Showing posts with label afyaclass. Show all posts
Showing posts with label afyaclass. Show all posts

TATIZO LA NGOZI YA KWAPA NA SHINGONI KUWA NYEUSI ZAIDI (Acanthosis nigricans)Afyaclass Forum •

 NGOZI

• • • • •

TATIZO LA NGOZI YA KWAPA NA SHINGONI KUWA NYEUSI ZAIDI  (Acanthosis nigricans)


Tatizo la ngozi ya baadhi ya sehemu za mwili kuwa nyeusi zaidi ni tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama "Acanthosis nigricans" na tatizo hili hutokea sana kwenye maeneo ya SHINGONI,KWENYE KWAPA,NA SEHEMU ZA SIRI.


Mabadiliko haya ya rangi ya ngozi kwa asilimia kubwa huwapata watu wanene,wenye tatizo la kisukari, watoto wadogo ambao wapo kwenye hatari ya kuwa na kisukari yaani type 2 diabetes, na mara chache sana huweza kuwa kama dalili ya saratani au kansa ya viungo mbali mbali vya ndani ya mwili kama vile ini,tumbo n.k


CHANZO CHA TATIZO HILI NI NINI?


- Tatizo la acanthosis nigricans huweza kutokea baada ya Hormone au kichocheo cha INSULIN kushindwa kufanya kazi hali ambayo hupelekea pia kutokea tatizo la kisukari yaani type 2 diabetes.


- Matatizo kwenye vichocheo vya mwili(Hormone disorders) kama vile kichocheo kinachoipa ngozi rangi yake ya asili kuzidi sana yaani Melanini hyperpigmentation kwenye sehemu zilizoathirika na pia kwa watu wenye matatizo kama vile; tatizo la ovarian cysts, matatizo kwenye tezi la thyroid kama vile underactive thyroids au matatizo ya tezi la Adrenaline(adrenal glands).


- Matumizi ya baadhi ya dawa pamoja na virutubisho mfano; Mtu kutumia dose kubwa ya niacin, vidonge vya majira yaani birth control pills, dawa za prednisone pamoja na dawa zingine kama vile dawa jamii ya corticosteroids huweza kusababisha tatizo hili la acanthosis nigricans.


- Na pia kama nilovyosema hapo awali,mara chache sana tatizo hili huweza kuhusishwa na saratani au kansa ya viungo mbali mbali vya mwili kama vile Ini, Tumbo,utumbo n.k


KUMBUKA; Tatizo hili huwapata sana watu ambao;


• Ni wanene au wenye tatizo la uzito uliopita kiasi


• Wenye magonjwa kama kisukari


• Na wale ambao wapo kwenye familia ambazo kuna watu wenye tatizo hili


MATIBABU YA TATIZO HILI LA ACANTHOSIS NIGRICANS


Tatizo hili huhisisha tiba za aina mbali mbali kulingana na chanzo chake,japo kwa ujumla kuna tiba kama vile;


✓ Kupunguza uzito wa mwili kama tatizo hili limetokana na mtu kuwa mnene au na uzito mkubwa


✓ Kuacha matumizi ya dawa ambazo huweza kusababisha tatizo hili


✓ Wengine hufanyiwa mpaka upasuaji ili kuondoa vivimbe au tumors kisha kusaidia ngozi ya mwili irudi kwenye rangi yake ya asili


✓ Lakini pia mtu huweza kutumia dawa mbali mbali kama vile;


   • Cream za kupaka kwenye ngozi


   • Baadhi ya sabuni za kuogea ambazo ni Antibacterial soaps


    • Dawa za kunywa yaani Oral acne medications N.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comment

KANSA YA KWENYE UUME,CHANZO,DALILI NA TIBA YAKEAfyaclass Forum •

UUME
• • • • •
KANSA YA KWENYE UUME,CHANZO,DALILI NA TIBA YAKE

Kansa ya Uume, ni ukuaji wa seli usio wa kawaida na usiodhibitika ndani ya uume ambapo kwa asilimia kubwa huanza kwenye seli za ngozi ya uume kisha kuingia ndani,
 Bila shaka aina hii ya kansa ya Uume itakuwa haitajwi sana kama aina zingine za kansa kwa wanaume kama vile kansa ya Tezi dume n.k, lakini kansa hii ipo na inapata baadhi ya Wanaume pia.


CHANZO CHA KANSA YA UUME

- Mpaka sasa hakuna sababu ya moja kwa moja ya kutokea kwa aina hii ya Kansa,japo kutokana na tafiti mbali mbali imeonekana Kansa ya Uume hupata sana makundi haya yafuatayo;


1. Wanaume wenye kirusi cha HUMAN PAPILLOMA VIRUS(HPV)


2. Wanaume wenye umri wa zaidi ya miaka 60


3. Wanaume wanaovuta sana Sigara


4. Wanaume wenye kinga ndogo ya mwili kutokana na sababu mbali mbali kama vile maambukizi ya UKIMWI au matumizi ya baadhi ya dawa n.k


5. Wanaume ambao hawajatahiriwa,ambapo maji maji pamoja na uchafu unaojulikana kama "smegma" hujikusanya chini ya ngozi ya uume na kukuweka katika hatari zaidi


6. Mwanaume kuwa na tatizo la phimosis ambapo ngozi ya uume hushikamana zaidi na kukakamaa hali ambayo hupelekea kuwa vigumu kusafishwa vizuri


7. Mwanaume kuwa kwenye matibabu ya psoriasis pamoja na matumizi ya dawa za psoralen au huduma ya mionzi(ultraviolet (UV) light



DALILI ZA KANSA YA KWENYE UUME NI PAMOJA NA;


• Ngozi ya kwenye uume kuanza kubadilika rangi hasa ngozi ya mbele kwa wale ambao hawajatahiriwa

• Ngozi ya uume kuwa laini zaidi kuliko kawaida

• Ngozi ya uume kuanza kuwa na vipele pele au rashes, makovu au vidonda kwenye uume n.k

• Kuwa na uvimbe ambao unakuwa au kuongezeka ambao una rangi ya blue kwenda brown

• Ngozi ya uume kuanza kutoa harufu mbaya

• Kuwa na vidonda kwenye uume ambavyo wakati mwingine huvuja damu

• Uume kuvimba kwa mbele au kuwa na uvimbe chini ya ngozi ya uume


KUMBUKA; Uwepo wa dalili hizi haimaanishi moja kwa moja una kansa ya Uume,inawezekana pia ukawa na magojwa mengine kama magonjwa ya zinaa,maambukizi mbali mbali au tatizo la Allergy,hivo ukiona dalili kama hizi ongea na wataalam wa afya kwanza kwa ajili ya vipimo zaidi.


MATIBABU YA KANSA KWENYE UUME

Kama ilivyo aina zingine za kansa, Mgonjwa ambaye kagundulika mapema kuwa na tatizo hilo la kansa ya uume hupata tiba na kupona kwa haraka zaidi kuliko ukichelewa kugundulika na kuanza tiba mapema, matibabu huhusisha njia mbali mbali kama vile;

- Matumizi ya baadhi ya dawa mbali mbali ikiwemo cream za kupaka pamoja na vidonge vya kunywa

- Mwanaume kutahiriwa kwanza kama hakutahiriwa

- Huduma ya Cryotherapy n.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.


0 Comment

Sababu za Mimba Kutunga Nje ya Kizazi pamoja na Dalili zake(Ectopic pregnancy)Afyaclass Forum •

   AFYA YA UZAZI

• • • •

Sababu za Mimba Kutunga Nje ya Kizazi pamoja na Dalili zake(Ectopic pregnancy)


 Kwa asilimia kubwa Mimba kutunga Nje ya kizazi yaani kwa kitaalam Ectopic pregnancy hutokea wakati yai lililorutubishwa kukwama ndani ya mirija ya uzazi(fallopian tubes) au kuelekea kwenye  njia ya uzazi, japo mimba kutunga sehemu nyingine yoyote mbali na sehemu yake ya kawaida ndani ya kizazi bado ni Ectopic pregnancy,


CHANZO CHA TATIZO HILI LA MIMBA KUTUNGA NJE YA KIZAZI


- mara nyingi mimba hutunga nje ya kizazi kwa sababu mirija ya uzazi yaani fallopian tubes imeharibiwa, kuziba au kufungwa vibaya. 


- Tatizo la mvurugiko wa vichocheo mwilini(hormone imbalance) au ukuaji usiokuwa wa kawaida wa yai lililorutubishwa pia linaweza kuchangia tatizo hili.



