Showing posts with label TANZIA. Show all posts
Showing posts with label TANZIA. Show all posts

TANZIA:Muuguzi auwawa na mpenzi aliyemsomesha kisa wivu wa mapenziAfyaclass Forum •

TANZIA:Muuguzi auwawa na mpenzi aliyemsomesha kisa wivu wa mapenzi

Ofisa Muuguzi wa Hospitali ya Mji Same mkoani Kilimanjaro, Asha Bakari (25), anadaiwa kuuawa kwa kukatwa shingo na mpenzi wake, huku chanzo cha tukio hilo kikihusishwa na wivu wa mapenzi.

Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Aprili 21, 2026, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Mgeni amesema tukio limetokea jana Jumatatu, Aprili 20, 2026, katika Kata ya Kisima, karibu na hospitali hiyo.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, amesema mauaji hayo yalitokea saa tatu usiku.

Amesema Asha alikuwa akifanya kazi kwa kujitolea hospitalini hapo na alishambuliwa akiwa nyumbani kwake.

“Mtumishi wa Hospitali ya Mji Same aliuawa kwa kuchomwa kisu na mpenzi wake katika eneo la makazi karibu na hospitali aliyokuwa akifanya kazi,” amesema Mgeni.

Ameongeza kuwa kabla ya kutokea kwa mauaji hayo, alipigiwa simu na mtuhumiwa akimtaka wakutane, ndipo alipofika nyumbani kwake na kutekeleza mauaji hayo.

Kwa mujibu wa taarifa ya mkuu huyo, marehemu alikuwa na uhusiano na wanaume wawili, lakini mmoja wao na ndiye aliyemsaidia kumsomesha hadi kufikia hatua ya kupata ajira.

“Inadaiwa kuwa baada ya kuanza kazi alianza uhusiano mwingine na mtumishi wa hospitali hiyo, jambo lililomkera mtuhumiwa na kusababisha kutokea kwa tukio hili la kikatili,” amedai mkuu huyo wa wilaya akirejea taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi wilayani Same.

Mgeni amesema baada ya kutekeleza mauaji hayo, mtuhumiwa ambaye ni dereva wa bodaboda alitoroka na kutokomea kusikojulikana, huku juhudi za kumsaka zikiendelea.

“Tayari tumemtambua kwa jina na kazi yake. Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka, akipatikana atafikishwa kwenye vyombo vya sheria,” amesema.

Amesema muuguzi huyo alifariki dunia muda mfupi baada ya kushambuliwa kwa kuchomwa kisu shingoni.

Akizungumzia tukio hilo, Diwani wa Kisima, Kei Mbwambo amesema ni tukio la kinyama na kifo hicho ni pigo kwa wakazi wa eneo hilo kwa sababu ndiyo kwanza alikuwa ameanza kazi ya kuwahudumia.

“Hili ni tukio la kusikitisha na la kikatili. Haikubaliki kwa mtu kuchukua uhai wa mwingine kwa namna hii, hata kama kulikuwa na tofauti zozote za kimahusiano,” amesema Mbwambo.

Via:Mwananchi

1 Comment

TANZIA: Rais wa zamani wa Nigeria Muhammadu Buhari, amefariki DuniaAfyaclass Forum •

Rais wa zamani wa Nigeria Muhammadu Buhari, amefariki akiwa na umri wa miaka 82 katika kliniki ya London, alikuwa mtawala wa zamani wa kijeshi na aliyejiita mwanademokrasia aliyebadili dini na alirejea madarakani kupitia uchaguzi lakini alijitahidi kuwashawishi Wanigeria kwamba angeweza kutekeleza mabadiliko aliyoahidi.



Kamwe hakuwa mwanasiasa wa asili, alionekana kama mtu asiye na hisia na mkali. Lakini alibaki na sifa ya uaminifu wa binafsi, jambo adimu kwa mwanasiasa nchini Nigeria.

Baada ya majaribio matatu kufeli, Buhari alipata ushindi wa kihistoria mwaka 2015, na kuwa mgombea wa kwanza wa upinzani nchini humo kushinda.

Mnamo 2019, alichaguliwa tena kwa muhula mwingine wa miaka minne.

Buhari mara zote amekuwa maarufu miongoni mwa maskini wa kaskazini (inayojulikana kama "talakawa" katika lugha ya Kihausa) lakini kwa kampeni ya 2015, alikuwa na faida ya kundi lililoungana la upinzani nyuma yake.

Wengi wa wale waliomuunga mkono walidhani historia yake ya kijeshi na sifa za kinidhamu ndizo ambazo nchi ilihitaji kukabiliana na uasi wa Kiislamu kaskazini. Buhari pia aliahidi kukabiliana na rushwa na upendeleo serikalini, na kuunda fursa za ajira kwa vijana wa Nigeria.

Lakini muda wake madarakani uliambatana na kuporomoka kwa bei ya mafuta duniani na mzozo mbaya zaidi wa kiuchumi nchini humo kuwahi kutokea kwa miongo kadhaa.

Utawala wake pia ulishutumiwa kwa namna ulivyokuwa ukishughulikia ukosefu wa usalama. Wakati akifanya kampeni aliahidi kulishinda kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Boko Haram. Lakini kundi hilo linasalia kuwa tishio na moja ya mirengo yake sasa inahusishwa na kundi linalojiita Islamic State.

Pia kulikuwa na ongezeko la mapigano makali kati ya wakulima na wafugaji wa kabila la Fulani katikati mwa Nigeria.

Bw.Buhari, Mfula, alishutumiwa kwa kutochukua hatua za kutosha kwa wafugaji au kufanya vya kutosha kukomesha mzozo huo.

Shughuli za wanaojiita majambazi katika eneo la kaskazini-magharibi mwa nchi zilishuhudia kutekwa nyara kwa mamia ya wanafunzi wa shule za sekondari.

Chini ya uangalizi wake vikosi vya jeshi vilishutumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu kama vile kuwafyatulia risasi waandamanaji waliokuwa wakipinga ukatili wa polisi kwenye lango la tollgate la Lekki huko Lagos mnamo Oktoba 2020.

Muhammadu Buhari alikuwa nani?

Muhammadu Buhari alizaliwa Desemba 1942 huko Daura katika jimbo la Katsina kaskazini mwa Nigeria, karibu na mpaka na Niger. Wakati huo, Nigeria ilikuwa inadhibitiwa na Waingereza na ilikuwa miaka 18 zaidi kabla ya nchi hiyo kupata uhuru.

Baba yake Buhari, ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka minne, alikuwa kutoka jamii ya Fulani, wakati mama yake, aliyemlea, alikuwa kutoka jamii ya Kanuri.

Katika mahojiano ya 2012, Buhari alizungumza kuwa mtoto wa 23 wa baba yake na wa 13 wa mama yake.

0 Comment

Rais Ruto atangaza maombolezo ya siku tatu kufuatia Moto Shuleni ulioua 18Afyaclass Forum •

Rais Ruto atangaza maombolezo ya siku tatu kufuatia Moto Shuleni ulioua 18

Rais wa Kenya William Ruto ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kuanzia Jumatatu baada ya watoto 18 kufa kwa kuungua moto kwenye bweni, katika shule ya msingi ya Hillside Endarasha katika kaunti ya Nyeri.

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio makamu wa Rais Rigathi Gachagua, alisema wanafunzi 70 hawajulikani walipo na 27 wako hospitali.

Gachagua ameutaja mkasa huo kuwa wa kutisha na kusema kwamba kazi ya uchunguzi kwa kutumia vinasaba DNA itahitajika ili kusaidia kuwabaini wahanga na kutoa wito kwa jamii kusaidia katika kuwatafuta waliopotea.

Polisi wa Kenya wameimarisha uchunguzi wao baada ya kutokea mkasa huo wa moto. Msemaji wa polisi ya Kenya Resila Onyango, ameliambia shirika la Habari la AFP kwamba miili iliyopatikana katika eneo la tukio ilikuwa imeteketezwa kiasi cha kutoweza kutambuliwa. Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.

Taharuki imetanda miongoni mwa wanafamilia wa watoto huku wakiwa wamekusanyika shuleni hapo wakisubiri kupata taarifa juu ya wapendwa wao ambao hawajapatikana bado.

Kulingana na jeshi la polisi, miili ya watoto iliyopatikana katika eneo la ajali imeungua kiasi cha kutotambulika.

Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya linasaidiana na mashirika mengi ya kukabiliana na hali ya dharura na pia linatoa msaada wa kisaikolojia kwa wanafunzi na wanafamilia waliopata kiwewe.

Muchai Kihara, mwenye umri wa miaka 56, amesema amebahatika kumpata mwanawe Stephen Gachingi mwenye umri wa miaka 12 akiwa hai alipokimbilia shuleni hapo mwendo wa saa saba mchana siku ya Ijumaa.

Amesema ana furaha kubwa kwa kuwa mwanawe yuko hai ingawa alipata majeraha sehemu ya nyuma ya kichwa chake na macho yake yameathiriwa na moshi.

Katikati mwenye tai nyekundu, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya akiwa katika shule ya illside Endarasha Academy, katika mji wa Kieni, kaunti ya Nyeri.Picha: Monicah Mwangi/REUTERS

Kenya imekumbwa na mikasa ya moto katika miaka ya nyuma, mnamo mwaka 2016, wanafunzi tisa walikufa baaya ya kuungua moto katika shule ya sekondari ya wasichana katika mtaa wa mabanda wa Kibera jijini Nairobi.

Mnamo mwaka 2001, wanafunzi 67 waliuawa katika shambulio la kuchomwa moto bweni lao katika shule ya upili katika mji wa Machakos ulio kusini mwa jiji la Nairobi.

Wanafunzi wawili walishtakiwa kwa mauaji, na mwalimu mkuu na naibu wake walipatikana na hatia ya kuwa wazembe.

Nchi Jirani za Tanzania na Uganda pia zimekumbwa na mikasa ya shule kuchomwa moto iliyosababisha hasara.

Chanzo: AFP

0 Comment

Mwanamuziki Mkongwe Sergio Mendes Afariki dunia baada ya Kuugua Uviko 19Afyaclass Forum •

Mwanamuziki Mkongwe Sergio Mendes Afariki dunia baada ya Kuugua Uviko 19

MWANAMUZIKI Mkongwe wa Brazil, Sergio Mendes (83), amefariki dunia jijini Los Angeles baada ya kuugua Uviko19 iliyomsumbua kwa muda mrefu.

Mpiga Piano na Mwandishi huyo wa nyimbo ni mmoja kati ya watu wa kwanza kuutambulisha Muziki wa Brazil “Genre bossa nova” Kimataifa katika miaka ya 1960 kupitia wimbo wake maarufu wa Mas Que Nada.

Mshindi huyo wa tuzo za Grammy amewahi kufanya kazi na Wanamuziki mashuhuri kama Stevie Wonder, Black Eyed Peas na Justin Timberlake.

Mwezi Novemba mwaka jana Mendes alifanya show zilizofanikiwa kuuza tiketi zote jijini Paris, London na Barcelona.

0 Comment

Mwanariadha wa Uganda Rebecca Cheptegei afariki duniaAfyaclass Forum •

Mwanariadha wa Uganda Rebecca Cheptegei amefariki Alhamisi alipokuwa akipatiwa matibabu katika hospitali moja mjini Eldoret nchini Kenya kutokana na kushindwa kwa viungo vya mwili, Mkurugenzi wa Huduma za Kliniki katika kituo hicho Owen Menach amethibitisha.

Cheptegei ambaye alishiriki katika Michezo ya Olimpiki ya mwaka huu alidaiwa kumwagiwa petroli na kuchomwa moto na mpenzi wake mjini Kitale Jumapili, na kusababisha mwili wake kuungua kwa asilimia 80 na hatimaye kufariki.

Shirikisho la Riadha la Uganda (UAF) pia limethibitisha kuaga dunia kwa Cheptegei katika chapisho kwenye akaunti yao rasmi ya X, na kutaka haki itendeke likisema “aliangukiwa na vurugu za nyumbani.” “Tuna masikitiko makubwa kutangaza kifo cha mwanariadha wetu Rebecca Cheptegei mapema leo asubuhi, ambaye alihusika na dhuluma za nyumbani.

0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD