Showing posts with label afya ya Figo. Show all posts
Showing posts with label afya ya Figo. Show all posts

Fahamu Vitu ambavyo Vinaharibu FIGO zako polepole bila kujuaAfyaclass Forum •

Fahamu Vitu ambavyo Vinaharibu FIGO zako polepole bila kujua

“Je, unajua kuna kitu unatumia kila siku ambacho kinaweza kuharibu figo zako polepole bila wewe kujua? Leo nakwambia ukweli ambao watu wengi hawajui!”

Baadhi ya Vitu ambavyo usipotumia kwa uangalifu huharibu kabsa Figo zako;

1.Kula chumvi nyingi kupita kiasi

Matumizi ya chumvi nyingi ni hatari kwa afya ya Figo kwani huweza kuongeza presha ya damu(Shinikizo la Damu)

Presha ya juu huharibu figo taratibu

2.Vinywaji vyenye sukari nyingi

Vinywaji kama Soda na juice za viwandani usipotumia kwa kiasi huweza kuleta madhara makubwa kwa figo zako, kwani vina kiwango kikubwa cha Sukari

3.Dawa za kienyeji zisizo na kipimo

Baadhi zina kemikali nzito (toxins),ambapo huumiza figo moja kwa moja

4.Matumizi mabaya ya dawa za maumivu

Fahamu kwamba Dawa zikitumika mara kwa mara bila ushauri wa daktari ikiwemo dawa za maumivu,pia huweza kusababisha matatizo ya Figo.

Huathiri mtiririko wa damu kwenye figo n.k.

5.Kunywa maji kidogo

Figo zinahitaji maji kusafisha sumu mwilini,

Upungufu wa maji huongeza hatari ya mawe kwenye figo na kupata matatizo mengine ya Figo.

6. Kula Vitu vyenye protein nyingi kupita kiasi

(hasa nyama nyekundu nyingi sana kila siku),Huongeza mzigo kwa figo kufanya kazi kupita kiasi.

 7. Kuvuta sigara

Hupunguza mtiririko wa damu kwenye figo,huongeza hatari ya magonjwa ya figo n.k

8. Pombe kupita kiasi

Huathiri uwezo wa figo kusafisha damu,Pia huongeza presha ya damu, vyote hivi huweza kuleta shida kwa Figo

Bonus Point;

 9. Maambukizi yasiyotibiwa mapema

Kama UTI (maambukizi ya njia ya mkojo),Yanaweza kuenea hadi figo na kuharibu figo zako

10. Magonjwa sugu kama kisukari na Shinikizo la Damu

Haya ndiyo visababishi vikubwa vya uharibifu wa figo duniani

Dalili za tahadhari (usizipuuze)

  • Miguu na uso kuvimba
  • Mkojo kuwa na povu au kubadilika rangi
  • Uchovu wa kupita kiasi
  • Maumivu ya chini ya mgongo n.k.

JE, UNA TATIZO HILI NA HUJAPATA TIBA BADO? Tuwasiliane kwa namba hizi: Call,Sms,Whatsapp +255758286584.

0 Comment

Je,Unatakiwa kunywa maji kiasi gani kwa Usalama wa Figo Zako?Afyaclass Forum •

Fahamu Figo ni moja ya viungo muhimu vya mwili wa mwanadamu, ambavyo vina majukumu mengi ya kuweka mwili katika afya njema.

Madaktari mara nyingi wanashauri kwamba ili kuweka figo kuwa na afya njema, kula kiasi cha chumvi, kuepuka sukari ya ziada na kutotumia dawa za maumivu bila ushauri wa daktari.

Hatua nyingine nyingi pia zinapendekezwa ili kuepuka shinikizo nyingi kwenye figo.

Kwa hivyo ni muhimu kunywa kiasi fulani cha maji ili kuweka figo kuwa na afya? Katika ripoti hii, tutajaribu kupata majibu kwa maswali haya.

Figo hufanya kazi ili kudumisha usawa wa electrolyte katika mwili wetu. Inadhibiti kiasi cha vipengele kama sodiamu na potasiamu.

Dkt. Vivekanand Jha, rais wa zamani wa Jumuiya ya Kimataifa ya Nephrology na mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya George ya Afya ya duniani, ni mtaalamu wa magonjwa ya figo.

Anasema, "Figo huondoa vitu visivyo vya lazima kutoka kwa mwili, ambavyo tunavipata kupitia chakula au kwa njia zingine. Na pia vitu ambavyo hutengenezwa mwilini kimetaboliki."

Dkt. Vivekanand Jha anasema, "Figo pia huzalisha aina nyingi za homoni mwilini, ambazo ni pamoja na kutengeneza damu, homoni zinazodhibiti shinikizo la damu na homoni za kudumisha usawa wa elektroliti."

Mtu wa kawaida anahitaji lita tatu hadi tatu na nusu za maji kila siku. Si lazima kwamba kiasi hiki kinatimizwa tu na maji ya kawaida. Inaweza kutimizwa na aina yoyote ya kioevu. Ikiwa tunadumisha usawa wa maji katika mwili, basi uwezekano wa maambukizi ya mkojo pia hupungua."

"Kwa watu wanaougua ugonjwa wa moyo au figo, kiasi cha maji kinachotumiwa huzuiwa kidogo ili kisiwe na shinikizo kubwa kwa viungo hivyo."

0 Comment

Fahamu kuhusu Dalili kuu za Ugonjwa wa FigoAfyaclass Forum •

Fahamu kuhusu Dalili kuu za Ugonjwa wa Figo.



Dalili za ugonjwa wa Figo,Madhara na jinsi ya kudhibiti Ugonjwa wa Figo

Moja ya viungo muhimu sana katika mwili wa binadamu ni pamoja na Figo, Figo ndyo huhakikisha sumu zote zinaweza kutolea nje ya mwili kwa njia ya Mkojo.

Kwa kawaida binadamu ana Figo mbili upande wa kushoto na kulia, japo kuna watu wachache huzaliwa na Figo moja,

Katika Makala hii tutajadili zaidi kuhusu Dalili za ugonjwa wa Figo,Madhara na jinsi ya kudhibiti Ugonjwa wa Figo.

Zifahamu dalili za ugonjwa wa Figo

  • Kuvimba uso na macho
  • Kuvimba miguu
  • Kukojoa sana hasa wakati wa usiku
  • Uchovu wa mwili
  •  Maumivu ya kifua na kupumua kwa shida
  • Kuwashwa kwa mwili
  • Mwili kupata michubuko kwa urahisi

Ukiona mojawapo ya dalili hizi, wahi kituo cha huduma za afya kwa ajili ya MSAADA ZAIDI(elimu ya afya,WizaraafyaTz)

DALILI ZA UGONJWA WA FIGO

Zipo Dalili za ugonjwa wa Figo,na dalili hizo za ugonjwa wa Figo ni kama vile;

– Kuvimba mwili mzima kuanzia uso, tumbo na miguu

– Kukosa au kupungua kiasi cha mkojo kwa siku

– Uchovu wa mwili

– Maumivu ya kifua na kupumua kwa shida

– Kuwashwa kwa mwili

– Mwili kupata michubuko kwa urahisi n.k

“Ukiona dalili hizi wahi kituo cha huduma za afya” endelea Zaidi kusoma hapa kuhusu dalili za ugonjwa wa Figo.

DALILI ZA UGONJWA WA FIGO

je wajua kudhibiti Presha yako husaidia pia kuboresha afya ya Figo?

Ukidhibiti Presha yako inasaidia pia kuleta afya ya Figo, Na Je wajua dalili za Ugonjwa wa Figo?

Hizi hapa ni baadhi ya dalili ambazo huweza kuashiria kwamba Figo ina Tatizo;

1. Mgonjwa wa Figo huvimba maeneo mbali mbali ya mwili kama vile; Kuvimba miguu,mikono,uso au macho.

2. Mgonjwa kuhisi kizunguzungu na hali ya kutapika kila mara

3. Mgonjwa kukosa usingizi pamoja na mwili kuchoka kupita kawaida

4. Mgonjwa kukamaa misuli ya mwili ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Muscle cramps

5. Mgonjwa kupoteza kabsa hamu ya kula na kuskia kichefuchefu pamoja na kutapika pia

6. Mgonjwa kuhisi Mkojo kila mara hasa nyakati za Usku

7. Mgonjwa kukojoa mkojo ambao umechanganyika na Damu,hii huweza kuwa ishara pia kwamba kwenye figo kuna shida

8. Mgonjwa kupata maumivu kwenye viungo vya mwili,misuli pamoja na joint

9. Tafiti zinaonyesha pia mgonjwa wa figo huweza kupata shida ya kukosa hedhi kama ni mwanamke

10. Ugonjwa wa figo hupoteza hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa mwanaume

11. Ugonjwa wa Figo huweza kusababisha mtu kuwa na matatizo ya presha pia, hasa presha ya kupanda

12. Ugonjwa wa figo huweza kusababisha uwepo wa kiwango kikubwa sana cha Potassium kwenye damu, na pia huweza kusababisha matatizo ya moyo kama vile; Moyo kuvimba N.K

