Showing posts with label mapacha. Show all posts
Showing posts with label mapacha. Show all posts

Mapacha tisa wa Mali watimiza miaka 4 kwa SasaAfyaclass Forum •

Mnamo mwaka 2021, dunia ilishuhudia muujiza wa kipekee: mama Halima Cissé kutoka Mali alijifungua watoto tisa kwa mpigo — wavulana wanne na wasichana watano — tukio ambalo halijawahi kutokea tena kwa mafanikio duniani!



Serikali ya Mali iliwasafirisha yeye na mume wake, Abdelkader Arby, hadi Morocco kwa matibabu ya hali ya juu baada ya kugundua alikuwa na ujauzito wa mapacha 7. Lakini walipofika Morocco, walipokea mshangao mkubwa — walikuwa ni mapacha tisa!

Kutokana na tukio hilo la kipekee, Halima Cissé aliandikishwa rasmi katika Kitabu cha Rekodi za Dunia cha Guinness (Guinness World Records) kama mwanamke wa kwanza kuwahi kujifungua watoto tisa kwa mpigo na wote wakaishi, jambo lililovutia dunia nzima.

Sasa mapacha hao wametimiza miaka minne, wakiwa na afya njema na furaha kubwa. Wazazi wao hivi karibuni walisherehekea siku hiyo ya kipekee kwa kushiriki picha na kumbukumbu kupitia Instagram, wakikumbuka safari yao ya ajabu ya uzazi.

0 Comment

Mapacha hawa; “Wanatumia miguu ya mtu mmoja na mfupa wa nyonga mmojaAfyaclass Forum •

Hii ni aina ya mapacha walioungana ambao kwa kitaalam hujulikana kama conjoined twins

Mapacha hawa; “Wanatumia miguu ya mtu mmoja na mfupa wa nyonga mmoja.

#PICHA:

“Wanatumia miguu ya mtu mmoja na mfupa wa nyonga mmoja.

“Wana uti za mgongo mbili tofauti na mishipa yao yote lakini kwa namna fulani wanaratibu kabisa kazi za viungo hivi sawa na hawana budi kuambiana jinsi ya kusogeza mkono au jinsi ya kusogeza mguu.”

Hawa ni Watoto mapacha walioungana(conjoined twins) waliotarajiwa kuishi siku chache tu, lakini wameimarika kinyume na matarajio ya madaktari na sasa wametimiza miaka saba.

Marieme na Ndeye hawakutarajiwa kuishi kwa zaidi ya siku chache walipozaliwa Senegal 🇸🇳 2016.

Kwa sasa wanafikiriwa kuwa pacha pekee wanaokua wakiwa wameunganika barani Ulaya.

Wataalam wa matibabu walionya familia hiyo kwamba, bila kuwatenganisha, hakuna mtoto anayeweza kuishi zaidi ya miezi michache.Lakini, madaktari walishauri, hatua ya kuwatenganisha ingempa Ndeye nafasi nzuri zaidi ya kuendelea kuishi.

“Ilikuwa ni kumuua mtoto wangu mmoja kwa ajili ya mwingine, ni jambo ambalo siwezi kufanya,” Ibrahima alisema wakati huo.

“Siwezi kuchagua nani ataishi na nani atakufa sasa.”

Ingawa wasichana wote wana haiba na hisia zao za kipekee, wanategemeana kuishi.

“Wanatumia miguu ya mtu mmoja na fupanyonga moja”..

Soma Zaidi aina hii ya mapacha walioungana(conjoined twins)

Mapacha hawa; “Wanatumia miguu ya mtu mmoja na mfupa wa nyonga mmoja
0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Forum Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Forum ASANTE.
UNDERSTOOD