Showing posts with label ugonjwa wa UTI. Show all posts
Showing posts with label ugonjwa wa UTI. Show all posts

Jinsi ya Kujikinga na Ugonjwa wa UTI,NEW!Afyaclass Forum •

Makala hii imeandikwa na Dr.Ombeni Mkumbwa,kwa kuzingatia Uzoefu,Idadi ya Wagonjwa wa UTI wanaoripoti hospital kila mara,historia zao,Tafiti mbali mbali za afya ikiwemo kutoka Shirika la Afya Duniani(WHO),pamoja na Taasisi zingine za afya kama vile HealthLine,WebMd n.k.

Jinsi ya kujikinga na Ugonjwa wa UTI

Tumia njia hizi kujikinga na Maambukizi ya njia ya Mkojo(UTI), Tips muhimu sana kwako:

1.Epuka tabia ya kubana Mkojo mara kwa mara

Kubana Mkojo mara kwa mara wakati mkojo unatakiwa utoke,huongeza hatari ya Bacteria kukaa kwenye kibofu cha Mkojo na kuzaliana zaidi,

Kama unahisi kukojoa,Please kojoa! hii itakusaidia sana kama ulikuwa hujui.

Hivo Epuka tabia hii ya kubana mkojo mara kwa mara.

2. Hakikisha Unakunywa maji mengi kila Siku

Ingawa maji sio Tiba Kamili ya UTI,Zipo tafiti nyingi huonyesha Mtu anayekunywa maji mengi angalau lita 2 kwa siku hupunguza uwezekano wa kushambuliwa na UTI za mara kwa mara kwa zaidi ya Asilimia 50%.

3. Usafi binafsi pamoja na Usafi wa Chooni

Moja ya Vitu ambavyo vinaongeza mashambulizi ya bacteria wa UTI(E.coli) ni kutumia vyoo vichafu,

Ndyo maana Watu wanaotumia Vyoo vya Kushare na Watu wengi(public toilets) kama vile Vyoo vya Stendi,Sokoni,Hospitalini Au hata nyumbani, kama havijafanyiwa Usafi vizuri huweza kusababisha hatari zaidi ya maambukizi ya UTI.

Kingine! Epuka tabia ya kutumia maji machafu chooni,tumia maji masafi, Kama maji yamekaa muda mrefu kwenye vyombo kama ndoo za maji,usiongezee masafi juu yake,mwaga, tumia maji Safi,

Maji machafu kwenye ndoo hizi,huongeza hatari ya bacteria wa UTI kukua na kuongezeka zaidi.

4. Epukaa kukaa na nguo za ndani mbichi

Hii si tu inaongeza hatari ya maambukizi haya ya Bacteria kwenye mfumo wa Mkojo,Lakini pia maambukizi kama ya Fangasi n.k....

Tazama Zaidi Video hii:

Rejea Zaidi:

0 Comment

Dalili ya Kutoka Vitu kama Usaha kwenye Njia ya MkojoAfyaclass Forum •

Dalili ya Kutoka Vitu kama Usaha kwenye Njia ya Mkojo

➡️FAHAMU:Dalili ya Kutoka Vitu kama Usaha kwenye Njia ya Mkojo,Si magonjwa ya Zinaa Pekee❌

📌Wapo ambao wana Ugonjwa wa UTI na Wanapata Dalili kama Hii Pia.

⚠️Kama una Tatizo hili na hujapata Tiba|👉Kwa Ushauri&Tiba Wasap +255758286584.

0 Comment

Ugonjwa wa UTI ni nini? na Dalili zake ni Zipi? Na je nani yupo kwenye hatari Zaidi kupata?Afyaclass Forum •

Ugonjwa wa UTI ni nini? na Dalili zake ni Zipi? Na je nani yupo kwenye hatari Zaidi kupata?

Ni kweli kwamba kuna Makala Nyingi sana Mtandaoni kuhusu Ugonjwa wa UTI, Lakini leo kupitia makala hii tutagusa vitu ambavyo pengine hujawahi kuvisikia popote.

Ugonjwa wa UTI

Ugonjwa wa UTI huhisisha maambukizi kwenye njia na mfumo mzima wa mkojo na kwa kitaalam hujulikana kama Urinary tract infections (UTIs),

Maambukizi haya hutokea pale ambapo viini vya magonjwa kama vile bacteria vinaposhambulia kwenye mfumo wa Mkojo.

Ugonjwa wa UTI ni ugonjwa sumbufu kwa watu wengi duniani sio Tanzania pekee, Mfano; kwa nchi ya Marekani pekee, Zaidi ya watu million 8.1 humuona daktari kila Mwaka kwa Sababu ya tatizo hili.

Ugonjwa huu huathiri maeneo mbali mbali kwenye mfumo wa Mkojo ikiwemo;

  • Figo
  • Njia ya mkojo,ureters,Urethra
  • Kibofu cha Mkojo n.k

Watu ambao wapo kwenye hatari ya Kupata UTI

Kutokana na utafiti wa Mwaka 2022 ulionyesha kwamba; Kundi hili la watu lipo kwenye hatari zaidi ya kupata Ugonjwa huu wa UTI;

  • Wanawake
  • Wajawazito
  • Wenye matatizo yanayosababisha upungufu wa kinga mwilini
  • Wazee
  • Wanaotumia Mpira wa mkojo maarufu kama Catheters
  • Waliopo kwenye Tiba ya mionzi(radiotherapy treatment)
  • Wenye matatizo ya Figo
  • Wenye Ugonjwa wa Kisukari
  • Wenye maambukizi ya UTI hapo awali
  • Wanaojisaidia kwenye mazingira machafu; mfano ya vyoo vichafu, maji machafu n.k

Kwa ujumla, wanawake wana uwezekano mkubwa wa kupata UTI kuliko wanaume, huku asilimia 40-60% ya wanawake wakipata maambukizi angalau mara moja katika maisha yao na asilimia 10% ya wanawake wanapata UTI mara moja kwa mwaka. Wanawake wako katika hatari zaidi kuliko wanaume kwa sababu mrija wao wa mkojo ni mfupi, ambayo inafanya iwe rahisi kwa bakteria kuingia kwenye kibofu.

Dalili za Ugonjwa wa UTI

Dalili za ugonjwa wa UTI tumezigawanya katika makundi mbali mbali ya watu mfano;

  • wazee,
  • watoto,
  • wanaume,
  • wanawake,
  • wajawajazito n.k

Kwa Ujumla,Nazo ni kama ifuatavyo;

– Kuhisi mkojo mara kwa mara na Kukojoa mara kwa mara

– Kupata maumivu,usumbufu wowote au kuhisi kuungua wakati wa kukojoa

– Kuhisi Mkojo kwa ghafla

– Mkojo kutoa harufu mbaya sana, na wakati mwingine kuwa kama na vidamu damu

– Kuhisi uchovu wa mwili kupita kiasi

– Kupata maumivu ya misuli,joints pamoja na mifupa

– Kuhisi maumivu ya kichwa

– Kuhisi homa

Ikiwa maambukizi yamepanda mpaka sehemu ya juu kwenye mfumo wa mkojo(upper urinary tract) inaweza kusababisha;

  • Homa: nyuzijoto 100.4 ºF (38 ºC)  au Zaidi
  • Hali kama ya kuchanganyikiwa
  • Kupata maumivu makali ya mgongo
  • Mwili kutetemeka sana
  • Kuhisi kichefuchefu na kutapika

Bacteria ambao husababisha Zaidi UTIs ni pamoja na;

– Escherichia coli

– Protus mirabilis

– Enterococcus faecalis

– Staphylococcus saprophyticus

– Klebsiella pneumoniae

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Ugonjwa wa UTI ni nini? na Dalili zake ni Zipi? Na je nani yupo kwenye
hatari Zaidi kupata?
0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD