KORODANI
• • • • •
TATIZO LA MWANAUME KUPATA UVIMBE KWENYE KORODANI(chanzo na tiba)
Tatizo hili la mwanaume kuvimba korodani huweza kutokea kwa korodani moja au zote mbili, na vile vile huweza kuambatana na maumivu makali au kutokuwa na maumivu yoyote.
CHANZO CHA TATIZO LA KUVIMBA KWA KORODANI
- Mtu kupata ajali yoyote na kuumia kwenye korodani zake, kugongwa na kitu kizito,kuchomwa na kitu cha ncha kali n.k
- Kupatwa na maambukizi ya magonjwa mbali mbali
- Kupatwa na tatizo la kansa ya korodani
- Kupatwa na tatizo la korodani kujaa maji yaani Hydrocele
- Kupatwa na tatizo la mshipa kuwa mkubwa ndani ya korodani
- Kupatwa na tatizo la korodani kujizungusha pamoja na mishipa kuziba yaani Testicular torsion
- Kupatwa na tatizo la hernia
n.k
MATIBABU YA TATIZO LA KORODANI KUVIMBA
- tiba ya tatizo hili la korodani kuvimba hutegemea na chanzo chake, hivo nenda hospital kwa ajili ya uchunguzi na kugundua chanzo cha tatizo,ndipo uanze tiba.
Japo kwa ujumla wake,mgonjwa huweza kupewa dawa mbali mbali pamoja na huduma ya upasuaji kama tatizo linahitaji upasuaji.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!