Showing posts with label Ugonjwa wa moyo. Show all posts
Showing posts with label Ugonjwa wa moyo. Show all posts

Waandishi wa Habari Kupimwa Moyo na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)Afyaclass Forum •

Waandishi wa Habari Kupimwa Moyo na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)

DAR-ES-SALAAM : TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)  inatarajia kufanya upimaji wa siku mbili wa  magonjwa ya moyo bure kwa waandishi wa habari na Wahariri wa Mkoa wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani ikiwa ni hatua ya kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza kwa kundi hilo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi  Mtendaji wa JKCI, Dk Peter Kisenge amesema upimaji huo maalum utafanyika Disemba 23 hadi 24 katika tawi la JKCI lililopo Ostabey ikiwa ni  sehemu ya utekelezaji wa ahadi aliyotoa kwa waandishi wa habari. 

"Tumekuwa tukifata watu mbalimbali ,mashirika na wadau kama wadau wa michezo,wasanii,wanafunzi wa shule za msingi,tulikutana na wahariri walipimwa afya ya moyo ilikuwa ni ahadi yangu kuwafikia waandishi wa habari kabla ya mwaka huu kuisha katika mkoa wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani kesho na kesho kutwa kuaanzia saa nne asubuhi hadi saa 10 tutanaanza kutoa huduma ,"amesisitiza Dk Kisenge.

0 Comment

Watu wenye ugonjwa wa moyo wanapaswa kupunguza ulaji wa sodiamuAfyaclass Forum •

Watu wenye ugonjwa wa moyo wanapaswa kupunguza ulaji wa sodiamu.

Taasisi ya Moyo ya nchini Marekani “The American Heart Association (AHA)” inapendekeza watu wazima ambao hawana au hawajulikani kuwa wako katika hatari ya kupata ugonjwa wa moyo wasitumie zaidi ya 2,300 mg ya sodiamu kwa siku. Hii ni sawa na kijiko kimoja cha chumvi.

Mtu wa kawaida aliye na ugonjwa wa moyo katika utafiti huu alizidi matumizi ya kiwango hicho kwa karibu miligramu 1,000.

Utafiti ulitumia data kutoka kwa washiriki 3,170 katika utafiti wa NHANEST  wa Kituo cha Kudhibiti Magonjwa. Sampuli hizi zilijumuisha wanaume na wanawake walio na umri wa zaidi ya miaka 20 na utambuzi wa ugonjwa wa moyo na mishipa ya damu yaani cardiovascular disease diagnosis.

Kati ya kundi hili, wengi walikuwa na umri wa miaka 65 au zaidi, walikuwa wazungu, na walikuwa na kiwango cha elimu cha chini ya wahitimu wa shule ya upili. Walikuwa Wanaume, ambao walichukua zaidi ya nusu ya masomo (56.4%), walikuwa na shida ya Uzito Mkubwa(overweight) na wastani wa ulaji wa kalori 1,862 kwa siku.

Ingawa ulaji mwingi wa sodiamu mara nyingi Watu wengi huchukulia  kama matokeo ya kutokula mlo wa kutosha au Mlo kamili swala ambalo hutokea Zaidi kwa watu wenye kipato cha Chini, utafiti huu hubadilisha nadharia hiyo,

Kundi lililokuwa na ulaji mkubwa wa sodiamu walikuwa watu wenye kipato cha Juu na wenye shahada ya chuo kikuu au zaidi.

Waandishi wa utafiti wanapendekeza kwamba watu walio na viwango vya juu vya elimu na mapato wangeweza kuwa bora katika kuripoti na kudhibiti ulaji wao wa sodiamu kila Siku kuliko wengine, ila haikuwa hivo,hii imechangia matokeo kuwa ya kushangaza Zaidi.

Nini kinatokea kwenye moyo ikiwa unatumia sodiamu nyingi?

Jina la kemikali kwenye chumvi ya mezani ni Sodium chloride(Nacl). Sodiamu ni madini ya asili, ambayo ni muhimu kwa afya ya binadamu kwa kiasi kidogo.

“Sodiamu husaidia kusawazisha maji katika mwili wako,” alielezea daktari wa magonjwa ya moyo Jayne Morgan, MD, mkurugenzi wa kimatibabu katika Shirika la Afya la Piedmont huko Atlanta, GA. “Inasaidia hata utendakazi mzuri wa misuli na mishipa.” (Dk. Morgan hakuhusika katika utafiti huo.)

“Kuna msemo Unasema, ‘Mahali sodiamu huenda, maji hufuata,'” aliiambia Medical News Today.

“Hii ndiyo sababu chumvi huongeza kiasi cha damu katika miili yenu. Madhara ya hili ni kuongezeka kwa shinikizo la damu(presha). Kuongezeka kwa shinikizo la damu basi hulazimisha moyo wako kufanya kazi kwa bidii zaidi, ambayo hatimaye inakuweka katika hatari ya kupata ugonjwa wa moyo,” Dk. Morgan alisema.

Dk. Morgan alibainisha kuwa sodiamu iliyozidi kwa muda mrefu imekuwa ikihusishwa na Tatizo la ugumu wa mishipa ya damu au kwa kitaalam atherossteosis.

SOURCES:Rejea Link;

– Taasisi ya Moyo ya nchini Marekani “The American Heart Association (AHA)”

Medical News Today Cited articles from“The American Heart Association (AHA)”

– Utafiti wa NHANEST

– Daktari wa magonjwa ya moyo Jayne Morgan, MD, mkurugenzi wa kimatibabu katika Shirika la Afya la Piedmont huko Atlanta, GA.

– Creator,Editor,Reviewer; Dr.Ombeni Mkumbwa, @afyaclass

Watu wenye ugonjwa wa moyo wanapaswa kupunguza ulaji wa sodiamu
0 Comment

Kifo cha Dk Msabaha:Familia yaeleza alisumbuliwa na tatizo la nyonga, ugonjwa wa moyo muda mrefuAfyaclass Forum •

Kifo cha Dk Msabaha:Familia yaeleza alisumbuliwa na tatizo la nyonga, ugonjwa wa moyo muda mrefu.

Kusumbuliwa na tatizo la nyonga na ugonjwa wa moyo kwa muda mrefu ni mambo yanayotajwa kusabisha kifo cha aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Dk Ibrahim Msabaha (72).

Dk Msabaha aliyejiuzulu nafasi hiyo mwaka 2008 kutokana na sakata la Richimond, amefariki dunia jana Jumanne, Februari 13, 2024 wakati akiwa njiani kutoka nyumbani kwake, Masaki kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Jijini Dar es Salaam kupatiwa matibabu.

Akizungumza na Mwananchi Digital, msemaji wa familia hiyo, Abubakar Msabaha amesema changamoto hiyo ilikuwa ikimsumbua kwa muda mrefu na ilikuwa kawaida kupelekwa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kufanyiwa vipimo vya uangalizi mara kwa mara.

“Mzee wetu alikuwa anasumbuliwa na nyonga pamoja na ugonjwa wa moyo kwa muda mrefu sasa na daima tulikuwa tunamleta Taasisi ya Moyo kupatiwa matibabu na hadi jana alikuwa kawaida,” amesema Abubakar.

Amesema hata mwezi uliopita alilazwa katika taasisi hiyo mara mbili kwa matatizo hayo hadi hali yake ilipokuwa sawa aliruhusiwa kurudi nyumbani.

“Afya yake ilivyokuwa ikibadilika tulikuwa tunamkimbiza hospitalini hapo kupatiwa matubabu,” amesema.

Amesema mipango na ratiba za mazishi ya Dk Msabaha ambaye pia aliwahi kuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na mbunge wa Kibaha, inaendelea na Leo, Februari 14, 2024 saa tisa alasiri wanatarajia kumzika katika kijiji cha Soga kilichopo Kongwe, Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani.

Kifo cha Dk Msabaha:Familia yaeleza alisumbuliwa na tatizo la nyonga,
ugonjwa wa moyo muda mrefu
0 Comment

Wagonjwa wa moyo zaidi ya 800 wafanyiwa upasuaji mkubwaAfyaclass Forum •

WAGONJWA WA MOYO ZAIDI YA 800 WAFANYIWA UPASUAJI MKUBWA WENGINE 2,000 WAFANYIWA UPASUAJI WA TUNDU DOGO JKCI

Na, WAF – Zanzibar

Wagonjwa wa moyo zaidi ya 800 wamefanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo huku wengine zaidi ya 2,000 kufanyiwa upasuaji wa tundu dogo kwa kutumia mtambo wa ‘cathlab’ kwa kipindi cha miaka Miwili katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Hayo yamesemwa Februari 9, 2024 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango wakati akifungua mkutano wa Kimataifa wa magonjwa ya moyo mjini Zanzibar.

“Lakini pia, wagonjwa wa moyo zaidi ya laki mbili wamepatiwa matibabu katika Taasisi hiyo kwa kipindi cha miaka miwili ambapo kati yao wagonjwa 2,400 walitoka nchi za jirani za Comoro, Congo DRC, Kenya, Malawi, Mozambique, Rwanda, Uganda pamoja na Zambia.” Amesema Dkt. Mpango

Amesema, kutokana na huduma zinazotolewa na Taasisi hiyo zimeweza kuifanya JKCI kuwa Taasisi ya umma inayoongoza katika kutoa huduma za matibabu ya moyo Afrika Mashariki na kati hivyo kuwavutia wanataaluma kutoka nchi za jirani zikiwemo nchi za Malawi, Zambia na Rwanda kujenga mashirikiano.

Aidha, Mheshikiwa Makamu wa Rais Dkt. Mpango amesema kupitia Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Serikali imeweza kuokoa Tsh: Bilioni 63 fedha za Kitanzania zilizokuwa zinatumika kwa ajili ya matibabu ya moyo nje ya nchi.

“Kati ya mafanikio yaliyofanywa na Taasisi hiyo ni pamoja na uanzishwaji wa kambi maalumu ya matibabu ya moyo ijulikanayo kwa jina la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan services ambayo imekuwa ikitoa huduma ya kuwajengea uwezo wataalamu wa Afya waliopo katika hospitali za mikoa na kuwafikishia karibu huduma za matibabu ya moyo wananchi wanaohitaji matibabu hayo.” Amesema Dkt. Mpango

Pia amesema, Serikali itaendelea kuwekeza kakika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete kwa kupanua huduma za matibabu na kumtaka Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu kufuatilia gharama za ujenzi utakaofanyika JKCI Dar Group na kuziwasilisha Serikalini mapema ili serikali iweze kuwekeza katika ujenzi huo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge amesema JKCI imeanzisha mkutano huo wa kisayansi kwa wataalamu wa Afya nchini ukiwa na lengo la kuwapa ujuzi wataalamu wa afya nchini kuhusu magonjwa ya moyo.

“Mkutano wetu unahusisha huduma za awali kabisa ambazo mgonjwa wa moyo anatakiwa kupata lengo likiwa kuokoa maisha ya wagonjwa wa moyo kwani wengi wao hufika JKCI kwa kuchelewa.” Amesema Dkt. Kisenge

Wagonjwa wa moyo zaidi ya 800 wafanyiwa upasuaji mkubwa
0 Comment

Ugonjwa wa moyo husababishwa na niniAfyaclass Forum •

Ugonjwa wa moyo husababishwa na nini?

Hili ni Swali ambalo watu wengi huuliza na wengi wao wanafahamu kama ugonjwa wa moyo ni ugonjwa mmoja, Hapana fahamu hapa…!!!

Ugonjwa wa Moyo;

Ni maneno yanayoelezea magonjwa yote yanayoathiri moyo au kwa kitaalam tunaita heart diseases, hakuna Ugonjwa mmoja wa moyo, ila kuna magonjwa mbali mbali yanayoathiri moyo.

Hivo mtu akikuambia una ugonjwa wa Moyo,muulize ugonjwa upi wa moyo?.

Mfano wa magonjwa hayo yanayoathiri moyo ni pamoja na;

  • Ugonjwa unaoathiri mishipa ya damu ndani ya moyo mfano; Coronary artery diseases.
  • Tatizo la mapigo ya moyo kutokueleweka-Irregular heartbeats (arrhythmias)
  • Tatizo kwenye muundo wa moyo ambapo unazaliwa nalo (congenital heart defects)
  • Tatizo la moyo kutanuka
  • Tatizo la Moyo kujaa maji
  • Ugonjwa wa kwenye misuli ya Moyo
  • Ugonjwa wa kwenye Valve za moyo
  • Ugonjwa wa kwenye mfumo wa umeme ndani ya moyo n.k

Dalili za Ugonjwa wa Moyo

Dalili zinategemea na aina ya Ugonjwa wa moyo unaokusumbua kwa wakati huo, Kwa Mfano;

Dalili za Ugonjwa wa Moyo unaoathiri mishipa ya damu(Coronary artery disease) ni pamoja na;

  1. Kupata maumivu ya kifua,kifua kuwa kizito au kubana
  2. Kukosa pumzi au mtu kupumua kwa shida
  3. Kupata maumivu ya shingo,taya, koo,sehemu ya juu ya tumbo au mgongoni
  4. Kuhisi hali ya ganzi kwenye viungo vya mwili,
  5. Viungo kama miguu au mikono kuhisi hali ya kupoa sana(baridi), kuwa dhaifu, au kupata ganzi n.k

Dalili za Ugonjwa wa moyo kutokana na shida ya mapigo ya moyo kutokuelewe irregular heartbeats (heart arrhythmias);

  1. Kupata maumivu ya kifua
  2. Kuhisi hali ya kizunguzungu
  3. Kuzimia
  4. Kuhisi maumivu ya kichwa
  5. Kupata shida ya mapigo ya moyo kwenda mbio zaidi (tachycardia)
  6. Kupata shida ya mapigo ya moyo kwenda taratibu(bradycardia)
  7. Mtu kukosa pumzi au kupumua kwa shida n.k

Dalili za Ugonjwa wa Moyo kutokana na hitilafu uliyozaliwa nayo(congenital heart defects);

  • Ngozi ya mwili kubadilika rangi na kuwa kijivu au blue (cyanosis)
  • Kuvimba miguu,tumbo au kuzunguka macho
  • Kukosa pumzi au kupumua kwa shida n.k

Dalili za Ugonjwa wa Moyo kutokana na shida kwenye misuli ya Moyo: heart muscle (cardiomyopathy);

  1. Kupata kizunguzungu
  2. Mwili kuchoka kupita kiasi
  3. Kupumua kwa shida baada ya kufanya kazi kidogo au hata ukiwa umepumzika
  4. Mapigo ya moyo kwenda mbio sana
  5. Kuvimba miguu,mikono n.k

Ugonjwa wa moyo husababishwa na nini?

Zipo sababu mbali mbali kulingana na aina ya Ugonjwa wa moyo, na Sababu hizo ni pamoja na;

– Kuwa na makovu kwenye misuli ya Moyo(Heart muscle scarring),

Hii inatokana na Sababu mbali mbali ikiwemo: kuumia/kupata ajali na kuwa na kidonda kwenye moyo n.k

– Kuwa na mafuta yanayosababisha kuziba kwenye mishipa ya damu ndani ya moyo(Coronary artery disease)

– Matatizo ya kurithi(Genetic issues).

– Kuwa na Matatizo kwenye Utendaji kazi wa Figo

– Maambukizi ya magonjwa mbali mbali, hapa tunazungumzia mtu kushambuliwa na viini mbali mbali vya magonjwa ikiwemo;

  • Bacteria
  • Fangasi
  • Virusi n.k

– Kuwa na matatizo kwenye tezi la Thyroid(Thyroid problems).

– Kuwa na magonjwa kama vile Rheumatic disease.

– Kuumia Sehemu ya moyo

– Kuwa na Shida ya shinikizo la Juu la Damu(High blood pressure)

– Kupata Shida ya Shambulio la Moyo(Heart attacks)

– Matumizi ya baadhi ya Dawa, mfano baadhi ya dawa za chemotherapy n.k

– Kuwa na magonjwa jamii ya Autoimmune diseases. n.k.

Vitu hizi huongeza hatari ya Mtu kupata Ugonjwa wa Moyo?

  • Kuwa Mzee
  • Kuwa na kiwango cha juu cha cholestrol kwenye damu
  • Kuwa na shinikizo la juu la damu
  • Matumizi ya tumbaku au Uvutaji wa Sigara
  • Unywaji wa Pombe
  • Kuwa na Uzito mkubwa wa mwili
  • Kutokufanya Mazoezi
  • Kuwa na Ugonjwa wa Kisukari
  • Kula vyakula vya mafuta mengi,chumvi nyingi n.k

Vipimo unavyoweza kufanya ili kugundua Ugonjwa wa Moyo ni pamoja na;

– Electrocardiogram (EKG or ECG).

– Ambulatory monitors.

– Echocardiogram (Echo).

– Cardiac computerized tomography (CT).

– Heart magnetic resonance imaging (MRI).

– Vipimo vya Damu(Blood tests) n.k

Matibabu ya Ugonjwa wa Moyo

Matibabu ya Ugonjwa wa Moyo yanategemea chanzo husika pamoja na aina ya Ugonjwa wa moyo, ila kwa Ujumla kuna;

  • Dawa
  • Upasuaji
  • Pamoja na kubadilisha kabsa mtindo wa maisha

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Bonus Tips; Zingatia Mambo Haya Muhimu;

✓ Hakikisha unadhibiti Uzito wako wa mwili, na kuwa na Uzito unaotakiwa kiafya

✓ Hakikisha unakula mlo bora kiafya(Healthly diet)

✓ Jitahidi kufanya Mazoezi ya mwili angalau kwa Nusu Saa(dakika 30) kila siku

✓ Epuka Uvutaji wa Sigara au matumizi ya tumbaku au dawa zozote za kulevyia

✓ Epuka Matumizi ya Pombe n.k…!!!!

Ugonjwa wa moyo husababishwa na nini
0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Forum Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Forum ASANTE.
UNDERSTOOD