Showing posts with label Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI). Show all posts
Showing posts with label Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI). Show all posts

Waandishi wa Habari Kupimwa Moyo na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)Afyaclass Forum •

Waandishi wa Habari Kupimwa Moyo na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)

DAR-ES-SALAAM : TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)  inatarajia kufanya upimaji wa siku mbili wa  magonjwa ya moyo bure kwa waandishi wa habari na Wahariri wa Mkoa wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani ikiwa ni hatua ya kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza kwa kundi hilo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi  Mtendaji wa JKCI, Dk Peter Kisenge amesema upimaji huo maalum utafanyika Disemba 23 hadi 24 katika tawi la JKCI lililopo Ostabey ikiwa ni  sehemu ya utekelezaji wa ahadi aliyotoa kwa waandishi wa habari. 

"Tumekuwa tukifata watu mbalimbali ,mashirika na wadau kama wadau wa michezo,wasanii,wanafunzi wa shule za msingi,tulikutana na wahariri walipimwa afya ya moyo ilikuwa ni ahadi yangu kuwafikia waandishi wa habari kabla ya mwaka huu kuisha katika mkoa wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani kesho na kesho kutwa kuaanzia saa nne asubuhi hadi saa 10 tutanaanza kutoa huduma ,"amesisitiza Dk Kisenge.

0 Comment

Wagonjwa wa moyo kutoka Sierra Leone kutibiwa TanzaniaAfyaclass Forum •

Wagonjwa wa moyo kutoka Sierra Leone kutibiwa Tanzania

Ujumbe wa wataalamu wa Wizara ya Afya kutoka Sierra Leone, wameingia makubaliano na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), kwa ajili ya kutibu wagonjwa wanaotoka nchini humo.

Wataalamu hao walikuja nchini kwaajili ya kujifunza namna ya kuanzisha matibabu ya moyo nchini kwao huku wakishangaa uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali, Taasisi ya JKCI.

Akizungumza wakati wa kupokea ujumbe huo, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dk. Peter Kisenge, amesema ziara hiyo inalenga kuendeleza ushirikiano wa matibabu ya moyo kati ya Tanzania na Sierra Leone ikiwa ni dhamira ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ya kutangaza utalii tiba kimataifa.

“Ujumbe huu umefika hapa nchini kujifunza uwekezaji wa matibabu ya moyo na usambazaji wa dawa na vifaa tiba kutoka kwa Bohari ya Dawa (MSD), ikiwa ni uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali ya Rais Dk. Samia,” amesema Dk. Kisenge.

Amesema ujumbe huo wa wataalamu kutoka Sierra Leone umekiri kujifunza mambo mengi kutoka JKCI na wataleta wagonjwa na wao kwenda kuanzisha taasisi yao kwa ushirikiano na taasisi ya JKCI.

Dk. Kisenge amesema wataalamu hao wa Sierra Leone, wamejifunza utendaji kazi mkubwa na imara kutoka kwa watumishi wa JKCI, ikiwamo namna ya kuhudumia wagonjwa mahututi.

Amesema kuwa ugeni huo ni hatua kubwa ambayo inatimiza malengo ya Rais Dk. Samia ya kukuza tiba utalii nchini kutokana na uwekezaji mkubwa alioufanya kwenye sekta ya afya.

Ameongeza kuwa, mbali na huduma za upasuaji wanazofanya hospitalini hapo, wanaendelea kutoa huduma za upimaji wa moyo kupitia mpango wao wa Dk. Samia, Tiba Mkoba.

Amesema mpango huo unasogeza huduma hizo karibu na wananchi huku wakizijengea uwezo hospitali zingine za kanda ikiwamo Benjamin Mkapa pia Chato na Geita.

Wagonjwa wa moyo kutoka Sierra Leone kutibiwa Tanzania
0 Comment

Upasuaji kwa njia ya tundu dogo wa kurekebisha mishipa ya damu iliyotanuka wafanyikaAfyaclass Forum •

Upasuaji kwa njia ya tundu dogo wa kurekebisha mishipa ya damu iliyotanuka wafanyika

Kwa mara ya kwanza wataamu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) wamefanya upasuaji kwa njia ya tundu dogo wa kurekebisha mishipa ya damu iliyotanuka na kupasuka sehemu ya kifua na tumbo kwa wagonjwa watano wenye matatizo hayo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alisema wagonjwa wenye matatizo hayo wengi wao walikuwa wakipoteza maisha na wale ambao walikuwa wanapona walipewa rufaa ya kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Dk Kisenge alisema upasuaji huo umefanywa na madaktari wazawa kwa kushirikiana na madaktari kutoka India na tayari mgonjwa mmoja  alishafanyiwa upasuaji huku wengine watatu  watafanyiwa upasuaji huo leo na mmoja kesho.

“Kwa mara ya tatu tunavunja rekodi tumefanya matibabu makubwa ya kurekebisha mishipa ya damu ambayo imetanuka na kupasuka hii ni tatizo ambalo watu wengi wanalipata na kupoteza maisha ghafla  na wanaobaki tunawapeleka nje ya nchi lakini hivi  sasa tutaanza kuwahudumia hapa nchini”,.

“Ni upasuaji mkubwa kufanyika Tanzania na Afrika Mashariki na Kati tumevunja rekodi tunampongeza Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapenda wananchi wake na kutoa  kiasi cha shilingi milioni 900 za matibabu ya kibingwa katika Taasisi yetu,”, alisema Dkt. Kisenge.

Mkurugenzi huyo Mtendaji ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo alisema  mishipa ya damu ya tumboni na kifuani kutanuka na kupasuka kunasabahishwa na vitu vingi ikiwemo shinikizo la juu la damu  ambayo haitibiwi vizuri,uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe uliokithiri na uzito mkubwa.

Dkt. Kisenge alisema katika Taasisi hiyo kuna wagonjwa wapatao 30 wanaosubiri kupata matibabu hayo ambapo gharama zake ni shilingi milioni 80 endapo mgonjwa atatibiwa hapa nchini na milioni 150 akitibiwa nje ya  nchi.
“Tutaendelea kutoa matibabu haya na tutaendelea kuwa na matibabu mapya mengine kwani wataalamu wetu wanajifunza kila siku. Upasuaji huu tulioufanya ukifanyika kwa njia ya kufungua kifua unachukua saa nane ila kwa njia ya tundu dogo ni saa mbili hii ni njia nzuri japo gharama ni kubwa ila Mhe. Rais wetu ametoa  fedha ili wananchi wasaidiwe”, alisema Dkt.Kisenge.

Upasuaji kwa njia ya tundu dogo wa kurekebisha mishipa ya damu
iliyotanuka wafanyika
0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD