Utafiti:Utapiamlo unaweza kusababisha aina mpya ya kisukari

Utafiti:Utapiamlo unaweza kusababisha aina mpya ya kisukari

#1

Utafiti:Utapiamlo unaweza kusababisha aina mpya ya kisukari

Utafiti mpya uliochapishwa katika jarida la The Lancet Global Health unaonyesha kuwa zaidi ya watu milioni 25 duniani wanaishi na aina mpya ya ugonjwa wa kisukari unasababishwa na njaa.

Wataalamu wa afya wamependekeza kutambuliwa rasmi kwa aina hiyo mpya ya kisukari inayotokana na utapiamlo, hatua hiyo ya utambuzi itasaidia kupambana na ugonjwa huo katika nchi zinazoendelea zinazokumbwa na njaa na umaskini.

Utafiti uliochapishwa katika jarida la The Lancet Global Health, unaonesha zaidi ya watu milioni 25 duniani wanaishi na aina hii ya kisukari, ambayo huathiri zaidi vijana walio na umri chini ya miaka 30. Tofauti na aina nyingine za kisukari, aina hii haihusiani na unene bali na uzito mdogo unaosababishwa na ukosefu wa lishe bora.

Shirikisho la Kimataifa la Kisukari limeunga mkono pendekezo la kuitambua rasmi aina hii kama kisukari aina ya 5, licha ya kuwa aina ya 3 na 4 bado hazijapewa uhalali wa kisayansi.

Aina za kawaida za ugonjwa wa kisukari zinazojulikana, ni aina ya pili, kwa kimombo "DiabetesType two", ambayo husababishwa na hali ya mtu kunenepa sana au kuwa na uzito kupita kiasi na watu wazima mwili wa mgonjwa huwa sugu dhidi ya homoni ya insulin. Aina nyingine ni ile ya kwanza, kwa kimombo Diabetis Type one, ambayo hugundulika tangu utotoni, na ambayo hutokana na kongosho kushindwa kuzalisha insulin ya kutosha.

Awali, Shirika la Afya Duniani liliwahi kuainisha kisukari kinachohusiana na utapiamlo katika miaka ya 1980 na 1990, lakini utambuzi huo uliondolewa mwaka 1999 kutokana na kutokuwepo kwa makubaliano ya kitaalamu.

Tangu wakati huo, tafiti mbalimbali zimeendelea kuonyesha uhusiano kati ya utapiamlo na kisukari, lakini bado haijafahamika wazi jinsi hali hiyo inavyosababisha ugonjwa huo. Aidha, haijulikani iwapo matibabu yak yanaweza kuwa ya kawaida ya kisukari  ambayo mara nyingi hulenga kupunguza uzito kama wanavyoshauriwa wagonjwa wa kisukari wengine wenye uzito mkubwa.

Wataalamu wanashauri kuwa njia bora ya kukabiliana na kisukari aina ya 5 ni kuimarisha juhudi za kupambana na njaa na umaskini. Wanapendekeza watu wapewe chakula cha bei nafuu chenye virutubisho vya kutosha kama vile dengu, kunde, nafaka zilizoongezwa mafuta na nafaka zenye virutubisho.

Ugonjwa huo wa kisukari aina ya 5 huathiri uzalishaji wa insulini mwilini, lakini si kwa kiwango kikubwa kama kisukari aina ya 1. Watafiti wanasema wagonjwa wengi wa aina hii wanatoka katika nchi kama Bangladesh, Ethiopia, India, Indonesia, Nigeria, Uganda, Pakistan na Rwanda.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code