Showing posts with label Ukimwi. Show all posts
Showing posts with label Ukimwi. Show all posts

Je,Mate yanaambukiza UKIMWI? fahamu hapaAfyaclass Forum •

Je,Mate yanaambukiza UKIMWI? fahamu hapa

Hapana — mate hayaambukizi virusi vya UKIMWI (HIV).

Virusi vya HIV havipatikani kwa kiasi cha kutosha kwenye mate ili kusababisha maambukizi. Hata kama mtu ana HIV, kumeza, kubusiana, au kugusana kwa mate pekee hakuleti maambukizi.

Lakini kumbuka:

Kama mate yamechanganyika na damu, kwa mfano mtu ana vidonda wazi mdomoni, fizi zinavuja damu, au jeraha mdomoni — basi hatari inaweza kuwepo kidogo, ingawa bado ni ndogo sana.

Njia kuu za maambukizi ni:

1. Kujamiiana bila kinga (kondomu).

2. Kushiriki sindano au vifaa vya kuchoma ngozi.

3. Mama mwenye HIV kumwambukiza mtoto kupitia mimba, kujifungua, au kunyonyesha.

Kwa hiyo, mate peke yake hayaambukizi HIV.

0 Comment

Dawa za ARV,Matumizi Sahihi ya dawa za ARVAfyaclass Forum •

Dawa za ARV,Matumizi Sahihi ya dawa za ARV



Moja kati ya vitu vya msingi vya kuzingatia ukiwa muathirika wa ugonjwa wa VVU/UKIMWI ni matumizi sahihi ya dawa.Watu wengi wamepotoshwa na taarifa za uongo kuwa  dawa hizi hupunguza nguvu za kiume hivyo wagonjwa wengi wa UKIMWI hawatumii dawa  hizi na badala yake hutumia mitishamba au kutokutumia dawa kabisa.

Tafiti nyingi zimefanyika na kuonyesha kwamba dawa hizi zina uwezo mkubwa wa kuzuia magonjwa yatokanayo na UKIMWI na kuzuia vifo. Aidha dawa  hizi zimeonyosha uwezo mkubwa wa kupunguza maambukizi ya mama kwa mtoto.Matumizi ya dawa  za kufubaza makali ya virusi vya VVU/UKIMWI kwa waathirika wa ugonjwa huu yanahusishwa na  kupungua kwa hatari ya kueneza maambukizi ya virusi vya VVU/UKIMWI wakati wa kushiriki tendo la ndo  kwa sababu ya uwezo wake wa kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI.

KUKMBUKA dawa hizi sio tiba ya virusi vya VVU/UKIMWI.

Utaratibu wa Kuanza Dawa

Kulingana na miongozo ya matibabu ya VVU/UKIMWI anashauriwa kuanza dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI mara tu anapogundulika kuwa ni muathirika wa virusi vya VVU/UKIMWI na kupewa ushauri nasaha. Hii husaidia sana kupunguza makali ya virusi hivi.

Utaratibu wa kuanza dawa huambatana na kujisajili kwenye za kliniki za CTC ambazo zipo kwenye takribani vituo vyote vya afya nchini. Ukishajisajili utapewa namba pamoja na kadi ambayo itakuwa na taarifa zako zote muhimu kama muda au tarehe ya kumuona dakatri, aina na kiwango cha dawa  unachotumia , wingi wa virusi vya VVU kwenye damu (viral load) na kiwango cha CD4.

Endapo uligundulika na virusi vya VVU/UKIMWI na umeshaanza kupata magonjwa nyemelezi, basi utaanza matibabu ya magonjwa hayo na kuanzishiwa dawa za kufubaza virusi vya ukimwi ndani ya wiki mbili.

Kuna baadhi ya magonjwa ikiwemo kifua kikuu (PTB)   pamoja na ugonjwa wa kukakamaa shingo (Cryptococcoal Meningitis) huwa kuanza kutumia dawa haraka sio vizuri kwani inaongeza hatari ya kupata mchafuko wa kinga ya mwili (Immune Reconstitution Inflammatory Syndrome- IRIS) ambayo huzidisha dalili za magonjwa nyemelezi.

Hali hii hutokea kwa sababu madawa ya kufubaza virusi vya UKIMWI husaidia kuongeza kinga ya mwili na hivyo mwili huanza vita na magonjwa nyemelezi ambayo mwanzo mwili ulikuwa hauna uwezo wa kuyadhiti hii huleta mchafuko wa kinga ya mwili na kuzidisha  dalili zilizopo au kusababisha dalili mpya za magonjwa nyemelezi.

Matumizi Sahihi ya Dawa za Kufubaza Makali ya Virusi vya VVU/UKIMWI (ARV)

Matumizi sahihi ya dawa za kufubaza makali ya virusi vya VVU/UKIMWI ni muhimu sana kwani usipofanya hivyo unaweza kupata madhara makubwa zaidi ikiwemo ugonjwa wa UKIMWI kuja kwa kasi zaidi, hali hii huchangia sana mgonjwa kupoteza maisha. Hivyo hakikisha unapata maelekezo yote kuhusu utumiaji wa dawa kutoka kwa daktari wako.

Dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI zipo kwenye makundi mbalimbali. Tafiti tofauti pamoja na miongozo ya matibabu ya VVU/UKIMWI zimependekeza matumizi ya dawa zifuatazo; Tenofovir disoproxil fumarate(TDF), Lamuvidine(3TC), Dultegravir(DTG) kama dawa za kwanza dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI (first line treatment).

Yapo makundi mbalimbali ya mchanganyiko wa dawa za kufubaza makali ya virusi vya VVU/UKIMWI ambayo  yanaweza kutumika kulingana na kundi analotoka mgonjwa  mfano watoto wadogo, mama mjamzito au kulingana na jinsi ambavyo dawa hizi  hufanya kazi kwa mtu binafsi n.k

Dawa hizi za mchanganyiko hupatikana kama dawa moja  ambayo humezwa kila siku. Dawa hii ya mchanganyiko wa madawa mbalimbali ina nguvu sana hivyo unashauriwa kula lishe bora wakati wote ili kupunguza maudhi madogo madogo yanayotokana na dawa hizi.

Hata hivyo,imeripotiwa kuwa baadhi ya waathirika hupata madhara kutokana na matumizi ya dawa hizi zilizochanganywa  kwa pamoja, endapo mgonjwa atapata madhara ya dawa hizi, basi anashauriwa kumuona daktari haraka iwezekanavyo kwa ajili ya uchunguzi wa kina ili kugundua  ni aina gani  ya dawa inayomsababishia mgonjwa madhara.

Pindi unapougua epuka kununua madawa na kutumia bila kumuona daktari wako. Hii ni kwa sababu kuna baadhi ya dawa huingiliana na dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI katika utendaji kazi hivyo hupelekea kupungua kwa nguvu ya dawa au dawa kubaki mwilini kwa muda mrefu sana (toxicity). Mambo yote hayo tajwa yana madhara kwa mtumiaji.

Pia unashauriwa kupunguza na kuacha unywaji wa pombe.

Muhimu: Hakikisha unameza dawa kwa kufuata maelekezo ya daktari na epuka kuruka ruka kumeza dawa au utoro wa kuhurudhia kliniki ili kuepuka  madhara  zaidi. Credits:TanzMed.

0 Comment

UKIMWI:Mpango wa kutokomeza maambukizi ya vvu kwa watoto ifikapo 2030 wazinduliwa DRCAfyaclass Forum •

Wakati asilimia 91 ya watu wazima wa DRC wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi, (VVU) wanapokea matibabu, ni asilimia 44 tu ya watoto wanaopata huduma hiyo – pengo lisilokubalika ambalo limekuwepo kwa zaidi ya muongo mmoja, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeazimia kulitatua.



Katika hatua ya aina yake ya kuziba pengo la muda mrefu katika matibabu dhidi ya Virusi Vya UKIMWI, VVU, Rais Félix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC amezindua mpango wa kitaifa wa kutokomeza maambukizi ya UKIMWI kwa watoto nchini humo ifikapo mwaka 2030.

"Nchi yetu haiwezi tena kuvumilia watoto kuzaliwa na kukua na VVU wakati kuna zana za kuzuia, kugundua, na kutibu maambukizi haya kwa ufanisi," amesema Rais Tshisekedi wakati wa uzinduzi uliofanyika kwenye mkutano wa magavana huko Kolwezi, jimboni Lualaba.

"Kutokomeza UKIMWI kwa watoto ni wajibu wa maadili, hitaji la haki ya kijamii, na kiashiria cha heshima ya kibinadamu," ameongeza Rais Tshisekedi,  kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na UKIMWI, UNAIDS.

UNAIDS inasema mpango huu mpya, unaoitwa IPESE (Initiative Présidentielle pour l’Élimination du Sida chez l’Enfant), ni ishara ya kujitolea upya kitaifa kuwafikia watoto ambao, licha ya mafanikio makubwa katika huduma za VVU kwa watu wazima, bado wameachwa nyuma kwa kiasi kikubwa.

Nchini DRC, maelfu ya watoto bado wanaambukizwa VVU kila mwaka kutokana na ukosefu wa upimaji kwa wanawake wajawazito, fursa iliyopotea ya kuokoa maisha ya akina mama na kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Vipaumbele 4 muhimu

Mpango huu wa miaka mitano kutoka kwa Rais — ukiungwa mkono na ufadhili wa awali wa dola milioni 18 kutoka serikali ya kitaifa — unalenga kutoa mwitikio wa pamoja na wa kimkakati kupitia uongozi madhubuti wa kisiasa katika ngazi zote, ikiwemo magavana wa mikoa.

DRC imejizatiti kuharakisha maendeleo katika maeneo manne ya kipaumbele:

Kuboresha uchunguzi wa mapema na matibabu kwa watoto, vijana, na wanawake wajawazito

Kuzuia maambukizi mapya miongoni mwa watoto, vijana, na akina mama

Kuhakikisha matibabu ya haraka na ya moja kwa moja kwa wote waliogundulika kuwa na maambukizi

Kuondoa vikwazo vya kimfumo vinavyowazuia vijana kupata huduma za afya, kupitia njia zenye heshima, ushirikishwaji, na urafiki kwa vijana

Watoto wanaachwa nyuma

Wakati asilimia 91 ya watu wazima wanaoishi na VVU nchini DRC sasa wanapata matibabu ya kupunguza makali ya virusi (ARV), ni asilimia 44 tu ya watoto wanaoishi na VVU wanaopata huduma hizo — pengo ambalo limekuwepo kwa zaidi ya muongo mmoja.

Shukrani kwa ushirikiano kati ya serikali, jamii za kiraia, jumuiya za wenyeji, na washirika wa kimataifa kama PEPFAR, Mfuko wa Dunia, (Global Fund), UNAIDS, na Taasisi ya Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation, ufanisi wa matibabu kwa watu wazima umeongezeka kwa kasi. Lakini kwa watoto, mfumo bado unasuasua.

Kila mwaka, maelfu ya watoto wa DRC wanaambukizwa VVU, mara nyingi kwa sababu wanawake wajawazito hawachunguzwi — fursa iliyopotea ya kuokoa maisha ya mama na kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Hali hii inaonesha matatizo ya kimfumo: upatikanaji duni wa huduma bora za afya ya uzazi na jinsia kwa wanawake, ukosefu wa ujumuishaji mzuri wa huduma za VVU katika huduma ya afya ya mama na mtoto, minyororo dhaifu ya usambazaji wa dawa, na uratibu hafifu kati ya huduma za umma na jamii.

Huko Kolwezi, jimboni Lualaba nchini DRC, Rais Tshisekedi amesema kwamba DRC haitavumilia tena "watoto kuzaliwa na kukua wakiwa na VVU, ilhali kuna vifaa vya kuzuia, kugundua na kutibu maambukizi haya kwa ufanisi."

Tumaini jipya

UNAIDS imekaribisha mpango huu kama hatua muhimu inayohitajika sana wakati huu ambapo rasilimali za maendeleo ziko kwenye shinikizo kubwa.

"Katika kipindi ambapo ufadhili wa maendeleo unakabiliwa na changamoto na mifumo ya kusaidia walio hatarini zaidi imebanwa, uongozi wa Rais Félix Tshisekedi ni taa ya matumaini," amesema Dkt. Susan Kasedde, Mkurugenzi wa UNAIDS nchini DRC. “UNAIDS inaunga mkono kikamilifu mpango huu jasiri na wa kuhamasisha.”

Kupitia mpango huu, DRC inalenga kubadili mwelekeo wa kizazi kizima cha watoto ambao kwa muda mrefu wameachwa nyuma katika mapambano dhidi ya VVU.

"Tunatangaza ahadi ya kitaifa kuhakikisha kila mtoto wa Kongo ana haki ya kuzaliwa na kukua bila mzigo wa VVU," amesema Rais Tshisekedi. “Tuna njia za kufanikisha hili — na juu ya yote, tuna wajibu.”

TAGS: Afya/Afrika/DRC/VVU/PEPFAR/UNAIDS

0 Comment

Virusi vya UKIMWI huishi kwa Muda gani Nje ya Mwili?Afyaclass Forum •

Virusi vya UKIMWI huishi kwa Muda gani Nje ya Mwili?



Hakuna jibu moja la muda gani Virusi vya Ukimwi(VVU) vinaweza kuishi nje ya mwili, kama vile kwenye damu kavu au shahawa zikiwa nje ya mwili n.k, kwani inategemea mambo kadhaa.  Hata hivyo, Virusi vya Ukimwi(VVU) haviishi kwa muda mrefu nje ya mwili, na haviwezi kuongezeka yaani replication bila kuwa ndani ya binadamu(human host).

Kama nilivyosema muda wa Virusi vya Ukimwi kuishi nje ya mwili hutegemea mambo kadhaa,hivo utakutana na majibu tofauti kulingana na hali husika;

Mfano; Utakuta baadhi ya Tafiti zinasema,ndani ya muda mfupi sana, zingine ndani ya masaa kadhaa,ndani ya Siku kadhaa n.k.

Kwa mujibu wa Vituo vya kudhibiti na kuzuia Magonjwa yaani "The Centers for Disease Control and Prevention (CDC)";

Wakati hali ya joto na hali zingine zinapokuwa sawa, VVU vinaweza kuishi kwa muda wa siku 42 kwenye bomba la sindano, lakini hii kwa kawaida inahusisha uwekaji kwenye friji.

Licha ya kuishi kwa muda mrefu huu kwenye Syringe ikiwa joto lipo sawa(room temperature),Virusi hivi vya Ukimwi vinaweza kukaa kwa muda wa Siku 7 tu ndani ya Syringe endapo joto litakuwa kubwa Zaidi.



MAMBO HAYA HUATHIRI MUDA WA KUISHI KWA VIRUSI VYA UKIMWI(VVU) NJE YA MWILI;

1. Joto(Temperature): Virusi vya Ukimwi(VVU) hubaki hai na kufanya kazi wakati vikiwa kwenye baridi au joto la kawaida lakini huuawa na joto kali.

2 Mwanga wa Jua(Sunlight): Miale ya Mwangaza wa jua huweza kuharibu virusi, kwa hivyo haviwezi tena kuzaliana vikichomwa na miale hii mikali.

3. Kiwango cha Virusi kwenye fluid husika: Kwa ujumla, kadri kiwango cha virusi vya UKIMWI kilivyo juu katika fluid husika, ndivyo itakavyochukua muda mrefu kwa vyote kutofanya kazi au kuwa inactive.

4. Kiwango cha PH au Level of acidity. VVU huishi vyema zaidi kwa pH ikiwa karibu kwenye 7 na huacha kufanya kazi wakati mazingira yana asidi kubwa zaidi au kidogo.

Fahamu kwamba Virusi vya Ukimwi hupendelea mazingira ya PH ikiwa katikati ya 6.0 na 6.9. Na ndyo maana mazingira ya fluids mbali mbali za mwili kama vile Damu,Shahawa,Maziwa,au vaginal secretions, kwao ni rafiki sana.

Mazingira yakiwa yana Acid kubwa sana mfano (pH chini ya 4.0) au yana Base kubwa sana mfano (pH juu ya 9.0),Mazingira haya huwafanya Virusi kuwa inactive.

5. Unyevu unyevu kwenye Mazingira husika(Environmental humidity): Mazingira yakiwa makavu zaidi ndivo ambavyo hupunguza uwezo wa Virus kuwa active zaidi.

0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD