango vya joto katika maeneo mbalimbali nchini, hususan katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka. Ongezeko hilo limetokana na kusogea kwa Jua la Utosi pamoja na upungufu wa mvua katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni.

Kwa mujibu wa TMA, vipindi vya Jua la Utosi hufikia kilele mwishoni mwa Novemba wakati jua likielekea kusini kwenye Tropiki ya Kaprikoni, na hurudi tena mwezi Februari likielekea kaskazini kwenye Tropiki ya Kansa. Kipindi hicho Jua la Utosi huambatana na hali ya ongezeko la Joto kwa sababu uso wa Dunia katika eneo tajwa huwa karibu zaidi na Jua kuliko maeneo mengine.

Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha ongezeko kubwa la joto katika baadhi ya vituo vya hali ya hewa nchini, ambapo hadi kufikia tarehe 27 Novemba, 2025 kituo cha hali ya hewa cha Moshi (Kilimanjaro) kiliripoti kiwango cha juu zaidi cha nyuzi joto 35.7°C mnamo tarehe 21 Novemba, 2025 ikiwa ni ongezeko la nyuzi joto 4.2°C ukilinganisha na wastani wa muda mrefu kwa mwezi Novemba katika kituo hicho. Kituo cha hali ya hewa cha Ilonga (Morogoro) kiliripoti nyuzi joto 35.5°C mnamo tarehe 20 Novemba (ongezeko la nyuzi joto 2.7°C). 

Kituo cha hali ya hewa Morogoro kiliripoti nyuzi joto 34.5°C mnamo tarehe 26 Novemba (ongezeko la nyuzi joto 2.3°C). Kituo cha Ibadakuli (Shinyanga) kiliripoti nyuzi joto 33.6°C mnamo tarehe 14 Novemba (ongezeko la nyuzi joto 2.2°C), na Dar es salaam nyuzi joto 33.2 °C mnamo tarehe 19 na 21 Novemba (ongezeko la nyuzi joto 1.6°C).

Hata hivyo, mamlaka hiyo imesema kuwa katika kipindi cha mwezi Desemba, 2025 vipindi vya mvua vinatarajiwa kujitokeza katika maeneo mengi nchini. Hali hii inatarajiwa kusababisha kupungua kwa

Joto katika baadhi ya maeneo hususan yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.

TMA imewahimiza wananchi kufuatilia taarifa rasmi za utabiri wa hali ya hewa na kuchukua tahadhari ili kukabiliana na athari za vipindi vya joto kali.




0 Comment

TMA yatoa tahadhari ya hali Mbaya ya Hewa kwa siku 5Afyaclass Forum •

TMA yatoa tahadhari ya hali Mbaya ya Hewa kwa siku 5

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya hali mbaya ya hewa kwa siku tano zijazo, kuanzia leo Jumatatu, Oktoba 27, 2025.

Aidha katika taarifa yake kwa umma imeonya wakazi wa mikoa kadhaa ya pwani na maeneo ya Kaskazini-Mashariki mwa nchi kujiandaa kwa mvua kubwa, upepo mkali, na mawimbi makubwa baharini.

Taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo jana Jumapili imebainisha kuwa hali mbaya zaidi inatarajiwa kuanza leo Jumatatu na Jumanne katika maeneo yaliyotajwa.

Aidha TMA katika taarifa yake iuliyotolewa jana Jumapili imesema kwamba leo Jumatatu, Oktoba 27, 2025, TMA mvua kubwa inatarajiwa kunyesha kwa baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) na Morogoro. Pia tahadhari hiyo imetolewa kwa visiwa Visiwa vya Unguja na Pemba.

“Kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni kubwa… tunatarajia baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, pamoja na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi, uvuvi na usafirishaji baharini,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Wakati huo huo, angalizo la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2 limetolewa kwa ajili ya ukanda wote wa pwani ya Bahari ya Hindi, ikijumuisha mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (Mafia), Lindi, Mtwara na visiwa vya Unguja na Pemba.

Imeelezwa kuwa hali inatarajiwa kupungua kidogo Jumanne, Oktoba 28, 2025,japo kuna angalizo la mvua kubwa kwa maeneo machache ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Dar es Salaam, Pwani (Mafia) na Morogoro.

Mamlaka hiyo imewashauri wananchi wanaoishi katika maeneo ya hatari kuchukua tahadhari za kutosha, huku ikiwakumbusha wadau wa bahari, hasa wavuvi, kuwa makini katika kipindi chote cha tahadhari hiyo.

0 Comment

TMA yataja chanzo cha mvua zinazonyesha kwa Sasa,baadhi ya maeneoAfyaclass Forum •

TMA yataja chanzo cha mvua zinazonyesha kwa Sasa,baadhi ya maeneo

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema, mvua zinazoendelea kunyesha tangu jana katika baadhi ya mikoa nchini zimetokana na kuongezeka kwa joto la bahari magharimbi mwa Bahari ya Hindi katika mwambao wa pwani wa nchi.