• Vitu vingine ambavyo vinaweza kuchangia tatizo la mimba kutunga nje ya kizazi ni pamoja na:


 ✓ Kuwa na tatizo la mimba kutunga nje ya kizazi kwenye ujauzito wa nyuma. Ikiwa umewahi kuwa na ujauzito wa aina hii hapo awali, una uwezekano mkubwa wa kuwa na mwingine.


✓ Uvimbe au maambukizi ya magonjwa mbali mbali.  Maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama; kisonono au chlamydia, yanaweza kusababisha kuvimba kwenye mirija na viungo vingine vya karibu, na kuongeza hatari ya ujauzito kutunga nje ya kizazi(ectopic pregnancy).


✓ Matibabu kwa ajili ya kupata mtoto.  Utafiti mwingine unaonyesha kwamba wanawake ambao wamewahi kufanyiwa In- Vitro fertilization (IVF) kwa ajili ya kupata watoto au matibabu kama hayo wana uwezekano wa kuwa na tatizo la ujauzito kutunga nje ya kizazi(ectopic pregnancy). 


Pia kukaa kwa muda mrefu sana bila kuzaa au kuzaa mapema sana huweza kuongeza uwezakano wa tatizo


 ✓ Upasuaji katika mirija ya uzazi(Tubal surgery).  Upasuaji wa kurekebisha tatizo lolote kwenye mirija ya uzazi yaani fallopian tubes huongeza hatari ya Mwanamke kupatwa na tatizo la mimba kutunga nje ya kizazi.


 ✓ Aina ya njia ya uzazi wa mpango ulioichagua.  Uwezekano wa kupata ujauzito wakati unatumia kifaa kama intrauterine device (IUD) ni mdogo sana. 


Lakini endapo kwa bahati mbaya ikitokea umebeba mimba na una kifaa cha IUD ndani yako, uwezekano wa mimba kutunga nje ya kizazi ni mkubwa.


  Njia ya kufunga uzazi(Tubal ligation), njia hii ni ya kudumu ya kudhibiti uzazi lakini ikiwa utapata ujauzito baada ya utaratibu huu uwezekano wa mimba hyo kutunga nje ya kizazi ni asilimia 100.


✓ Uvutaji sigara.  Uvutaji sigara kabla tu ya kupata ujauzito unaweza kuongeza hatari ya ujauzito kutunga nje ya kizazi.  Kadri unavyovuta sigara, ndivyo hatari inavyo kuwa kubwa zaidi.


DALILI ZA MIMBA KUTUNGA NJE YA KIZAZI


 Huenda usione dalili yoyote mwanzoni. wanawake wengi ambao wana tatizo la mimba kutunga nje ya kizazi(ectopic pregnancy) wanapata dalili zote za awali za ujauzito  kama vile; kukosa period au kutokuona siku zao za hedhi, matiti kujaa, kichefuchefu N.k.


 Ikiwa unapima ujauzito au mimba, matokeo yatakuwa mazuri tu kama kawaida na kuonyesha kwamba wewe ni mjamzito.  Tofauti tu ni kwamba matatizo huanza kutokea pale ujauzito unavyozidi kukua.


 - Mara nyingi, dalili za kwanza kabsa kama una tatizo la mimba kutunga nje ya kizazi ni damu nyepesi kuanza kutoka ukeni na maumivu ya kiuno au nyonga.


 Ikiwa damu huvuja kutoka kwenye mirija ya uzazi(fallopian tubes), unaweza kuhisi maumivu ya bega au hamu ya kuwa na haja kubwa.  Dalili maalum hutegemea mahali damu inajikusanya na mishipa ipi inaathiriwa.


 Ikiwa yai lililorutubishwa linaendelea kukua kwenye mrija wa fallopian, linaweza kusababisha mrija huo wa uzazi kupasuka.  Matokeo yake ni Kutokwa na damu nzito ndani ya tumbo la uzazi.  Dalili  kama hii huweza kuhatarisha maisha,kusababisha maumivu makali ya kichwa, kuzimia na mshtuko.


 KUMBUKA; NENDA HOSPITAL HARAKA UKIONA DALILI KAMA HIZI HAPA;


 • Maumivu makali ya tumbo na kutokwa na damu ukeni


 • Maumivu makali ya Kichwa au kuzimia


 • Maumivu ya bega N.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comment

DALILI 8 AMBAZO MTU HUWEZA KUZIPATA BAADA YA KIDONDA CHAKE KUSHAMBULIWA NA BACTERIAAfyaclass Forum •

DALILI 8 AMBAZO MTU HUWEZA KUZIPATA BAADA YA KIDONDA CHAKE KUSHAMBULIWA NA BACTERIA


1. Homa

 Baada ya upasuaji, ni kawaida kwa wagonjwa kuwa na homa kwa kiwango cha chini ya digrii 100 Fahrenheit. lakini, ikiwa joto la mwili lipo juu hadi 101 au zaidi, hiyo inaweza kuonyesha uwezekano wa maambukizi ya vimelea vya magonjwa kama vile Bacteria katika kidonda. 

 Wagonjwa ambao wana homa wanaweza pia kuwa na tatizo la maumivu ya kichwa na kupungua kwa hamu ya kula.

Vidonda vilivyoshambiwa na Bacteria vinaweza kupatiwa tiba ya antimicrobial drugs n.k.

 2. Mwili kuchoka kupita kiasi

 Kumuuliza mgonjwa jinsi anavyohisi inaweza kusaidia kutathmini uwepo wa maambukizi katika kidonda.

Kupata uchovu wa mwili kupita kiasi pamoja na mwili kukosa nguvu huweza kuwa kiashiria mojawapo cha uwepo wa maambukizi kwenye kidonda au jeraha ulilonalo.

 3. Kidonda kutoa usaha au maji maji yenye rangi ya Kijani au Njano

 Katika hali ya kawaida kidonda kinatakiwa kiwe na rangi nyekundu, hii ndyo ishara nzuri ya kidonda kuelekea kupona kwa urahisi

 4. Kuongezeka kwa Maumivu katika Jeraha au Kidonda

 Kwa ujumla, mgonjwa anayeendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji au  kuwa na jeraha/kidonda anapaswa kuona unafuu na maumivu yanayopungua na sio kuongezeka.  

Ikiwa mgonjwa ana maumivu yanayoongezeka badala kupungua, hiyo inaweza kuwa dalili ya maambukizi katika jeraha au kidonda. 

 5.Uwekundu Kuzunguka Jeraha au kidonda huku ndani ya kidonda kukiwa na rangi ya tofauti kama vile njano au kijani

 Hapo awali, vidonda vinaonekana vyekundu kidogo kwa sababu ya mchakato wa uchochezi wa asili wa uponyaji, lakini uwekundu huo unapaswa kupungua polepole kwa takribani siku 5-7. 

 Uwekundu zaidi karibu na jeraha huku ndani ya kidonda kukiwa na rangi nyingine ya tofauti kama njano au kijani ni ishara ya maambukizi katika jeraha. 

 6. Uvimbe wa Eneo Lililojeruhiwa

 Kama uwekundu, uvimbe ni kawaida katika hatua za mwanzo za uponyaji wa jeraha. lakini, uvimbe unapaswa kupungua kila wakati.  Uvimbe wa kudumu inaweza kuwa ishara ya maambukizi au shida zingine kwenye kidonda.

 7. Joto La Ngozi Inayozunguka kidonda

 Ingawa inaweza kuwa kawaida kwa ngozi inayozunguka jeraha kuhisi joto kali, Lakini endapo ngozi inayozunguka kidonda huhisi joto sana kwa kugusa bila kupoa, hiyo inaweza kuonyesha kwamba mwili unapanga mashambulizi dhidi ya maambukizi. 

 Joto husababishwa na kutolewa kwa kemikali za vasoactive zinazoongeza mtiririko wa damu kwenye eneo hilo.  Kwa kuongezea, mfumo wa kinga hutoa joto zaidi kwa kutuma lymphocyte kutoa kingamwili kuharibu pathogen na phagocytes kumeza bakteria waliokufa.

 8. Kupoteza uwezo wa kufanya kazi katika kiungo chenye jeraha au kidonda

 Ishara nyingine ya maambukizi kwenye jeraha ambayo inaweza kuhitaji matibabu, ni wakati mgonjwa amepoteza uwezo wa kiutendaji kwenye kiungo au eneo lilithoathiriwa. 

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD