TMA yatoa tahadhari ya hali Mbaya ya Hewa kwa siku 5

TMA yatoa tahadhari ya hali Mbaya ya Hewa kwa siku 5

#1

TMA yatoa tahadhari ya hali Mbaya ya Hewa kwa siku 5

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya hali mbaya ya hewa kwa siku tano zijazo, kuanzia leo Jumatatu, Oktoba 27, 2025.

Aidha katika taarifa yake kwa umma imeonya wakazi wa mikoa kadhaa ya pwani na maeneo ya Kaskazini-Mashariki mwa nchi kujiandaa kwa mvua kubwa, upepo mkali, na mawimbi makubwa baharini.

Taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo jana Jumapili imebainisha kuwa hali mbaya zaidi inatarajiwa kuanza leo Jumatatu na Jumanne katika maeneo yaliyotajwa.

Aidha TMA katika taarifa yake iuliyotolewa jana Jumapili imesema kwamba leo Jumatatu, Oktoba 27, 2025, TMA mvua kubwa inatarajiwa kunyesha kwa baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) na Morogoro. Pia tahadhari hiyo imetolewa kwa visiwa Visiwa vya Unguja na Pemba.

“Kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni kubwa… tunatarajia baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, pamoja na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi, uvuvi na usafirishaji baharini,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Wakati huo huo, angalizo la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2 limetolewa kwa ajili ya ukanda wote wa pwani ya Bahari ya Hindi, ikijumuisha mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (Mafia), Lindi, Mtwara na visiwa vya Unguja na Pemba.

Imeelezwa kuwa hali inatarajiwa kupungua kidogo Jumanne, Oktoba 28, 2025,japo kuna angalizo la mvua kubwa kwa maeneo machache ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Dar es Salaam, Pwani (Mafia) na Morogoro.

Mamlaka hiyo imewashauri wananchi wanaoishi katika maeneo ya hatari kuchukua tahadhari za kutosha, huku ikiwakumbusha wadau wa bahari, hasa wavuvi, kuwa makini katika kipindi chote cha tahadhari hiyo.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code