Mvua hizo ziliibua sintofahamu kutokana na majira ya Juni kuwa ya kipupwe, huku TMA ikitaja mikoa ambayo inapata mvua hizo.

Mikoa hiyo ni yote  ya ukanda wa Pwani,ukanda wa ziwa Victoria kwenye mikoa ya Kagera, Simiyu, Geita na Mara na maeneo ya Nyanda za juu Kaskazini Mashariki katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara na Kaskazini mwa mkoa wa Kigoma.

Meneja wa Utabiri wa TMA, Dk Mafuru Kantamla leo Jumatano Juni 19, 2024 ameiambia Mwananchi Digital kwamba mvua hizo hazina madhara.

“Ni mvua za kawaida, kama itatokea mifumo ikasoma zitakuwa na madhara pia tutasema, watu waendelee kufuatilia utabiri kwa kuwa mifumo inapoimarika zaidi ndipo kunasababisha mvua kuwa nyingi kidogo, kwa sasa mifumo inaonyesha mvua hizi hazina madhara,” amesema.

Amesema, kwenye ukanda wa pwani mvua zitayesha leo Juni 19 na kesho Juni 20 kisha itapungua na vipindi vya jua vitaendelea kama kawaida baada ya siku hizo mbili.

“Hata mikoa mingine, si kama zitakuwa na muendelezo, mifumo inaonyesha ni za kutafuta na ilionekana katika msimu huu wa kipupwe pamoja na kuwa na vipindi vya ukavu na upepo mkali, kutakuwa na mvua kutokana na kuongezeka kwa joto Magharibi mwa Bahari ya Hindi.” amesema.

TMA yataja chanzo cha mvua zinazonyesha kwa Sasa,baadhi ya maeneo
0 Comment

Mwenendo wa kimbunga HIDAYA kwa SasaAfyaclass Forum •

KIMBUNGA HIDAYA KINASOGEA HUKU KIKIPUNGUA NGUVU – TMA

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa ya mwenendo wa kimbunga “HIDAYA” kilichopo karibu na maeneo ya Pwani ya nchi ambapo hadi kufikia saa 9 usiku wa kuamkia leo, Kimbunga “HIDAYA” kilikuwa katika eneo la bahari takribani kilomita 125 kutoka Pwani ya Kilwa (Mkoa wa Lindi), kilomita 93 kutoka pwani ya Mafia na kilomita 128 kutoka pwani ya Dar es Salaam kikiwa na mgandamizo wa hewa wa kiasi cha 985 hPa na kasi ya upepo unaofika kilomita 120 kwa saa.

Taarifa ya TMA imeeleza kuwa tangu usiku wa kuamkia leo, matukio ya upepo mkali na mvua kubwa zinazosababishwa na uwepo wa kimbunga “HIDAYA” yameendelea kujitokeza ambapo hadi kufika saa 3 asubuhi, kituo cha hali ya hewa cha Kilwa Masoko (Lindi) kimeripoti mvua ya jumla ya kiasi cha milimita 111.3 kwa kipindi cha masaa 6 yaliyopita.

Hata hivyo Kiwango hicho cha mvua ni kikubwa sana ukizingatia kuwa wastani wa mvua kwa mwezi Mei kwa kituo cha Kilwa Masoko ni milimita 96.6 tu.

TMA imesema kiasi cha mvua kilichonyesha ndani ya saa 24 katika kituo cha Kilwa Masoko ni takribani asilimia 115 ya wastani wa mvua kwa mwezi Mei kwa kituo cha Kilwa Masoko.

Viwango vya mvua vilivyopimwa katika vituo vingine katika kipindi hicho ni milimita 90.7 kwa Mtwara na milimita 85.3 katika kituo cha hali ya hewa Naliendele (Mtwara).

Kiwango cha mvua cha milimita 90.7 kilichonyesha Mtwara ndani ya saa 24 ni takribani asilimia 168 ya wastani wa mvua kwa mwezi Mei kwa Mtwara (milimita 54), vipindi vya mvua kubwa bado vinaendelea katika maeneo hayo ya ukanda wa Pwani ya Kusini.

Hata hivyo TMA imebainisha kuwa katika vituo vya hali ya hewa vya Mtwara, Kilwa, Zanzibar, Tanga na Dar es Salaam, upepo mkali unaozidi kilomita 50 kwa saa umeweza kupimwa katika nyakati tofauti kuanzia usiku wa kuamkia leo hadi asubuhi hii.

Aidha, kimbunga “HIDAYA” kinatarajiwa kuendelea kusogea karibu zaidi na ukanda wa pwani ya nchi yetu huku kikipungua nguvu taratibu kuelekea usiku wa kuamkia Jumapili tarehe 05 Mei 2024.

Via:ITV

Mwenendo wa kimbunga HIDAYA kwa Sasa
0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD