Vifaa vya afya vya kuimarisha tiba ya magonjwa ya mlipuko-WHO

Vifaa vya afya vya kuimarisha tiba ya magonjwa ya mlipuko-WHO

#1

Shirika la Afya Duniani (WHO) kupitia Wizara ya Afya limekabidhi vifaa vya afya vya kuimarisha tiba ya magonjwa ya mlipuko katika wilaya za Biharamulo na Muleba mkoani Kagera vyenye thamani ya Shilingi Milioni 112 ikiwa ni s muendelezo wa kupambana na magonjwa ya mlipuko ambayo yamekuwa yakijitokeza katika mkoa huo.



Akipokea vifaa hivyo Julai 15, 2025 kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Grace Magembe Kaimu Mkurugenzi wa Dharura na Maafa kutoka Wizara ya Afya Dkt. Erasto Sylvanus amesema kuwa vifa vilivyopokelewa ni vitanda vya kisasa vya kulaza wagonjwa, mshine za kufulia mashuka,stendi za kuwekea dawa ndoo za kuhifadhi maji na kufanyia usafi katika vituo vya afya pamoja na vifaa vya kufanya uchunguzi wa kina.

“vifaa hivi vilivyopokelewa ni jitihada zinazoendelea kufanyika katika kurejesha hali nzuri ya kupambana na magonjwa ya mlipuko na kupitia vifaa hivi vitaongeza ujuzi na utendaji kazi kwa wataalam wa afya mkoani Kagera tunaishukuru WHO kwa utayari na usaidizi mzuri katika kipindi chote ambacho nchi ya Tanzania na mkoa wa Kagera ulikumbwa na mlipuko wa ugonjwa,” amesema Dkt. Silvanus.

Aidha Dkt Slvanus ametoa wito kwa halmashauri zote za mkoa wa Kagera kutenga bajeti ya ndani kwa ajili ya kukabiliana magonjwa ya mlipuko yanayojitokeza kwa dharura kwakuwa mpaka sasa tayari wamekuwa na uzoefu juu ya magonjwa mbalimbali ya mlipuko.

Naye Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa WHO Dkt. Galberth Fadjo amesema kuwa shirika hilo kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameweka jitihada kubwa na kuchukua hatua za haraka ya kudhibiti magonjwa yenye nguvu kama Murbug yasisambae zaidi.

Mwakilishi wa huduma za Afya Ustawi wa Jamii na Lishe Kutoka Ofisi ya Rais na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi Dkt. Ernest Kyungu amesema wizara hiyo itaendelea kuratibu ili vifa hivyo vitumike kwa usahihi kutokana na miongozo na kanuni ikiwemo kuwapatia ujuzi watumiaji kupitia mafunzo kazini.

Katibu tawala wa mkoa wa Kagera Stephen Ndaki amesema Mkoa wa Kagera utaendelea kujiweka tayari kwa ajili ya kukabiliana na dharura zote za mlipuko kutokana mkoa huo kupakana na nchi jirani za ukanda wa Afrika Mashariki na ambazo hukumbwa na magonjwa ya milipuko na kutoa wito kwa wataalamu kuvitunza vizuri vifaa hivyo vilivyotolewa na kuongeza ujuzi wa kuvitumia pamoja na kuendelea kutoa taarifa kwa wananchi juu ya kujikinga na ugonjwa huo bila kujali kama Kuna ugonjwa au hakuna ugonjwa.

Ugongwa wa mlipuko wa Marburg ulitokea nchini Tanzania mwezi Machi mwaka 2023 katika Wilaya ya Bukoba ambapo watu sita walifariki dunia kati ya visa tisa vilivyoripotiwa.

Mnamo Januari 20 mwaka 2025 tovuti ya wizara ya Afya ilitangaza mlipuko wa pili katika wilaya ya Biharamulo na jumla ya watu 10 walifariki dunia ambapo wawili kati yao walithishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Marburg na wanne walihesabika.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code