Afyaclass JE UNAWEZA KUISHI NA FIGO MOJA BILA MADHARA YOYOTE?

 FIGO

• • • • •

JE UNAWEZA KUISHI NA FIGO MOJA BILA MADHARA YOYOTE?


Kabla ya kujibu swali hili, fahamu kwamba kuna baadhi ya watu huzaliwa na Figo moja na maisha yanaendelea kama kawaida,


Je kuna madhara yoyote mtu akiwa na Figo moja?


Hakuna madhara yoyote ya mtu kuwa na figo moja, kitu cha msingi sio idadi ya figo ulizonazo, Kitu cha msingi ni uwezo wa Figo yako kufanya kazi vizuri bila matatizo yoyote.


MUHIMU; Kama una figo moja unachotakiwa kukifanya ni kuilinda sana kwa sababu huna nyingine, na ulinzi huo ni pamoja na Kufanya mambo yafuatayo;


✓ Kuacha matumizi ya pombe kabsa


✓ Kula vyakula ambavyo vina virutubisho vyote na kuepuka kula vyakula vya mafuta sana


✓ Kufanya mazoezi ya mwili


✓ Kuhakikisha uzito wako unakuwa wa kawaida na kuepuka matatizo kama unene au uzito kupita kiasi


✓ Epuka matumizi ya Dawa hovio


✓Hakikisha shinikizo lako la damu linakuwa kwenye hali nzuri au hali ya kawaida


✓ Epuka hali ya msongo wa mawazo kwa muda mrefu


✓ Jenga utaratibu wa kufanya checkup mara kwa mara,sio mpaka uumwe

N.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE LILE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




You, Mehreen and others

WEKA MAONI HAPA(Reply)

Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD