Rais wa zamani wa Nigeria Muhammadu Buhari, amefariki akiwa na umri wa miaka 82 katika kliniki ya London, alikuwa mtawala wa zamani wa kijeshi na aliyejiita mwanademokrasia aliyebadili dini na alirejea madarakani kupitia uchaguzi lakini alijitahidi kuwashawishi Wanigeria kwamba angeweza kutekeleza mabadiliko aliyoahidi.
Kamwe hakuwa mwanasiasa wa asili, alionekana kama mtu asiye na hisia na mkali. Lakini alibaki na sifa ya uaminifu wa binafsi, jambo adimu kwa mwanasiasa nchini Nigeria.
Baada ya majaribio matatu kufeli, Buhari alipata ushindi wa kihistoria mwaka 2015, na kuwa mgombea wa kwanza wa upinzani nchini humo kushinda.
Mnamo 2019, alichaguliwa tena kwa muhula mwingine wa miaka minne.
Buhari mara zote amekuwa maarufu miongoni mwa maskini wa kaskazini (inayojulikana kama "talakawa" katika lugha ya Kihausa) lakini kwa kampeni ya 2015, alikuwa na faida ya kundi lililoungana la upinzani nyuma yake.
Wengi wa wale waliomuunga mkono walidhani historia yake ya kijeshi na sifa za kinidhamu ndizo ambazo nchi ilihitaji kukabiliana na uasi wa Kiislamu kaskazini. Buhari pia aliahidi kukabiliana na rushwa na upendeleo serikalini, na kuunda fursa za ajira kwa vijana wa Nigeria.
Lakini muda wake madarakani uliambatana na kuporomoka kwa bei ya mafuta duniani na mzozo mbaya zaidi wa kiuchumi nchini humo kuwahi kutokea kwa miongo kadhaa.
Utawala wake pia ulishutumiwa kwa namna ulivyokuwa ukishughulikia ukosefu wa usalama. Wakati akifanya kampeni aliahidi kulishinda kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Boko Haram. Lakini kundi hilo linasalia kuwa tishio na moja ya mirengo yake sasa inahusishwa na kundi linalojiita Islamic State.
Pia kulikuwa na ongezeko la mapigano makali kati ya wakulima na wafugaji wa kabila la Fulani katikati mwa Nigeria.
Bw.Buhari, Mfula, alishutumiwa kwa kutochukua hatua za kutosha kwa wafugaji au kufanya vya kutosha kukomesha mzozo huo.
Shughuli za wanaojiita majambazi katika eneo la kaskazini-magharibi mwa nchi zilishuhudia kutekwa nyara kwa mamia ya wanafunzi wa shule za sekondari.
Chini ya uangalizi wake vikosi vya jeshi vilishutumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu kama vile kuwafyatulia risasi waandamanaji waliokuwa wakipinga ukatili wa polisi kwenye lango la tollgate la Lekki huko Lagos mnamo Oktoba 2020.
Muhammadu Buhari alikuwa nani?
Muhammadu Buhari alizaliwa Desemba 1942 huko Daura katika jimbo la Katsina kaskazini mwa Nigeria, karibu na mpaka na Niger. Wakati huo, Nigeria ilikuwa inadhibitiwa na Waingereza na ilikuwa miaka 18 zaidi kabla ya nchi hiyo kupata uhuru.
Baba yake Buhari, ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka minne, alikuwa kutoka jamii ya Fulani, wakati mama yake, aliyemlea, alikuwa kutoka jamii ya Kanuri.
Katika mahojiano ya 2012, Buhari alizungumza kuwa mtoto wa 23 wa baba yake na wa 13 wa mama yake.
REPLY HAPA
image quote pre code