MADHARA YA UGONJWA WA FIGO NI PAMOJA NA;

Haya hapa ni baadhi ya madhara ya ugonjwa wa Figo;

– Kusababisha Kifo

– Kukosa hamu ya tendo la ndoa kwa mwanaume

– Kupatwa na magonjwa ya moyo

– Kupatwa na matatizo ya shinikizo la Damu au Presha

– Mwili kuvimba ikiwemo uso,macho,mikono na miguu pia n.k

Njia za kudhibiti na kutibu ugonjwa wa Figo

Zingatia mambo haya ili Kujikinga na ugonjwa wa Figo;

  1. Hakikisha unafanya Mazoezi,fanya mazoezi angalau kwa muda wa Nusu Saa kila Siku
  2. Epuka matumizi ya Pombe Kupit kiasi
  3. Epuka uvutaji wa Sigara au tumbaku
  4. Dhibiti Uzito wako wa Mwili na epuka Uzito mkubwa
  5. Epuka ulaji wa vyakula vya mafuta mengi,Sukari nyingi au chumvi nyingi
  6. epuka vinjwaji vyenye kiwango kikubwa cha Caffeine kama kahawa n.k
  7. Dhibiti Presha yako ya damu
  8. Dhibiti Sukari yako
  9. Omba Msaada kutoka kwa wataalam wa afya,Ukiona dalili zozote za ugonjwa wa Figo

FAQs:Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Je, ugonjwa wa Figo una Dalili Zipi?

Dalili za Ugonjwa wa Figo ni pamoja na;Kuvimba mwili mzima kuanzia uso,tumbo na miguu,Kukosa au kupungua kiasi cha mkojo kwa siku,Uchovu wa mwili, Maumivu ya kifua na kupumua kwa shida,Kuwashwa kwa mwili,Mwili kupata michubuko kwa urahisi n.k

Hitimisho

Ugonjwa wa Figo ni miongoni mwa magonjwa ambayo huwapata watu wengi na Kusababisha Vifo Duniani kote,

Ni muhimu sana kufahamu dalili za Ugonjwa wa Figo,Ili kupata Msaada mapema pale unapohisi haupo Sawa,

Zipo Dalili za ugonjwa wa Figo,na dalili hizo za ugonjwa wa Figo ni kama vile;

– Kuvimba mwili mzima kuanzia uso, tumbo na miguu

– Kukosa au kupungua kiasi cha mkojo kwa siku

– Uchovu wa mwili

– Maumivu ya kifua na kupumua kwa shida

– Kuwashwa kwa mwili

– Mwili kupata michubuko kwa urahisi n.k

“Ukiona dalili hizi wahi kituo cha huduma za afya” endelea Zaidi kusoma hapa kuhusu dalili za ugonjwa wa Figo.

KUMBUKA:Zingatia mambo haya ili Kujikinga na ugonjwa wa Figo;

  1. Hakikisha unafanya Mazoezi,fanya mazoezi angalau kwa muda wa Nusu Saa kila Siku
  2. Epuka matumizi ya Pombe Kupit kiasi
  3. Epuka uvutaji wa Sigara au tumbaku
  4. Dhibiti Uzito wako wa Mwili na epuka Uzito mkubwa
  5. Epuka ulaji wa vyakula vya mafuta mengi,Sukari nyingi au chumvi nyingi
  6. epuka vinjwaji vyenye kiwango kikubwa cha Caffeine kama kahawa n.k
  7. Dhibiti Presha yako ya damu
  8. Dhibiti Sukari yako
  9. Omba Msaada kutoka kwa wataalam wa afya,Ukiona dalili zozote za ugonjwa wa Figo

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Ugonjwa wa Kuharibika kwa chujio za Figo ama GlomerulonephritisAfyaclass Forum •

Ugonjwa wa Kuharibika kwa chujio za Figo ama Glomerulonephritis

Kuharibika kwa chujio za Figo ama Glomerulonephritis ni aina ya ugonjwa wa figo unaoathiri sehemu maalum ya figo (chujio) inayohusika na uchujaji wa maji pamoja na uchafu kutoka katika damu. Sehemu hii huitwa glomelurus au chujio kama tutakavyokuwa tukitumia katika mada hii.

Visababishi

Mara nyingi chanzo halisi cha kuharibika kwa chujio za figo (glomerulonephritis) huwa hakijulikani. Hata hivyo wakati mwingine uharibifu huu unaweza kusababishwa na kushambuliwa na mfumo wa kinga ya mwili. Uharibifu katika chujio husababisha damu pamoja na protini kuingia katika mkojo.

Tatizo hili hukua kwa haraka na figo linaweza kupoteza uwezo wake wa kuchuja maji na uchafu kwa kasi ndani ya muda mfupi wa kati wiki chache mpaka miezi kadhaa. Aina hii ya kuharibika kwa chujio za figo kwa haraka hujulikana kitalaamu kama rapidly progressive glomerulonephritis.

Ukubwa wa tatizo na vihatarishi vyake

Takribani robo ya watu wanaopatwa na tatizo sugu la glomerulonephritis huwa hawana historia ya kuwa na ugonjwa wowote wa  figo hapo kabla.

Kuna mambo kadhaa yanayoweza kumfanya mtu awe katika hatari ya kupata glomerulonephritis. Mambo hayo ni pamoja na:

Matatizo katika mfumo wake wa damu au lymph

Kuwahi kutumia vimiminika vilivyotengenezwa kwa kemikali za hydrocarbon

Wenye historia ya saratani

Maambukizi ya bakteria aina ya streptococcus, virusi, majipu au maambukizi katika moyo

Mambo mengine yanayoweza kuongeza hatari ya kupatwa na glomerulonephritis ni pamoja na:

Magonjwa ya mishipa ya damu kama vile vasculitis au polyarteritis

Matumizi yaliyopitiliza ya dawa za kutuliza maumivu za jamii ya Non steroidal anti-inflammatory drugs kama vile aspirin na diclofenac

Magonjwa ya mfumo wa kinga ya mwili kama vile Anti-glomerular basement membrane antibody disease na IgA nephropathy

Makovu katika chujio (Focal segmental glomerulosclerosis) au hali ya chujio kuwa na kuta nene kuliko kawaida (Membranoproliferative GN)

Magonjwa yanayoathiri viungo mbalimbali vya mwili kama vile Henoch-Schonlein purpura, IgA nephropathy, Goodpasture’s syndrome au Lupus nephritis

Ugonjwa wa kimetaboliki wa Amyloidosis

Dalili

Dalili kuu za glomerulonephritis ni kuwa na damu katika mkojo (hali inayoufanya mkojo kuwa na rangi kama nyeusi, kutu au samawati; mkojo kuwa kama wenye povu jingi (kwa sababu ya kuwa na protini nyingi kuliko kawaida) na kuvimba uso, macho, miguu au tumbo (hali inayojulikana kama edema)

Dalili nyingine ni pamoja na

Maumivu ya tumbo

Kutapika damu

Kuharisha au kupata choo kikubwa chenye kuchanganyika na damu

Kukohoa pamoja na kupumua kwa shida

Kukojoa kupita kiasi

Homa

Maumivu ya misuli na viungo, uchovu, maumivu ya mwili mzima pamoja na kukosa hamu ya kula

Kutokwa na damu puani

Baada ya muda, figo hushindwa kufanya kazi na mgonjwa huanza kuwa na dalili za mtu mwenye ugonjwa sugu wa figo.

 Uchunguzi na vipimo

Kwa kawaida tatizo la uharibifu wa chujio za figo hutokea tatratibu sana hali inayoweza kufanya ugunduzi wake kuchelewa pia. Wengi wa wagonjwa wenye tatizo hili hugunduliwa pale wanapokwenda hospitali kwa ajili ya uchunguzi wa matatizo mengine. Mara nyingi hali hii hujidhihirisha kwa kuwepo na hitilafu katika kipimo cha urinalysis.

Mambo makuu matatu yanaweza kuonesha kuwepo kwa uharibifu katika chujio za figo. Mambo hayo ni upungufu wa damu (anemia), shinikizo la damu kuwa juu na ishara za kupungua kwa utendaji kazi wa figo.

Vipimo vinavyoweza kufanywa hujumuisha vipimo vya mkojo, damu pamoja na picha kama vile Ultrasound, CT au SPECT/CT.

Vipimo vya mkojo kama vile urinalysis husaidia kuonesha:

Utendaji kazi wa figo yaani Creatinine clearance pamoja na Urine creatinine

Uchunguzi wa mkojo kwa kutumia hadubini

Kiasi cha protini katika mkojo

Kiasi cha tindikali ya urea katika mkojo

Chembe nyekundu za damu (RBC) katika mkojo

Specific gravity ya mkojo na kiasi cha chumvi kwenye mkojo (yaani urine osmolality)

Vipimo vingine ni pamoja na CT scan, ultrasound ya figo, X-ray ya kifua au Intravenous pyelogram (IVP)

Vipimo vya damu husaidia kuonesha:

Kiasi cha protini ya albumin katika damu

Utendaji kazi figo kuchunguza kiasi cha BUN na creatinine katika damu

Viasili vinavyohusika katika mfumo wa kinga ya mwili kama vile Anti-glomerular basement membrane antibody, Anti-neutrophil cytoplasmic antibodies (ANCAs), Anti-nuclear antibodies au Complement levels.

Ili kuthibitisha uwepo wa tatizo hili na aina yake, kipimo cha biopsy (renal biopsy) hutumika.

Matibabu

Matibabu ya glomerulonephritis hutegemea sana na kisababishi cha tatizo hili, aina yake pamoja na ukubwa wa tatizo lenyewe yaani wingi wa dalili pamoja na uzito wake. Dalili ya muhimu sana kuithibiti ni ongezeko la shinikizo la damu ingawa kwa kawaida huwa ni ngumu sana kuthibiti shinikizo la damu kuwa katika kiwango cha kawaida.

Mgonjwa anashauriwa pia kupunguza kiasi cha chumvi katika chakula chake na pia kiasi cha protini na maji anayokunywa ili kusaidia utendaji kazi wa figo.

Dawa zinazoweza kutumika kwa mgonjwa mwenye tatizo hili ni pamoja na:

Zile za kushusha na kuthibiti shinikizo la damu hususani za jamii ya Angiotensin-converting enzyme (ACE) inhibitors kama vile captopril, Lisinopril au Enalapril; na zile za jamii ya Angiotensin receptor blockers kama vile losartan, Valsartan na Irbesartan.

Zile za jamii ya Corticosteroids kwa ajili ya kupunguza na kuondoa mcharuko mwili

Zile za kupunguza nguvu ya mfumo wa kinga ya mwili

Iwapo dawa za kupunguza nguvu ya kinga ya mwili zimeshindwa kufanya kazi na kuna uthibitisho kuwa glomerulonephritis imesababishwa na mashambulizi ya seli za kinga ya mwili katika figo, mgonjwa anaweza kufanyiwa tiba inayoitwa plasmapheresis. Katika tiba hii, sehemu ya damu yenye seli za kinga ya mwili zijulikanazo kama antibodies huondolewa kwa kubadilishwa na maji maji (plasma) yasiyo na antibodies zozote zile. Kuondoa antibodies husaidia kupunguza mcharuko mwili na uharibifu zaidi katika chujio za figo.

Iwapo figo zitashindwa kufanya kazi kabisa, mgonjwa anaweza kuhitaji kufanyiwa dialysis au kupandikizwa figo mpya.

Matarajio

Kuharibika kwa chujio za figo kunaweza kuwa ni tatizo la muda na lenye kurekebishika au linaweza kudorora na kuwa la kudumu. Kudorora kwa chujio za figo kunaweza kusababisha kupungua kwa utendaji kazi wa figo au ugonjwa sugu wa figo kushindwa kufanya kazi (chronic renal failure), au kufa kabisa kwa figo zote (end-stage renal disease).

Madhara

Pamoja na kusababisha shinikizo la damu kuwa juu, uharibifu katika chujio za figo unaweza pia kusababisha mlinganyo usio sawa wa madini katika damu (electrolytes imbalance) kama vile ongezeko la madini ya potassium (hyperkalemia); maambukizi yanayojirudia katika njia ya mkojo, uwezekano wa kupata maambukizi ya mwili, mrundikano wa maji mwilini hali inayoweza kusababisha moyo kushindwa kufanya kazi (congestive heart failure) au maji kujaa katika mapafu (pulmonary edema); au ugonjwa wa figo ujulikanao kama Nephrotic syndrome (utaelezwa katika makala zijazo).

Kinga

Inawezekana kuzuia uharibifu wa chujio za figo kwa baadhi ya watu ingawa, kwa ujumla ni ngumu kufanya hivyo. Baadhi ya mambo ya kufanya ili kuepuka kupatwa na tatizo hili ni pamoja na kuepuka matumizi ya vimiminika vyenye kemikali za hydrocarbons, matumizi ya madini ya zebaki pamoja na matumizi ya muda mrefu ya dawa za jamii ya nonsteroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDs) kama vile Aspirin.

0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD