Showing posts with label utapiamlo. Show all posts
Showing posts with label utapiamlo. Show all posts

Utafiti:Utapiamlo unaweza kusababisha aina mpya ya kisukariAfyaclass Forum •

Utafiti:Utapiamlo unaweza kusababisha aina mpya ya kisukari

Utafiti mpya uliochapishwa katika jarida la The Lancet Global Health unaonyesha kuwa zaidi ya watu milioni 25 duniani wanaishi na aina mpya ya ugonjwa wa kisukari unasababishwa na njaa.

Wataalamu wa afya wamependekeza kutambuliwa rasmi kwa aina hiyo mpya ya kisukari inayotokana na utapiamlo, hatua hiyo ya utambuzi itasaidia kupambana na ugonjwa huo katika nchi zinazoendelea zinazokumbwa na njaa na umaskini.

Utafiti uliochapishwa katika jarida la The Lancet Global Health, unaonesha zaidi ya watu milioni 25 duniani wanaishi na aina hii ya kisukari, ambayo huathiri zaidi vijana walio na umri chini ya miaka 30. Tofauti na aina nyingine za kisukari, aina hii haihusiani na unene bali na uzito mdogo unaosababishwa na ukosefu wa lishe bora.

Shirikisho la Kimataifa la Kisukari limeunga mkono pendekezo la kuitambua rasmi aina hii kama kisukari aina ya 5, licha ya kuwa aina ya 3 na 4 bado hazijapewa uhalali wa kisayansi.

Aina za kawaida za ugonjwa wa kisukari zinazojulikana, ni aina ya pili, kwa kimombo "DiabetesType two", ambayo husababishwa na hali ya mtu kunenepa sana au kuwa na uzito kupita kiasi na watu wazima mwili wa mgonjwa huwa sugu dhidi ya homoni ya insulin. Aina nyingine ni ile ya kwanza, kwa kimombo Diabetis Type one, ambayo hugundulika tangu utotoni, na ambayo hutokana na kongosho kushindwa kuzalisha insulin ya kutosha.

Awali, Shirika la Afya Duniani liliwahi kuainisha kisukari kinachohusiana na utapiamlo katika miaka ya 1980 na 1990, lakini utambuzi huo uliondolewa mwaka 1999 kutokana na kutokuwepo kwa makubaliano ya kitaalamu.

Tangu wakati huo, tafiti mbalimbali zimeendelea kuonyesha uhusiano kati ya utapiamlo na kisukari, lakini bado haijafahamika wazi jinsi hali hiyo inavyosababisha ugonjwa huo. Aidha, haijulikani iwapo matibabu yak yanaweza kuwa ya kawaida ya kisukari  ambayo mara nyingi hulenga kupunguza uzito kama wanavyoshauriwa wagonjwa wa kisukari wengine wenye uzito mkubwa.

Wataalamu wanashauri kuwa njia bora ya kukabiliana na kisukari aina ya 5 ni kuimarisha juhudi za kupambana na njaa na umaskini. Wanapendekeza watu wapewe chakula cha bei nafuu chenye virutubisho vya kutosha kama vile dengu, kunde, nafaka zilizoongezwa mafuta na nafaka zenye virutubisho.

Ugonjwa huo wa kisukari aina ya 5 huathiri uzalishaji wa insulini mwilini, lakini si kwa kiwango kikubwa kama kisukari aina ya 1. Watafiti wanasema wagonjwa wengi wa aina hii wanatoka katika nchi kama Bangladesh, Ethiopia, India, Indonesia, Nigeria, Uganda, Pakistan na Rwanda.

0 Comment

El Niño yapelekea ongezeko la viwango vya njaa na utapiamlo MalawiAfyaclass Forum •

El Niño yapelekea ongezeko la viwango vya njaa na utapiamlo Malawi

#PICHA:Majaribio ya upandaji maharagwe yanayostahimili ukame nchini Malawi. (Maktaba)

Takriban watu milioni tisa nchini Malawi wanakumbwa na athari mbaya za mafuriko na ukame unaosababishwa na El Niño hali iliyo haribu mavuno na kupelekea ongezeko la viwango vya njaa na utapiamlo.

Wakizungumza wakiwa mjini Blantyre nchini Malawi, Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya Mgogoro wa Mabadiliko ya Tabianchi na El Niño Bi. Reena Ghelani, Mkurugenzi wa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP Dkt. Menghestab Haile na Mkurugenzi la shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO nchini humo Dkt. Patrice Talla wamesisitiza umuhimu mkubwa wa msaada wa kimataifa kwa Serikali na watu kwa Malawi.

kufuatia Rais wa Malawi kutangaza janga la kitaifa viongozi hao kwa pamoja wamefanya ziara maalum nchini humo na kukutana na wadau wa masuala ya kibinadamu na maendeleo, pamoja na maafisa wa Serikali, ikiwa ni pamoja na mamlaka ya Usimamizi wa Hatari za Maafa.

Alipokutana na washirika wa kibinadamu na maendeleo, Dk. Menghestab Haile alisema kuwa “Ni jambo la kusikitisha kuona wakulima wakiwa wamekata tamaa kutokana na ukame, ambao siyo kosa lao kwani walipanda wakitarajia mazuri lakini mvua haikutosha.” Alielezea kuwa hakutakuwa na chochote cha kuvuna na jamii hizi zitakabiliana na njaa kali kwa mwaka mwingine msaada usipoongezwa, hali ambayo inaweza kuwa mbaya zaidi kufuatia upungufu wa akiba ya chakula na kuongezeka kwa bei ya mahindi.

Kipindi hiki cha El Niño kinatokea wakati msururu wa majanga na hatari umeongezeka, na kuathiri sana maendeleo ya Malawi kwani  hapo awali, zaidi ya watu milioni 2.2 walikumbwa na kimbunga kilichoharibu miundombinu muhimu nchini humo, kilichofuatiwa  mlipuko mbaya zaidi wa kipindupindu.

Kwa upande wake Dkt. Talla kutoka FAO alieleza kuwa “Viwango na mfululizo wa gharama ya athari za mabadiliko ya tabianchi zinatoa msisitizo wa umuhimu wa kuongeza usaidizi katika kujiandaa na kupambana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na mnepo.”

Naye Dkt Ghelani anahimiza uwekezaji katika kusaka suluhisho endelevu zinazolenga kushughulikia mizizi ya udhaifu pamoja na kuipa kipaumbele misaada ya dharura ya wakati uliopo. Vilevile amehimiza kuungwa mkono jamii za Malawi ili kujenga mustakabali wa dhabiti na usalama wa chakula.

Msaada zaidi unahitajika

Ukame umeathiri vibaya mavuno ya mahindi ya msimu huu, na kusababisha upungufu unaokadiriwa kuwa asilimia 45 ikilinganishwa na wastani wa miaka mitano. Ifikapo mwisho wa mwaka huu, inatabiriwa takriban asilimia 40 ya watu watakumbwa na njaa kali.  Aidha, takriban watu 14,000 walihamishwa kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi katika sehemu ya kaskazini mwa nchi.

Ingawa Serikali ya Malawi imetoa ombi zaidi la msaada katika kupatiwa msaada kwenye mkakati wake wa umwagiliaji wa kitaifa, juhudi hizi zinakwamishwa na upungufu wa fedha kwani ni asilimia 40 tu ya fedha zilizohitajika kwa mwaka 2023 zilizopatikana.

Mwishoni mwa mwaka 2023, Mfuko Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Kukabiliana na Dharura ulitoa dola milioni 4 kusaidia watu walioathiriwa na majanga ya tabianchi na hivi karibuni ilitangaza dola milioni 13.5 za ziada kusaidia juhudi za kukabiliana na El Niño katika ukanda wa Kusini mwa Afrika. Hata hivyo bado kuna mengi zaidi yanahitaji kufanyika.

Via:UN

El Niño yapelekea ongezeko la viwango vya njaa na utapiamlo Malawi
0 Comment

Mtoto mwenye umri wa mwaka 1 anafanyiwa uchunguzi wa matibabu kama kuna dalili za utapiamloAfyaclass Forum •

#PICHA;Mtoto mwenye umri wa mwaka 1 anafanyiwa uchunguzi wa matibabu kama kuna dalili za utapiamlo katika kituo cha mapokezi kwenye mpaka wa Sudan na Sudan Kusini.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP leo limetia saini mikataba miwili na Saudi Arabia yenye thamani ya dola milioni 1.4 ili kutibu na kuzuia utapiamlo nchini Sudan na Sudan Kusini.

Taarifa ya WFP kutoka Nairobi Kenya na Riyadh Saudi Arabia inaeleaza kuwa fedha hizo zitasaidia zaidi ya watoto 35,000 na wajawazito pamoja na wamama wanaonyonyesha walioathirwa na vita, mtikisiko wa kiuchumu na mabadiliko ya tabianchi.

Idadi hiyo inajumuisha wasudan 29,000 ambao wameathirika na vita vinavyoendelea pamoja na wa Sudan Kusini 6,000 ambao wameathirika na mgogoro wa misaada ya kibinadamu uliosababishwa na machafuko, kiuchumi na mabadiliko ya tabianchi.

“Fedha hizi zinakuja katika wakati mahususi, ni takriban mwaka mmoja sasa tangu kuanza kwa vita tangu hapo vimeendelea kuongezekza mpaka kuwa moja ya majanga kabaya ya kidunia” amesema Michael Dunford Mwakilishi wa WFP ukanda wa Afrika Mashariki.

Mwakilishi huyo amesema tayari wameanza kupokea ripoti za watoto kufa njaa huko nchini Sudan hivyo programu za usaidizi wa lishe ni muhimu zaidi katika kuzuia vido na kuleta mustakabali bora wa baadae wa watoto.

Kwa upande wake Dkt.Abdullah Al Moallem ambaye ni mkurugenzi wa Idara ya Afya ya Mazingira ya Ksrelief ya Saudi Arabia ameeleza kuwa wamejitolea kusaidia kundi hilo ambalo lipo kwenye mazingira magumu ili kukuza mustakabali wenye afya na uthabiti zaidi kwa jamii nzima.

“Mipango hii itawawezesha wale wanaohitaji kupata msaada muhimu wa chakula na matibabu na itatusaidia kupambana na njaa na utapiamlo katika nchi zote mbili,” alisema Dk. Al Moallem.

Nchini Sudan, watoto milioni 4.9 wenye umri wa chini ya miaka mitano na wanawake wajawazito au wale wanaonyonyesha wana utapiamlo, hili likiwa ni ongezeko la asilimia 22 kutoka mwaka uliopita.

Kati ya hao, watoto 730,000 wanakabiliwa na utapiamlo mkali.

Nchini Sudan Kusini, watoto milioni 1.6 na wanawake 870,000 wajawazito na wanaonyonyesha wanatarajiwa kukosa lishe bora mwaka huu.

Mtoto mwenye umri wa mwaka 1 anafanyiwa uchunguzi wa matibabu kama kuna
dalili za utapiamlo
0 Comment

Udumavu ni nini?chanzo,dalili na Tiba yakeAfyaclass Forum •

Udumavu ni nini?chanzo,dalili na Tiba yake

Udumavu ni tatizo la kiafya linalotokana na utapiamlo wa muda mrefu, hususani katika kipindi cha ukuaji wa mtoto, kutoka mimba hadi miaka mitano ya kwanza ya maisha. Tatizo hili linaathiri ukuaji wa mtoto kimwili na kiakili, na linaweza kuwa na madhara ya muda mrefu.

Baadhi ya watu huchanganya hivi vitu viwili(Udumavu&Utapiamlo); Udumavu ni matokeo ya utapiamlo,na kuna tofauti kati ya Udumavu na utapiamlo;

Soma Zaidi hapa; Utapiamlo ni nini?,chanzo,dalili na Tiba yake

Maana ya Udumavu

Udumavu ni hali inayojitokeza wakati mtoto ana uzito au urefu mdogo ukilinganishwa na umri wake. Hali hii inaonyesha kuwa mtoto hajapata virutubisho vya kutosha vinavyohitajika kwa ukuaji na maendeleo yake ya kawaida.

Chanzo cha Udumavu

Chanzo kikuu cha udumavu ni utapiamlo au lishe duni. Hii inaweza kutokana na:

(1) Upungufu wa Chakula:

Ukosefu wa chakula cha kutosha, kilicho na virutubisho muhimu.

(2) Maradhi:

Maambukizi ya mara kwa mara yanayosababisha mwili kutumia virutubisho haraka au kupoteza virutubisho kwa njia ya kuharisha, mfano;

  • malaria,
  • minyoo,
  • Pamoja na magonjwa ya njia ya utumbo.

(3) Matatizo ya Kiuchumi na Kijamii:

Umaskini, ukosefu wa elimu, na ufikiaji mdogo wa huduma za afya.

(4) Mazingira:

Maji yasiyo salama, usafi duni, na mazingira machafu yanayochangia maradhi.

Dalili za Udumavu

Dalili za udumavu zinaweza kujumuisha:

– Kuwa na Urefu au uzito mdogo ukilinganishwa na umri.

– Maendeleo duni ya kiakili na kimwili.

– Uchovu wa mara kwa mara

– kupungua,mwili kuwa dhaifu au mwili kukosa nguvu.

– Mfumo dhaifu wa kinga, hivyo kuwa rahisi kupata maambukizi.

– Mtoto Kuchelewa kuanza kuzungumza au kutembea.n.k

Madhara ya Udumavu

Madhara ya udumavu ni makubwa na ya muda mrefu, yakiwemo:

• Ukuaji duni wa akili na kimwili.

• Ongezeko la hatari ya kupata magonjwa sugu katika maisha ya baadaye kama vile kisukari na magonjwa ya moyo.

• Utendaji duni shuleni na katika shughuli za kila siku.

• Matatizo katika uzalishaji na uchumi wa taifa kwa ujumla kutokana na kupungua kwa ufanisi wa kazi.n.k

Tiba ya Udumavu

Kuaddress tatizo la udumavu kunahitaji mkakati wa kina unaojumuisha:

✓ Lishe Bora:

Kuhakikisha watoto wanapata chakula bora chenye virutubisho vyote muhimu, kama vile protini, vitamini, na madini.

✓ Usafi na Maji Salama:

Kuboresha usafi na kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama.

✓ Elimu ya Afya na Lishe:

Kuwaelimisha wazazi na jamii kuhusu umuhimu wa lishe bora na afya.

✓ Huduma za Afya:

Kuimarisha huduma za afya za msingi kwa watoto, kama vile chanjo na matibabu ya maradhi ya utotoni.

✓ Msaada wa Kiuchumi na Kijamii:

Kutoa msaada kwa familia masikini ili kuboresha upatikanaji wa chakula na huduma za afya.

Hitimisho

Kwa kuhitimisha, udumavu ni tatizo la kiafya linalohitaji mkakati wa pamoja kati ya serikali, asasi za kiraia, na jamii. Kupitia elimu, maboresho ya lishe, huduma za afya, na usafi, inawezekana kupunguza na hatimaye kumaliza tatizo la udumavu katika jamii.

Soma Zaidi hapa; Utapiamlo ni nini?,chanzo,dalili na Tiba yake

Udumavu ni nini?chanzo,dalili na Tiba yake
0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD