Waandishi wa Habari Kupimwa Moyo na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)
DAR-ES-SALAAM : TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) inatarajia kufanya upimaji wa siku mbili wa magonjwa ya moyo bure kwa waandishi wa habari na Wahariri wa Mkoa wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani ikiwa ni hatua ya kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza kwa kundi hilo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dk Peter Kisenge amesema upimaji huo maalum utafanyika Disemba 23 hadi 24 katika tawi la JKCI lililopo Ostabey ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi aliyotoa kwa waandishi wa habari.
"Tumekuwa tukifata watu mbalimbali ,mashirika na wadau kama wadau wa michezo,wasanii,wanafunzi wa shule za msingi,tulikutana na wahariri walipimwa afya ya moyo ilikuwa ni ahadi yangu kuwafikia waandishi wa habari kabla ya mwaka huu kuisha katika mkoa wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani kesho na kesho kutwa kuaanzia saa nne asubuhi hadi saa 10 tutanaanza kutoa huduma ,"amesisitiza Dk Kisenge.









image quote pre code