Showing posts with label Shirika la Afya Duniani(WHO). Show all posts
Showing posts with label Shirika la Afya Duniani(WHO). Show all posts

Vifaa vya afya vya kuimarisha tiba ya magonjwa ya mlipuko-WHOAfyaclass Forum •

Shirika la Afya Duniani (WHO) kupitia Wizara ya Afya limekabidhi vifaa vya afya vya kuimarisha tiba ya magonjwa ya mlipuko katika wilaya za Biharamulo na Muleba mkoani Kagera vyenye thamani ya Shilingi Milioni 112 ikiwa ni s muendelezo wa kupambana na magonjwa ya mlipuko ambayo yamekuwa yakijitokeza katika mkoa huo.



Akipokea vifaa hivyo Julai 15, 2025 kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Grace Magembe Kaimu Mkurugenzi wa Dharura na Maafa kutoka Wizara ya Afya Dkt. Erasto Sylvanus amesema kuwa vifa vilivyopokelewa ni vitanda vya kisasa vya kulaza wagonjwa, mshine za kufulia mashuka,stendi za kuwekea dawa ndoo za kuhifadhi maji na kufanyia usafi katika vituo vya afya pamoja na vifaa vya kufanya uchunguzi wa kina.

“vifaa hivi vilivyopokelewa ni jitihada zinazoendelea kufanyika katika kurejesha hali nzuri ya kupambana na magonjwa ya mlipuko na kupitia vifaa hivi vitaongeza ujuzi na utendaji kazi kwa wataalam wa afya mkoani Kagera tunaishukuru WHO kwa utayari na usaidizi mzuri katika kipindi chote ambacho nchi ya Tanzania na mkoa wa Kagera ulikumbwa na mlipuko wa ugonjwa,” amesema Dkt. Silvanus.

Aidha Dkt Slvanus ametoa wito kwa halmashauri zote za mkoa wa Kagera kutenga bajeti ya ndani kwa ajili ya kukabiliana magonjwa ya mlipuko yanayojitokeza kwa dharura kwakuwa mpaka sasa tayari wamekuwa na uzoefu juu ya magonjwa mbalimbali ya mlipuko.

Naye Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa WHO Dkt. Galberth Fadjo amesema kuwa shirika hilo kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameweka jitihada kubwa na kuchukua hatua za haraka ya kudhibiti magonjwa yenye nguvu kama Murbug yasisambae zaidi.

Mwakilishi wa huduma za Afya Ustawi wa Jamii na Lishe Kutoka Ofisi ya Rais na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi Dkt. Ernest Kyungu amesema wizara hiyo itaendelea kuratibu ili vifa hivyo vitumike kwa usahihi kutokana na miongozo na kanuni ikiwemo kuwapatia ujuzi watumiaji kupitia mafunzo kazini.

Katibu tawala wa mkoa wa Kagera Stephen Ndaki amesema Mkoa wa Kagera utaendelea kujiweka tayari kwa ajili ya kukabiliana na dharura zote za mlipuko kutokana mkoa huo kupakana na nchi jirani za ukanda wa Afrika Mashariki na ambazo hukumbwa na magonjwa ya milipuko na kutoa wito kwa wataalamu kuvitunza vizuri vifaa hivyo vilivyotolewa na kuongeza ujuzi wa kuvitumia pamoja na kuendelea kutoa taarifa kwa wananchi juu ya kujikinga na ugonjwa huo bila kujali kama Kuna ugonjwa au hakuna ugonjwa.

Ugongwa wa mlipuko wa Marburg ulitokea nchini Tanzania mwezi Machi mwaka 2023 katika Wilaya ya Bukoba ambapo watu sita walifariki dunia kati ya visa tisa vilivyoripotiwa.

Mnamo Januari 20 mwaka 2025 tovuti ya wizara ya Afya ilitangaza mlipuko wa pili katika wilaya ya Biharamulo na jumla ya watu 10 walifariki dunia ambapo wawili kati yao walithishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Marburg na wanne walihesabika.

0 Comment

Zaidi ya vifo milioni 3 kila mwaka hutokana na matumizi ya pombe na madawa ya kulevya-WHOAfyaclass Forum •

Zaidi ya vifo milioni 3 kila mwaka hutokana na matumizi ya pombe na madawa ya kulevya, wengi miongoni mwao ni wanaume.

Ripoti mpya kutoka kwa Shirika la Afya Duniani (WHO) inaonyesha kwamba vifo milioni 2.6 kila mwaka vilitokana na unywaji pombe, ambayo ni asilimia 4.7 ya vifo vyote, na vifo milioni 0.6 kutokana na matumizi ya dawa za kulevya.Vifo milioni 2 kwa watumiaji wa pombe na milioni 0.4 ya vifo vinavyotokana na madawa ya kulevya vilikuwa miongoni mwa wanaume.

Ripoti ya hali ya Ulimwenguni kutoka WHO kuhusu pombe na afya, Na matibabu ya matatizo ya matumizi ya dawa za kulevyia hutoa Taarifa pana kulingana na data za mwaka 2019 kuhusu athari za afya ya umma kwenye matumizi ya pombe na dawa za kulevya na hali ya unywaji pombe na matibabu ya matatizo ya matumizi ya dawa za kulevyia duniani kote.

Ripoti hiyo inaonyesha takriban watu milioni 400 waliishi na matatizo yanayotokana na matumizi ya pombe duniani. Kati yao,watu milioni 209 waliishi na utegemezi wa pombe.

“Matumizi ya dawa za kulevyia hudhuru sana afya ya mtu binafsi, huongeza hatari ya magonjwa sugu, hali ya afya ya akili, na kwa kusikitisha Zaidi husababisha mamilioni ya vifo vinavyoweza kuzuilika kila mwaka,

Huweka mzigo mzito kwa familia na jamii, na kuongeza uwezekano wa ajali, majeraha na vurugu, Alisema Dk Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa WHO. “Ili kujenga jamii yenye afya na usawa zaidi, ni lazima tujitolee kwa haraka kuchukua hatua za kijasiri ambazo zitapunguza matokeo mabaya ya kiafya na kijamii ya unywaji pombe na kufanya matibabu ya matatizo yanayotokana na matumizi ya dawa za kulevyia kupatikana na yawe ambayo mtu anaweza kumudu.”

Ripoti hiyo inaangazia hitaji la dharura la kuharakisha Kwa hatua ulimwenguni kote kufikia Lengo la Maendeleo Endelevu (SDG) lengo la 3.5 ifikapo 2030 kwa kupunguza matumizi ya pombe na dawa za kulevya na kuboresha upatikanaji wa matibabu bora kwa matatizo ya matumizi ya dawa.

Matokeo ya kiafya ya unywaji pombe
Ripoti hiyo inaangazia kwamba licha ya kupungua kwa viwango vya vifo vinavyotokana na pombe tangu 2010, idadi ya jumla ya vifo kutokana na unywaji pombe bado ni juu,hali isiyokubalika na inafikia milioni 2.6 mnamo 2019, na idadi kubwa zaidi ni katika Kanda ya Ulaya na kanda ya Afrika.

Viwango vya vifo vinavyotokana na unywaji pombe kwa lita moja ya pombe inayotumiwa ni vya juu zaidi katika nchi zenye mapato ya chini,na chini kabisa katika nchi zenye mapato ya juu.

Kati ya vifo vyote vilivyotokana na pombe mwaka wa 2019, inakadiriwa vifo milioni 1.6 vilitokana na magonjwa yasiyoambukiza, vikiwemo vifo 474,000 kutokana na magonjwa ya moyo na mishipa na 401,000 kutokana na saratani.

Baadhi ya vifo 724,000 vilitokana na majeraha, kama vile ajali za barabarani, kujidhuru na ghasia kati ya watu. Vifo vingine 284,000 vilihusishwa na magonjwa ya kuambukiza. Kwa mfano, unywaji wa pombe umeonyeshwa kuongeza hatari ya maambukizi ya VVU kutokana na kuongezeka kwa hatari ya kujamiiana bila kinga na kwa kuongeza hatari ya kuambukizwa TB na vifo vinavyotokana na Kinga ya Mwili kuwa dhaifu Sana.

Sehemu kubwa zaidi (13%) ya vifo vilivyotokana na pombe mnamo 2019 vilikuwa kati ya vijana wenye umri wa miaka 20-39.

Zaidi ya vifo milioni 3 kila mwaka hutokana na matumizi ya pombe na
madawa ya kulevya-WHO
0 Comment

Chad yafanikiwa kuondoa Ugonjwa wa trypanosomiasis,WHO yatangazaAfyaclass Forum •

Hii ni Nchi ya 51 kutambuliwa na WHO kwa kutokomeza ugonjwa huu wa kitropiki uliosahaulika,

Shirika la Afya Duniani (WHO) linaipongeza Chad kwa kuondoa aina ya gambinse ya trypanosomiasis kwa binadamu, pia inajulikana kama ugonjwa wa kulala yaani sleeping sickness,

#SOMA Zaidi hapa Kuhusu Ugonjwa huu wa sleeping sickness,

kama shida ya afya ya umma,Inakuwa ugonjwa wa kwanza wa kitropiki uliopuuzwa kuondolewa nchini CHAD.

Chad ni nchi ya kwanza kutambuliwa kwa kutokomeza ugonjwa wa kitropiki uliosahaulika mnamo 2024, na kuwa nchi ya 51 kufikia lengo kama hilo ulimwenguni,

“Naipongeza serikali na watu wa Chad kwa mafanikio haya. Inafurahisha kuona Chad ikijiunga na kundi linalokua la nchi ambazo zimeondoa angalau NTD moja. Lengo la nchi 100 liko karibu na linaweza kufikiwa” alisema Dk Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa WHO.

Ugonjwa Huu wa kulala yaani sleeping sickness, unaweza kusababisha dalili kama za mafua mwanzoni lakini hatimaye kusababisha mabadiliko ya tabia, kuchanganyikiwa, usumbufu wa mzunguko wa kulala au hata kukosa fahamu, mara nyingi husababisha kifo.

Upatikanaji ulioboreshwa wa utambuzi na matibabu ya mapema, pamoja na ufuatiliaji na mwitikio umethibitisha kuwa nchi zinaweza kudhibiti na hatimaye kuondoa maambukizi haya.

Kufikia sasa, nchi saba zimeidhinishwa na WHO kwa kuondoa aina ya gambinse ya trypanosomiasis kwa binadamu, nchi hizo ni: Togo (2020), Benin (2021), Côte d’Ivoire (2021), Uganda (2022), Equatorial Guinea (2022), Ghana. (2023), na Chad (2024). Aina ya ugonjwa wa rhodesiense imeondolewa kama tatizo la afya ya umma katika nchi moja, Rwanda, kama ilivyothibitishwa na WHO mnamo 2022.

“Kuondolewa kwa aina ya gambinse ya trypanosomiasis kwa binadamu nchini Chad kunaonyesha dhamira yetu ya kuboresha afya ya watu wetu. Mafanikio haya yanatokana na juhudi za kujitolea za miaka mingi za wahudumu wetu wa afya, jamii na washirika. Tutaendelea na kasi hii ya kukabiliana na mambo mengine.” magonjwa ya kitropiki yaliyosahaulika na kuhakikisha maisha bora ya baadaye kwa wananchi wote wa Chad” alisema Mhe. Dk Abdel Modjid Abderahim Mahamat, Waziri wa Afya, Chad.

Kufikia Juni 2024, katika kanda ya Afrika ya WHO, nchi 20 zimeondoa angalau ugonjwa mmoja wa kitropiki uliosahaulika, huku Togo ikiwa imeondoa magonjwa 4 na Benin na Ghana zimeondoa magonjwa 3 kila moja.

Chad yafanikiwa kuondoa Ugonjwa wa trypanosomiasis,WHO yatangaza
0 Comment

Afya za watu bilioni 1.8 duniani matatani kwa kutokufanya Mazoezi – WHOAfyaclass Forum •

Je wewe ni mtu ambaye unafanya mazoezi? Kama la, ni vema ufahamu kuwa wewe ni sehemu ya watu bilioni 1.8 duniani kote ambao wako hatarini kupata magonjwa kwa sababu tu ya kutofanya mazoezi.

Shirika la Afya ulimwenguni(WHO) kupitia taarifa yake iliyotolewa leo Geneva, Uswisi , linasema idadi hiyo ni sawa na theluthi moja au asilimia 31 ya watu wazima duniani kote kwani kwa utafiti uliofanyika mwaka 2022 watu hao hawakidhi viwango vinavyotakiwa vya kufanya mazoezi.

Idadi hiyo imeongezeka kwa asilimia 5 kati ya mwaka 2010 na 2022.

WHO inapendekeza kuwa watu wazima wanapaswa kuwa na angalau dakika 150 kila wiki za mazoezi ya kawaida au dakika 75 za mazoezi mazito kidogo ya mwili ili kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa kama vile ya moyo, kiharusi, kisukari aina ya II, kusahau, na saratani ya titi na utumbo mpana.

Utafiti huo ulifanywa na watafiti kutoka WHO pamoja na wanazuoni na kuchapishwa katika jarida la kitabibu la Lancet.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus anasema matokeo haya mapya ya utafiti yanaangazia fursa zinazopotea za kupunguza saratani, na magonjwa ya moyo na kuimarisha afya ya akili na mwili kwa kuongeza mazoezi ya mwili.

Amesema ni wakati sasa wakurejelea azma ya kuongeza kiwango cha mazoezi na kupatia kipaumbele hatua za kijasiri ikiwemo kuimarisha sera, ufadhili na kubadili mwelekeo huu unaotia wasiwasi.

Kiwango cha juu cha mazoezi kilibainika kwenye ukanda wa kipato cha juu Asia na Pasifiki, (48%) kisha Asia Kusini (45%) huku viwango vya ukosefu wa mazoezi ya mwili vikianzia asilimia 28 kwenye nchi za kipato cha juu za magharibi hadi asilimia 14 huko Ocenia.

Wanawake kama kawaida hawashiriki zaidi kwenye mazoezi kama ilivyo kwa wanaume.

“Ukosefu wa mazoezi ya mwili ni tishio lililo kimya dhidi ya afya duniani, na kuchangia kwa kiasi kikubwa kwenye mzigo wa magonjwa sugu,” amesema Dkt. Rüdiger Krech, Mkurugenzi wa WHO Idara ya kuendeleza afya.

Hivyo amesema ni vema kusaka mbinu bunifu za kuhamasisha watu kufanya mazoezi ya mwili kwa kuzingatia umri, mazingira na utamaduni wao, na kuwezesha huduma za mazoezi kufikiwa, ziwe nafuu kwa kila mtu na hivyo kupunguza hatari ya mtu kupata magonjwa kwa kukosa mazoezi.

Soma taarifa nzima hapa.

Afya za watu bilioni 1.8 duniani matatani kwa kutokufanya Mazoezi – WHO
0 Comment

Angalizo utoaji wa Dawa za Semaglutides,baada ya dawa bandia kuongezekaAfyaclass Forum •

Hii ni notisi ya kwanza rasmi iliyotolewa na WHO baada ya kuthibitisha baadhi ya ripoti hizo.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari WHO imeeleza kuwa tahadhari hiyo ni kwa ajili ya makundi matatu ya bidhaa ya Semiglutide hususan kwa chapa ya Ozempic ambayo wameeleza imegundulika huko nchini Brazili mwezi Oktoba 2023, Uingereza na Ireland Kaskazini mwezi Oktoba 2023, na Marekani mwezi Desemba 2023.

Mfumo wa Ufuatiliaji na Uangalizi wa WHO (GSMS) umekuwa ukiangalia ongezeko la ripoti kuhusu bidhaa zisizo halisi (feki) za semaglutide katika maeneo yote ya kijiografia tangu mwaka 2022.

Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa WHO wa Upatikanaji wa Dawa na Bidhaa za Afya Dkt. Yukiko Nakatani

Amewashauri wataalamu wa afya na mamlaka za udhibiti na umma kufahamu kuhusu makundi haya ya dawa zisizo halisi, “Tunatoa wito kwa wadau kuacha matumizi yoyote ya dawa zinazotiliwa shaka na kutoa taarifa kwa mamlaka husika”.

Uhaba wa dawa wachangia bidhaa bandia

Dawa hizi za Semaglutides, pamoja na bidhaa maalum za chapa ambayo si halisi zinatolewa kwa wagonjwa wa kisukari cha aina ya 2 ili kupunguza viwango vyao vya sukari kwenye damu. Semaglutides pia hupunguza hatari ya magonjwa ya moyo na mishipa.

Bidhaa nyingi za semaglutide zinapaswa kudungwa chini ya ngozi kila wiki lakini pia zinapatikana kama vidonge vya kumeza kila siku.

Katika nchi nyingine dawa hizi zimeonesha kupunguza hamu ya kula pamoja na kupunguza viwango vya sukari ya damu, na kwa hivyo zinazidi kuagizwa kwa ajili ya matumizi ya kusaidia kupunguza uzito wa mwili kwa watu.

WHO imekuwa ikifuatilia kwa ukaribu ongezeko la mahitaji ya dawa hizi pamoja na ripoti kuhusu bidhaa bandia. Bidhaa hizi zisizo halisi zinaweza kuwa na madhara kwa afya ya watu; dawa bandia zinaweza kusababisha matatizo makubwa ya kiafya.

Katika hali nyingine, kiungo tendaji ambacho hakijatangazwa kinaweza kuwa kwenye kifaa cha sindano, kama insulini, na kusababisha anuwai isiyotabirika ya hatari za kiafya au shida.

Semaglutides si sehemu ya matibabu yanayopendekezwa na WHO kwa ajili ya udhibiti wa kisukari kutokana na gharama yake kuwa ya juu kwa sasa. Kizuizi cha gharama kinafanya bidhaa hizi kutofaa kama mbinu ya afya ya umma.

Pia, kuna matibabu ya bei nafuu zaidi yanayopatikana kwa ugonjwa wa kisukari, na yana matokeo sawa na yale ya semaglutides kwenye sukari ya damu na hatari ya moyo na mishipa.

Wito kwa watu wote

Ili kujilinda dhidi ya dawa zisizo halisi na madhara yake, wagonjwa wanaotumia bidhaa hizi wanaweza kuchukua hatua kama vile kununua dawa kutoka kwa madaktari walio na leseni na kuepuka kununua dawa kutoka kwa vyanzo visivyojulikana au ambavyo havijathibitishwa.

Watu wanapaswa kuangalia vifungashio na tarehe za mwisho wa matumizi ya dawa wanapozinunua, na watumie bidhaa kama ilivyoelekezwa.

Watumiaji wa semaglutides ya sindano, wanapaswa kuhakikisha kuwa wamehifadhiwa kwenye jokofu.

Iwapo utagundua dawa uliyonunua ni bandia unaweza kuwajulisha WHO kupitia barua pepe rapidalert@who.int.

Angalizo utoaji wa Dawa za Semaglutides,baada ya dawa bandia kuongezeka
0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Forum Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Forum ASANTE.
UNDERSTOOD