Vilabu vya Simba na Yanga vyapigwa faini, Yanga faini ya Tsh. milioni 5,Simba SC faini ya Tsh. milioni 1

#1

Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji ya Bodi ya Ligi Kuu Soka Tanzania imevitoza faini Vilabu vya Simba na Yanga kwa kufanya makosa kadhaa katika mchezo dhidi yao uliyochezwa Novemba 5 2023 na Yanga kushinda 5-1.

Kamati hiyo imeipiga Yanga faini ya Tsh. milioni 5 kwa kosa la kuingia uwanjani kwa kutumia mlango sio rasmi kuelekea mchezo huo uliochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa.

Klabu ya Simba SC imetozwa faini ya Tsh. milioni 1 kwa kosa la Wachezaji wake kuchelewa kutoka vyumbani na kupelekea mchezo huo kuchelewa kuanza kwa takribani dakika 4 kutoka vyumba vya kubadilishia nguo na kupelekea kuharibu program za mrushaji matangazo (Azam TV).

Consultation ya Afya Moja kwa Moja

Mimi ni Dr. Ombeni Mkumbwa. Nakupa ushauri wa kitaalamu kuhusu tatizo lolote la kiafya kwa siri, haraka na uhakika.

WhatsApp

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code