Showing posts with label chakula na Lishe. Show all posts
Showing posts with label chakula na Lishe. Show all posts

Mikakati mitano ya kuimarisha utekelezaji wa afua za lishe, TangaAfyaclass Forum •

Tanga: Halmashauri ya Mji Handeni imeainisha mikakati mitano ya kuimarisha utekelezaji wa afua za lishe, ili kukabiliana na changamoto za utapiamlo na kupunguza idadi ya watoto wanaozaliwa wakiwa na uzito pungufu.

Akisoma taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Afua za Lishe kwa Robo ya Kwanza, Novemba 11, 2025, Ofisa Lishe wa Halmashauri hiyo, Ester Herman, amesema mikakati hiyo inalenga kuongeza uelewa wa jamii kuhusu lishe bora na kuhakikisha huduma muhimu za lishe zinatolewa kikamilifu katika ngazi zote.

Ametaja baadhi ya mikakati hiyo kuwa ni kuhamasisha jamii kuhakikisha watoto chini ya miaka mitano wanaendelea kuhudhuria kliniki hata baada ya kukamilisha chanjo, na kushirikiana na idara za elimu msingi, sekondari pamoja na kamati za lishe za kata kuhamasisha wazazi kuchangia huduma za chakula shuleni.

Aidha, amesema halmashauri imejipanga kuhimiza wajawazito kufika mapema kwenye vituo vya afya, ili kupunguza idadi ya watoto wanaozaliwa wakiwa na uzito pungufu, sambamba na kushirikiana na Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kutoa elimu ya kilimo na ufugaji bora wa kuku, bata na sungura ili kuongeza upatikanaji wa chakula chenye virutubisho.

0 Comment

Kwanini Usitumie chumvi nyingi sana,hizi hapa ni Sababu kuuAfyaclass Forum •

Kwanini Usitumie chumvi nyingi sana,hizi hapa ni Sababu kuu

Sababu kuu za kuto kutumia chumvi nyingi sana ni kwamba chumvi (hasa chumvi ya kawaida – sodium chloride) ikizidi mwilini inaleta madhara kwa afya. Hapa kuna sababu muhimu:

1. Shinikizo la damu kupanda (High blood pressure)
Kiasi kikubwa cha sodium hufanya mwili ushikilie maji mengi, na hivyo kuongeza mzigo kwenye moyo na mishipa ya damu. Hii husababisha presha ya damu kupanda.

2. Hatari ya magonjwa ya moyo na kiharusi
Shinikizo la damu la muda mrefu huongeza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo na kiharusi.

3. Madhara kwa figo
Figo ndizo husafisha chumvi iliyozidi mwilini. Kiwango kikubwa cha chumvi huzichosha figo na kuongeza uwezekano wa kupata;

4. Uvimbe mwilini (Edema)
Kwa sababu chumvi huvuta maji, matumizi makubwa husababisha miguu, uso au mikono kuvimba kutokana na maji kuzidi mwilini.

5. Osteoporosis (mifupa kuwa dhaifu)
Chumvi nyingi husababisha mwili kupoteza calcium kupitia mkojo, jambo linaloweza kudhoofisha mifupa na kuongeza hatari ya kuvunjika kwa urahisi.

6. Madhara kwa tumbo
Utafiti unaonyesha chumvi nyingi huongeza hatari ya vidonda vya tumbo na hata saratani ya tumbo (stomach cancer).

🔹 WHO inapendekeza mtu mzima asitumie zaidi ya gramu 5 za chumvi kwa siku (takribani kijiko cha chai kimoja cha chumvi).

0 Comment

Vyakula vya kupunguza damu mwiliniAfyaclass Forum •

Vyakula vya kupunguza damu mwilini

Je,Vyakula vya kupunguza damu mwilini ni Vipi?

Kwa habari ya vyakula vya kupunguza damu mwilini ni ngumu kupata vyakula ambavyo huweza kupunguza damu moja kwa moja,

badala yake unaweza kuangalia vyakula ambavyo huweza kudhibiti uzalishaji wa damu au huweza kuwa na mchango kwenye mchakato wa utengenezaji wa damu kisha uvidhibiti.

Mfano; Kuepuka vyakula vyenye madini ya chuma: Madini ya chuma yanahitajika kwa ajili ya kutengeneza hemoglobini. Kupunguza ulaji wa vyakula vyenye madini chuma, kama vile nyama nyekundu, spinach, na maharagwe, kunaweza kusaidia katika kudhibiti uzalishaji wa seli nyekundu za damu, na kisha kusaidia kupungua uzalishwaji wa Damu.

Kula Vyakula visivyo na wingi wa vitamini B12: Vitamini B12 inachangia katika uzalishaji wa seli nyekundu za damu. Kupunguza ulaji wa vyakula vyenye vitamini B12 nyingi kama nyama, mayai, na maziwa kunaweza kuongeza kiwango cha Damu mwilini.

Hivo basi,kupunguza kula vyakula vinavyopandisha kiwango cha damu haraka huweza kuwa njia mbadala ya kupunguza kiwango cha damu mwilini,vyakula hivo ni pamoja na;

  • kupunguza ulaji wa Maharage
  • Kupunguza kula nyama hasa nyama nyekundu
  • Kupunguza kula mboga za majani kama vile tembele
  • Kuacha kabsa kutumia juice kama vile za Beetroot,Rozella n.k

Sababu za Upungufu wa Damu mwilini:

1. Upungufu wa Virutubisho muhimu kwa ajili ya Utengenezaji wa Damu mwilini 

Virutubisho hivyo ni kama vile; 

  • Madini Chuma(Iron): Hiki ni kiambato muhimu kinachohusika na uzalishaji wa hemoglobini, Hivo upungufu wa madini chuma huweza kusababisha Upungufu wa damu mwilini
  • Upungufu wa vitamini B12: Vitamini B12 ni muhimu kwa uzalishaji wa seli nyekundu za damu. Upungufu wake unaweza kusababisha pia tatizo la Upungufu wa damu mwilini au anemia
  • Upungufu wa folate (vitamini B9): Folate ni muhimu kwa uzalishaji wa seli nyekundu za damu. Upungufu wa folate pia unaweza kusababisha tatizo la Upungufu wa damu mwilini.

2. Magonjwa yanayoathiri utengenezaji wa damu: Magonjwa kama vile;

  • Magonjwa ya mifupa: Magonjwa kama leukemia au myelofibrosis yanayohusisha kuathiri uzalishwaji wa seli nyekundu za damu yanaweza kupunguza uzalishaji wa damu.

3. Kupoteza damu kwa njia mbali mbali kama vile:

  • Kuungua au majeraha makubwa: Majeraha makubwa au ajali ambazo husababisha kupoteza damu nyingi zinaweza kusababisha upungufu wa damu mwilini.
  • Kuvuja damu nyingi na kwa muda mrefu wakati wa hedhi: Wanawake wanaopata hedhi nyingi sana na kwa muda mrefu wanaweza kupoteza kiasi kikubwa cha damu kila mwezi, hali inayoweza kusababisha tatizo la Upungufu wa Damu mwilini.
  • Kuwa na Vidonda vya tumbo au vidonda vya utumbo,: Vidonda vya tumbo au utumbo ambavyo vinavuja damu vinaweza kusababisha kupoteza damu kidogo kidogo lakini kwa muda mrefu, na kusababisha upungufu wa damu mwilini.

4. Magonjwa mengine ni pamoja na;

-Magonjwa ya figo: Ugonjwa wa figo unaweza kusababisha upungufu wa homoni inayoitwa erythropoietin, ambayo inahitajika kwa uzalishaji wa seli nyekundu za damu.

- Magonjwa ya autoimmune:

Magonjwa kama lupus au rheumatoid arthritis yanaweza kuathiri uwezo wa mwili kuzalisha seli nyekundu za damu au kushambulia seli nyekundu za damu zilizopo, na kusababisha tatizo la Upungufu wa damu mwilini.

- Ugonjwa wa bandama:

Pia Wagonjwa wengi wenye matatizo ya bandama,kama vile bandama kuvimba n.k,hupata shida ya kupungua kwa damu mwilini 

- Maambukizi au magonjwa kama vile;

Ugonjwa wa homa ya Ini(hepatitis), au Ugonjwa wa malaria yanaweza kuathiri uzalishaji wa damu au kuharibu seli za damu zilizopo.

5. Matumizi ya baadhi ya dawa:

Dawa fulani, kama vile dawa za kemoterapia, antibiotics, au dawa za kulevya, zinaweza kudhoofisha uzalishaji wa seli nyekundu za damu au kuharibu seli zilizopo, na kusababisha kupungua kwa damu mwilini.

6. Hali kama Vile ya UJAUZITO

Pia Wajawazito wengi hukumbwa na hali ya Damu kupungua mwilini hasa kadri Ujauzito unavyokuwa Mkubwa.

KUMBUKA:

Kupungua kwa damu mwilini ni hali inayohitaji uchunguzi wa daktari ili kubaini chanzo na kupewa matibabu stahiki. Ikiwa unadhani unakutana na dalili za upungufu wa damu mwilini kama vile; uchovu, kizunguzungu, viganya vya mikono,Lips za mdomo,pamoja na ngozi ndani ya jicho kuwa nyeupe sana au kupumua kwa shida, ni muhimu kupata huduma za afya mara moja.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Madhara ya Mafuta ya kupikiaAfyaclass Forum •

Madhara ya Mafuta ya kupikia

Tafiti zinaonyesha Idadi ya Watu wanene kupindukia Imeongezeka hivi karibuni, Je,Mafuta ya Kupikia nayo ni chanzo? Soma hapa kufahamu...!!!!

Idadi ya watu wanaosumbuliwa na tatizo la unene imeongezeka Sana katika miaka ya hivi karibuni,si katika nchi zilizoendelea pekee bali hata za kipato cha Chini."

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani, watu wapatao bilioni 2.5 duniani kote walikuwa na tatizo la uzito mkubwa au Uzito kupita kiasi mnamo mwaka 2022.

Lakini pia Unene wa kupindukia miongoni mwa watoto umeongezeka mara nne.

Unene umekuwa tatizo linalotia wasiwasi si miongoni mwa watoto tu bali pia miongoni mwa watu wazima.

Mafuta yakupikia yana Athari gani mwilini?

Mtindo mbaya wa Maisha ikiwemo Ulaji mbaya unatajwa kuwa sababu kuu za kunenepa kupita kiasi.

Hata hivyo, mara nyingi watu hupuuza ukweli kwamba mafuta tunayoongeza kwenye mlo wetu kila siku huchangia tatizo hilo.

Mafuta ya kupikia hutumiwa kufanya chakula chochote kiwe kitamu zaidi.

Kutokana na hili, miili yetu hukusanya mafuta, Na Kwa kuwa hatufanyi mazoezi mengi, mafuta mwilini hayayeyuki."

Pia Asilimia kubwa ya Watu hula Mlo wenye wanga nyingi sana, Wanga huu hubadilika na kuwa mafuta baada ya kuingia mwilini,

Zaidi ya hayo, mafuta pia hujilimbikiza katika miili yetu. Hii huongeza hatari ya unene kupita kiasi."

"Kiwango cha mafuta ya miili yetu huwa juu kila wakati.

Hata kama mtu ni mwembamba, mafuta ya mwili wake bado ni 30-40%, ambayo ni ya juu sana. Kwa upande mwingine, wanariadha wana 7-8% ya mafuta ya mwili."

"Ikiwa tuna mafuta mengi katika miili yetu, Matokeo yake ni uzito wa mwili kuongezeka Zaidi"

"Kutumia mafuta ya kula kuliko kiasi kinachopendekezwa kunapunguza kasi ya ufanyajikazi wa miili yetu,Hii inasababisha kuongezeka kwa mafuta ya mwili na uzito.

Zaidi ya hayo, hutupatia kalori za ziada badala ya kutupa nyuzinyuzi, vitamini muhimu na madini."

Miili yetu hupata kalori zake nyingi kutoka kwenye mafuta,Kwa kila kalori nne tunazopata kutoka kwenye protini, tunapata kalori tisa kutoka kwenye mafuta.

Kwa hivyo, chochote tunachokula na kalori nyingi kinaweza kusababisha kunenepa, hasa kwa watu ambao tayari ni wanene."

Unapaswa kutumia mafuta kiasi gani?

Unene unaweza kudhibitiwa kwa kutumia mafuta kidogo,Kadiri watu wanavyotumia mafuta mengi, kiasi cha mafuta mwilini huongezeka.

Dk. Mahendra Narwaria, rais wa All India Society for Advanced Study and Obesity, anasema, "Chakula cha Wahindi kina wanga na mafuta mengi

Dk. Parmeet Kaur alisema, "Mafuta hutusaidia kuyeyusha vitamini kama vile A, D, E, na K katika miili yetu.

Kwa hiyo, miili yetu inahitaji kiasi fulani cha mafuta."

Pia anasema, "Watu wanapaswa kutumia mafuta kulingana na umri wao.

Hata hivyo, mtu ambaye hana shughuli nzito anapaswa kutumia vijiko 4-5 tu vya mafuta kwa siku.

Hiyo ni, gramu 20-25 za mafuta kwa siku.

Hii ni nyingi kwa mtu mmoja."

Hata hivyo, mafuta sio sababu pekee ya uzito kuwa mkubwa.

Credits Also to:BBC

0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD