Showing posts with label magonjwa ya wanawake. Show all posts
Showing posts with label magonjwa ya wanawake. Show all posts

Ndizi 1 tu husaidia kupunguza na kuondoa Maumivu wakati wa HedhiAfyaclass Forum •

Kwa Mwanamke anayepata maumivu makali wakati wa hedhi anaelewa jinsi maumivu hayo yanavyokuwa. Sasa hapa kuna kitu rahisi ambacho kinaweza kusaidia kidogo - ndizi.

Ndizi zina magnesiamu na vitamini B6, ambazo zote zina jukumu la kulegeza misuli na kupunguza Mkazo. Maumivu ya hedhi hutokea kwa sababu uterasi yako inasisimka na kubana zaidi(Contracts) ili kutoa utando wake. Magnesiamu husaidia kulegeza misuli laini, ambayo inaweza kupunguza nguvu ya mikazo hiyo. Utafiti fulani pia unaonyesha kwamba viwango vya kutosha vya magnesiamu vinaweza kupunguza prostaglandini -ambayo husababisha maumivu yanayoambatana na mikazo.

Hivi ndivyo ndizi inavyoweza kukusaidia wakati wa hedhi:

• Magnesiamu ndani yake husaidia kulegeza misuli ya uterasi

• Vitamini B6 inaweza kupunguza uvimbe,Mkazo na mabadiliko ya hisia

• Sukari asilia hutoa nishati ya haraka ikiwa unahisi dhaifu sana mwilini

• Potasiamu husaidia kuzuia maumivu ya misuli na uchovu

Ndizi moja haitaondoa kabsa maumivu makali, lakini inaweza kuwa msaada wa kupunguza maumivu na wa asili kama sehemu ya lishe bora kwa ujumla.

 Kwa matokeo bora, changanya na:

• Kunywa maji Vizuri,Uji au maziwa,Tangawizi,Maji ya uvuguvugu n.k.

• Kufanya mazoezi mapesi kama kujinyoosha au kutembea

• Kutumia Warm compress kwenye tumbo la chini

• Kulala vya kutosha n.k.

Kumbuka: Ikiwa maumivu yako ya hedhi ni makali, Hali inazidi kuwa mbaya, au yanaathiri maisha yako ya kila siku, ni muhimu kushauriana na mtaalamu wa afya. Hali kama vile endometriosis au PCOS zinahitaji mwongozo sahihi wa kimatibabu. Na Kwa ushauri zaidi unaweza kutuma Neno Afyaclass Inbox.

0 Comment

Kupata Damu Ya Hedhi Nyeusi inaashiria nini?Afyaclass Forum •

Kupata Damu Ya Hedhi Nyeusi inaashiria nini?

Kupata damu ya hedhi nyeusi mara nyingi si tatizo kubwa, bali inaashiria damu ya zamani iliyokaa muda mrefu ndani ya mji wa mimba (uterasi) kabla ya kutoka. Damu inapokaa muda, hukosa hewa (oxidation) na kuwa rangi ya kahawia au nyeusi.

Tuangalie nini huashiria Damu ya Hedhi ikitoka Nyeusi,Hapa kuna maana mbalimbali:

1. Damu ya zamani kutoka

Hii Huonekana mwanzoni au mwishoni mwa hedhi,na inakuwa;

  • Kiasi kidogo
  • Na Haina harufu kali

Hii huwa ni kawaida.

2. Mzunguko wa hedhi kuchelewa

Kama hedhi ilichelewa, damu inaweza kuwa nzito na nyeusi

Huambatana na maumivu kidogo ya tumbo

3. Mabaki ya mimba (kama Mimba iliwahi kuharibika)

Kama Mimba iliharibika na kukuwa na mabaki ndani,Damu nyeusi inaweza kutoka kwa siku kadhaa,Na Huambatana na maumivu makali au damu nyingi.

4. Maambukizi ya Kwenye Via vya Uzazi (kama PID au UTI kali)

Ikiwa tatizo ni maambukizi haya,Damu nyeusi yenye na harufu mbaya sana inaweza kutoka,Lakini pia unaweza kupata dalili Zingine kama vile;

  • Maumivu wakati wa tendo la ndoa
  • Maumivu ya tumbo la chini au Chini ya Kitovu

Hapa inahitaji kuonana na daktari au Kuongea na Wataalam wa afya kwa Ushauri wa haraka.

5. Dalili za mimba changa (implantation bleeding)

Damu kidogo sana, rangi kahawia au nyeusi huweza kutokea kabla ya tarehe ya hedhi, hii ikiwa inaashiria Mimba changa inapojishikiza kwenye mji wa Mimba,Damu hii kitaalamu hujulikana kama Implantation bleeding.

Kumbuka: Hakikisha Unaongea na daktari kama damu inatoka nyeusi na Inaambatana na Dalili hizi;

  • Kuna harufu kali sana
  • Unapata Maumivu makali ya tumbo
  • Damu nyingi isiyo ya kawaida
  • Hali inaendelea miezi kadhaa

Je,Una tatizo hili na hujapata Tiba bado? 

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Maumivu ya Tumbo chini ya Kitovu kwa Mwanamke Afyaclass Forum •

Maumivu ya Tumbo chini ya Kitovu kwa Mwanamke 

Watu wengi huhusisha kimakosa maumivu ya tumbo chini ya kitovu kwa wanawake na matatizo ya uzazi pekee. Hii si sahihi. Hali nyingi za kiafya zinaweza kusababisha Maumivu ya Tumbo chini ya Kitovu kwa Mwanamke, na utambuzi sahihi ni muhimu kwa matibabu bora kwa wanawake wa rika zote.

Chanzo cha Maumivu ya Tumbo chini ya Kitovu kwa Mwanamke 

Maumivu ya tumbo chini ya kitovu kwa mwanamke yanaweza kusababishwa na mambo mbalimbali, Nitayaeleza kwa lugha rahisi ili uweze kujitathmini, lakini bado ni muhimu kumuona mtaalamu kama maumivu ni makali au yanaendelea.

1. Maumivu ya Siku za Hedhi

Maumivu haya yanaweza kuhusiana na siku za hedhi, hasa kabla au wakati wa hedhi kutokana na kukaza kwa mfuko wa uzazi.

2. Maambukizi ya bacteria kwenye via vya uzazi vya Mwanamke(PID) yanaweza kusababisha maumivu chini ya kitovu, na mara nyingi huambatana na uchafu usio wa kawaida ukeni, harufu mbaya au maumivu wakati wa kujamiiana.n.k.

3. Tatizo la Uvimbe kwenye kizazi(Fibroids) au Tatizo la Vivimbe maji(Ovarian cysts)

Ovari cysts pia husababisha maumivu ya upande mmoja au chini ya tumbo kwa Wanawake wengi,

Uvimbe kwenye kizazi ni uvimbe ambao huonekana sana kwa wanawake hasa wenye umri wa miaka 30-40. Ingawa baadhi ya wanawake wanaweza kuwa hawana dalili zozote, wengine wanaweza kupata maumivu ya tumbo, maumivu ya mgongo, maumivu wakati wa tendo la ndoa, au ugumu wa kupata mimba.

Lakini pia tatizo la Endometriosis ambalo huhisha tishu za uterasi kukua nje ya uterasi(mfuko wa uzazi), Hali hii mara nyingi huhusishwa na maumivu ya tumbo chini ya kitovu na inaweza kuchangia Mwanamke asipate Ujauzito.

4. Maambukizi kwenye njia ya Mkojo(UTI)

Sababu nyingine ni matatizo ya mfumo wa mkojo ikiwemo Maambukizi ya njia ya mkojo (UTI) husababisha maumivu chini ya kitovu, hisia ya kuchoma wakati wa kukojoa, kukojoa mara kwa mara au mkojo wenye harufu kali n.k. Na Wakati mwingine maumivu huongezeka unapobana mkojo.

5. Tatizo la Mimba kutunga nje ya Kizazi(Ectopic pregnancy)

Mimba kutunga nje ya kizazi hutokea wakati kiinitete kinapopandikizwa na kukua nje ya uterasi(mfuko wa uzazi), Na mara nyingi hutokea kwenye mirija ya uzazi yaani fallopian tubes.

Hii ni hali inayohatarisha maisha,na hali hii huweza kuambatana na dalili mbali mbali ikiwemo; maumivu makali ya tumbo (mara nyingi huonekana upande mmoja), kutokwa na damu ukeni, kichefuchefu, na kizunguzungu. Hapa Ushauri wa haraka wa kimatibabu unahitajika.

6. Magonjwa ya Zinaa-Sexually Transmitted Infections (STIs)

Maumivu ya Tumbo chini ya Kitovu kwa Mwanamke yanaweza kusababishwa pia na magonjwa ya zinaa kama vile;

Dalili zingine ni pamoja na maumivu wakati wa kukojoa, kutokwa na uchafu usio wa kawaida ukeni, na kutokwa na damu isiyo ya kawaida katikati ya hedhi. Ushauri wa haraka wa kimatibabu ni muhimu ili kuzuia maambukizi na matatizo Zaidi.

7. Tatizo la Mawe kwenye Figo(Kidney Stones)

Tatizo hili pia huweza kusababisha hali ya Maumivu hasa pale Mawe haya Yanaposogea, yanaweza kusababisha maumivu ya tumbo chini ya kitovu.

8. Kwa Upande wa mfumo wa chakula pia unaweza kuwa chanzo

Gesi tumboni, kuvimbiwa, au matatizo ya utumbo kama IBS husababisha maumivu ya chini ya tumbo yanayokuja na kuondoka. Kama maumivu yapo zaidi upande wa kulia na yanaongezeka taratibu, Tatizo la appendicitis au kidole tumbo(Appendix) pia huanza kama maumivu chini ya kitovu kisha kuhamia upande wa kulia.

Kwa mwanamke aliye katika umri wa kupata ujauzito, mimba pia ni chanzo muhimu cha kuzingatia. Maumivu chini ya tumbo yanaweza kuwa ya kawaida mwanzoni mwa mimba, lakini kama yanaambatana na damu ukeni, kizunguzungu au maumivu makali upande mmoja, inaweza kuwa mimba nje ya mfuko wa uzazi (ectopic pregnancy) ambayo ni hatari na huhitaji matibabu ya haraka.

Je,Una tatizo hili na hujapata Tiba bado?

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Soma pia Maumivu ya Tumbo chini ya Kitovu kwa Mjamzito https://www.afyaclass.com/2024/09/maumivu-ya-chini-ya-kitovu-kwa-mjamzito.html

Rejea Link:

https://www.vinmec.com/eng/blog/what-is-dull-lower-abdominal-pain-in-women-1

https://my.clevelandclinic.org/health/symptoms/24530-lower-abdominal-pain

https://www.medicalnewstoday.com/articles/319931

0 Comment

Mbegu kutoka ukeni baada ya tendo chanzo chake na TibaAfyaclass Forum •

Mbegu kutoka ukeni baada ya tendo chanzo chake na Tiba

Tatizo la mbegu kutoka nje ya Uke baada ya tendo la ndoa chanzo kikubwa ni nini



Tatizo la mbegu kutoka nje baada ya tendo la ndoa ni jambo linalowahusu wanandoa au wapenzi wengi, hasa wale wanaojaribu kupata mtoto. Kwa kawaida, baada ya mwanaume kumwaga mbegu ndani ya uke, ni kawaida kiasi kidogo cha shahawa kurudi nje. Hata hivyo, ikitokea kiasi kikubwa kinatoka mara kwa mara, inaweza kuwa sababu ya kushindwa kupata mimba, japo si mara zote.

Sababu Zinazowezekana za Mbegu kutoka Nje:

  1. Mwili wa mwanamke kuwa wima haraka baada ya tendo
    – Kusimama au kwenda bafuni mara moja baada ya tendo kunaweza kusababisha mbegu kutoka kabla hazijaingia ndani vizuri.

  2. Shughuli ya misuli ya uke
    – Misuli ya uke inaweza kushindwa kuzuia mbegu ndani, hasa kama hakuna mshikamano mzuri wa misuli ya nyonga.

  3. Wingi wa shahawa
    – Wakati mwingine, kama mwanaume anatoa shahawa nyingi kupita kiasi, ni kawaida nyingine kutoka nje kwa sababu nafasi ya uke haitoshi kuziweka zote mara moja.

  4. Kutoingia kwa uume vizuri
    – Ikiwa uume haujaingia vizuri au tendo limefanyika kwa haraka sana, mbegu huweza kumwagwa karibu na mlango wa uke na kutoka kirahisi.

  5. Uwezekano wa matatizo ya mlango wa kizazi
    – Kama mlango wa kizazi (cervix) hauko katika nafasi nzuri ya kupokea mbegu (mfano mwanamke akiwa juu), mbegu haziwezi kuelekezwa vizuri ndani.

Je, hali hii ni tatizo kubwa?

Kwa kawaida, si tatizo kubwa na haitoshi peke yake kueleza kuwa Sababu ya Mwanamke kutokubeba mimba ingawa inaweza kuchangia pia. Kwa Wanawake wengi, kiasi cha mbegu kinachobaki ndani kinatosha kabisa kwa ajili ya kurutubisha yai. Kwa hiyo, ikiwa mnaendelea kufanya tendo mara kwa mara katika kipindi cha ovulation, kuna uwezekano mkubwa wa kushika mimba.

Njia za kusaidia kupunguza tatizo hili:

  1. Kubadilisha mikao ya tendo la ndoa:
    – Mikao kama mwanamke akiwa chini (missionary style) inasaidia mbegu kuingia zaidi na kukaa kwa muda mrefu.

  2. Kubaki umelala kwa mgongo baada ya tendo:
    – Mwanamke abaki amelala dakika 15–30 baada ya tendo, akiegesha mto chini ya nyonga ili mbegu ziende juu kuelekea kwenye kizazi.

  3. Epuka kusimama au kuoga haraka baada ya tendo

  4. Tumia mazoezi ya nyonga (Kegel exercises)
    – Husaidia kuimarisha misuli ya uke na kuzuia mbegu kutoka kwa haraka.

Wakati wa Kumwona Daktari:

Fikirieni kuonana na daktari au mtaalamu wa afya ya uzazi iwapo:

  • Mmejaribu kupata mimba kwa zaidi ya miezi 12 bila mafanikio.
  • Kuna dalili nyingine kama maumivu wakati wa tendo, kutokwa na uchafu usio wa kawaida, au hedhi isiyo ya kawaida.
  • Unashuku tatizo la uzazi kwa mmoja wenu.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Maumivu wakati wa tendo la ndoa kwa mwanamke chanzo na TibaAfyaclass Forum •

Maumivu wakati wa tendo la ndoa kwa mwanamke (yanayojulikana kitaalamu kama dyspareunia) ni tatizo la kawaida linaloweza kusababishwa na mambo mengi ya kimwili au kisaikolojia. Hebu tuchambue kwa undani:

Sababu Kuu za Maumivu Wakati wa Tendo la Ndoa

1. Ukavu wa uke (Vaginal dryness)

Sababu: kukosa ute wa asili unaolainisha uke. Hii Hutokea zaidi kwa: 

  • Wanawake baada ya kujifungua au wanaonyonyesha.
  • Wanaotumia dawa fulani (mfano antihistamines, antidepressants).
  • Wanawake waliokaribia au walio katika kipindi cha kukoma hedhi.

Lakini pia huweza kusababishwa na sababu mbali mbali ikiwemo; mabadiliko ya Vichocheo mwilini,maambukizi ya magonjwa n.k.

2. Maambukizi ya uke (Vaginitis)

Dalili: harufu mbaya, kutokwa na uchafu, kuwasha, au kuchoma,Ukavu ukeni n.k.

Yapo maambukizi ya magonjwa kama vile: fangasi (candida), bakteria, au magonjwa ya zinaa. Haya huweza kusababisha tatizo hili.

Tiba hutegemea na chanzo: ila dawa kama jamii ya antifungal, antibiotic, au dawa za STI, huweza kutumika kutibu hali hii.

3. Maambukizi ya bacteria kwenye Via vya Uzazi vya Mwanamke (Pelvic Inflammatory Disease – PID)

Maambukizi ya kizazi, mirija ya uzazi, au ovari.

Dalili huweza kuwa: maumivu chini ya tumbo, homa, uchovu, maumivu wakati wa tendo.n.k

4. Kuwa na michubuko au Vidonda kwenye mlango wa kizazi au kuvimba (Cervical inflammation / erosion)

Hali hii Huleta maumivu ya ndani zaidi (deep pain) wakati wa tendo.

Kuvimba pamoja na Michubuko pia huweza kuwepo kwenye eneo la ukeni,hali hii inachangia maumivu pia wakati wa tendo.

5. Matatizo ya kihisia au kisaikolojia

Msongo wa mawazo, hofu, kutopata raha au mapenzi kwa mwenza, au uzoefu mbaya wa nyuma. n.k.

Suluhisho juu ya hili: 

  • Mazungumzo ya wazi na mwenza.
  • Ushauri wa kisaikolojia au sex therapy.

6. Tatizo la Uvimbe kwenye kizazi,Endometriosis au Fibroids

Haya ni magonjwa ya mfumo wa uzazi yanayosababisha maumivu ya kina ndani ya Uke

Dalili huweza kuwa: maumivu wakati wa hedhi, tendo, au wakati wa haja kubwa.

Suluhisho: uchunguzi wa kitaalamu (ultrasound / laparoscopy) na tiba maalum.

Zingatia Mambo haya ya Kufanya Nyumbani Kabla ya Kuenda Hospitali

•Hakikisha unapata muda wa kutosha wa maandalizi “foreplay” ili uke uwe na unyevunyevu wa kutosha.

•Epuka tendo kama una maumivu makali au uchafu usio wa kawaida.

•Kunywa maji mengi na kula matunda (hasa yenye vitamin C na E).

•Vaa nguo za ndani zisizobana, zenye material ya pamba sio mpira.

Wakati wa Kumwona Daktari kwa haraka

Ongea na daktari au Nenda hospitali ukiona mojawapo ya haya:

-Maumivu makali kila mara unapofanya tendo.

-Kutokwa na uchafu, damu, au harufu isiyo ya kawaida.

-Maumivu ya tumbo la chini yanayoendelea.

-Homa au uchovu unaoambatana na maumivu hayo. n.k..

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Kutokwa na damu wakati wa tendo kwa mwanamkeAfyaclass Forum •

Kutokwa na damu wakati wa tendo kwa mwanamke

Kuna wanawake wengi hupatwa na tatizo hili la kutokwa na damu ukeni wakati au baada ya kufanya mapenzi au tendo la ndoa,

Je chanzo cha tatizo hili ni nini?

CHANZO CHA MWANAMKE KUTOKWA NA DAMU WAKATI NA BAADA YA KUFANYA MAPENZI

Kuna sababu mbali mbali ambazo husababisha mwanamke kuvuja damu wakati akifanya mapenzi au baada ya kufanya mapenzi, na sababu hizo ni kama vile;

- Maambukizi katika via vya uzazi vya mwanamke yaani PELVIC INFLAMMATORY DISEASE(PID)

- Mwanamke kupatwa na magonjwa mbali mbali ya zinaa kama vile ugonjwa wa Pangusa au CHLAMYDIA

- Mwanamke kuwa na tatizo la ukavu ukeni ambao hupelekea michubuko na kuvuja damu wakati wa tendo la ndoa

- Mwanamke kuwa na tatizo la Saratani au Kansa ya kizazi au shingo ya kizazi

- Maambukizi ya magonjwa ambayo huweza kusababisha shingo ya kizazi au uke kuvimba yaani Cervicitis and Vaginitis

- Mwanamke kuwa na uvimbe kwenye shingo ya kizazi au kizazi yaani FIBROIDS,  ovarian Cysts N.k

- Kufanya mapenzi bila maandalizi ya kutosha hali ambayo huweza kupelekea michubuko na kuvuja damu ukeni

- N.k

Chanzo cha Mwanamke  Kuvuja Damu nyingi wakati wa Hedhi soma hapa kujua

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

 

Kutokwa na damu wakati wa tendo la ndoa kwa mwanamke siyo hali ya kawaida, na inaweza kusababishwa na mambo mbalimbali — mengine madogo, mengine yanayohitaji matibabu.

Sababu Zinazowezekana

  1. Ukavu wa uke (vaginal dryness)

    • Hutokea hasa kwa wanawake waliokoma hedhi au wanaotumia vidonge vya uzazi wa mpango.
    • Hufanya uke kuwa mkavu, hivyo msuguano husababisha michubuko na damu.
  2. Mabadiliko ya homoni

    • Wakati wa kunyonyesha, ujauzito au baada ya kujifungua, kiwango cha estrogeni hupungua na kufanya ukuta wa uke kuwa mwembamba na rahisi kuumia.
  3. Maambukizi ya uke au shingo ya kizazi

    • Kama vile Trichomonas, Gonorrhea, Chlamydia, au yeast infection.
    • Dalili zingine ni harufu mbaya, kuwasha, au maumivu wakati wa tendo.
  4. Vidonda au uvimbe kwenye uke/shingo ya kizazi

    • Mfano: Cervical polyp, fibroid, au cancer ya shingo ya kizazi (cervical cancer).
    • Mara nyingi damu hutoka baada ya tendo au katikati ya mzunguko wa hedhi.
  5. Msuguano mkali au tendo bila maandalizi ya kutosha

    • Huchana tishu za uke hasa kama hakukuwa na ute wa kutosha (ukosefu wa lubrication).
  6. Kuwa bikira (mara ya kwanza)

    • Damu ndogo kutokana na kuchanika kwa himeni (kifuniko cha bikira).
Wakati wa Kwenda Hospitali

Mwone daktari mapema kama:

  • Damu ni nyingi au inatokea mara kwa mara.
  • Kuna maumivu makali, harufu, au usaha.
  • Damu inatokea hata bila tendo.
  • Umeshawahi kuwa na historia ya Pap smear isiyo kawaida au haujafanya kabisa.
Vipimo Vinavyoweza Kufanyika
  • Uchunguzi wa uke (pelvic exam)
  • Pap smear au HPV test
  • Kipimo cha maambukizi (STD screening)
  • Ultrasound
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comment

kutoa vitu vyeupe ukeni chanzo ni nini?Afyaclass Forum •

Kutoa vitu vyeupe ukeni chanzo ni nini?

Fahamu Leo katika Makala hii,tumechambua Kila Kitu.......

Kutokwa na Uchafu mweupe ukeni huashiria nini?

Uchafu mweupe ukeni ukitoka na rangi nyeupe, kuonekana vizuri, pasipo na harufu ni kawaida, Ingawa mabadiliko haya huweza kuashiria tatizo;

  • Kutoka Mwingi
  • Kutoka mfululizo
  • Kubadilika rangi
  • Kuwa na harufu n.k

Uchafu Mweupe Ukeni(Clear or white):

Uchafu mweupe Ukeni ukiwa Mzito na kuambatana na harufu pamoja na miwasho huweza kuashiria maambukizi kama vile ya Fangasi(yeast infection).

NB: Kutokwa na uchafu ukeni hutokea kwa kawaida katika mzunguko wako wa hedhi. Baadhi ya mabadiliko katika kutokwa na uchafu ukeni yanaweza kutokea kutokana na hali fulani za matibabu, au maambukizi ya magonjwa kama vile fangasi.

Fahamu ni Majimaji ambayo husaidia kuweka uke safi na bila maambukizi, kutokwa na uchafu mweupe ukeni ni asili kabisa. Lakini rangi yake, kiwango au kiasi chake kinaweza kutofautiana, ikitegemea umri wako na mahali ulipo katika mzunguko wako wa hedhi.

Mabadiliko kadhaa, hata hivyo, yanaweza kuwa ishara ya hali ya kiafya. Haya yanaweza kujumuisha mabadiliko makubwa ya rangi au harufu pamoja na tofauti ya uwiano.

Ni vizuri Zaidi kufanya uchunguzi Kuanzia aina na sababu hadi wakati Uchafu mweupe ukeni unatoka, ili ikiwa kuna tatizo lolote au mabadiliko yoyote ufahamu mapema na kutafta Msaada wa kitaalam.

Aina za Uchafu Ukeni

Hizi ni aina Mbali mbali za uchafu Ukeni, Aina hizi mara nyingi huwekwa kulingana na rangi;

(1) Uchafu Mweupe Ukeni(White)

Kutokwa na Uchafu Mweupe ukeni ni kawaida, na mara nyingi hutokea hasa karibu na wakati wa kuanza kwa mzunguko wa hedhi au mwishoni mwa mzunguko wa hedhi.

Kawaida ya Uchafu huu ni kuwa mweupe, wenye kuvutika lakini usio na harufu mbaya.

(2) Uchafu mweupe mwithili ya maji(Clear and watery)

Karibu na kipindi cha yai kutoka(ovulation), Unaweza kupata uchafu mweupe wenye kuvutika Zaidi, na unafanana kabsa na ule ambao mwanamke akisisimka zaidi kihisia wakati wa kufanya mapenzi hutoka, Au hata wakati wa Ujauzito.

(3) Uchafu wa Brown au Nyekundu(bloody)

Kutokwa na uchafu wa kahawia au kama damu kunaweza kutokea wakati au mara baada ya mzunguko wako wa hedhi. Unaweza pia kupata kutokwa na damu kidogo kati ya hedhi. Hii inaitwa spotting.

Kutokwa na Uchafu kunakotokea wakati wa kawaida wa kipindi chako cha hedhi na baada ya kufanya ngono huweza kuwa na Ishara kiafya.

Na kutokwa na damu mapema kunaweza kuwa ishara ya kuharibika kwa mimba ikiwa wewe ni mjamzito.

(4) Uchafu wa Njano au kijani(Yellow or green)

Kutokwa na uchafu ukeni wa manjano au kijani kibichi zaidi – haswa ikiwa ni Mzito, na ukiambatana na harufu mbaya- ni ishara ya tatizo kiafya, hivo hakikisha unapata msaada kutoka kwa mtaalamu wa afya.

Chanzo cha Kutokwa na Uchafu Ukeni

Kutokwa na uchafu ukeni ni utendaji mzuri wa mwili unaotokana na mabadiliko ya asili katika viwango vya vichocheo aina ya estrojeni. Kiasi cha kutokwa na majimaji au uchafu ukeni kinaweza kuongezeka kutokana na kuwa kwenye kipindi cha yai kutoka(ovulation), msisimko wakati wa kufanya mapenzi, matumizi ya vidonge vya kudhibiti uzazi, na ujauzito.

Rangi, harufu na mwonekano wa uchafu unaotoka ukeni unaweza kuathiriwa vibaya na mabadiliko ya usawa wa bakteria wa ukeni. Hiyo ni kwa sababu idadi ya bakteria hatari inapoongezeka, maambukizo kwenye uke yanawezekana zaidi.

Hapa kuna baadhi ya maambukizi yanayoweza kupelekea shida hii ya Kutokwa na Uchafu Ukeni;

– Maambukizi ya bacteria(Bacterial vaginosis)

Bacterial vaginosis ni maambukizi ya bakteria, maambukizi haya Husababisha kuongezeka kwa uchafu kutoka ukeni ambao una harufu kali,  na wakati mwingine kuwa na harufu kama shombo ya samaki.

Kutokwa na uchafu kunaweza pia kuonekana kwa rangi ya kijivu, mwembamba, na majimaji. Na Katika hali nyingine, maambukizi haya hayatoi dalili zozote.

Ingawa ugonjwa wa bakteria vaginosis hauambukizwi kupitia mawasiliano ya ngono, una hatari kubwa ya kuupata ikiwa unafanya ngono au umepata mwenzi mpya hivi karibuni. Maambukizi yanaweza pia kukuweka kwenye hatari kubwa zaidi ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa (STI).

– Trichomoniasis

Trichomoniasis ni aina nyingine ya maambukizi ambayo chanzo chake ni parasite.

Kawaida huenezwa kwa mawasiliano ya ngono(huu ni ugonjwa wa Zinaa), lakini pia unaweza kuambukizwa kwa kutumia taulo au nguo za kuoga.

Nusu ya watu walioathiriwa hawana dalili zozote. Lakini kwa Wale wenye dalili mara nyingi wataona kutokwa na uchafu wa njano, kijani, au povu na harufu isiyofaa. Maumivu, kuvimba na kuwasha kuzunguka uke na vilevile wakati wa kukojoa au kufanya ngono pia ni dalili za kawaida.

– Maambukizi ya Fangasi(Yeast infection)

Maambukizi ya Fangasi hutokea wakati ukuaji wa fangasi unapoongezeka kwenye uke. Husababisha kutokwa na uchafu mzito kama maziwa ya mtindi na mweupe unaofanana na jibini.

Dalili zingine ni pamoja na kuwashwa karibu na uke pamoja na maumivu wakati wa tendo au wakati wa kukojoa.

Yafuatayo yanaweza kuongeza uwezekano wa kupata maambukizi Zaidi ya Fangasi sehemu za Siri;

– kuwa na Msongo wa  mawazo(stress)

– Ugonjwa wa kisukari

– matumizi ya dawa za kupanga uzazi

– Kuwa na mimba

– Matumizi ya antibiotics, hasa matumizi ya muda mrefu zaidi ya siku 10 n.k

– Ugonjwa wa kisonono na Pangusa(Gonorrhea and chlamydia)

Kisonono na chlamydia ni magonjwa ya zinaa ambayo yanaweza kusababisha kutokwa na uchafu ukeni usio wa kawaida kutokana na kuambukiza eneo la seviksi. Mara nyingi huwa na rangi ya manjano, kijani kibichi au mawingu.

Unaweza pia kupata:

  • maumivu wakati wa kukojoa
  • maumivu ya tumbo
  • kutokwa na damu ukeni baada ya kujamiiana
  • kutokwa damu katikati ya mzunguko wa hedhi

Lakini watu wengine wanaweza pia wasionyeshe dalili zozote.

– Genital herpes

Ugonjwa huu ni miongoni mwa magonjwa ya zinaa yanayoweza kusababisha kutokwa na uchafu mzito ukeni huku kukiwa na harufu kali, hasa baada ya kufanya mapenzi.

Vidonda na malengelenge yanaweza kutokea sehemu za siri pamoja na kutokwa na damu katikati ya mzunguko wa hedhi na kupata hisia ya kuwaka moto wakati wa kukojoa.

– Ugonjwa wa PID(Pelvic inflammatory disease)

Kutokwa na uchafu mwingi na harufu mbaya pamoja na maumivu ndani ya tumbo, baada ya ngono, au wakati wa hedhi au kukojoa kunaweza kuwa dalili za ugonjwa wa maambukizi ya bacteria kwenye via vya uzazi vya mwanamke(PID).

Hii hutokea wakati bakteria Kuingia kwenye uke na kufika hadi kwenye viungo vingine vya uzazi na inaweza kusababishwa na magonjwa ya zinaa ambayo yameachwa bila kutibiwa kama vile klamidia au kisonono.

– Maambukizi ya HPV au Saratani ya Shingo ya Kizazi(Human papillomavirus or cervical cancer)

Maambukizi ya virusi vya Human papilloma(HPV) huenezwa kwa njia ya ngono na yanaweza kusababisha saratani ya shingo ya kizazi. Ingawa kunaweza kuwa hakuna dalili, aina hii ya saratani inaweza kusababisha:

  • kutokwa na damu, Uchafu wa kahawia, au majimaji yenye harufu mbaya ukeni
  • kutokwa na damu isiyo ya kawaida katikati ya mzunguko wa hedhi au baada ya kujamiiana
  • maumivu wakati wa kukojoa au kuongezeka kwa hamu ya kukojoa

Katika hali ya nadra, kutokwa na majimaji ya hudhurungi au damu kunaweza pia kuwa ishara ya saratani ya endometriamu, fibroids, au ukuaji mwingine wa seli.

Ikiwa una dalili za Matatizo haya, hakikisha unapata matibabu.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Dalili za ovarian cyst,dalili za uvimbe MajiAfyaclass Forum •

Dalili za ovarian cyst (uvimbe maji kwenye ovari) hutegemea ukubwa wa uvimbe na aina yake, lakini mara nyingi zinafanana. Zifuatazo ni dalili kuu zinazoweza kujitokeza:

Dalili za Ovarian Cyst (Uvimbe Maji kwenye Ovari):

  1. Maumivu upande wa chini wa tumbo (hasa upande mmoja – kulia au kushoto).
  2. Maumivu makali wakati wa hedhi au hedhi kuwa nzito kuliko kawaida.
  3. Maumivu wakati wa tendo la ndoa.
  4. Kuvimba au kujaa tumboni (bloating) – kuhisi kama tumbo limejaa hewa.
  5. Kichefuchefu au kutapika, hasa kama cyst imepasuka.
  6. Mkojo wa mara kwa mara – kwa sababu cyst inasukuma kibofu cha mkojo.
  7. Kuchelewa kwa hedhi au mabadiliko katika mzunguko wa hedhi.
  8. Kuhisi uzito sehemu ya chini ya tumbo.
  9. Maumivu makali ghafla (acute pain) endapo cyst itapasuka au kujisokota (torsion).
Dalili hatarishi zinazohitaji uende hospitali haraka:
  • Maumivu makali ya ghafla kwenye tumbo la chini.
  • Kizunguzungu, kuishiwa nguvu au kupoteza fahamu (Hizi ni dalili za kuvuja damu kwa ndani).
  • Homa, kichefuchefu Kikali, au tumbo kuwa gumu sana.
Vipimo vya kuthibitisha:
  • Ultrasound (Pelvic Ultrasound) – ndio kipimo cha msingi.
  • Blood tests (kama CA-125) – hutumika kuangalia kama kuna hatari ya uvimbe kuwa wa saratani (hasa kwa wanawake waliokoma hedhi).
Matibabu hutegemea:
  • Aina ya cyst (functional, dermoid, endometriotic, n.k.)
  • Ukubwa wake
  • Umri wa mgonjwa
  • Dalili alizonazo

Je,Una tatizo hilo na hujapata Tiba bado?

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Sababu za hedhi kuchelewa na kubadilika badilikaAfyaclass Forum •

Sababu za hedhi kuchelewa na kubadilika badilika

Nini kinasababisha hedhi kuchelewa

Endapo una aina ya mzunguko wa hedhi ambao haubadiliki badiliki yaani regular menstrual cycles, kuna wakati unaweza kukutana na vipindi vya hedhi kuchelewa kuliko kawaida,

Hii huweza kukupa wasi wasi nini kinaendelea mwilini, Moja ya Sababu ya haraka haraka ambayo unaweza kufikiria ni kuhusu kubeba Mimba.

Katika Makala ya Leo,tumechambua Sababu kuu zinazoweza kukusababishia Hedhi yako ichelewe.

Nini kinasababisha hedhi kuchelewa

Zipo Sababu nyingi ambazo huweza kuchangia tatizo hili, na Baadhi ya Sababu hizo ni pamoja na;

1.Ujauzito,

2.Mabadiliko ya homoni – msongo wa mawazo, uchovu mwingi, au mabadiliko ya chakula/mazingira yanaweza kuchelewesha siku.

3.Magonjwa ya mfumo wa uzazi – mfano PCOS (polycystic ovarian syndrome), matatizo ya tezi (thyroid), au maambukizi.

4.Dawa fulani – mfano dawa za homoni, kupanga uzazi, au zingine.

5.Uzito kubadilika ghafla – kupungua sana au kuongezeka haraka.

Tuchambue Vizuri Sababu hizo.....

1. Kufanya Mazoezi kupita kiasi, Exercising Rigorously

Kila kitu kinataka kiasi, hata Mazoezi tunasema yana Faida nyingi mwilini lakini pia yanataka Kiasi,

Unaweza kuona shida ya kuchelewa kwa hedhi kutokana na kufanya mazoezi mazito. Mazoezi ya nguvu ya mara kwa mara yanaweza kusababisha vipindi visivyo kawaida vya hedhi ikiwemo kukosa hedhi. Unaweza pia kupata hedhi isiyo ya kawaida ikiwa utaanza kufanya mazoezi tena baada ya kutofanya kwa muda.

Mazoezi kupita kiasi husababisha physical stress mwilini mwako, Hali ambayo huuambia Ubongo Kuacha kuzalisha vichocheo yaani reproductive hormones.

Moja ya vichocheo hivo ni Pamoja na gonadotropin-releasing hormone (GnRH).  Hormone hii ndyo inayohusika na Muda wa Hedhi yako kutoka,Ikiwa Ubongo haujaitoa au unaitoa Taratibu sana hedhi inaweza kuacha Kutoka.

2.  Mabadiliko kwenye Uzito wa Mwili

Kichocheo cha Estrogen kwa asilimia kubwa huzalishwa kutoka kwenye tishu zinazotengeneza mafuta baada ya kipindi cha Ukomo wa Hedhi(menopause),tishu hizi hufahamika kama adipose tissue,

Ingawa,Mwanamke mwenye mafuta yaliyozidi,mwili wake huweza kuzalisha estrogen nyingi kipindi chochote cha Maisha yake sio tena baada ya kufikia ukomo wa hedhi. Hii ina maana kadri kiwango cha Mafuta kinapozidi mwilini ndivo kiwango cha estrogen huongezeka pia.

Matokeo yake,Estrogen ikizidi huathiri mzunguko wa hedhi na kuleta madhara kama vile;

  • Kuvuja damu nyingi ya Hedhi
  • Kukosa Hedhi
  • Hedhi kuchelewa kutoka
  • Au Hedhi kutokutoka kwa mpangilio

Hivo ukiwa na Uzito Mkubwa upo kwenye hatari hii,

FAHAMU,Kama Uzito wako wa mwili unapungua kupita kiasi kwa kasi sana upo kwenye hatari ya Kupata mabadiliko ya Hedhi Pia.

Estrojeni ni muhimu kwa ajili ya kujenga ukuta wa uterasi kwa mimba inayoweza kutokea wakati wa mzunguko wa hedhi. Unapopoteza uzito mwingi, mwili wako hautoi estrojeni ya kutosha.

3. Kuwa na Msongo wa Mawazo au Stress

Hali ya Stress inaweza kusababisha mabadiliko ya Hedhi ikiwemo hedhi kuchelewa kutoka,

Utafiti umeonyesha kuwa watu walio na viwango vya juu vya mfadhaiko,Msongo wa mawazo au Stress pia walikuwa wakipata vipindi visivyo kawaida vya HEDHI.

Wakati STRESS inaathiri muda wa hedhi, inaweza kuathiri uzazi Pia. Wale ambao wana Stress kwa kiwango kikubwa wanaweza kuwa na wakati mgumu zaidi wa kupata mimba au kuwa na ujauzito usio na matatizo.

4. Mabadiliko ya vichocheo au Hormones mwilini

Mfano kwenye tezi la thyroid—Homoni za tezi la Thyroid huwajibika kwa udhibiti wa nishati ya mwili wako na huathiri viungo vingi. Viwango vya homoni za tezi hili vinapokuwa juu au chini, utendaji wa mwili wako unaweza kubadilika—pamoja na utendajikazi wako wa mzunguko wa hedhi.

Kwa wale wanaozalisha kiwango kikubwa cha thyroid hormone— huweza kupata Hedhi karibu karibu , Na wale ambao hawazalishi thyroid hormone ya kutosha huweza kupata hedhi kwa kuchelewa au mara chache Zaidi

5. Kuwa kwenye Mazingira yenye Dawa za kuua wadudu,Exposure to Pesticides

Pesticides zinaweza kuwa na uhusiano wa karibu na mabadiliko ya Hedhi yaani irregular periods.

Washiriki wa utafiti mmoja walikuwa wamekabiliwa na dawa za kuulia wadudu kutokana na kufanya kazi kwenye mashamba, kuishi ndani yake, au vyote viwili.

Wengi walikabiliwa na viuatilifu vya kemikali vinavyovuruga mfumo wa endocrine, dawa ya kuua wadudu inayojulikana kusababisha mabadiliko ya hedhi. Washiriki waliripoti hitilafu katika urefu wa mzunguko wao na kutokuwepo kwa kipindi chao cha Hedhi kwa zaidi ya siku 90.

6. Unyonyeshaji

Ukichagua kunyonyesha mara kwa mara, kipindi chako cha Hedhi hakirudi mara moja. Hii inajulikana kama Lactational amenorrhea, Na hutokea baada ya mtu kujifungua na huongeza muda wa mtu kupata mimba tena. Kwa sababu hiyo, baadhi ya watu huitumia kama njia ya uzazi wa Mpango.

7. Umri

Kipindi chako cha Hedhi kinaweza kisiwe cha kueleweka hadi miaka yako inapofikia 20. Hata hivyo, unapokaribia kukoma hedhi, hedhi inaweza kuwa isiyo ya kawaida tena.

Ingawa labda unatarajia kupata Hedhi kidogo unapokaribia kukoma kwa hedhi, inaweza kutofautiana kulingana na wakati wake. Kwa mfano, hedhi yako inaweza kusimama kwa miezi michache kisha kurudi bila kutarajia.

Hizo ndyo baadhi ya Sababu za Kuchelewa kwa Hedhi…!!!!

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILINE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Hedhi ya muda mrefu au hedhi mfululizo chanzo chakeAfyaclass Forum •

Hedhi ya muda mrefu au hedhi mfululizo (inayodumu zaidi ya siku 7 au kurudi mara kwa mara bila kupumzika) mara nyingi ni ishara ya tatizo la kiafya. Sababu zake kuu ni:



Vyanzo vya hedhi ya muda mrefu/mfululizo

1. Mabadiliko ya homoni, au Tatizo la hormone imbalance

  • Upungufu wa homoni ya progesterone au ongezeko la estrogen huchangia ukuta wa mfuko wa uzazi kukua kupita kiasi na kutoka damu nyingi.
  • Mara nyingi hutokea kwa wasichana walio katika balehe au wanawake wanaokaribia kukoma hedhi.

2. Uvimbe na ukuaji usio wa kawaida

Hapa tunazungumzia matatizo mbali mbali kwenye kizazi kama vile;

  • Tatizo la Fibroids (uvimbe kwenye mfuko wa uzazi).
  • Polyps za kwenye kizazi.
  • Saratani ya mfuko wa uzazi au shingo ya kizazi.n.k

3. Magonjwa ya damu na matatizo ya kuganda kwa damu

Upungufu wa chembe sahani (platelets).

Magonjwa ya kurithi ya damu kama hemophilia.n.k. huweza pia kuchangia hali hii

4. Matumizi ya baadhi ya dawa,Mfano;

Vidonge vya uzazi wa mpango visivyotumika ipasavyo.

Dawa za kupunguza damu (anticoagulants).n.k.

5. Madhara ya baadhi ya Njia za uzazi wa mpango,kama vile;

  • Vidonge
  • Sindano n.k.

6. Maambukizi ya magonjwa mbali mbali

Mfano; Maambukizi ya bacteria kwenye via vya uzazi vya Mwanamke au (PID).n.k.

7. Sababu nyingine

Msongo wa mawazo, uzito mkubwa kupita kiasi au kupungua ghafla, matatizo ya tezi (thyroid disorders). n.k.

🔔 Tahadhari:
Hedhi ya muda mrefu au mfululizo huweza kusababisha upungufu wa damu (anemia) kwa haraka.

Ikiwa damu inatoka kwa wingi sana (unabadili pedi kila chini ya saa 1–2), unaona damu yenye mabonge makubwa, au unahisi kizunguzungu na kuchoka sana, unapaswa kumuona daktari haraka.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Jipu kwenye shavu la uke chanzo chake na TibaAfyaclass Forum •

Jipu kwenye shavu la uke chanzo chake na Tiba

Jipu kwenye shavu la uke (labia) mara nyingi hutokea kutokana na maambukizi ya bakteria yanayoingia kupitia ngozi au vinyweleo vidogo. Chanzo chake kinaweza kuwa:

  1. Folliculitis (maambukizi ya vinyweleo vya nywele) – nywele zinapoota baada ya kunyolewa au kung’olewa, zinaweza kusababisha maambukizi.
  2. Usafi duni au unyevu mwingi – uke ni eneo lenye joto na unyevu, hali inayowezesha bakteria kuzaliana.
  3. Kuvimba tezi za Bartholin – hizi tezi zipo kando ya uke, na zikiziba na kuambukizwa huweza kutoa jipu.
  4. Kuvua au kuvaa nguo za ndani zinazobana – msuguano husababisha michubuko midogo ambayo huingiza vijidudu.
  5. Kuwepo kwa bakteria aina ya Staphylococcus aureus – mara nyingi ndiyo husababisha majipu kwenye ngozi na sehemu za siri.
  6. Kingamwili za mwili zikiwa chini – mfano wagonjwa wa kisukari au wenye kinga dhaifu huwa na uwezekano mkubwa wa kupata majipu.

⚠️ Ikiwa jipu ni kubwa, linauma sana, linaendelea kuongezeka, au unapata homa, ni vyema kumuona daktari kwa uchunguzi na matibabu (ikiwemo antibiotics au kutoa usaha kitaalamu).

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Chanzo cha mwanamke kukosa hamu ya tendo la ndoaAfyaclass Forum •

Chanzo cha mwanamke kukosa hamu ya tendo la ndoa (au libido ya chini) kinaweza kuwa kutokana na sababu mbalimbali za kibaiolojia, kisaikolojia, au mazingira.



Hapa chini ni maelezo ya baadhi ya sababu kuu:

1. Sababu za Kisaikolojia na Kihisia

  • Msongo wa mawazo (stress): Majukumu mengi, matatizo ya kifamilia au ya kazi huathiri sana hisia za kimapenzi.
  • Tatizo la depression: Huondoa kabisa hamu ya mapenzi.
  • Kutokujiamini: Mwanamke anayejiona si mrembo au hana mvuto anaweza kukosa hamu.
  • Matatizo ya mahusiano: Kutokuelewana na mwenza, kutothaminiwa au kutotimiziwa mahitaji kihisia kunaweza kuzima hamu.
  • Matukio ya kihistoria kama unyanyasaji wa kingono: Hili huathiri sana hamu hata kama lilitokea zamani.

2. Sababu za Kimwili/Kibaiolojia

  • Homoni kubadilika:
    • Wakati wa ujauzito, baada ya kujifungua, au kipindi cha kukoma hedhi (menopause).
    • Upungufu wa homoni ya estrogen au testosterone.
  • Magonjwa:
    • Kisukari, shinikizo la damu, matatizo ya tezi (thyroid), saratani n.k.
  • Dawa:
    • Dawa za msongo wa mawazo (antidepressants), dawa za usingizi, dawa za presha n.k.
  • Maumivu wakati wa tendo (dyspareunia): Maumivu huchangia mwanamke kukwepa tendo.

3. Sababu za Kimazingira na Kijamii

  • Kuchoka sana (physical exhaustion): Kufanya kazi nyingi bila mapumziko.
  • Ukosefu wa faragha: Watoto kuwa chumbani au nyumba kuwa na watu wengi.
  • Mwenzi kutokuwa na usafi au kutokuwa mvutia.
  • Kutokuridhika na tendo la ndoa: Kama mwenza haridhishi au anajali mahitaji yake tu.

Ufumbuzi Unaoweza Kusaidia

  • Kufanya mawasiliano ya wazi na mwenza kuhusu hisia na matarajio.
  • Kupumzika vya kutosha na kupunguza msongo.
  • Kufanya mazoezi: Huchangamsha homoni na kuleta afya ya mwili na akili.
  • Kushauriana na daktari au mshauri wa ndoa/saikolojia, hasa kama ni tatizo sugu.
  • Kubadilisha dawa ikiwa tatizo lilianza baada ya kutumia dawa fulani (kwa ushauri wa daktari).
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comment

Hatari ya kutoa mimba,Fahamu hapa hatari kubwa ya kufanya hiviAfyaclass Forum •

Hatari ya kutoa mimba,Fahamu hapa hatari kubwa ya kufanya hivi.

Madhara ya kutoa mimba 

Wanawake wengi huanza kukutana na matatizo mengi baada ya kutoa Mimba ikiwemo;Kuvuja damu sana na kwa muda mrefu,Kupata maumivu ya tumbo mara kwa mara, tumbo kukaza n.k,Kupata shida ya kizunguzungu au hata kuzimia,Kupata kichefuchefu na kutapika n.k

Madhara ya kutoa mimba yanaweza kuwa ya muda mfupi au muda mrefu, na hutegemea sana:

  • Njia iliyotumika kutoa mimba (dawa au upasuaji).
  • Umri wa ujauzito ulipo.
  • Usalama wa mazingira ya utoaji mimba (kama ilifanyika kwa mtaalamu au kwa njia hatari).
  • Afya ya mama kabla ya kutoa mimba.

Madhara ya Muda Mfupi:

  1. Maumivu ya tumbo: Maumivu ya tumbo chini kutokana na mabadiliko ya mfuko wa uzazi.
  2. Kutokwa na damu nyingi: Hali hutokea wakati au baada ya mimba kutoka, na damu nyingi kupita kiasi ni hatari.
  3. Kuvuja damu kwa muda mrefu: Damu huweza kutoka kwa siku chache hadi wiki, lakini ikiwa zaidi ya hapo, ni dalili ya tatizo zaidi.
  4. Kuchoka, kizunguzungu na kupoteza nguvu: Kutokana na upotevu wa damu.
  5. Maambukizi (Infection): Hali hii hutokea kama sehemu ya uzazi haikusafishwa vizuri au vifaa vilivyotumika havikuwa safi.
  6. Kichefuchefu, kutapika, kuhara au homa: Mara nyingine hutokana na dawa za kutoa mimba au maambukizi.

Madhara ya Muda Mrefu:

  1. Matatizo ya hedhi: Mzunguko wa hedhi unaweza kubadilika au kukoma kwa muda mfupi baada ya kutoa mimba.
  2. Kupata maambukizi ya bacteria kwenye via vya uzazi (Pelvic Inflammatory Disease - PID): Maambukizi kwenye viungo vya uzazi yanaweza kusababisha ugumba.
  3. Matatizo ya kizazi: Maumivu ya kudumu kwenye nyonga, au makovu ndani ya mfuko wa uzazi (Asherman’s Syndrome) ambayo yanaweza kusababisha ugumba au mimba kutoka baadaye.
  4. Kutunga kwa mimba nje ya mfuko wa uzazi (Ectopic pregnancy): Hatari huongezeka ikiwa mtu alipata maambukizi baada ya kutoa mimba.
  5. Ugumba (Infertility): Mara chache sana, lakini mimba zilizoondolewa kwa njia isiyo salama zinaweza kuharibu uwezo wa kupata mimba tena.
  6. Msongo wa mawazo (Stress), huzuni, au majuto: Watu wengine hupitia hisia za huzuni au msongo wa mawazo baada ya kutoa mimba.

Madhara ya Kisaikolojia:

  • Huzuni ya muda mrefu.
  • Hatia au kujilaumu.
  • Msongo wa mawazo au wasiwasi.n.k.





Madhara ya kutoa mimba changa

Haya hapa ni Madhara ambayo huweza kutokea kwa Mtu kutoa Mimba;

1. Kuharibika kwa Kizazi au shingo ya kizazi(womb/cervix)

2. Kupata tatizo la kuvuja damu kupita kiasi

3. Mimba kutoka na kuacha mabaki mengine ndani(Incomplete abortion),

Hali hii ni ya hatari na inaweza kuleta madhara zaidi, hivo hatua za haraka ni muhimu,

Hii huweza kusababisha hata hatua kama (surgical abortion procedure) kufanyika.

4. Kupata maambukizi ya kizazi au mirija ya kizazi(uterus/fallopian tubes)

5. Kusababisha kovu au makovu ndani ya Kizazi

6. Kukuweka kwenye hatari Zaidi ya kupata maambukizi ya bacteria ambayo huingia moja kwa moja kwenye damu, na kisha kuleta madhara makubwa zaidi(Sepsis/Septic shock)

7. Kusababisha tatizo la kutoboka kwenye kizazi(Uterine perforation)

8. Utoaji Mimba Pia unaweza Kusababisha KIFO. n.k

Kwa Mujibu wa NCBI;

Zaidi ya asilimia 2% ya Wanaotoa Mimba hupata Matatizo kama vile;

  • Kupata Maumivu makali ya Tumbo
  • Kuvuja damu sana
  • Maambukizi ya magonjwa n.k

Utafiti wa NCBI unaendelea Kuonyesha; Na wengine hupata Madhara makubwa ikiwemo;

– Tatizo la misuli ya kizazi kushindwa kurudi mahali pake,tatizo ambalo kitaalam hujulikana kama uterine atony

– Kuvuja damu mvululizo(Subsequent hemorrhage)

– Kutoboka kwa Kizazi(uterine perforation),

– Kuumia kwa viungo vya karibu na kizazi kama vile; kibofu cha Mkojo au eneo la haja kubwa(injuries to adjacent organs (bladder or bowels),

– Kuchanika kwa mlango wa kizazi(cervical laceration),

– Mimba kushindwa kutoka, na kuleta madhara Zaidi(failed abortion),

– Kupata maambukizi hatari ya bacteria kwenye damu baada ya kutoa mimba( septic abortion)

– Kupata matatizo ya damu kuganda:disseminated intravascular coagulation.n.k

Kadri Mimba inavyokuwa kubwa Zaidi ndivyo hatari na madhara huongezeka Zaidi.

Maambukizi kwenye eneo la Via vya Uzazi(Pelvic Infection):

Bakteria (vijidudu) kutoka kwenye uke au mlango wa uzazi wanaweza kuingia kwenye uterasi na kusababisha maambukizi.

Matumizi ya Antibiotics yanaweza kusaidia kuondokana na maambukizi hayo.

Mimba kushindwa kutoka kabsa(Incomplete abortion):

Mabaki ya ujauzito kubaki ndani ya kizazi hali ambayo ni hatari Zaidi na huhitaji matibabu ya haraka.

Pia Utoaji mimba usio kamili unaweza kusababisha maambukizi na kutokwa na damu Zaidi.

Damu kuganda na kutengeneza Blood clots ndani ya kizazi:

Shida hii huweza kusababisha maumivu makali ya tumbo, lakini hatari zaidi ya kupoteza maisha, baada ya blood clots kusafiri kwenye damu mpaka kwenye mapafu na Kuziba.

Kuvuja damu kupita Kiasi:

Kutokwa na damu nyingi sio kawaida na kunaweza kusababisha madhara Zaidi.

Kuchanika kwa Mlango wa kizazi(cervix):

Kutoboka kwa kuta za kizazi(Perforation of the uterus wall:

Kifaa cha matibabu kinaweza kupitia ukuta wa uterasi na kutoa.Kwa Mujibu wa NCBI;

Kiwango kilichoripotiwa ni moja(1) kati ya kila utoaji mimba 500. Kulingana na ukali, utoboaji unaweza kusababisha maambukizi, kutokwa na damu nyingi au vyote viwili. Upasuaji unaweza kuhitajika ili kurekebisha tishu za uterasi, na katika hali mbaya zaidi kutoa kizazi chochote au hysterectomy inaweza kuhitajika.

Madhara Mengine ya Muda mrefu ya Kutoa Mimba ni pamoja na;

  • Mwanamke Kushindwa kubeba Mimba tena
  • kuwa kwenye hatari ya kupata Saratani za matiti,Ovari au kizazi(breast, ovarian and endometrial cancer).

Kupata madhara kisaikolojia(Emotional Side of an Abortion)

Unapaswa kujua kwamba wanawake hupata hisia tofauti baada ya kutoa mimba, Baadhi ya wanawake wanaweza kujisikia hatia, huzuni au kuwa na Msongo wa mawazo ambao hauishi baada ya kutoa Ujauzito,

wakati wengine wanaweza kuhisi utulivu kwamba utaratibu umekwisha. Baadhi ya wanawake wameripoti madhara makubwa ya kisaikolojia baada ya kutoa mimba, ikiwa ni pamoja na;

  • mfadhaiko,
  • huzuni,
  • wasiwasi,
  • kujidharau
  • majuto,
  • Woga
  • kurudi nyuma kwa kila kitu anchofanya
  • na kuingia kwenye matumizi mabaya ya dawa za kulevya.

Hisia hizi zinaweza kuonekana mara baada ya utoaji mimba au hatua kwa hatua kwa muda mrefu. Hisia hizi zinaweza kujirudia au kuhisiwa kuwa na nguvu zaidi wakati wa utoaji mimba mwingine, au kuzaa kwa kawaida, au siku ya kumbukumbu ya utoaji mimba.

Ushauri au usaidizi kabla na baada ya kutoa mimba ni muhimu sana. Ikiwa haupati msaada na utegemezo wa familia, huenda ikawa vigumu kwako kukabiliana na hisia zinazotokea baada ya kutoa mimba.

Kuzungumza na mshauri wa kitaalamu kabla ya kutoa mimba kunaweza kumsaidia mwanamke kuelewa vyema uamuzi wake na hisia anazoweza kupata baada ya utaratibu huu.

Ikiwa ushauri nasaha haupatikani kwa mwanamke, hisia hizi zinaweza kuwa ngumu zaidi kushughulikia. Vituo vingi vinavyohusika na kesi za ujauzito hutoa huduma za ushauri kabla na baada ya kutoa mimba.

0 Comment

Dalili za uvimbe kwenye kizazi pamoja na Chanzo chakeAfyaclass Forum •

UVIMBE KWENYE KIZAZI NI NINI?

Uvimbe kwenye Kizazi ambapo kwa Kitaalam Hujulikana kama "FIBROIDS"- ni aina ya Uvimbe ambao hutokea katika kuta za ndani za Mji wa mimba(Kizazi)au huweza kutokea katikati ya kuta za Mji wa mimba,hivo kuleta madhara mengi. 



Kuta hizo za Mji wa mimba au Uterus zimegawanyika katika Maeneo au sehemu kuu Tatu.

  1. Ukuta wa Ndani kabsa-ambao hujulikana kitaalam kama Endometrium
  2. Ukuta wa katikati-ambao kitaalam hujilikana kama Myometrium
  3. Na ukuta wa Nje ya Uzazi-ambao kitaalam hujulikana kama Perimetrium

Kumbuka; Uvimbe kwenye kizazi Huweza kutokea katika maeneo mbali mbali ya Kizazi Mfano;  

- Kuna Uvimbe unaoweza kutokea kwenye vifuko vya mayai

- Kuna uvimbe kwenye kuta za Mji wa Uzazi kama nilivyoelezea hapo mwanzoni

- Kuna uvimbe unaoweza kutokea kwenye Mirija ya Uzazi n.k.

CHANZO CHA UVIMBE KWENYE KIZAZI NI NINI?

Hakuna sababu ya Moja kwa moja ya mtu kupata Tatizo hili la Uvimbe wa kizazi,Japo kuna vitu ambavyo huweza kuongeza hatari ya mtu kupata Uvimbe huu wa kwenye Kizazi, Kama vile;

1. Mabadiliko ya Vichocheo muhimu mwilini,hasa vile vinavyohusika na Ukuaji wa seli hai za mwili kama vile progesterone,estrogen,n.k

2. Tatizo la Unene pamoja na Uzito kupita kiasi

3. Kuwa na historia ya Tatizo la Uvimbe wa Kizazi katika Familia yenu

4. Mabadiliko flani ya Kigenetic,Kitaalam hujulikana kama genetic mutations

5. Umri mkubwa, Mwanamke ambaye hajawahi kupata mtoto hadi kufikia umri mkubwa anaweza kuwa kwenye hatari hii pia

6. Mwanamke kuwahi Sana kupata Hedhi au tunasema Hedhi ya Mapema: Kuanza kupata hedhi katika umri mdogo kunaweza kuwa sababu ya hatari

7. Baadhi ya vyakula,Zipo tafiti mbali mbali ambazo huonyesha kwamba ulaji mwingi wa nyama nyekundu na pombe unaweza kuongeza hatari hii, ilhali ulaji mwingi wa matunda, mboga mboga, na nyuzinyuzi unaweza kuwa kinga kwa tatizo hili.

DALILI ZA TATIZO LA UVIMBE WA KIZAZI

Hizi hapa ni baadhi ya Dalili ambazo huweza Kujitokeza kwa mtu mwenye tatizo la Uvimbe kwenye kizazi;

  • Kutokwa na Damu nyingi ya Hedhi (Heavy menstrual bleeding)
  • Kupata period kwa muda mrefu bila kukata au kupata period katikati ya mwezi au mara kwa mara
  • Kupata Maumivu makali ya Tumbo wakati wa Hedhi
  • Kupata maumivu makali ya Tumbo na Kiuno hasa wakati wa Tendo la Ndoa
  • Kutokwa na Uchafu mwingi ukeni na wakati mwingine huambatana na harufu kali sehemu za Siri,hasa hasa kama uvimbe umeziba mirija ya Uzazi(fallopian Tubes)
  • Kutokwa na Damu wakati wa tendo la Ndoa
  • mvurugiko wa Mpangilio wa siku za Hedhi.
  • Lakini pia Uvimbe ukiwa Mkubwa sana huweza kuleta dalili kama;Kukojoa mara kwa mara,kwani nafasi kubwa ya uvimbe husababisha mgandamizo wa kibofu cha Mkojo, Kupata Choo kigumu sana,hata kukuletea maumivu makali sehemu ya Haja kubwa pamoja na Michubuko

MADHARA YA KUWA NA TATIZO LA UVIMBE WA KIZAZI 

1. Maumivu makali wakati wa Hedhi na wakati wa Tendo la Ndoa

2. Kutokwa na Uchafu mwingi ukeni na wenye harufu mbaya

3. kutolewa kizazi chote wakati wa matibabu kama uvimbe umeathiri sehemu kubwa ya Kizazi

4. Tatizo la kushindwa kubeba Ujauzito

5. Mvurugiko wa siku za Hedhi,ikiwemo kupata hedhi katikati ya mwezi

MATIBABU YA UVIMBE WA KIZAZI 

Kama una tatizo la Uvimbe kwenye kizazi Wasiliana na wataalam wa afya, Kuna dawa za kusaidia Uvimbe huu kuisha, Lakini pia endapo tatizo litashindikana,Njia ya mwisho kabsa ni kufanyiwa Upasuaji na Uvimbe huo kutolewa kabsa.

KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Ugonjwa wa ovarian cyst,chanzo,dalili na Tiba yakeAfyaclass Forum •

Ugonjwa wa ovarian cyst,chanzo,dalili na Tiba yake







Ovarian Cyst: Chanzo, Dalili na Tiba yake

Ovarian Cyst ni nini?

Ovarian cyst ni uvimbe maji (au mara chache, unajazwa na vitu vingine) unaotokea ndani au juu ya ovari ya mwanamke. Aina nyingi za ovarian cyst ni salama (si za Saratani) na huondoka zenyewe bila matibabu. Hata hivyo, baadhi ya cyst zinaweza kusababisha dalili na kuhitaji uangalizi wa kitabibu.

Chanzo cha Ovarian Cyst

Sababu kuu ya kutokea kwa ovarian cyst ni mzunguko wa kawaida wa hedhi. Cyst hizi huitwa “functional cysts” na ni pamoja na:

  • Follicular cysts: Hutokea wakati yai halitoki kwenye mfuko wake (follicle) wakati wa ovulation.
  • Corpus luteum cysts: Hutokea baada ya yai kutoka, ambapo follicle inajifunga na kujazwa na majimaji.

Sababu nyingine ni:

  • Polycystic Ovary Syndrome (PCOS): Hali ya homoni inayosababisha uwepo wa cyst nyingi ndogo katika ovari.
  • Endometriosis: Tishu zinazofanana na zile za ndani ya mfuko wa uzazi hukua nje ya uterus na zinaweza kuathiri ovari.
  • Maambukizi ya nyonga (pelvic infections): Maambukizi makali yanaweza kufika kwenye ovari na kusababisha cyst.

Dalili za Ovarian Cyst

Ovarian cyst nyingi hazina dalili. endapo zitajitokeza,dalili zinaweza kujumuisha:

  • Maumivu ya nyonga au presha upande mmoja wa tumbo
  • Kuvimba au kuhisi tumbo limejaa
  • Maumivu wakati wa tendo la ndoa
  • Maumivu wakati wa hedhi au mzunguko wa hedhi usio wa kawaida
  • Haja ya kukojoa mara kwa mara au ugumu wa kutoa mkojo
  • Maumivu ya mgongo Sehemu ya chini
  • Kichefuchefu au kutapika (hasa iwapo cyst imepasuka)
  • Maumivu makali ya ghafla tumboni (huashiria cyst imepasuka au imesokoteka – hali ya dharura)

Vipimo vya Utambuzi

Madaktari wanaweza kugundua ovarian cyst kwa:

  • Uchunguzi wa nyonga (pelvic exam)
  • Ultrasound: Kuangalia ukubwa, umbo, na muundo wa cyst
  • Vipimo vya damu: Mfano CA-125, hasa kwa wanawake walioanza kupata hedhi ili kuchunguza uwezekano wa saratani
  • Laparoscopy: Upasuaji mdogo kwa kutumia kamera kuangalia na wakati mwingine kuondoa cyst

Matibabu ya Ovarian Cyst

Matibabu yanategemea ukubwa, aina, na dalili za cyst:

  1. Kusubiri kwa uangalizi: Cyst nyingi, hasa zile za kawaida, huondoka zenyewe ndani ya miezi michache.
  2. Dawa za homoni: Husaidia kuzuia kutokea kwa cyst mpya kwa kudhibiti mzunguko wa hedhi.
  3. Upasuaji: Unahitajika iwapo cyst ni kubwa, haiondoki, au ina dalili. Upasuaji unaweza kuwa:
    • Cystectomy: Kuondoa cyst pekee bila kuathiri ovari
    • Oophorectomy: Kuondoa ovari nzima iwapo ni lazima
    • Mara nyingi hufanyika kwa njia ya laparoscopy (upasuaji mdogo)

Wakati wa Kumwona Daktari

Wasiliana na daktari mara moja endapo utapata:

  • Maumivu makali ya ghafla ya nyonga au tumbo
  • Maumivu yanayoambatana na homa au kutapika
  • Dalili za mshtuko (shinikizo la damu kushuka, kuhisi baridi, mapigo ya moyo kwenda mbio, au kizunguzungu)

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Vyanzo vilivyotumika:

  • Mayo Clinic – Ovarian Cysts
  • Cleveland Clinic – Ovarian Cysts
  • Johns Hopkins Medicine – Ovarian Cysts

0 Comment

Sababu za Kukosa Hedhi kwa MwanamkeAfyaclass Forum •

Sababu za Kukosa Hedhi kwa Mwanamke



TATIZO LA MWANAMKE KUKOSA SIKU ZAKE ZA HEDHI

Tatizo hili la Mwanamke kukosa siku zake za hedhi kwa kitaalam hujulikana kama Amenorrhea,

ambapo huweza kutokea mara moja au zaidi, kwenye Kukosa hedhi kuna Vitu viwili; tuna Primary na Secondary amenorrhea

(1) Primary amenorrhea,Hii inahusu kutokuwepo kwa hedhi kwa Mwanamke ambaye hajapata hedhi kufikia umri wa miaka 15.

Sababu za kawaida za aina hii ya kukosa hedhi ni pamoja na viwango vya homoni, ingawa matatizo ya Kimaumbile pia yanaweza kusababisha shida hii.

(2) Secondary Amenorrhea,Hii inahusu Mwanamke kukosa hedhi ndani ya vipindi vitatu au zaidi mfululizo kwa mwanamke ambaye amekuwa akipata hedhi hapo awali.

Mimba ndio sababu ya kawaida ya kukosa hedhi hii kwenye secondary amenorrhea, ingawa matatizo ya homoni pia yanaweza kusababisha shida hii.

KUMBUKA,Kwa Upande wa Tiba,Matibabu ya tatizo la Kukosa hedhi yanategemea na chanzo husika.

Moja ya vitu ambavyo wanawake wengi hupata shida sana ni pale ambapo hawaoni siku zao za hedhi,

katika makala hii tumechambua baadhi ya sababu ambazo huweza kusababisha Mwanamke kutokupata siku zake za hedhi(Miss period).

BAADHI YA SABABU HIZO NI KAMA VILE;

1. Ujauzito, Hii ndyo sababu kubwa ambayo husababisha Wanawake Wengi kutokuona siku zao za hedhi,

ndyo maana wanawake wengi wasipoona siku zao za hedhi,kitu cha kwanza ambacho wanawaza ni MIMBA.

2. Tatizo la Stress, Wanawake wengi hawajui ukiwa na msongo wa mawazo au STRESS, inaweza kuvuruga kabsa mzunguko wako wa hedhi,

Stress huweza kusababisha Mwanamke kublid kwa muda mrefu, kuzidisha maumivu wakati wa hedhi,kublid kwa muda mfupi sana kuliko kawaida, au kutokuona kabsa siku zake za hedhi.

3. Kupungua uzito wa mwili kwa gafla(Sudden weight loss), Fahamu kwamba kupungua uzito wa mwili kwa kiasi kikubwa sana au kwa gafla huweza kusababisha Mwanamke kutokuona siku zake za hedhi,

Hii ni kwasababu ya kuzuiwa kwa uzalishwaji wa hormones au vichocheo ambavyo huhitajika kwa ajili ya kitendo cha Ovulation.

4. Kuwa na uzito mkubwa kuliko inavyotakiwa(overweight/obesity), ukiwa na shida hii ya uzito mkubwa huweza kusababisha mwili wako kuzalisha kiwango kikubwa sana cha vichocheo vya OESTROGEN,

Uzalishwaji mwingi wa Hormone hii huweza kuathiri mzunguko wako wa hedhi ikiwemo na kuchangia Mwanamke kutokuona siku zake za hedhi.

5. Mwanamke kufanya mazoezi ya mwili kupita kiasi, ukiwa unafanya mazoezi kwa kiasi kikubwa sana huweza kuathiri hormones zinazohusika na kurekebisha mzunguko wako wa hedhi ikiwa ni pamoja na kukosa siku za hedhi hasa pale ambapo mwili hupoteza kiasi kikubwa cha mafuta(body fat) wakati wa mazoezi.

6. Matumizi ya njia mbali mbali za uzazi wa mpango, Wanawake wengi wanaotumia njia za uzazi wa mpango kama vile vidonge, vijiti,Sindano n.k huweza kukosa siku zao za hedhi kama ilivyokawaida.

Ingawa siku zako za hedhi hutakiwa kurudi kwenye hali yake yakawaida baada ya kuacha kutumia njia hizi.

7. Mwanamke kufikia kipindi cha ukomo wa hedhi yaani Menopause, Mwanamke anapokaribia ukomo wa hedhi,huanza kutokuona siku zake za hedhi,

Hii ni kwasababu kiwango cha Oestrogen huanza kupungua sana na mzunguko wa hedhi huanza kutokueleweka kabsa, kitendo cha Ovulation hakifanyiki tena Na hapa ndipo hufata hali hii ya mwanake kukosa kabsa siku zake za hedhi,

8. Sababu zingine ni matatizo kama vile; Tatizo la Polycystic ovary syndrome (PCOS), na wakati mwingine matatizo kama

• Magonjwa ya moyo

• Kuwa na ugonjwa wa kisukari ambao haujadhibitiwa(uncontrolled diabetes)

• Shida ya Overactive thyroid n.k

DALILI ZA AMENORRHEA

Dalili Za Tatizo hili la Kukosa Hedhi(Amenorrhea)

Kulingana na sababu ya amenorrhea, unaweza kupata ishara au dalili zingine pamoja na kutokuwepo kwa hedhi, kama vile:

• Kutokwa na maziwa kwenye chuchu

• Kupoteza nywele

• Kupata Maumivu ya kichwa

• Mabadiliko kwenye kuona

• Kuwa na Nywele nyingi usoni

• Kupata Maumivu ya nyonga

• Kuwa na Chunusi n.k

MADHARA YA TATIZO HILI LA KUKOSA HEDHI,

Je kuna madhara yoyote ya kukosa hedhi, Ndyo kulingana na chanzo cha kukosa Hedhi

Tatizo la kukosa hedhi linaweza kusababisha matatizo mengine pia,Ikiwa ni pamoja na:

1. Mwanamke kushindwa kubeba Mimba,

Ikiwa hupati ovulation na hupati hedhi, huwezi kuwa mjamzito,

Wakati mwingine tatizo la kukosa hedhi hutokana na shida kwenye vichocheo mwilini,Kutokuwa na Usawa wa vichocheo mwilini(hormones imbalance),

Hii huweza kusababisha hata Usibebe Ujauzito

2. Pia inaweza kusababisha kuharibika kwa mimba au matatizo mengine wakati wa ujauzito.

3. Matatizo ya kisaikolojia, Mwanamke kukosa hedhi wakati wenzako wanapata huweza kusababisha hali ya mfadhaiko,msongo wa mawazo n.k, haswa kwa vijana ambao wanabadilika kuwa watu wazima.

4.Kupatwa na matatizo mengine kama vile Osteoporosis na ugonjwa wa moyo(cardiovascular disease),

Matatizo haya mawili yanaweza kusababishwa na kutokuwa na kiwango cha estrogen ya kutosha.

Osteoporosis ni tatizo linalohusisha kudhoofika kwa mifupa,

cardiovascular disease ni ugonjwa wa moyo ambao huweza kuleta shida kwenye mishipa ya damu na misuli ya moyo.

5. Kupata Maumivu ya nyonga. Ikiwa tatizo la Kimaumbile linasababisha amenorrhea,

Hii inaweza pia kusababisha maumivu katika eneo la nyonga(Pelvic).

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comment

Tatizo la harufu mbaya ukeni,sababu na tiba yakeAfyaclass Forum •

Tatizo la harufu mbaya ukeni,sababu na tiba yake

Harufu mbaya ukeni ni mojawapo ya matatizo ya kawaida yanayowakumba wanawake wengi, na mara nyingi husababisha wasiwasi au aibu. Ingawa mara nyingine harufu ya uke ni ya kawaida kutokana na mabadiliko ya homoni au shughuli za kila siku, harufu mbaya inayodumu au inayosababisha usumbufu ni dalili ya tatizo linalohitaji kufanyiwa uchunguzi na matibabu.

SABABU ZA HARUFU MBAYA UKENI

1. Bacterial Vaginosis (BV)

Hili ni tatizo linalosababishwa na kukosekana kwa usawa kati ya bakteria wazuri na wabaya ukeni. BV ni chanzo kikuu cha harufu ya samaki ukeni. Dalili nyingine ni pamoja na:

  • Kutokwa na majimaji meupe au ya kijivu.
  • Kuwashwa au kuungua kidogo.

2. Maambukizi ya fangasi (Yeast Infection)

Ingawa kawaida fangasi haisababishi harufu kali, maambukizi makali yanaweza kubadilisha hali ya kawaida ya uke. Dalili ni:

  • Kutokwa na majimaji mazito meupe au uchafu kama maziwa mtindi
  • Kuwashwa sana ukeni na wekundu.
  • Uke kuwa na harufu isiyo ya kawaida.

3. Trichomoniasis

Ni ugonjwa wa Zinaa (STI) unaosababishwa na protozoa aitwaye Trichomonas vaginalis. Dalili zake ni:

  • Harufu kali na mbaya.
  • Majimaji ya kijani au ya njano.
  • Maumivu wakati wa kukojoa au kujamiiana.

4. Kuvuja kwa mkojo au kinyesi

Wakati mwingine, matatizo ya nyonga au kibofu yanaweza kusababisha mkojo au kinyesi kuvujia ukeni, na hivyo kutoa harufu mbaya. Mfano kwa Mtu mwenye tatizo la Fistula.

5. Matumizi ya sabuni zenye kemikali kali au dawa za kuosha uke (douching)

Douching huondoa bakteria wa asili wanaolinda uke, na hivyo kusababisha kutokuwa na usawa wa bakteria ukeni na hatimaye harufu mbaya.

6. Kujisafisha vibaya

Kutokuosha vizuri sehemu za siri, au kuvaa chupi zisizopitisha hewa, husababisha bakteria kukua haraka na kutoa harufu mbaya.

7. Kuingia kwa kitu ukeni (kama tampon iliyosahaulika)

Tampon au kondomu iliyosahaulika ndani ya uke inaweza kuoza na kutoa harufu mbaya sana.

8. Mabadiliko ya homoni (kama vile kipindi cha hedhi au ujauzito)

Mabadiliko haya huathiri muundo wa majimaji ukeni na pH, na kusababisha harufu tofauti au isiyo ya kawaida.

MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA KUEPUKA HARUFU MBAYA UKENI

  • Jisafishe kwa maji safi tu, epuka sabuni zenye manukato.
  • Vaa nguo za ndani za pamba zinazoruhusu hewa kupita.
  • Badilisha pedi au tampon mara kwa mara.
  • Epuka douching au kuweka vitu visivyo vya lazima ukeni.
  • Tumia kondomu kujikinga dhidi ya maambukizi ya magonjwa ya Zinaa.
  • Tembelea daktari wa wanawake (gynaecologist) kwa uchunguzi pale unapohisi harufu isiyo ya kawaida.

HITIMISHO

Harufu mbaya ukeni si jambo la kawaida kama ikidumu au kuwa kali. Ni dalili ya kuwa kuna tatizo la kiafya linalopaswa kushughulikiwa. Kujua chanzo ni hatua ya kwanza kuelekea matibabu sahihi. Usione haya kutafuta msaada wa kitabibu — afya yako ni muhimu.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Madhara ya p2,haya ni madhara ya matumizi ya Vidonge vya P2Afyaclass Forum •

Madhara ya p2,haya ni madhara ya matumizi ya Vidonge vya P2


Madhara baada ya kutumia p2,Fahamu hapa

Fahamu P2 ni dawa ya dharura yaani kwa kitaalam hujulikana kama emergency contraceptive pill, dawa hii inazuia mtu asipate Mimba kwenye mazingira ambayo umefanya mapenzi pasipo kupanga na upo siku za hatari,au umelazimishwa kufanya mapenzi au umebakwa,ili kuzuia mimba zisizotarajiwa unalazima Kunywa hizi dawa.

Ukweli ni kwamba dose ya hormones ndani ya p2 ni kubwa kuliko vidonge vya kawaida vya Uzazi(birth control pills) kitu ambacho kinaifanya isifae kwa Matumizi ya kila siku,

Hii husababisha madhara Zaidi kwa Mtu mwenye mazoea ya kuzitumia mara kwa mara. Na moja ya madhara ni mzunguko wako wa hedhi kuathiriwa sana – Periods yako inaweza isitoke kama kawaida, inaweza kuwa nyingi,zito sana,isiyoeleweka(Irregular bleeding) n.k.

Pia baadhi ya Wanawake huongezeka uzito, Hivo basi P2 haishauriwi kabsa kwa matumizi ya kila siku au kutumia kama njia ya uzazi wa mpango ya muda mrefu.

Madhara baada ya kutumia p2,

Haya ni baadhi ya Madhara au matokeo baada ya kutumia p2(emergency contraceptive pills):

  • Kupata kichefuchefu
  • Kutapika
  • Mwili kuchoka Sana
  • Kupata kizunguzungu
  • Kupata maumivu ya kichwa
  • Kupata maunivu ya tumbo
  • Maziwa kuuma au kuvuta zaidi
  • Kubadilika kwa hedhi yako ya kawaida,ikiwemo kuvuja damu nyingi au kwa muda mrefu,au kuvuja katikati ya mzunguko n.k

Kutokwa na Vitone vya damu mara kwa mara(spotting) – Unaweza kupata vitone vya damu ndani ya wiki ijayo baada ya kumeza kidonge cha dharura cha kuzuia mimba yaani P2,

Pia, hedhi yako inayofuata inaweza kuwa nyepesi au nzito, ikawahi kutoka mapema au kuchelewa kuliko kawaida. Hakikisha unapata Msaada wa Tiba ikiwa unakutana na changamoto hizi.

Mzunguko wa hedhi usio wa kawaida(Irregular menstrual cycle) – Kwa sababu ya tembe za dharura za kuzuia mimba(p2), kipindi chako cha hedhi kinaweza kufika mapema au kuchelewa, jambo ambalo hutokea sana kwa wanawake wanaotumia vidonge hivi. Hata hivyo, unapaswa kufanya kipimo cha ujauzito ikiwa hupati kipindi chako cha hedhi ndani ya wiki mbili za tarehe inayotarajiwa.

MADHARA YA KUTUMIA P2

P2 Ni Dawa iliyotengenezwa kutumiwa mara chache tu,inapokulazimu.Sio dawa unayotakiwa kutumia kama njia ya uzazi wa mpango ya muda mrefu. Kuna wanawake humeza p2 kila mwezi,hii haitakiwi. Katika mazingira ya kawaida,haipaswi kumezwa zaidi ya mara 3 kwa mwaka. Kuendekeza kila mwezi kunywa hizi p2 sio sahihi,Unatakiwa ende hospitali ili upate njia sahihi ya uzazi wa mpango ya muda mrefu.

Baadhi ya Side effects/madhara ni ya matumizi holela ya dawa hizi ni

1.Unaweza kujisikia kichefuchefu au kutapika baada ya kumeza,

2.Maumivu ya tumbo

3.Matiti kuuma na kujaa

4.Pia hedhi zako zinazofuata zinaweza zikawahi au zikachelewa au zikatoka nyingi sana( ukiona zimezidi siku 8 fika muone daktari) au ukawa unapata hedhi nyepesi sana,au pia haupati hedhi kabisa (amenorhoea)

5.Kichwa kuuma na kizunguzungu

6.Mabadiliko ya Ute ukeni (change in cervical secretion,hapa unakuta Ute wa ovulation mtu hapati).

7.Kupata maambukizi ukeni,vaginal infections

8.Hatari ya kupata PID

9.Maumivu wakati wa sex(dyspareunia)

10.Mama anakuwa hatarini kutungisha mimba nje ya kizazi yaani ectopic pregnancy.

11.Lakini pia kuna wanawake hupata Ovarian cyst,vivimbe kwenye mfuko wa mayai.

Kuna sababu hapo juu kama PID,kutopata UTE,infections kwenye uke hizi zinakuja athiri mwanamke anakuwa anapata taabu kwenye Kupata mimba

Kama hujapanga kupata mimba,tafadhari fuata njia ya uzazi wa mpango ya muda mrefu inayokufaa,achana na kumeza p2 kila mwezi.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Chanzo Cha Tatizo La Uke Kujamba Pamoja Na Tiba YakeAfyaclass Forum •

Chanzo Cha Tatizo La Uke Kujamba Pamoja Na Tiba Yake

Baada ya tafiti mbali mbali kufanyika imeonekana baadhi ya sababu mbali mbali huchangia shida ya uke kujamba,hasa wakati wa kufanya mapenzi, na sababu hizo ni kama;

- Kulegea kwa misuli ya uke,hivo kupelekea uke kuwa wazi  mara nyingi na kuruhusu hewa kuingia na kujaa ukeni. Hivo kusababisha uke kujamba.

- Kuosha uke kwa maji ya moto mara kwa mara pia huchangia hali ya uke kujamba kwani huchangia misuli ya uke kulegea na kusababisha uke kuwa wazi na kusababisha hewa kujaa ukeni.

- Kulala hivo hivo mara tu baada ya kufanya mapenzi bila kujisafisha ukeni, hali hii  huathiri joto la ndani ya uke na kupelekea shida mbali mbali kama hii ya uke kujamba.

Soma: Tatizo la Uke Kulegea,chanzo,dalili na Tiba yake

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Tatizo la Uke kutoa hewa au Uke Kujamba ni tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama Vaginal flatulence,vaginal flatus, au queef,

Hali hii ni utoaji wa hewa iliyonaswa kutoka kwenye uke.  Kujaa gesi kwenye uke ni jambo la kawaida kwa Wanawake wengi, Na Mara nyingi hutokea wakati wa kufanya Tendo la Ndoa au mazoezi. Kwa kiasi kikubwa, hali hii haina Athari yoyote kwenye afya ya Uzazi.

Dalili za Tatizo hili la Uke Kujamba au Uke kutoa Hewa

-Dalili kubwa ya Uke kutoa hewa ni Kujamba Ukeni,mithili ya Mtu ambaye amejamba kwa njia ya haja kubwa,

Hivo mtu mwenye hali hii huweza kusikia Sauti ya Kijambo Ukeni,kama unavyojamba kawaida.

-Tofauti na Kujamba Kwa kawaida,Kujamba Ukeni hakutoi harufu yoyote mbaya kwa Asilimia kubwa, labda kama una tatizo Lingine la Kiafya.

Hizi ni baadhi ya Dalili za Tatizo hili la Uke Kujamba au Uke kutoa Hewa.

Sababu Zingine za Uke Kutoa hewa au Uke kujamba

Hizi hapa ni baadhi ya Sababu hizo pamoja na Vitu ambavyo huongeza hatari ya Mwanamke kutoa hewa Ukeni;

• Aina za Staili ya Kujamiiana au Kuingiza Kitu kwenye Uke, Kitu kinapoingizwa kwenye uke, kinaweza kusababisha hewa kuingia ndani ya Uke.

• Pia Inawezekana gesi kuingia Ukeni wakati wa uchunguzi wa fupanyonga, wakati daktari anapoingiza au kuondoa kifaa kama speculum.

• Aina ya Mazoezi na jinsi unavyofanya Mazoezi vinaweza kusababisha hewa kunasa ndani ya uke. 

 Wanawake mara nyingi huripoti gesi Ukeni wakati wa shughuli fulani za kimwili, kama vile kufanya mazoezi aina ya yoga. n.k

• Ujauzito au Kukoma kwa Hedhi,

 Baadhi ya wanawake huripoti matukio zaidi ya kujaa gesi ukeni wakati wa ujauzito au kukoma hedhi.

• Baada ya Kujifungua, 

Wanawake wengi pia huripoti shida hii ya kujamba Ukeni au kutoa hewa Ukeni baada ya kujifungua kwa Njia ya Kawaida.

Kuzaa mtoto na hali zingine zinazoweka shinikizo kwenye tishu za fupanyonga zinaweza kusababisha hili.

• Muundo au Anatomia ya Sakafu ya Pelvic,

Sakafu ya fupanyonga ya kila mtu ni ya kipekee kidogo, na kwa baadhi ya Wanawake inaweza kuwa rahisi zaidi kuliko wengine kutoa hewa iliyonaswa.

• Pia mara chache tatizo la kujaa hewa kwenye uke huhusishwa na fistula ya ukeni,

Fistula ni tundu au mwanya usio wa kawaida unaounganisha uke na kiungo kingine, kama vile kibofu cha mkojo, koloni, au rektamu. 

 Ikiwa fistula imeunganishwa na koloni au rectum, inaweza kusababisha mkusanyiko wa kinyesi kutoka kwa njia ya uke.  

Kuzaa, matibabu ya saratani, kuumia, na taratibu fulani za upasuaji zinaweza kusababisha kuundwa kwa fistula. Mwone daktari wako ikiwa kujamba kwako Ukeni au Hewa inayotoka ukeni ina harufu mbaya, au ukigundua inaambatana na kutokwa kwa maji yasiyo ya kawaida Ukeni.

Jinsi ya Kugundua tatizo la Uke kujamba(Diagnosis of Vaginal Flatulence)

Ingawa hakuna vipimo maalum au taratibu za kubainisha chanzo cha hewa kutoka kwa uke, daktari wako anaweza kufanya uchunguzi wa pelvic ili kudhibiti ikiwa kuna tatizo kubwa zaidi.

Hivo unaweza kufanyiwa na aina zingine za Vipimo kulingana na dalili ulizonazo kwa wakati huo.

Matibabu ya Tatizo hili la Uke Kujamba au Uke kutoa Hewa

Matibabu yake asilimia 100% hutegemea na chanzo husika, Hivo baada ya kugundua chanzo utapewa Tiba Sahihi.

Zipo dawa pamoja na Vitu vya Kufanya na Kuzingatia ili kukusaidia hali hii kuisha

NA KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Hakikisha Unapata Msaada mapema ikiwa Tatizo hili la Uke Kujamba au Uke kutoa Hewa linaambatana na matatizo Kama haya;

  • Kutoa harufu mbaya Ukeni
  • Kutokwa na Usaha au uchafu mwingine Ukeni
  • Kutokwa na kinyesi Ukeni
  • Unapata maumivu ukeni
  • Unahisi muwasho mkali
  • Unaumia Ukeni,kwenye mashavu ya uke au wakati wa kujamiiana
  • Unapata maambukizi ya mara kwa mara ya UTI au maambukizi Ukeni

Jinsi ya Kuzuia Tatizo hili la Uke Kujamba au Uke kutoa Hewa

Mara nyingi hakuna njia za moja kwa moja za kuzuia hali hii Lakini unaweza kuzingatia baadhi ya mambo;Epuka staili za Mapenzi ambazo hujaza hewa nyingi Ukeni n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.


0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Forum Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Forum ASANTE.
UNDERSTOOD