TANZIA:Ali Hassan mwinyi afariki duniaAfyaclass Bongo Social •

TANZIA:Ali Hassan mwinyi afariki dunia,

Raisi Mstaafu awamu ya Pili Mzee Ali Hasani mwinyi afariki Dunia.

Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi afariki dunia leo Alhamisi Februari 29,2024. Tangazo la kifo chake Limetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 98.

Mzee Ally Hassan Mwinyi amefariki Dunia leo Februry 29,2024 saa 11:30 jioni Hospitalini Jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa saratani ya mapafu.

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza msiba huo leo ambapo amesema Mzee Mwinyi ambaye alikuwa Rais kuanzia mwaka 1985 hadi 1995, amekuwa akipatiwa matibabu tangu November 2023 London Uingereza na baadaye kurejea Nchini na kuendelea na matibabu Jijini Dar es salaam.

Rais Samia ametangaza siku saba za maombolezo kuanzia kesho kufuatia kifo hicho.

Ali Hassan Mwinyi (8 Mei 1925-29 February 2024) alikuwa Rais wa pili wa Tanzania kuanzia mwaka 1985 hadi 1995.

Aliyemtangulia ni Mwalimu Julius Nyerere, na aliyemfuata ni Benjamin Mkapa. Pia alikuwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanzia mwaka 1990 hadi 1996.

Ali Hassan Mwinyi alizaliwa Mei 8, 1925 Kivure mkoani Pwani. Alikuwa rais wa pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia 1985 – 1995. Aliwahi pia kuwa rais wa Zanzibar, makamu wa rais na waziri wa Mambo ya ndani.

0 Comment

Jinsi ambavyo Seli za Saratani hujificha zisishambuliwe na Kinga yako ya MwiliAfyaclass Bongo Social •

Jinsi ambavyo Seli za Saratani hujificha zisishambuliwe na Kinga yako ya Mwili

“Seli za saratani ya utumbo mpana(colon cancer) zikiwa katika hatua za mwanzo hutumia mikakati maalum ya kukwepa mashambulizi ya kinga ya mwili na kupelekea kuwa tumors kubwa,

Hii ni kutokana na utafiti uliofanywa na “the Massachusetts Institute of Technology and the Dana-Farber Cancer Institute”.

Katika kiwango kikubwa, saratani ni kile kinachotokea wakati mgawanyiko wa seli unapotokea na seli kukua bila kudhibitiwa.

Moja ya kazi ya mfumo wa kinga ya mwili ni kutambua na kuondoa seli hizi zisizo za kawaida kabla hazijaongezeka sana,

Jambo kubwa hapa ni;Kutambua mahali ambapo mfumo wa kinga unadhoofika katika kushughulikia seli za saratani, kwa hivyo, ni moja wapo ya maeneo muhimu ya utafiti kwa matibabu ya saratani na moja ya shabaha kubwa ya dawa za saratani.

Maelezo kutoka kwa utafiti wa saratani na mfumo wa kinga katika Kuangalia tumors za saratani ya koloni/utumbo mpana zilizopandikizwa kwenye panya, watafiti walipata seli za saratani hii ikiwa katika hatua za mwanzo zinazozalishwa na kuamsha jeni inayoitwa SOX17, ambayo husaidia kuficha seli hizi kutoka kwa mfumo wa kinga ya mwili.

Aidha, walisema uanzishaji wa SOX17 unahakikisha seli zitazalisha molekuli chache zinazoitwa MHC protini, ambazo ni protini zinazohakikisha antijeni zinazohusiana na saratani zinaonekana kwenye mfumo wa kinga.

SOX17 pia inaweza kusimamisha utengenezaji wa vipokezi muhimu ambavyo vitaelekeza mfumo wa kinga kuagiza seli hizi za saratani kujiangamiza.

“Uanzishaji wa mpango wa SOX17 katika mwanzo wa kukua kwa saratani ya colorectal ni hatua muhimu ambayo hulinda seli za saratani kutoka kwenye mfumo wa kinga.

Ikiwa tunaweza kuzuia mpango wa SOX17, tunaweza kuwa na uwezo bora wa kuzuia saratani ya koloni, haswa kwa wagonjwa ambao wana uwezekano wa kupata polyps ya koloni, “alisema Dk, Omer Yilmaz, mwandishi wa masomo na profesa msaidizi wa MIT wa biolojia na mshiriki wa Taasisi ya MIT ya Koch ya Utafiti wa Saratani Shirikishi, katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Wanasayansi pia waligundua kuwa seli hizi za saratani ya koloni zilikua na kuwa tumors kubwa na kubadilika kwenye viungo vingine, wakati kuonekana kwa SOX17 kulipungua.

Jinsi ambavyo Seli za Saratani hujificha zisishambuliwe na Kinga yako
ya Mwili
0 Comment

WHO: Wakimbizi wapo kwenye hatari ya kupata mlipuko wa magonjwaAfyaclass Bongo Social •

#PICHA: Wakimbizi wa ndani katika kambia ya wakimbizi ya Bulengo nchini DR Congo.

Nchini Jamhuri ya kidemokrasia kongo DRC Jimboni kivu kaskazini zaidi ya wakimbizi milioni 2.5 wanaishi katika kambi za wakimbizi ambazo zina hali mbaya ambayo ni tishio kwa afya zao. Shirika la afya ulimwenguni WHO linatoa usaidizi kwa wakimbizi hao.

Kambi ya wakimbizi ya Bulengo iliyoko jimboni kivu kaskazini, Video ya WHO inaonesha maelfu ya mahema meupe chini udongo mweusi wa mfinyazi, mamia ya watu wanaenda huku na kule ndani ya kambi hiyo.

WHO inahofia mlundikano huu wa wakimbizi kuleta mlipuko wa magonjwa kama Malaria, magonjwa ya kupumua, ya kuhara na mengine ya kuambukiza. WHO ikishirikiana na wadau wengine wameanzisha vituo vya afya na wagonjwa wanafika kupata huduma, mmoja wao ni Desange Ndamwenge na mwanae.

“Nimemleta mtoto wangu hapa asubuhi kwa ajili ya matibabu na ili tupate dawa. Mtoto ana mwaka mmoja na nimgonjwa sana ndio maana nimemleta hapa. Na mimi pia ni mgonjwa. Tumepata dawa wameshatupatia dawa za maji.”

Aubedi Dunia Sebirayi ni nesi mkuu katika kambi ya Bulengo na anasema

“Hapa tunatoa huduma ya afya ya msingi, wakimbizi hawa wanapokuja na ninwagonjwa hawana hela ya kwenda hospitali kupata matibabu. Tunatoa huduma bure, kwa siku tunaona wagonjwa kati ya 80 mpaka 120 na kati yao unakuta wagonjwa wawili au watatu tunawapeleka katika hospitali.”

Kwa mujibu wa Meneja wa Matukio wa WHO nchini DRC Dkt. Guy Kalambayi wakimbizi hao wa ndani wanakabiliwa na changamoto nyingi za kiafya lakini kwa kuwapatia dawa, kutoa huduma za kujifungua, kutoa chanjo, na kutibu kipindupindu wanazuia vifo vingi sana na kuokoa maisha.

Takwimu za WHO zinaonesha kwa wastani tangu mwezi Februari 2023 kwa mwezi wanawake 100 wanajifungua na hakuna kifo cha mjamzito hata mmoja tangu wameanza kutoa huduma. Kavira Mwaliweka ni mkunga katika kituo cha afya ya Bulengo

“Kama tusingekuwa na wodi hii ya kujifungulia hapa Bulengo tungekuwa na vifo vingi sana vya wajawazito kwasababu kambi hii iko mbali sana na kituo cha afya. Tunajisika kuwa na bahati sana kwa kutokuwa na kifo hata kimoja cha mjamzito.”

Elise ni mmoja ya wajawazito waliojifungua salama na sasa anarejea nyumbani kambini na mwanaye kwa furaha.

WHO: Wakimbizi wapo kwenye hatari ya kupata mlipuko wa magonjwa
0 Comment

Familia ya Mtanzania, Abraham Mgowano aliyefariki Marekani yafungukaAfyaclass Bongo Social •

Familia ya Mtanzania, Abraham Mgowano aliyefariki Marekani yafunguka

Dar es Salaam. Familia ya Mtanzania, Abraham Mgowano aliyefariki dunia kwa kuanguka kutoka kwenye boti iliyokodiwa ikifanya safari katika Mto Miami nchini Marekani, imesema taratibu za maziko zinaendelea na mwili wa ndugu yao utarejeshwa nyumbani hivi karibuni.

“Mpango wa kurudisha mwili wake Tanzania unaendelea. Tunatarajia itachukua kati ya siku 10 hadi 15 kuanzia leo,” Alexender Mgowano, kaka wa marehemu, ameiambia Mwananchi Digital.

Amesema mdogo wake huyo amekuwa Marekani tangu Septemba 2010, alipojiunga na Chuo Kikuu cha Stanford na alianza kufanya kazi Google mwaka 2014 baada ya kumaliza shahada yake ya kwanza.

Mwili wa Mgowano (35), aliyekuwa akifanya kazi kampuni ya Google kama mhandisi wa programu, ulipatikana Jumanne baada ya kupotea tangu alipoanguka kutoka kwenye boti hiyo yenye urefu wa futi 44 Jumamosi ya wiki iliyopita.

Mwili wa Mgowano ulipatikama mwishoni mwa wiki ukielea majini, polisi wamethibitisha.

Kwa mujibu wa maofisa wa Tume ya Kuhifadhi Samaki na Wanyamapori ya Florida (FWC), Mgowano alianguka kutoka kwenye boti yenye urefu wa futi 44 karibu na Hifadhi ya Lummus kwenye kitalu namba 400 katika eneo la kaskazini mwa mto huo.

Tangu siku hiyo, Polisi wa Miami na viongozi wengine walikuwa wakimsaka Mgowano kwa njia ya anga na hata kuwaita wazamiaji kumtafuta majini. Pamoja na jitihada zao, hawakuupata mwili huo hadi walipopigiwa simu juzi kuhusu maiti iliyoonekana ikielea mtoni, hivyo wakaenda kuiopoa.

Hata hivyo, polisi hawakutoa maelezo kuhusu mahali ambapo maiti ya Mgowano ilipatikana au ni nani aliyeipata. Kwa mujibu wa ripoti ya awali ya tukio hilo iliyotolewa na FWC, watu wengine 12 waliokuwa pamoja na Mgowano waliwaambia wapelelezi wa tukio hilo kwamba walimuona akielea juu ya maji, kisha akazama na hakutokea tena.

Ripoti hiyo inaeleza aliyekuwa akiendesha boti hiyo, Eddy Espinosa Hernandez (39), alikuwa nahodha aliyekodiwa na abiria hao. Hata hivyo, hakupatikana kutoa maelezo yake.

Polisi wamebainisha katika ripoti yao kwamba “hakuonyesha dalili za kuharibika.” Mgowano anatokea Tanzania na alikuwa Marekani akifanya kazi katika kampuni ya Google kama mhandisi wa programu, kama mitandao yake ya kijamii inavyoonyesha.

Mmoja wa marafiki zake wa karibu, Joseph Rwembiza amesema wamempoteza mtu aliyekuwa na mapenzi ya kweli kwa kila mtu na siku zote walikutana kila alipokuja Tanzania kutoka Marekani.

Katika taarifa ya pamoja waliyoitoa kwa Mwananchi Digital, marafiki wa Mgowano walisema, “Abraham alikuwa bora wakati wote. Tunamwita genius (mwenye akili nyingi); alikuwa na moyo mkuu; alitupenda siku zote na kutuonyesha upendo wa kweli. Alituunganisha kila mara alipokuja Tanzania kutembea.”

Rwehumbiza na washiriki wengine wa kikundi hicho kinachoitwa Loyolite, kilichojumuisha wanafunzi wenzake wa zamani waliosoma katika shule ya sekondari ya Loyola, walimaliza kidato cha nne mwaka 2006.

Familia ya Mtanzania, Abraham Mgowano aliyefariki Marekani yafunguka
0 Comment

Mtanzania mfanyakazi wa Google afa maji nchini MarekaniAfyaclass Bongo Social •

Mtanzania mfanyakazi wa Google afa maji nchini Marekani.

Miami, Florida:

Vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti tukio la kusikitisha la kifo cha Mtanzania aliyekuwa akifanya kazi Google.

Mwili wa Mtanzania aliyeanguka kutoka kwenye boti iliyokodishwa aliyokuwa amepanda katika Mto Miami nchini Marekani mwishoni mwa juma umepatikana ukielea majini.

Abraham Mgowano, 35, ambaye alifanya kazi kama mhandisi wa programu za Google, alipatikana Jumanne baada ya kupotea tangu aanguke kutoka kwenye boti ya urefu wa futi 44 ya Sea Ray cabin cruiser siku ya Jumamosi.

Mtanzania mfanyakazi wa Google afa maji nchini Marekani
0 Comment

Kipande cha Ubavu chavunwa na kuwekwa kama Kiungio cha FUVU kwa mtuAfyaclass Bongo Social •

Kipande cha Ubavu chavunwa na kuwekwa kama Kiungio cha FUVU kwa mtu.

Muhimbili kwa mara ya kwanza yavuna kipande cha ubavu na kukiweka kama kiungio cha fuvu ili kumtengenezea mgonjwa taya jipya.

Katika mwendelezo wa utoaji huduma za kibingwa na ubingwa bobezi unaotokana na kujenga uwezo wa watalaam wazawa chini ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Hospitali ya Taifa Muhimbili, leo kwa mara ya kwanza imefanya upasuaji wa kutoa mfupa kwenye ubavu na kutengeneza kiungio (joint) cha taya la chini na fuvu ili kumtengenezea mgonjwa taya jipya la kulia lililoathiriwa na uvimbe.

Akizingumza baada ya upasuaji huo, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Uso na Taya Dkt Arnold Augustino amesema, mgonjwa huyo amefanyiwa upasuaji wa kuondoa taya lote la kulia lililoathiriwa na uvimbe na hivyo kumtengenezea taya jipya kwa kuchukua mfupa kutoka kwenye ubavu ambapo mfupa huo umepandikizwa kwenye kiungio cha taya.

Ameongeza kuwa mifupa mingine imechukuliwa kutoka kwenye nyonga pande zote mbili ili kuunganishwa na mfupa uliotolewa kwenye ubavu kuwezesha kutengenezwa kwa taya sawasawa na taya lake la awali na kisha kuunganishwa na kipandikizi cha chuma maalum kutengeneza sehemu ya taya iliyoharibika na ugonjwa.

Amesema, mara baada ya upasuaji huu mgonjwa huyo anategemea kuendelea kula na kutafuna kama kawaida kwani atawekewa meno bandia kwenye mfupa wa taya aliotengenezewa

Ameongeza kuwa mgonjwa huyo amefanyiwa upasuaji aina tatu tofauti kwa wakati mmoja, wa kutoa kipande cha mfupa kwenye ubavu, wa pili ni kutoa mifupa kwenye nyonga zote mbili na wa tatu ni kuondoa uvimbe ambapo umechukua saa saba umeshirikisha timu watalaam wa MNH madaktari bingwa wa taya na uso (5) wataalamu usingizi na ganzi (2) manesi wa upasuaji (3) na wataalamu wengine waliokuwepo ni pamoja madaktari wanaosomea ubingwa wa kupasua mataya na uso (3).

Kipande cha Ubavu chavunwa na kuwekwa kama Kiungio cha FUVU kwa mtu
0 Comment

Benjamin yaendelea kupandikiza betri kwenye moyoAfyaclass Bongo Social •

Benjamin yaendelea kupandikiza betri kwenye moyo.

Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma upasuaji wa kupandikiza betri kwenye moyo kwa watu watatu leo.

Upandikizaji wa betri kwenye moyo ambao kitaalamu inaitwa _pacemakers_ _implantation_ unafanyika kwa watu wenye matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo na kusababisha mapigo ya moyo kuwa chini ya kiwango kinachotakiwa kwa mtu wa kawaida ambayo ni 60-100 kwa dakika.Wengi wao huwa ni chini ya 40.

Mkuu wa Kliniki ya Moyo wa BMH, Daktari Bingwa wa Moyo, Happiness Kusima, amesema leo kuwa BMH imefikisha upandikizaji kwa watu 18 toka huduma ianzishwe mwaka 2021.

“Jana tumepandika watu watatu (3), leo tutapandikiza watu wawili,” amesema Daktari huyo Bingwa wa Moyo.

Dkt Happiness amesema upandikizaji huu unafanyika kwenye kambi ya pamoja kati ya Madaktari Bingwa wa Moyo wa BMH na Daktari Bingwa wa Moyo, George Longopa, kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam.

Kambi hii ya moyo ya pamoja kati ya BMH na JKCI imeanza leo na itakamilika kesho. @wizara_afyatz @ummymwalimu

Benjamin yaendelea kupandikiza betri kwenye moyo
0 Comment

Mwanasoka wa Ivory Coast, Archange Defrignan Mondou afariki duniaAfyaclass Bongo Social •

Mwanasoka wa Ivory Coast, Archange Defrignan Mondou afariki dunia.

Mchezaji kandanda wa Ivory Coast Archange Defrignan Mondou, umri miaka 19, amefariki dunia baada ya mwili wake kupatikana nyumbani kwake bila kujua chanzo cha kifo chake ni nini.

Mondou, 19, alichezea klabu kuu ya Norway HamKam huko Eliteserien kabla ya kifo chake.

Kiungo huyo aliyepewa jina la utani Achilles, alihama kutoka Ivory Coast Aprili mwaka jana na awali alijiunga na kikosi cha pili cha HamKam, akicheza mechi tatu na kufunga bao moja.

Mondou alipatikana katika nyumba yake huko Hamar, maili 60 kaskazini mwa mji mkuu wa Norway Oslo Jumanne, Februari 27. Sababu ya kifo chake haifahamiki mpaka Sasa..!!!!

Katika taarifa, HamKam ilisema: ‘Ni kwa huzuni kubwa kwamba HamKam Football imepokea taarifa kwamba Achilles ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 19.

‘Alipatikana katika nyumba yake. Katika kipindi hiki kigumu tupo pamoja na familia yake na jamaa.

Sababu ya kifo haijajulikana.’

Meneja mkuu wa HamKam Bent Svele aliongeza: ‘Hii ni siku ngumu sana kwa kila mtu aliyeguswa.’

Wakati huo huo, polisi wa eneo hilo walisema chanzo cha kifo cha Mondou hadi sasa hakijajulikana.

Walieleza: ‘Alipatikana amekufa, na tumeomba uchunguzi wa maiti.

“Hakukuwa na chochote cha kutilia shaka juu ya kifo hicho, zaidi ya kusema sababu haijulikani. Alipatikana na wengine nyumbani, na akafa peke yake.’

Mondou alilazimika kujitenga na soka Septemba mwaka jana kufuatia tukio lililotekea mazoezini, huku kiungo huyo akitumia muda hospitalini baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.

Mwanasoka wa Ivory Coast, Archange Defrignan Mondou afariki dunia
0 Comment

Dalili za sickle cell kwa mtoto pamoja na matibabu yakeAfyaclass Bongo Social •

Dalili za sickle cell kwa mtoto

Katika Makala hii tunachambua Zaidi kuhusu Dalili za sickle cell kwa mtoto,chanzo cha ugonjwa wa Sickle cell pamoja na Matibabu yake.

Sickle cell ni nini?

Sickle cell ambapo kiswahili chake ni “Seli mundu” ni ugonjwa ambao upo kwenye kundi la inherited red blood cell disorders,

kwa kawaida seli nyekundu za damu(red blood cells) huwa na umbo linalojulikana kama biconcave disks, lakini Ugonjwa wa sickle cell husababisha umbo la seli nyekundu za damu kuwa kama ‘C’ yaani C-shaped au “sickle.” na hapa ndipo jina la ugonjwa huu kuitwa Sickle cell hutokea.(tazama shape kwenye picha)

kutokana na seli nyekundu za damu kuwa na shape au umbo lisilo la kawaida,hii hupelekea seli hizo kufa mapema zaidi,

Na hiki ndyo chanzo kikubwa cha wagonjwa wa Sickle cell kuwa na tatizo la Upungufu wa damu kila mara.

Hayo ndyo maelezo mafupi ya utangulizi kuhusu ugonjwa wa Sickle cell.

Aina za Ugonjwa wa Sickle cell

Kuna aina mbali mbali za ugonjwa wa sickle cell ikiwemo;

  • HbSS
  • HbSC
  • HbS beta-thalassemia
  • HbSD
  • HbSE
  • HbSO
  • HbAS n.k

Chanzo cha Ugonjwa wa Sickle cell

Sickle cell ni ugonjwa ambao mtoto huzaliwa nao, ugonjwa huu wa sickle Cell au Seli mundu hutokana na kurithi kwa genes mbili ambazo huleta shida,

Mtoto hupokea genes mbili,moja kutoka kwa baba,na nyingine kutoka kwa mama, ambazo husababisha(code) matatizo kwenye hemoglobin kisha kupelekea uzalishwaji wa hemoglobin zenye shida yaani abnormal hemoglobin,

Na hapo ndipo ugonjwa wa Sickle cell hutokea.

Jinsi ya Kugundua ugonjwa wa sickle cell

ugonjwa wa sickle cell huweza kugundulika kwa kufanya vipimo vya damu yaani simple blood test.

Dalili za sickle cell kwa mtoto

Dalili za ugonjwa wa sickle cell kwa Ujumla zinahusisha zile zote za Mtu ambaye kaishiwa damu au ana tatizo la ANEMIA kama vile;

– Kushindwa kupumua vizuri

– Kizunguzungu

– Maumivu ya kichwa

– Ubaridi katika viganja na miguuni

– Unjano katika macho na ngozi au jaundice

– Weupe katika viganja, na eneo la macho liitwalo conjuctiva, ulimi na midomo

– Maumivu ya tumbo

– Homa

– Maumivu ya viungo (joint pains)

– Maumivu ya kifua

– Damu katika mkojo (hematuria)

– maumivu ya mfupa

– kuziba kwa ateri kuu (CRAO) n.k

Matibabu ya Ugonjwa wa Sickle cell kwa Mtoto

Kwa mujibu wa chapisho la Vituo vya kudhibiti na kuzuia magonjwa yaani centers for diseases control and prevention(CDC)

Tiba pekee ya ugonjwa wa sickle cell ambayo huweza kutibu kabsa tatizo hili ni;

  • bone marrow transplant
  • Au stem cell transplant.

FAQs: Maswali ambayo huulizwa mara kwa mara

Je, ugonjwa wa seli mundu ni nini?

Seli mundu ni ugonjwa ambao upo kwenye kundi la inherited red blood cell disorders, ugonjwa huu kwa jina lingine hujulikana kama “Sickle cell”

kwa kawaida seli nyekundu za damu(red blood cells) huwa na umbo linalojulikana kama biconcave disks, lakini Ugonjwa wa seli mundu husababisha umbo la seli nyekundu za damu kuwa kama ‘C’ yaani C-shaped au “sickle.” na hapa ndipo jina la ugonjwa huu kuitwa Sickle cell hutokea.

Je, chanzo cha ugonjwa wa seli mundu ni kipi?

Seli mundu ni ugonjwa ambao mtoto kuzaliwa nao, ugonjwa wa Seli mundu hutokana na kurithi kwa genes mbili ambazo huleta shida,

Mtoto hupokea genes mbili,moja kutoka kwa baba,na nyingine kutoka kwa mama, ambazo husababisha(code) matatizo kwenye hemoglobin kisha kupelekea uzalishwaji wa hemoglobin zenye shida yaani abnormal hemoglobin,

Na hapo ndipo ugonjwa wa Seli mundu hutokea.

Hitimisho

Ni muhimu sana kufahamu kuhusu Dalili za Sickle cell kwa Mtoto ili kupata msaada kwa haraka zaidi,

Dalili za ugonjwa wa sickle cell au seli mundu kwa Ujumla zinahusisha zile zote za Mtu ambaye kaishiwa damu au ana tatizo la ANEMIA kama vile;

– Kushindwa kupumua vizuri

– Kizunguzungu

– Maumivu ya kichwa

– Ubaridi katika viganja na miguuni

– Unjano katika macho na ngozi au jaundice

– Weupe katika viganja, na eneo la macho liitwalo conjuctiva, ulimi na midomo

– Maumivu ya tumbo

– Homa

– Maumivu ya viungo (joint pains)

– Maumivu ya kifua

– Damu katika mkojo (hematuria)

– maumivu ya mfupa

– kuziba kwa ateri kuu (CRAO)

• Soma zaidi hapa kuhusu Ugonjwa wa Sickle cell(seli mundu)

Dalili za sickle cell kwa mtoto pamoja na matibabu yake
0 Comment

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umefanya maboresho ya Kitita cha MafaoAfyaclass Bongo Social •

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umefanya maboresho ya Kitita cha Mafao kwa wanachama wake ambayo utekelezaji wake utaanza rasmi Machi 1, 2024.

Hayo yamebainishwa leo Februari 28, 2024 na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Bernard Konga akizungumza na waandishi wa habari Dar Es Salaam kwa lengo la kuutaarifu umma juu ya maboresho hayo.

“Kitita cha mafao ni orodha ya huduma za matibabu ambazo zinatolewa kwa wanufaika wa NHIF na bei zake ambazo hutumika wakati wa malipo kwa madai ya watoa huduma za matibabu. Maboresho ya mwisho ya kitita cha mafao cha NHIF kinachotumika sasa yalifanyika Juni, 2016 takribani miaka nane iliyopita na hivyo kuwepo kwa umuhimu wa kufanya marejeo yake kutokana na sababu mbalimbali kama zinavyoanishwa kwenye taarifa hii,” amesema Konga.

Konga ametaja malengo ya maboresho ya kitita cha mafao kuwa ni kuboresha upatikanaji wa huduma bora kwa wanachama ikiwa ni pamoja na kuongeza huduma ambazo hazikuwepo awali, Kufanya maboresho ya huduma na gharama zake kwa kuzingatia maendeleo ya teknolojia na hali halisi ya bei katika soko na Kuwianisha Kitita cha Mafao na miongozo ya tiba iliyoboreshwa ili kuongeza ubora wa huduma zinazotolewa kwa wanufaika wa Mfuko.

Malengo mengine ni Kujumuisha maoni na mapendekezo mbalimbali ya Wadau, Kutekeleza ushauri wa Taarifa ya Mapendekezo ya Tathmini ya Uhai na Uendelevu wa Mfuko kwa kipindi kinachoishia tarehe 30 Juni, 2021 na Kuimarisha udhibiti katika mianya ya udanganyifu.

Konga ameeleza kuwa Mfuko ulianza zoezi la kufanya marejeo ya kitita kuanzia mwaka 2018, hata tenhivyo utekelezaji wa kitita kipya haukufanyika kutokana na uhitaji wa kuhusisha wadau zaidi ili kuwa na uelewa na maoni zaidi kuboresha kitita hicho.

Maboresho ya Kitita cha Mafao yamehusisha kufanyika kwa Tathmini ya Uhai na Uendelevu wa Mfuko na kutekeleza mapendekezo yake ambapo tathmini ya mwisho ilifanyika Juni, 2021 ambapo Kifungu Na 15.2 cha Mkataba baina ya Mfuko na Watoa Huduma kinautaka Mfuko kutoa notisi ya miezi mitatu (3) ya kusudio la kufanya maboresho katika kitita chake kabla ya kuanza kutumika.

Amesema katika kutekeleza takwa hilo la mkataba, 1 Agosti 1, 2022 Mfuko kupitia barua yenye Kumb. Na. EA.35/269/01-A/32 ulitoa Notisi ya miezi mitatu (3) ya kusudio la kufanya maboresho ya Kitita chake cha Mafao ambapo tangu tarehe ya kutolewa kwa Notisi hiyo, Mfuko uliendelea kushirikisha wadau, kukusanya na kupokea maoni, ushauri na mapendekezo kutoka kwa wadau wake kwa lengo la kuboresha Kitita chake cha Mafao ambapo kwa nyakati tofauti Mfuko ulifanikiwa kukutana na Watoa Huduma za Matibabu wa Umma na Binafsi na Madhahebu ya Dini na Vyama mbalimbali vya taaluma za afya.

Konga ametaja maeneo yaliyofanyiwa mapitio na maboresho katika Kitita cha Mafao ni pamoja na ada ya usajili na kupata ushauri wa daktari, huduma za dawa, huduma za vipimo, huduma za upasuaji, na gharama za kliniki za kawaida na kibingwa.

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umefanya maboresho ya Kitita cha
Mafao
0 Comment

Bodaboda Tanga Wachoma Basi La Saibaba Lililomgonga MwenzaoAfyaclass Bongo Social •

Bodaboda Tanga Wachoma Basi La Saibaba Lililomgonga Mwenzao

Basi la Kampuni ya Saibaba Express lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea mkoani Arusha limechomwa moto na kundi la bodaboda katika Kata ya Mtonga, Halmashauri ya wilaya ya Korogwe mkoani Tanga baada ya mwenzao kugongwa na basi hilo wakati likijaribu kupita lori eneo lisiloruhusiwa.

Akizungumza Kamishina Msaidizi wa Polisi mkoani humo, Almachius Mchunguzi amesema ajali hiyo imetokea Februari 27, 2024 majira ya saa saba mchana ambapo baada ya bodaboda kupata taarifa ya mwenzao kugongwa waliamua kulifuatilia basi hilo na kulichoma moto.

“Hakuna abiria aliyejeruhiwa, kwa bahati nzuri abiria waliweza kutoka salama na kutoa baadhi ya vitu vyao, lakini vitu vichache tu ndio vimeungua, lakini asilimia kubwa ya vitu vingi abiria walitoa,” ameeleza Kamishna.

Ameongeza kuwa bodaboda aliyegongwa na basi hilo amefariki mara baada ya kufikishwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

Aidha, amesema mpaka sasa jeshi la polisi linamshikilia dereva wa basi hilo kwa ajili ya mahojiano zaidi, huku likiendelea na uchunguzi kwa yeyote aliyehusika kufanya uhalifu wowote ili sheria ichukue mkondo wake.

Bodaboda Tanga Wachoma Basi La Saibaba Lililomgonga Mwenzao
0 Comment

kuwashwa mgongoni chanzo chake,na Tiba yakeAfyaclass Bongo Social •

kuwashwa mgongoni chanzo chake,na Tiba yake

Kuwashwa mgongoni ni hali inayoweza kusababishwa na sababu mbalimbali, zikiwemo za kiafya, kimazingira, au hata za kisaikolojia. Kuwashwa huku kunaweza kuwa kwa muda mfupi au kudumu kwa muda mrefu, kulingana na chanzo chake. Kuelewa chanzo cha kuwashwa mgongoni ni hatua ya kwanza katika kutafuta tiba inayofaa.

Chanzo cha Kuwashwa Mgongoni

– Magongwa ya Ngozi: Hali kama vile eczema, psoriasis, na urticaria (hives) zinaweza kusababisha kuwashwa mgongoni.

– Allergies(Mzio): Mizio ya vitu mbalimbali kama vile sabuni, vipodozi, au hata vyakula vinavyosababisha tatizo la allergic contact dermatitis.

Tatizo hili huweza kusababisha hali ya kuwashwa kwenye ngozi ikiwemo maeneo ya mgongoni.

– Ukavu wa Ngozi: Ukavu wa ngozi (xerosis) unaweza kusababisha kuwashwa. Hali hii inaweza kuchochewa na hali ya hewa baridi au matumizi ya maji ya moto mara kwa mara.

– Wadudu: Kuuma kwa wadudu na vimelea kama vile chawa, viroboto, na mbu kunaweza kusababisha kuwashwa.

Lakini pia hata minyoo inweza kuwa chanzo cha mtu kuwashwa kwenye ngozi maeneo mbali mbali ya mwili ikiwemo mgongoni.

>>Soma Zaidi hapa; Dalili za Minyoo

– Magonjwa ya Ndani: Baadhi ya magonjwa kama vile ugonjwa wa ini, ugonjwa wa figo, na kisukari yanaweza kusababisha kuwashwa kwa ngozi kote mwilini, ikiwemo mgongoni.

– Msongo wa Mawazo: Msongo wa mawazo na hali za kisaikolojia zinaweza kuchochea au kuzidisha hali ya kuwashwa kwa ngozi.

Hizo ndyo baadhi ya Sababu ambazo huweza kupelekea mtu kuwa na tatizo la kuwashwa mgongoni.

Tiba ya Kuwashwa Mgongoni

Tiba ya kuwashwa mgongoni inategemea chanzo cha kuwashwa. Hata hivyo, kuna hatua za jumla ambazo mtu anaweza kuchukua ili kupunguza au kumaliza hali hii:

Matibabu ya Nyumbani: Kutumia losheni au mafuta ya ngozi kunaweza kusaidia kupunguza ukavu wa ngozi na kuwashwa. Vilevile, kuepuka maji ya moto sana na kutumia sabuni zenye unyevu unyevu kunaweza kusaidia.

Epuka Allergens: Kujua na kuepuka vitu vinavyosababisha mizio au allergies kwako kunaweza kusaidia kupunguza kuwashwa.

Dawa za Antihistamine: Dawa za kuzuia histamine zinaweza kusaidia kupunguza kuwashwa kwa wale wanaokabiliwa na allergies au hives.

Corticosteroids za Topical: Creams na ointments zenye corticosteroids zinaweza kutumika kwa maelekezo ya daktari kudhibiti kuwashwa kunakotokana na hali kama vile; ugonjwa wa pumu ya ngozi au eczema psoriasis.n.k

Matibabu ya Magonjwa ya Ndani: Iwapo kuwashwa kunasababishwa na magonjwa ya ndani, kama vile;

  • ugonjwa wa ini
  • au kisukari,n.k

kutibu hali hiyo ya msingi kunaweza kupunguza au kumaliza kabsa tatizo la kuwashwa.

Kupunguza Msongo wa Mawazo: Mbinu za kupunguza msongo wa mawazo kama vile kufanya mazoezi na ushauri wa kisaikolojia zinaweza kusaidia kudhibiti kuwashwa kunakotokana na msongo wa mawazo.

   >>Soma Zaidi hapa; mbinu za kupunguza Msongo wa mawazo

Kuonana na Daktari: Iwapo kuwashwa kunaendelea kwa muda mrefu, hali inazidi kuwa mbaya, au kunaambatana na dalili nyingine kama vile vipele, mabadiliko ya rangi ya ngozi, au uchovu, ni muhimu kumuona daktari. Daktari anaweza kufanya vipimo kubaini chanzo cha kuwashwa na kupendekeza tiba inayofaa.

Hitimisho

Kuwashwa mgongoni kunaweza kuwa na athari kubwa kwa ubora wa maisha, hivyo ni muhimu kutafuta chanzo na tiba inayofaa. Kwa kufuata maelekezo ya kitaalamu na kuchukua hatua stahiki, mtu anaweza kupata nafuu na kuboresha hali yake ya maisha.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

kuwashwa mgongoni chanzo chake,na Tiba yake
0 Comment

Hatari ya Mlipuko wa Surua,kwa watoto kukosa kinga dhidi ya ugonjwa wa suruaAfyaclass Bongo Social •

Hatari ya Mlipuko wa Surua,kwa watoto kukosa kinga dhidi ya ugonjwa wa surua

Janga la Uviko -19 lilitatiza utoaji wa chanjo za kawaida dhidi ya ugonjwa wa Surua duniani kati ya mwaka 2020 na 2021 na kuacha mamilioni ya watoto wengi katika nchi maskini, wakiwa hawana kinga dhidi ya ugonjwa huo.

Kulingana na data za Kituo vya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa nchini Marekani (CDC), kufikia mwisho wa 2024, zaidi ya nusu ya nchi zote duniani zitakuwa katika hatari ya mlipuko wa Surua.

moja ya magonjwa ya kuambukiza, ambayo yanaweza kusababisha upofu, homa ya mapafu na hata kifo. 

>>Soma Zaidi hapa; Ugonjwa wa Surua,chanzo,dalili,kinga.

Wengi wa watu wanaokufa kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo wa Surua ni watoto. Kabla ya kuanza kufurahia utoto wao, wanakufa kutokana na ugonjwa huu unaoweza kuzuilika kwa urahisi, anasema Abdirizak Ahmed,  mkurugenzi wa shirika la msaada la Save the Children mjini Jijiga nchini Ethiopia ambalo liliripoti kesi 10,000 za ugonjwa huo mwaka 2023, hii ikiwa idadi kubwa zaidi duniani baada ya Yemen, Azerbaijan, Kazakhstan na India. Takwimu hizi ni kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO.

Juhudi za Ahmed za kupambana na mripuko wa surua nchini Ethiopia zilipata pigo mwezi uliopita wakati wafanyakazi wenzake wawili walipopoteza watoto wao kutokana na ugonjwa huo, ambao umeibuka tena kutoka barani Afrika kuelekea India na Uingereza.

Watoto hao wote wa kiume walifariki kabla ya kufikisha miezi 13 ama 14 ya maisha yao, hali ambayo Ahmed anasema ni ya kusikitisha.

Watoto 12,000 wafa kwa surua, utapiamlo

Katika kile ambacho wataalamu wa afya wamekiita “kurudi nyuma zaidi katika kizazi kimoja”, nchi 51 – nyingi yao zikiwa barani Afrika – zilishuhudia  miripuko mikubwa na ya kutatiza ya ugonjwa wa Surua mwaka jana, hili likiwa ongezeko kutoka nchi 37 katika mwaka wa 2022 na nchi 22 mwaka 2021, huku hali hiyo ikitarajiwa kuendelea kuwa mbaya zaidi.

Kulingana na data za Kituo vya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa nchini Marekani (CDC), kufikia mwisho wa 2024, zaidi ya nusu ya nchi zote -takriban 105 – zitakuwa katika hatari kubwa ya mripuko wa ugonjwa wa Surua.

Katika ujumbe wa msemaji wa CDC alioandikia kupitia barua pepe, kati ya nchi zinazokabiliwa na hatari, takribani nusu ni zile zenye mapato ya chini na ya kadri, huku watoto wakikabiliwa na hatari zaidi ya kupata ugonjwa huo.

Kwa kawaida, ugonjwa wa Surua husababisha homa kali, kikohozi na upele. Miongoni mwa wanawake wajawazito, ugonjwa huo huongeza hatari ya kuharibika kwa mimba na kuzaliwa mapema kwa mtoto.

Ugonjwa wa surua unaongezeka kufuatia wazazi kutowapa chanjo watoto wao

Ugonjwa wa surua unaongezeka kufuatia wazazi kutowapa chanjo watoto wao.

Hata hivyo, wataalamu wanasema kwa miaka mingi, ufanisi wa chanjo ya Surua umesababisha hali ya kuridhika na sasa idadi inayoongezeka ya wazazi katika nchi ambazo ugonjwa wa Surua ulikuwa umetokomezwa kwa muda mrefu, ikiwa ni pamoja na Marekani na Ulaya, wanachagua kutowapa chanjo watoto wao.

Mnamo mwezi Desemba, WHO ilisema kulikuwa na ongezeko la mara 30 zaidi la visa vya ugonjwa wa surua kote Ulaya.

Uingereza, ambayo ilikuwa imeshauangamiza ugonjwa huo mnamo 2017, sasa inajitahidi kudhibiti maambukizo yanayoongezeka kwa sababu ya kupungua kwa idadi ya chanjo inayotolewa.

DR Congo: Vifo kutokana na ugonjwa wa surua vyapindukia 6000

Imani katika umuhimu wa chanjo kwa watoto dhidi ya magonjwa sugu kama Surua na Polio ilipungua wakati wa janga hilo katika nchi 52 kati ya 55 zilizofanyiwa utafiti na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, mwaka 2023.

Niklas Danielsson, mtaalamu mkuu wa chanjo katika shirika la UNICEF, amesema habari potofu kuhusu chanjo za UVIKO- 19

huenda zimesababisha kushuka kwa imani katika chanjo nyingine.

Kulingana na WHO, Surua inaweza kuzuilika kwa dozi mbili za chanjo. Hata hivyo, watoto milioni 22 ulimwenguni kote walikosa dozi yao ya kwanza mnamo mwaka 2022 na wengine milioni 11 dozi yao ya pili, hii ikiwa hatua bora kidogo ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Mashirika ya misaada na watalaamu wa afya wanasema kuwa mifumo ya afya barani Afrika iko hatarini haswa kutokana na ukosefu wa fedha na wafanyakazi, hasa katika nchi kama vile Ethiopia ambako migogoro, ukame, mafuriko na utapiamlo kunawafanya watoto kuwa katika hatari zaidi ya kuambukizwa magonjwa hatari.

Hatari ya Mlipuko wa Surua,kwa watoto kukosa kinga dhidi ya ugonjwa wa
surua
0 Comment

Watoto pacha waliozaliwa wameungana wakatenganishwa wameruhusiwa LeoAfyaclass Bongo Social •

Muhimbili:Watoto pacha waliozaliwa wameungana wakatenganishwa wameruhusiwa Leo.

watoto pacha waliozaliwa wakiwa wameungana na kufanyiwa upasuaji wa kutenganishwa leo wameruhusiwa:

muhimbili yaishukuru awamu ya sita kutokana na uwekezaji

Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) umeishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na uwekezaji uliofanyika hospitalini hapa ambao umewezesha huduma mbalimbali za kibingwa na ubingwa bobezi kufanyika ikiwemo upasuaji mkubwa wa kutenganisha watoto pacha.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuwaruhusu watoto pacha waliozaliwa kwa nje wakiwa wameungana tumbo na kifua, ndani waliungana ini na mfupa wa kidari, Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof. Mohamed Janabi, amesema uwekezaji wa kusomesha watalaam, kuboresha miundombinu na ununuzi wa vifaa vya uchunguzi vya kisasa umeiwezesha hospitali hiyo kutoa huduma zinazolingana na hadhi yake.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto MNH, Dkt. Victor Ngota ameeleza kuwa upasuaji wa kuwatenganisha watoto hao, ulichukua saa sita na kuhusisha jopo la wazawa lenye utaalam mchanganyiko wa hali ya juu wa madaktari bingwa wa upasuaji watoto, upasuaji rekebishi, usingizi na ganzi, watalaam wa lishe pamoja na radiolojia.

“Tuliwapokea watoto hawa tarehe 11 Machi 2023 wakiwa na jumla ya kilo nne hivyo tulianza mchakato wa kuwahusisha wataalam ambao wanahusika na huduma hizi, ilituchukua takribani muda wa miezi kumi kuangalia mwenendo wao wa afya kwa ujumla kabla ya kuwatenganisha ili kuweza kupata dira ya namna watakavyoishi mara baada ya kutenganishwa ambapo hadi wanatenganishwa walikua na kilo 16 sawa na kilo nane kwa kila mmoja” amefafanua Dkt. Ngota.

Mzazi wa watoto hawa Bi. Mariam Shabani, mkazi wa Kigamboni Jijini Dar es Salaam, ameishukuru Serikali na watoa huduma wote wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na jinsi alivyohudumiwa katika kipindi chote alichokuwa hapo.

Watoto pacha waliozaliwa wameungana wakatenganishwa wameruhusiwa Leo
0 Comment

Mama mjamzito kula hivi ili kuwa na uzazi SalamaAfyaclass Bongo Social •

Mama mjamzito unatakiwa kula Vipi? ili kuwa na uzazi Salama:

Kuna umuhimu mkubwa wa kufahamu Lishe Sahihi kwa mama mjamzito ili kuwa na Uzazi bora,

Mtaalamu wa Lishe Kerry Torrens anaelezea jinsi ya kula vizuri kwa usalama wako na kwa mtoto wako kila miezi mitatu ya ujauzito(trimester).

Lishe bora na yenye afya ni muhimu kwa afya njema, na zaidi unapokuwa mama mtarajiwa. Unapaswa kula vyakula fulani na baadhi ya vyakula vinastahili viepukwe.

>>Soma Zaidi hapa vyakula vya kuepuka wakati wa Ujauzito

Kando na kufuata mapendekezo ya jumla ya ulaji wenye afya – kama vile kula vyakula vitano kwa siku, kula nafaka nzima, kuchagua baadhi ya nyama na vyakula vyenye kalsiamu nyingi, kuna mabadiliko mengine muhimu ya mlo ya kuzingatia unapotarajia mtoto.

Jinsi ya kufuata lishe yenye afya wakati wa ujauzito?

Haishangazi kwamba unahitaji virutubisho zaidi wakati wa ujauzito ili kusaidia ukuaji na maendeleo ya mtoto wako, lakini inawezekana kufikia hili bila kuongeza ulaji wako wa chakula.

Wakati huu, mwili wako huwa na ufanisi zaidi katika kunyonya virutubisho.

Je, nichukue virutubisho vya chakula wakati wa ujauzito?

Akina mama wajawazito wanashauriwa kujiimarisha kwa kutumia;folic acid toka wakati unajaribu kubeba mimba hadi mwisho wa wikI kadhaa baada ya kujifungua, Pata virutubisho vya folic acid, lakini usisahau kula vyakula vingi vya asili vyenye vitamini hii (folate), kama vile:

  • Mboga za kijani kibichi, kama vile mchicha na kale
  • Mboga zilizokaushwa, kama vile mbaazi, maharagwe yenye macho meusi, na dengu
  • Matunda, hasa stroberi na machungwa n.k

Ikiwa una kisukari, umekuwa na tatizo la mimba zenye kasoro ikiwemo matatizo yanayohusiana na upungufu wa folic acid kama vile kuzaa watoto wenye mgongo wazi,vichwa vikubwa, au unatumia dawa za kutibu kifafa, hitaji lako la folic acid linaweza kuwa kubwa zaidi –Uliza kwa Ushauri Zaidi.

Vitamini D ni muhimu kwa kunyonya kalsiamu. Mfano kwa nchi kama Uingereza inapendekeza nyongeza ya mcg 10 kwa siku wakati wa ujauzito na kunyonyesha. Hata hivyo, ikiwa uko katika hatari kubwa ya upungufu, mahitaji yako yanaweza kuwa makubwa zaidi – wasiliana na daktari wako.

Watu wanaofuata lishe ya mboga wanaweza kuhitaji virutubisho vya ziada kama vile iodini, asidi ya mafuta ya omega-3 na vitamini B12.

Jinsi ya kula katika robo ya kwanza?

Tatizo la kichefuchefu na kutapika(morning sickeness) ni kawaida zaidi katika ujauzito na, licha ya jina lake, hali hii inaweza kutokea wakati wowote wa mchana au usiku. Dalili hutofautiana na kama una shida Zaidi hakikisha unaongea na daktari wako au mkunga, ingawa kwa watu wengi dalili hupotea kwa wiki ya 20.

Katika hali mbaya, vidokezo hivi rahisi vinaweza kusaidia;

✓ Kula kidogo na mara kwa mara, weka milo na vitafunio vyako kwenye vyakula vya wanga kama mkate, uji, biskuti za kawaida, mikate, oatcakes, tambi, wali au viazi.

✓ Punguza kula vyakula vyenye harufu kali.

✓ Punguza vyakula vya mafuta ambavyo ni vigumu kusaga.

✓ Chagua mapishi ya haraka na rahisi.n.k

Jinsi ya kula katika robo ya pili?

Mama wengi huripoti kuongezeka kwa hisia ya ladha na harufu karibu na wakati huu, ambayo husababisha tamaa ya chakula au kutopenda baadhi ya vyakula. Mabadiliko haya hayana uwezekano wa kuwa na athari mbaya, mradi lishe yako ni sawa na tofauti.

Ikiwezekana, panga milo yako mapema, fuata mapendekezo ya ulaji wenye afya na jaribu kula vitu kama samaki wiki isiishe, pamoja na vitu kama vile dagaa, sardini.n.k

Kwa kuwa kuvimbiwa,kupata choo kigumu au kukosa kabsa choo kunaweza kuwa tatizo, kuzingatia vyakula vya nafaka nzima, ikiwa ni pamoja na mkate wa nafaka, nafaka au pasta, pamoja na shayiri, matunda, mboga mboga, kunde, karanga na mbegu.n.k ni vizuri Zaidi,bila kusahau ulaji wa Matunda mengi.

Dumisha unywaji wako wa maji kwa kulenga glasi 6 hadi 8 za maji yaliyochujwa, chai ya mitishamba au juisi za matunda kila siku.

Ujauzito wako unapoendelea, jumuisha vyakula vingi vya madini ya chuma katika mlo wako:

  • kama vile kuku, hasa nyama nyeusi zaidi kama vile ya mapaja,
  • na samaki,
  • pamoja na vyanzo vya mboga kama parachichi, mboga za kijani na kunde.

Mwili haunyonyi chuma kutoka kwa vyakula vya mmea kwa urahisi, lakini kwa kuongeza chanzo cha vitamini C kwenye mlo wako (kama vile glasi ya juisi ya machungwa), unaweza kuongeza kiwango cha chuma kinachofyonzwa.

Jinsi ya kula katika robo ya tatu?

Tatizo katika kusaga chakula pamoja na kiungulia kinaweza kuwa tatizo kadiri ujauzito unavyoendelea. Kwa bahati nzuri, kwa watu wengi, hii ni ya muda tu – kula chakula kidogo, mara kwa mara, kuepuka kulala chini au kuinama baada tu ya kula, na kupunguza vyakula vya mafuta na viungo kunaweza kupunguza dalili hizi.

Mahitaji yako ya nishati huongezeka katika trimester ya mwisho, na kalori 150 hadi 200 za ziada kwa siku huhitajika.

Mahitaji yako ya kalsiamu pia huongezeka na huenda hata maradufu wakati wa ujauzito, hasa katika wiki kumi zilizopita wakati ulaji wa kalsiamu ni muhimu kwa kuimarisha mifupa ya mtoto wako.

Mbali na bidhaa za maziwa, vyanzo vyema vya kalsiamu ni mboga za kijani kibichi, samaki, mifupa laini ya chakula (salmoni, sardines na pilchards), almond, parachichi, ufuta, tofu, juisi ya machungwa iliyoimarishwa na maziwa ya soya n.k.

Ni vyakula gani unapaswa kuviepuka wakati wa ujauzito?

Baadhi ya vyakula vinaweza kuwa hatari kwa mtoto wako ambaye hajazaliwa, kwa hivyo ni bora kuviepuka:

– Mayai mabichi au ambayo hayajaiva vizuri.

– Samaki mbichi na nyama zisizoiva vizuri.

– Jibini laini kama vile Brie, Camembert, jibini fulani la mbuzi, pamoja na jibini la bluu kama vile Roquefort.

– Bidhaa za maziwa ambazo hazijapikwa.

– Popsicles – mashine zinazotumiwa kutoa ice cream zinaweza kuwa na listeria.

– Saladi zilizohifadhiwa kwenye jokofu zilizotayarishwa mapema, kama vile viazi na saladi za coleslaw.

– Aina fulani za samaki, kama vile swordfish na marlin, huku zikipunguza nyama ya tuna na samaki walio na mafuta mengi kama lax, sardines na makrill mara mbili kwa wiki.

Baadhi ya nchi zinashauri dhidi ya kula vyakula vya baridi kama vile salami, prosciutto na pepperoni, , ingawa Uingereza kwa sasa inashauri kuwa waangalifu badala ya kuzuia vyakula hivi.

– Kafeini inapaswa kupunguzwa hadi miligramu 200 kwa siku, au vikombe viwili vya kahawa au vikombe vitatu vya chai kwa siku.

Ni bora kuepuka pombe wakati wa ujauzito na kuiweka kwa kiwango cha chini wakati wa kunyonyesha.

>> Soma Zaidi hapa: Vyakula vya mama mjamzito anavyostahili kula na anavyotakiwa kuepuka

Mama mjamzito kula hivi ili kuwa na uzazi Salama
0 Comment

Mwanaume wa Marekani anakaribia kutangazwa kuwa ameponywa VVU na saratani ya damuAfyaclass Bongo Social •

Mwanaume wa Marekani anakaribia kutangazwa kuwa ameponywa VVU na saratani ya damu.

Paul Edmonds, mwenye umri wa miaka 68, kutoka California ambaye alitrend kwenye vichwa vya habari vya kimataifa mnamo 2023 alipotoa hadithi yake, bado hana athari za hali zote mbili miaka mitano baada ya kupandikizwa seli ambazo ziliondoa magonjwa yote mawili mwilini.

Katika makala mpya ya timu ya madaktari waliomtibu, madaktari walisema alipona rasmi saratani na miaka miwili kabla ya kutangazwa kuwa amepona VVU.

Safari ya matibabu ya Edmonds ilianza alipogundulika kuwa na UKIMWI mwaka 1988, wakati ambapo virusi hivyo viliua wanaume wengi wanaofanya mapenzi ya jinsia moja.

Licha ya kuwatazama marafiki zake wengi wakifa kutokana na maambukizo hayo, hakufa, na aliishi hadi utambuzi mbaya wa leukemia mnamo 2018 nusura ukatize matumaini yake ya kuishi maisha marefu.

Alitibiwa saratani hiyo kwa tiba ya seli shina, ambayo inahusisha kuchukua nafasi ya seli zilizoharibiwa na chemotherapy na zile zenye afya kutoka kwa wafadhili, wakati madaktari waliona fursa ya kipekee: kupata wafadhili na mabadiliko ya jeni yanayokinzana na VVU.

Madaktari walitaka kujua kama wanaweza kuiga mafanikio ya wagonjwa wa awali ambao walikuwa wameripotiwa kuponywa VVU na saratani kwa njia hii.

Kulingana na kliniki ya City of Hope huko California, Edmonds ni mmoja wa watano walioshinda magonjwa yote mawili na mtu mzee zaidi kufanya hivyo.

‘Ninashukuru sana… siwezi kuwashukuru vya kutosha,’ Bw Edmonds alisema kuhusu madaktari wake katika kliniki ya City of Hope huko California.

Kupandikiza seli shina ni sehemu ya mwisho ya matibabu ya saratani ya damu kama vile leukemia na lymphoma.

Inatolewa wakati seli za shina zinazounda damu kwenye uboho wa mgonjwa zimeuawa na mionzi au chemotherapy.

Mnamo Novemba 2018, Bw Edmonds alianza matibabu,Alihitaji raundi tatu ili kufikia hatua nzuri, ambapo katikati ya Januari 2019 alifanikiwa.

Mwezi uliofuata alipokea seli kutoka kwa wafadhili wake.

Seli shina alizopewa zilikuwa na nakala mbili za mabadiliko ya nadra ya kijeni inayoitwa CCR5 delta-3, ambayo huwafanya watu kuwa sugu kwa VVU. Asilimia moja hadi mbili tu ya watu wana mabadiliko haya.

VVU hutumia kipokezi CCR5 kuingia na kushambulia mfumo wa kinga, lakini mabadiliko ya CCR5 huzuia virusi kuingia kwa njia hii.

Inakadiriwa kuwa watu milioni 36.3 wamekufa kutokana na magonjwa yanayohusiana na UKIMWI tangu kuanza kwa janga hilo mnamo 1981.

Mwanaume wa Marekani anakaribia kutangazwa kuwa ameponywa VVU na
saratani ya damu
0 Comment

Wagonjwa 40 kubadilishwa nyonga MOIAfyaclass Bongo Social •

Wagonjwa 40 kubadilishwa nyonga MOI

Na Radhia Balozi-MOI

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) Prof. Abel Makubi amewapokea madaktari bingwa wabobezi wa upasuaji wa nyonga Watatu kutoka nchi ya Pakistan watakaoendesha kambi ya siku tano ya upasuaji wa nyonga kwa wagonjwa 40 kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa MOI.

Katika kambi hiyo iliyoanza jana Februari, 26, 2024 jumla ya wagonjwa 40 wanatarajia kufanyiwa upasuaji wa kubadilisha nyonga ambapo pia itatumika kama sehemu ya kuwajengea uwezo wa umahiri madaktari wazawa.

“Nashukuru kwa kuja kwenu, mjisikie mko nyumbani na iwapo mtapata changamoto yeyote msisite kuwasiliana nasi, uwepo wenu hapa ni wa umuhimu kwetu, tunaahidi kuendeleza ushirikiano huu muhimu kwa ustawi wa maendeleo ya tiba hapa MOI” amesema Prof. Makubi

Kwa upande wake kiongozi wa wataalam hao kutoka Pakistan Abdullah Amjad ameushukuru uongozi wa MOI kwa mapokezi mazuri, ukarimu na ushirikiano walioupata.

“Tunashukuru kwa mapokezi mazuri, na tunaahidi kuendeleza ushirikiano huu mzuri” amesema Amjad

Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Mifupa, Nyonga na Magoti Dkt. Athony Assey amesema kambi hiyo imeanza kwa upasuaji wa wagongwa wawili na baadae kuendelea na wengine hadi Machi, 01, 2024 kambi hiyo itakapomalizika.

Kambi hii ni matokeo ya jitihada za Serikali ya awamu ya sita baada ya kuiwezesha MOI kuwa na vipandikizi vyakutosha (Implants) ambapo hapo awali wagonjwa walisubiri huduma hii muda mrefu kutokana na uhaba wa vifaa.

Wagonjwa 40 kubadilishwa nyonga MOI
0 Comment

Mwanajeshi AARON aliyejichoma moto afariki DuniaAfyaclass Bongo Social •

Mwanajeshi AARON aliyejichoma moto afariki Dunia

Mwanajeshi wa Jeshi la Anga la Marekani Aaron Bushnell mwenye umri wa miaka 25 ambaye alijirekodi video akipinga vita dhidi ya Wapalestina, amefariki dunia saa chache baada ya kujichoma moto nje ya Ubalozi wa Israel uliopo Washington DC Nchini Marekani.

Japo Maofisa wa usalama waliokua karibu na eneo la tukio walifanya jitihada za kumuokoa kwa kuuzima moto huo muda mfupi baadae, imeonekana tayari Aaron alikua amejeruhiwa kwa kiasi kikubwa kwani majeraha aliyoyapata ndio yaliyosababisha kifo chake leo.

Aaron ambaye anatokea San Antonio, Texas alisikika akisema maneno yafuatayo kwenye video aliyojirekodi “Sitashiriki tena katika mauaji ya halaiki, nitashiriki katika kitendo cha kupinga kilichokithiri, Palestina huru (ikomboe Palestina!), sehemu ya video hiyo ipo kwenye slide ya pili.

Tukio hili la Aaron limekuja wakati maandamano yakiongezeka nchini Marekani kupinga vita ya Israel dhidi ya Palestina.

Mwanajeshi AARON aliyejichoma moto afariki Dunia
0 Comment

Star wa AFCON 2023, Troost-Ekong kutoka Super Eagles kufanyiwa UpasuajiAfyaclass Bongo Social •

Star wa AFCON 2023, Troost-Ekong kutoka Super Eagles kufanyiwa Upasuaji

Nahodha wa Super Eagles ya NIGERIA, William Troost-Ekong ameripotiwa kuwasili nchini Finland kufanyiwa upasuaji mdogo.

William alipata jeraha hilo wakati wa mchezo wa pili wa Kundi A wa Nigeria kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2023.

Troost-Ekong, ambaye alicheza kwa dakika 90 kwenye mchezo, alifunga bao la ushindi kwa Waafrika Magharibi kutoka kwa penalti katika dakika 55.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari za michezo, Fabrizio Romano, beki huyo wa PAOK atafanyiwa upasuaji nchini Finland kesho ili kurekebisha sehemu iliyopasuka ya biceps femoris katika mguu wake wa kulia.

Beki huyo alikosa mchezo wa mwisho wa kundi la Nigeria dhidi ya Guinea-Bissau kutokana na jeraha.

Beki huyo hata hivyo alirejea kwa ushindi wa Raundi ya 16 dhidi ya Indomitable Lions ya Cameroon.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 pia alicheza kila dakika ya Super Eagles mechi tatu zilizofuata.

Troost-Ekong, mchezaji bora wa mashindano ya AFCON 2023 anatarajiwa kurejea kuichezea PAOK Salonica ya Ugiriki kuelekea mwisho wa msimu.

Star wa AFCON 2023, Troost-Ekong kutoka Super Eagles kufanyiwa Upasuaji
0 Comment

Dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi(ARVs)Afyaclass Bongo Social •

Dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi(ARVs)

ARVs ni kifupi cha neno antiretroviral drugs, ikiwa na maana ya dawa kwa ajili kupunguza makali ya Virusi vya Ukimwi,

Hivo basi ARV sio dawa moja bali ni kundi au mjumuisho wa dawa zote ambazo hutumika kwa Mgonjwa mwenye virusi vya Ukimwi(VVU) na mfano wa dawa hizo ni kama vile;

  •  Zidovudine
  • Tenofovir
  • Abacavir
  • Lamivudine
  • Didanosine
  • Emtricitabine n.k

Dawa za VVU zinaweza kusaidia kupunguza wingi wa virusi, kupambana na maambukizi, na kuboresha maisha yako. Zinaweza kupunguza uwezekano wa kusambaza VVU pia, lakini kama ukizitumia vibaya, bado unaweza kuwapa wengine VVU,

Kumbuka pia; Dawa hizi za ARVs Sio tiba ya kuondoa kabsa VVU.

>>Malengo ya dawa hizi ni:

  • Kudhibiti ukuaji wa virusi vya Ukimwi(VVU)
  • Kuboresha mfumo wako wa kinga ya mwili Kufanya kazi vizuri
  • Kupunguza Dalili au kuzuia kabsa dalili za Ukimwi kujitokeza
  • Kuzuia maambukizi ya VVU kwa wengine.n.k

Imeidhinishwa matumizi ya zaidi ya dazeni mbili za dawa za kurefusha maisha kwa ajili ya maambukizi ya VVU. Mara nyingi dawa hizi(ARVs) hugawanywa katika makundi sita kwa sababu hufanya kazi kwa njia tofauti. Madaktari wanapendekeza kuchukua mchanganyiko au “cocktail” ya angalau dawa kwenye makundi mawili. Hii inaitwa tiba ya kurefusha maisha, au antiretroviral therapy(ART).

Daktari wako atakujulisha hasa jinsi unapaswa kutumia dawa zako kwa usahihi. Unahitaji kufuata maagizo haswa, na haupaswi kukosa hata dozi moja. Ukikosa dozi, unaweza kupata aina za VVU zinazokinzana na dawa, na dawa zako zinaweza kuacha kufanya kazi.

Dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi(ARVs)

Haya ni baadhi ya makundi ambapo dawa za ARVs zimegawanywa;

1. Nucleoside/Nucleotide Reverse Transcriptase Inhibitors (NRTIs)

Kwenye kundi hili kuna dawa kama vile;

  • Abacavir, or ABC (Ziagen)
  • Emtricitabine, or FTC (Emtriva)
  • Lamivudine, or 3TC (Epivir)
  • Tenofovir alafenamide, or TAF (Vemlidy)
  • Tenofovir disoproxil fumarate, or TDF (Viread)
  • Zidovudine or ZDV (Retrovir)

2.Non-nucleoside Reverse Transcriptase Inhibitors (NNRTIs)

Hapa kuna dawa kama vile;

  • Doravirine, or DOR (Pifeltro)
  • Efavirenz or EFV (Sustiva)
  • Etravirine or ETR (Intelence)
  • Nevirapine or NVP (Viramune)
  • Rilpivirine or RPV (Edurant)

3.Protease Inhibitors (PIs)

Kwenye kundi hili kuna dawa kama vile;

  • Atazanavir or ATV (Reyataz)
  • Darunavir or DRV (Prezista)
  • Lopinavir + ritonavir, or LPV/r (Kaletra)
  • Ritonavir or RTV (Norvir)

4. Integrase Inhibitors

Kwenye kundi hili kuna dawa kama vile;

  • Bictegravir or BIC (combined with other drugs as Biktarvy)
  • Cabotegravir and rilpivirine (Cabenuva)
  • Dolutegravir or DTG (Tivicay)
  • Elvitegravir or EVG (Vitekta)
  • Raltegravir or RAL (Isentress)

5.Fusion Inhibitors

Kwenye kundi hili kuna dawa kama vile;

  • Enfuvirtide, or ENF or T-20 (Fuzeon)

6.Capsid Inhibitor

Kwenye kundi hili kuna dawa kama vile;

  •  Lenacapavir(Sunlenca) n.k

Kumbuka; Dawa hizi hutumii moja peke yake zinakuwa kwenye mchanganyiko wa zaidi ya dawa moja(combination) Mfano;

Atazanavir + cobicistat, or ATV/c (Evotaz)
Darunavir + cobicistat, or DRV/c (Prezcobix)
Elvitegravir + TDF + FTC + cobicistat, or EVG/c/TDF/FTC (Stribild)
Elvitegravir + TAF + FTC + cobicistat, or EVG/c/TAF/FTC (Genvoya)

Bictegravir + tenofovir alafenamide + emtricitabine, or BIC/TAF/FTC (Biktarvy)
Dolutegravir + abacavir + lamivudine, or DTG/ABC/3TC (Triumeq)
Dolutegravir + rilpivirine, or DTG/RPV (Juluca)
Dolutegravir  + lamivudine, or DTG/3TC (Dovato)
Elvitegravir + cobicistat +  tenofovir alafenamide + emtricitabine, or EVG/c/TAF/FTC (Genvoya)
Elvitegravir + cobicistat + tenofovir disoproxil fumarate + emtricitabine, or EVG/c/TDF/FTC (Stribild)

Atazanavir + cobicistat, or ATV/c (Evotaz)
Darunavir + cobicistat, or DRV/c (Prezcobix)
Darunavir + cobicistat + tenofovir alafenamide + emtricitabine, or DRV/c/TAF/FTC) (Symtuza)
Non-nucleoside reverse transcriptase inhibitor (NNRTI)-based:

Doravirine + tenofovir disoproxil fumarate + lamivudine, or DOR/TDF/3TC (Delstrigo)
Efavirenz + tenofovir disoproxil fumarate + emtricitabine, or EFV/TDF/FTC (Atripla)
Rilpivirine + tenofovir alafenamide + emtricitabine , or RPV/TAF/FTC (Odefsey)
Rilpivirine + tenofovir disoproxil fumarate + emtricitabine, or RPV/TDF/FTC (Complera)

Abacavir + lamivudine, or ABC/3TC (Epzicom)
Abacavir + lamivudine + zidovudine, or ABC/3TC/ZDV (Trizivir)
Tenofovir alafenamide + emtricitabine, or TAF/FTC (Descovy)
Tenofovir disoproxil fumarate + emtricitabine, or TDF/FTC (Truvada)
Tenofovir disoproxil fumarate + lamivudine, or TDF/3TC (Cimduo)
Zidovudine + Lamivudine or ZDV/3TC (Combivir) N.K

>> Soma pia hapa kuhusu Muda sahihi wa Kutumia dawa za ARVs

>> Tofauti ya ARVs na PEP

Kuna PEP,PrEP,ARVS

Dawa za Kurefusha maisha(ARVs);

Dawa hizi sio za kutibu au kuponyesha kabsa Ukimwi bali hufanya kazi ya kupunguza Virusi vya ukimwi (Viral Load) hali ambayo huupa nafasi Mfumo wa kinga ya mwili kupambana vizuri na maambukizi haya.

Ili dawa hizi zilete matokeo mazuri unashauriwa kutokuacha kutumia dawa kutokana na maelekezo uliyopewa, kwani ni hatari na unaweza kutengeneza hali ya virusi kutokusikia dawa yaani Drug resistance.

Je ni Muda gani wa kuanza dawa za ARVs baada ya kugundulika una HIV?

Zipo Dhana mbali mbali kwenye jamii kuhusu Muda wa Kuanza dawa za ARVs baada ya kugundulika una Virusi vya UKIMWI,

Huku baadhi ya watu wakisema,hutakiwi kuanza dawa za ARVs mpaka uanze kuumwa, je ni kweli?

Soma zaidi hapa chini…!!!

Tiba ya VVU inahusisha unywaji wa dawa zenye ufanisi mkubwa yaani antiretroviral therapy (ART) ambazo hufanya kazi kudhibiti virusi.

ART inapendekezwa kwa kila mtu mwenye VVU.

Watu walio na VVU wanapaswa kuanza ART haraka iwezekanavyo baada ya utambuzi (hata siku hiyo hiyo).

Nimatumaini yangu kwamba umepata majibu kuhusu Muda wa kuanza dawa za kufubaza Virusi vya Ukimwi maarufu kama ARVs.

Dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi(ARVs)
0 Comment

CPR ni nini? na kwanini huokoa maisha baada ya mshtuko wa moyoAfyaclass Bongo Social •

CPR ni nini? na kwanini huokoa maisha baada ya mshtuko wa moyo.

Hivi karibuni mara nyingi tunasikia habari za hata vijana waliokufa kutokana na mshtuko wa moyo. Pia Tunaweza kuona watu wengi wanaougua ugonjwa wa moyo.

Katika mazingira kama haya mara nyingi watu walio na mshtuko wa moyo hawapati huduma ya kwanza na husababisha vifo zaidi.

Ulimwenguni, matibabu ya huduma ya kwanza iitwayo CPR hutolewa kwa watu ambao wamepata mshtuko wa moyo.

Imethibitishwa pia kuwa, kuna watu wengi walionusurika kupitia njia hii. CPR ni nini wakati wa hatari? Nani anaweza kuitoa? Hebu tuone jinsi ya kufanya hivyo.

CPR inatolewa kama matibabu ya huduma ya kwanza kwa wale ambao wamepata mshtuko wa moyo

CPR ni nini?

CPR inajulikana zaidi kama huduma ya kuuamsha Moyo na Mapafu. Kawaida hutolewa kama matibabu ya huduma ya kwanza kwa watu ambao wamepata mshtuko wa moyo.

Tiba hii inaweza kutolewa wakati mtu amepoteza fahamu au ana shida ya kupumua au anaacha kupumua.

Kumpa mtu matibabu haya atapata oksijeni kwenye mapafu yake. Oksijeni hiyo husafiri katika mwili wote kupitia damu.

Hii inaweza kumsaidia mtu kupumua kwa muda. Ulimwenguni kote, kila mtu anatakiwa kufundishwa huduma hii, kutoka kwa watoto hadi watu wazima wamefunzwa kusimamia huduma hii ya kwanza.

Mtu anapokuwa na mshtuko wa moyo, piga simu kupata msaada na umpe CPR mara moja

Huduma hii inapaswa kutolewa wakati gani ?

Mara nyingi katika kumbi za sinema na mitandao ya kijamii, tumeona watu wanaopatwa na mshtuko wa moyo, wakiwekewa mikono kifuani na kupewa pumzi kwenye mdomo kwa aliyepata tatizo. Kisha huonesha mtu huyo akipata fahamu zake.

Sio tu kwenye skrini lakini pia katika hali halisi, matibabu haya yamekuwa yakiokoa maisha kwa wengi. Lakini hii haipaswi kufanywa bila mafunzo sahihi au mwongozo.

Kulingana na tovuti ya British Heart Association, mtu anapopatwa na mshtuko wa moyo, piga simu kwa huduma za dharura na utoe CPR mara moja.

Huduma ya Kitaifa ya Afya ya Uingereza inashauri kwamba wakati mtu amepoteza fahamu na hawezi kupumua kawaida, piga simu kwa gari la wagonjwa mara moja na umpe CPR.

Shirika la Msalaba Mwekundu linatoa mafunzo kwa wafanyakazi wa kujitolea duniani kote. Pia mafunzo haya hutolewa kwa wale wote wa idara ya afya.

Kutoa CPR huongeza nafasi za kuokoa maisha ya mtu huyo.

Hufanyika kitu gani wakati mshtuko wa moyo unapotokea?

Mshtuko wa moyo unapotokea na moyo unaacha kufanya kazi au mapigo ya moyo yanakuwa yasiyo ya kawaida, damu haitiririki kwa kawaida kwenye ubongo na viungo vingine muhimu. Hii inaathiri utendaji kazi wa ubongo.

Wakati mwingine husababisha kifo. Lakini kutoa CPR huongeza nafasi za kuokoa maisha ya mtu huyo.

Daktari Bingwa wa Taasisi ya Kitaifa ya Mishipa ya Moyo ya Bangladesh. Ashraf ur Rehman Damal alisema, “Mashambulizi ya moyo yanaweza kutokea sio tu kwa wagonjwa wa moyo lakini pia kwa wagonjwa wasio na moyo.

Ikiwa mtu amejeruhiwa vibaya na moyo wake unasimama, basi kwa kumpa CPR, muda wake wa kuishi unaweza kuongezeka.”

Pia, tuna muda mfupi tu wakati moyo unasimama. Itachukua dakika 5 hadi 7 tu. Kwa hivyo, ni muhimu kuanza CPR mara moja, anasema.

Mtu aliyeathiriwa anapaswa kuchunguzwa kama anatokwa na damu mahali popote

Njia 7 za kutoa huduma ya CPR

Shirika la Msalaba Mwekundu limeunda matibabu ya CPR katika hatua saba.

Kwanza unahitaji kuhakikisha usalama wa eneo ulilopo. Wakati mwingine ajali inapotokea katika maeneo yenye mafuriko au yaliyoathiriwa na moto, mtu aliyeathiriwa anapaswa kuhamishwa mara moja kutoka eneo hilo.

Seti ya PPE au vifaa sawa vya kinga vinapaswa kutumika ikiwa ni lazima.

Hatua ya pili ni kujua hali ya mtu aliyeathirika kwa kumgusa au kumwita kwa jina. Pia, angalia ikiwa anavuja damu popote.

Katika hatua ya tatu, piga namba ya huduma ya dharura mara moja ikiwa mtu hana fahamu, haitikii, au hana mapigo ya moyo.

Baada ya kukandamiza mara 30 katika mzunguko mmoja, pumzika kidogo.

Katika hatua ya nne, mtu anapaswa kuwekwa kwenye sakafu au kitanda na mikono mbele na kukaa karibu naye.

Katika hatua ya tano, CPR inapaswa kuanza. Kwanza weka mikono yako yote kwenye kifua chake. Weka mkono mmoja juu ya mkono mwingine na ushike vidole kwenye kiganja. Shinikizo linapaswa kuwa angalau inchi 2.

Kila wakati mkono unapaswa kuinuliwa kikamilifu na kukandamiza kifuani. Wakati huo kifua kitarudi kwa kawaida. Bonyeza kwa kiwango cha shinikizo la 100 au 120 kwa dakika. Baada ya kukandamiza mara 30 katika mzunguko mmoja, pumzika kidogo.

Katika hatua ya sita, pumua kupitia kinywa chake. Kwa hili, weka kichwa cha mtu sawa. Shikilia pua yake na kuvuta pumzi kubwa na kuilazimisha kikamilifu ndani ya kinywa chake.

Hii hutokea kwa sekunde. Kisha angalia ikiwa kifua kinapanuka. Vuta pumzi vizuri kabla ya kuvuta pumzi inayofuata.

Hata hivyo, ikiwa kifua hakipanuki au kuinuka mara ya kwanza, fungua macho na mdomo wake ili kuangalia kizuizi.

Katika awamu ya saba, ukandamizaji wa kifua 30 na pumzi mbili zinapaswa kufanyika kwa pande zote. Lakini hakikisha kwamba kila mkandamizo wa kifua hauendelei kwa zaidi ya sekunde 10. CPR inapaswa kuendelezwa hadi usaidizi uwasili.

CPR inatolewa kwa watoto wenye matatizo ya moyo na matatizo ya kupumua.

Huduma ya CPR kwa watoto

Wakati mwingine watoto pia wanahitaji CPR. Inatolewa kwa watoto wenye matatizo yanayohusiana na moyo na matatizo ya kupumua.

Huduma ya Kitaifa ya Afya ya Uingereza inasema kuna mambo machache ya kukumbuka wakati wa kutoa CPR kwa watoto.

Kwanza weka mkono mmoja juu ya kichwa cha mtoto na ukiinue kutoka nyuma. Ikiwa kitu chochote kimekwama kwenye kinywa na pua, kinapaswa kutolewa nje.

Baada ya hayo kushikilia pua ya mtoto na kupumua kwa kinywa chake. Wakati huo huo, angalia ikiwa kifua kinainuka au la.

Kisha weka kiganja kimoja kwenye kifua cha mtoto na uweke shinikizo kwa inchi mbili. Ikiwa huwezi kufanya hivyo kwa mkono mmoja, unaweza kutumia mikono yote miwili.

Ndiyo sababu inashauriwa kutumia vidole viwili tu badala ya mikono miwili ikiwa mtoto ni chini ya mwaka mmoja. Inchi moja na nusu tu ya shinikizo inapaswa kutumika.

Pia, pumzi 100 hadi 120 kwa dakika zinaweza kutolewa mara mbili kwa mdomo katika pumzi 30-30. CPR inapaswa kuendelea hadi huduma ifike.​

CPR ni nini? na kwanini huokoa maisha baada ya mshtuko wa moyo
0 Comment

Muigizaji wa Smallville Chris Gauthier amefariki akiwa na umri wa miaka 48Afyaclass Bongo Social •

Muigizaji wa Smallville Chris Gauthier amefariki akiwa na umri wa miaka 48.

Muigizaji wa Kanada Chris Gauthier, anayejulikana sana kwa uigizaji wake katika filamu za Once Upon a Time, Eureka, na Smallville, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 48, wawakilishi walithibitisha.

TriStar Appearances’ Chad Colvin alichapisha kuhusu hilo,kwenye taarifa yake ndani ya mtandao wa Facebook mnamo Jumapili, Februari 25.

Colvin aliandika kwamba mke wa Gauthier “aliponifikia jana na habari hizo, nililia kwa saa nyingi kwa sababu ya kutoamini. Imenichukua hadi sasa kujiimarisha kiakili na kihisia kuandika haya.”

Tristar Appearances/Event Horizon Talent baadaye alithibitisha habari hizo kwa Fox News Digital katika taarifa, akiandika kwamba Gauthier alifariki Ijumaa asubuhi, Februari 23.

Sababu ya kifo haikutangazwa lakini usimamizi wake ulisema “alikufa kutokana na ugonjwa wa muda mfupi ambao haukutajwa.”

Gauthier ana sifa zaidi ya 100 kwa jina lake, kulingana na IMDb. Ni Miongoni mwa watu mashuhuri zaidi,pamoja na mhusika Smee katika safu ya uigizaji kwenye, Once Upon a Time, na Vincent huko Eureka.

“Chris alikuwa ufafanuzi halisi wa kitabu cha muigizaji,” Colvin aliandika kwa heshima.

“Unaweza kuwa hujui jina lake lakini ulijua sura yake, ulijua sauti yake, na ulijua kwamba ikiwa alikuwa kwenye skrini, ulikuwa kwenye safari ya heluva.

“Iwapo alikuwa amesimama kidole-kwa-mguu dhidi ya Clark Kent huko Smallville kama Toyman, akimtesa Dean juu ya Miujiza, kwenye sitaha na Hook kama Smee katika Once Upon A Time au katika majukumu ya wageni katika maonyesho mengi ambayo alikuwa ndani, alitoa kila wakati. yote ni yake wakati kamera ilipokuwa inazunguka.”

Mwigizaji mwenza wa Gauthier’s Once Upon a Time, Colin O’Donoghue, alishiriki picha kwenye Instagram ya wanandoa hao wakirekodi mfululizo huo pamoja na heshima yake mwenyewe: “Rest in Peace Chris! Umevunjika moyo! Mapenzi na mawazo yangu yanaenda kwa Erin na wavulana! Utakumbukwa ndugu! Ulikuwa nahodha wa kweli!!”

Gauthier ameacha mke na watoto.

Muigizaji wa Smallville Chris Gauthier amefariki akiwa na umri wa miaka
48
0 Comment

Hii ndyo hali ya Ally Kamwe baada ya kuwaishwa na kulazwa hospitaliniAfyaclass Bongo Social •

Hii ndyo hali ya Ally Kamwe baada ya kuwaishwa na kulazwa hospitalini.

Club ya Yanga imethibitisha kuwa Meneja wake wa Idara ya Habari na Mawasiliano Ally Kamwe alipata changamoto ya afya na kuwaishwa hospitali muda mfupi kabla ya mechi ya Yanga na CR Belouizdad kumalizika.

Imeelezwa kwamba Kamwe anaendelea vizuri kwa sasa baada ya kupatiwa matibabu na ameonesha kuimarika kiafya wakati alipotembelewa Hospitalini hapo na Rais wa Yanga Hersi Said, Makamu wa Rais wa Yanga Arafaj Haji, Wachezaji wa Yanga Pacome Zouzoua na Azizi Ki na Waziri wa Madini Anthony Mavunde.

Kwa Updates mbali mbali za Afya; Link in https://afyaclass.com

Hii ndyo hali ya Ally Kamwe baada ya kuwaishwa na kulazwa hospitalini
0 Comment

Dawa ya kupunguza kuzaliana kwa Virusi vya Ukimwi hii hapaAfyaclass Bongo Social •

Dawa ya kupunguza kuzaliana kwa Virusi vya Ukimwi.

Utafiti mpya waonyesha; Novel RNA nanomedicine kupunguza kuzaliana kwa virusi vya Ukimwi yaani HIV replication kwa asilimia 73%,

Mpaka sasa hakuna Tiba kamili ya kuponyesha kabsa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(HIV/AIDS), ingawa dawa zinazotumika kwa waathirika wa VVU husaidia kudhibiti dalili zake kwa kiwango kikubwa.

Soma Zaidi hapa; Dawa zinazotumika kwa waathirika wa HIV

Watafiti wa Kanada wamebuni njia mpya ya kutumia RNA kusaidia kupambana na VVU kwa kutumia tiba ya jeni yaani “gene therapy”.

Takwimu zinaonyesha; Kufikia mwaka wa 2022, takriban watu milioni 39 duniani kote wanaishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi, vinavyojulikana zaidi kama VVU.

HIV(VVU) ni virusi vinavyoshambulia mfumo wa kinga ya mwili na seli zake nyeupe za damu. Hii inafanya mtu kuwa Kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi na magonjwa mengine.

Mpaka Hivi sasa, hakuna tiba ya VVU. Madaktari wanaweza kutumia tiba ya kurefusha maisha (ART) ili kusaidia kudhibiti ugonjwa huo. Hata hivyo, bado si tiba kamili ya kuondoa kabsa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU).

Sasa, watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Waterloo nchini Kanada wamebuni njia ya kutumia ribonucleic acid (RNA) kulingana na Chanzo Kinachoaminika ili kupambana na VVU kwa kutumia tiba ya jeni(gene therapy).

Utafiti huu umechapishwa hivi karibuni kwenye jarida la “The Journal of Controlled Release”.

Je, ni nini RNA hufanya kwenye VVU(HIV)?

Kwa utafiti huu, watafiti waliunda nanomedicine mpya iliyojazwa na vifaa vya kijeni inayoitwa RNAs ndogo zinazoingilia (siRNA)

“siRNA ilichaguliwa kama tiba inayoweza kutumika kwa sababu inaweza kuundwa ili kudhibiti udhihirisho wa jeni maalum katika mwili,” mwandishi mkuu wa utafiti Dk. Emmanuel Ho, profesa msaidizi katika Shule ya Famasia katika Chuo Kikuu cha Waterloo, alielezea Medical News.

“Faida za hii ni pamoja na uwezekano mdogo wa athari kwa kulinganisha na dawa za kawaida za molekuli ndogo.”

Kwa vile siRNAs zinaweza kuamuru ni jeni ipi au protini zipi zinaweza kuguswa au kuzimwa kwenye seli, watafiti waliripoti kuwa zilisababisha kupunguza kuzaliana kwa Virusi vya Ukimwi(VVU) kwa asilimia 73%.

Zaidi ya hayo, dawa mpya ya nanomedicine ilisaidia kukabiliana na masuala yanayowasilishwa na VVU linapokuja suala la autophagy “mpango wa kuchakata tena” wa mwili ambapo hutumia tena sehemu za seli za zamani na zilizoharibiwa na pia husaidia mwili kuondokana na virusi na bakteria.

“Dawa za sasa za VVU huingilia mzunguko wa maisha ya virusi katika hatua tofauti, hivyo mchanganyiko wa dawa ni muhimu kukandamiza ukuaji wote wa VVU,”

“Ikiwa virusi vya UKIMWI vimezuiliwa kwenye seli iliyoambukizwa na seli itajiharibu yenyewe, basi virusi haviwezi kuzidi au kuzaliana mwili mzima na kuharibu seli muhimu za kinga, ziitwazo msaidizi wa T-cells.

Wakati chembe-saidizi za kutosha za T zinaharibiwa, mfumo wa kinga ya mtu hudhoofika na mtu anakuwa katika hatari ya kuambukizwa tena.”

Dk. Liu alisema pamoja na kwamba madaktari wanapata baadhi ya dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi, lakini hazijawa na nguvu nyingi na haziwezi kuzuia VVU peke yake.

“Dawa zenye nguvu zaidi za VVU kwa sasa ni zile zinazosimamisha mzunguko wa maisha ya virusi, lakini bado zina madhara ya muda mrefu, ingawa ni kwa kiasi cha chini sana kuliko dawa za VVU za kizazi cha kwanza.

Ikiwa dawa hii ya nanomedication itatumika kuzuia maambukizi ya VVU, inapaswa kusaidia katika kupunguza idadi ya maambukizi ya VVU ulimwenguni kote. Kuzuia VVU ni bora zaidi kuliko kujaribu kutibu wagonjwa ambao tayari wameambukizwa.

– Dk. Edward Liu, mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza anasema; Bado kuna uhitaji unaoendelea wa matibabu mapya ya VVU,

Dk. Ho alisema kutokana na kukosekana kwa chanjo madhubuti ya VVU, tiba mpya za VVU bado zinahitajika.

“Matibabu ya sasa ya VVU husaidia kupunguza kiasi cha VVU mwilini, lakini kwa sasa hakuna tiba kamili,” alisema.

“Zaidi ya hayo, wagonjwa wengine wanaweza kupata aina za VVU zinazokinzana na dawa, na hivyo kufanya matibabu ya sasa yasiwe na matokeo.”

Tafiti za awali ziliripoti kuwa asilimia 10% ya watu wazima wanaoanza matibabu ya VVU wana ukinzani kwa aina ya tiba ya kurefusha maisha inayoitwa non-nucleoside reverse transcriptase inhibitors (NNRTSs)Chanzo Kinachoaminika kiliripoti.

Mbali na kupata UKIMWI, watu wenye VVU wako katika hatari kubwa ya magonjwa kadhaa, ikiwa ni pamoja na:

RNA inaweza kusaidia kukulinda dhidi ya maambukizi ya VVU,Na Wanasayansi walitengeneza dawa mpya ya nanomedicine ili iweze kutumika kwa njia ya uke, kupunguza kuzaliana kwa virusi vya Ukimwi yaani HIV replication.

Dawa ya kupunguza kuzaliana kwa Virusi vya Ukimwi hii hapa
0 Comment

Zaidi ya wanawake 100 wahukumiwa kifungo kwa kuwatuma watoto wao kuwa omba ombaAfyaclass Bongo Social •

Zaidi ya wanawake 100 wahukumiwa kifungo kwa kuwatuma watoto wao kuwa omba omba.

Mahakama nchini Uganda imewahukumu zaidi ya wanawake 100 kifungo cha mwezi mmoja kila mmoja baada ya kukiri kuwatuma watoto wao kuwa omba omba katika mji mkuu wa Kampala.

Mahakama hiyo pia imepiga marufuku wanawake hao kurejea mjini na kuamuru warudishwe kijijini kwao, gazeti la kibinafsi la Daily Monitor liliripoti.

Hata hivyo wanawake hao waliomba kuhurumiwa, huku wengine wakisema ni wajane na wengine ni mama wasio na wenza, gazeti la serikali la New Vision liliripoti.

Je, hatua ya namna hiyo itasaidia kupunguza watoto ombaomba mtaani?

Zaidi ya wanawake 100 wahukumiwa kifungo kwa kuwatuma watoto wao kuwa
omba omba
0 Comment

Raia wa Togo ni miongoni mwa watu waliokuwemo katika ajali ARUSHAAfyaclass Bongo Social •

Raia wa Togo ni miongoni mwa watu waliokuwemo katika ajali iliyotokea Februari 25. 2024 katika eneo la Ngaramtoni mkoani Arusha
na kusababisha vifo vya watu 25 na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa.

Kwa sasa Apelo anapatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Arusha, Mount Meru ambapo ameishukuru Serikali kwa huduma nzuri za matibabu anazopatiwa hospitalini hapo.

Amesema kwa namna ajali hiyo ilivyokuwa na huduma alizopatiwa kama asingekuwa Tanzania angekuwa amekwishafariki dunia na kwamba ukarimu wa Watanzania ndio uliookoa maisha yake.

“Kwa ajali hii ningekuwa nchini kwetu tayari ningekuwa nimepoteza maisha, kwani kule bila kulipia huduma za matibabu hupatiwi huduma, lakini kwa Tanzania walivyo wakarimu na weledi wameweza kuokoa maisha yangu mpaka sasa naendelea vizuri na naweza kuongea,” Amesema raia huyo wa Togo

Apelo alikuja Tanzania kushiriki kwenye semina iliyokuwa ikifanyika mkoani Arusha, ambapo pia walikwenda kufanya utalii na walipokuwa wakirejea ndipo wakapata ajali.

Raia wa Togo ni miongoni mwa watu waliokuwemo katika ajali ARUSHA
0 Comment

Idadi waliofariki dunia kwenye Ajali Arusha yafika 25Afyaclass Bongo Social •

Idadi waliofariki dunia kwenye Ajali Arusha yafika 25

Gari la Shule ya Mchepuo wa Kiingereza ya New Vision, likinyanyuliwa baada ya kugongwa na lori katika eneo la Kibaoni (Ngaramtoni), wilayani Arumeru leo Jumamosi Februari 24, 2024 katika Barabara Kuu ya Arusha-Namanga

Ajali ilitokea Februari 24, 2024 eneo la Kibaoni (Ngaramtoni), wilayani Arumeru ikihusisha magari manne.

Arusha. Idadi ya vifo vilivyotokana na ajali iliyohusisha magari manne eneo la Kibaoni (Ngaramtoni), Barabara Kuu ya Arusha-Namanga imeongezeka na kufikia 25, majeruhi wakiwa 21.

Ajali ilitokea Jumamosi Februari 24, 2024 ikihusisha lori na magari mengine madogo matatu.

Akitoa taarifa jana usiku katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru, Kamishna wa Polisi Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Awadhi Juma Haji amesema miongoni mwa waliofariki  wanawake ni 11, akiwamo mtoto mdogo wa kike na raia wa kigeni saba.

Ajali ilihusisha lori lenye namba za usajili KAC 943 H aina ya Mack lenye tela namba ZF 6778 mali ya kampuni ya KAY Construction ya Nairobi nchini Kenya.

“Idadi ya majeruhi ni 21 kati yao wanaume ni 14 na wanawake ni saba,” amesema.

Magari mengine yaliyopata ajali katika tukio hilo ni T 623 CQF aina ya Nissan Caravan, T 879 DBY aina ya Mercedes Benz Saloon na T 673 DEW aina ya Toyota Coaster mali ya shule ya mchepuo wa Kingereza ya New Vision.

Kuhusu chanzo cha ajali, amesema uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa ni kufeli mfumo wa breki wa lori, hivyo kusababisha liyagonge magari mengine yaliyokuwa mbele yake.

Amesema Jeshi hilo linaendelea kumsaka dereva wa lori hilo anayedaiwa kutoroka baada ya ajali.

Awali, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo alitaja idadi ya waliofariki kuwa ni 15 na kati yao raia wa kigeni walikuwa watatu.

Credits:Mwananchi.

Idadi waliofariki dunia kwenye Ajali Arusha yafika 25
0 Comment

Tatizo la mwili kuchoka sana,Chanzo,dalili na TibaAfyaclass Bongo Social •

Tatizo la mwili kuchoka sana,Chanzo,dalili na Tiba

Tatizo la mwili kuchoka sana ni hali ambayo mtu anajisikia uchovu mkubwa, unaoweza kuathiri utendaji wa kazi za kila siku. Hali hii inaweza kuwa ni ishara ya matatizo ya kiafya, msongo wa mawazo, au hata mtindo wa maisha usiofaa. Kuelewa chanzo, dalili, na tiba ya uchovu mkubwa ni muhimu katika kuchukua hatua za kuboresha afya na ustawi wa mwili kwa jumla.

Tatizo la mwili kuchoka sana huweza kutokea kwa Sababu nyingi tofauti zinazohusu hali ya kiakili pamoja na kimwili(mental and physical health conditions),

Katika Sababu hizo, baadhi huhitaji matibabu ya haraka maana ni hatari zaidi(Serious), na zingine huhusisha tu njia za kwaida za kubadili mtindo wa miasha(lifestyle) ili kuondoa uchovu wa mwili kama vile;

  • Kuanza kufanya mazoezi
  • Kuzingatia mlo wenye afya
  • Kupata usingizi wa kutosha n.k

Chanzo cha Mwili Kuchoka Sana

Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha mwili kuchoka sana, zikiwemo:

1. Msongo wa Mawazo na Mahangaiko:

Msongo wa mawazo wa muda mrefu unaweza kupelekea mwili kujisikia uchovu mkubwa.

2. Matatizo ya Kiafya:

Kuna hali ambazo huweza kusababisha tatizo la nwili kuchoka sana ikiwa kama Ishara au dalili ya tatizo flani la kiafya,

Mfano,Hali kama vile;

3. Lishe Duni:

Ukosefu wa virutubisho muhimu kama vile madini ya chuma, vitamini B12, na magnesium unaweza kusababisha mwili kujisikia dhaifu.

4. Ukosefu wa Usingizi: Kutopata usingizi wa kutosha au usingizi usio na ubora kunaweza kupelekea uchovu wa muda mrefu.

Hivo hakikisha unapata muda wa kutosha wa kulala kama una shida ya uchovu sana wa mwili.

5.Matumizi ya Pombe na Dawa za Kulevya:

Matumizi mabaya ya pombe na dawa za kulevya yanaweza kuchangia uchovu.

6. Matatizo ya Akili:

Hali kama vile mfadhaiko(depression),msongo wa mawazo(stress) na wasiwasi zinaweza kuwa na dalili ya uchovu. n.k

Dalili za Mwili Kuchoka Sana

Dalili za uchovu mkubwa zinaweza kujumuisha:

– Kujisikia uchovu hata baada ya kupumzika au kulala.

– Kupungua kwa motisha au nia ya kufanya shughuli.

– Ugumu wa kuzingatia vitu au kukumbuka.

– Kujisikia dhaifu kimwili au kiakili.

– Kuwa na Hisia za kukosa nguvu au uchovu unaoendelea.n.k

Tiba ya Mwili Kuchoka Sana

Tiba ya uchovu mkubwa inategemea chanzo cha tatizo. Hata hivyo, kuna hatua kadhaa za jumla ambazo zinaweza kuchukuliwa ikiwemo:

✓ Kuboresha Lishe Yako: Hakikisha unapata lishe bora inayojumuisha matunda, mboga, protini, na wanga wenye afya. Virutubisho kama vile madini ya chuma na vitamini B12 vinaweza kuwa muhimu hasa ikiwa uchovu unasababishwa na upungufu wa damu.

✓ Pata Usingizi wa Kutosha: Hakikisha unapata usingizi wa kutosha na wenye ubora kwa kufuata ratiba ya kulala na kuamka, na kuepuka vichocheo kama vile caffeine na vifaa vya Kielektroniki kama vile Simu,TV n.k kabla ya kulala.

✓ Dhibiti Msongo wa Mawazo: Jifunze mbinu za kupunguza msongo wa mawazo kama vile kufanya mazoezi ya viungo n.k. Kupata ushauri wa kitaalamu pia kunaweza kusaidia.

Soma Zaidi hapa; Jinsi ya kudhibiti tatizo la Msongo wa mawazo

✓ Fanya Mazoezi ya Mara kwa Mara: Mazoezi ya mara kwa mara yanaweza kuboresha nguvu za mwili, hali ya akili, na ubora wa usingizi.

✓ Epuka Pombe na Dawa za Kulevya: Kupunguza au kuacha matumizi ya pombe na dawa za kulevya kunaweza kusaidia kupunguza uchovu.

✓ Angalia Afya Yako ya Akili: Kutafuta msaada wa kitaalamu kwa matatizo ya akili kama vile unyogovu na wasiwasi kunaweza kuboresha hali ya uchovu.

✓ Pata Uchunguzi wa Kitabibu: Kama uchovu unaendelea licha ya kuchukua hatua hizi, ni muhimu kufanya uchunguzi wa kitabibu ili kutambua iwapo kuna magonjwa yanayosababisha uchovu huo.

Hitimisho

Kwa kumalizia, mwili kuchoka sana ni hali inayoweza kusababishwa na sababu nyingi, na inaweza kuathiri maisha ya kila siku. Kuchukua hatua kuelekea mtindo wa maisha wenye afya, kudhibiti msongo wa mawazo, na kutafuta ushauri wa kitaalamu kunaweza kusaidia katika kushughulikia tatizo hili.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Tatizo la mwili kuchoka sana,Chanzo,dalili na Tiba
0 Comment

Majeraha kichwani yasababisha tatizo la kukosa Usingizi kwa miaka 40Afyaclass Bongo Social •

Mwanajeshi Kern Paul kutoka Hungury hakuwahi kulala kwa miaka 40 baada ya kupigwa risasi kichwani wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia.

Usingizi ni moja kati ya vitu muhimu kwa binadamu. Ingawa baadhi ya watu hulala saa chache na wengine hulazimika kutumia vinywaji kama kahawa, ili kuwa macho muda mrefu, hii imekuwa tofauti kwa Kern Paul, mwanajeshi kutoka nchini Hungury ambaye hakuwahi kusinzia kwa miaka 40.

Stori hii inaanza miaka ya 1914, wakati dunia inaingia kwenye vita ya kwanza ya dunia iliyoibuka baada ya kuuawa kwa aliyekuwa kiongozi wa Austria, Archduke Franz Ferdinand na mke wake.

Kern, alikuwa mmoja kati ya wananchi waliojiunga na jeshi kwa ajili ya vita na akapangwa kwenye kikosi maalumu cha elite shock troop.

Kikosi hicho mara nyingi ndio huwa mstari wa mbele kwenye vita, hivyo askari wake huwa kwenye hatari ya kuuawa ama kupata majeraha makubwa.

Mwaka 1915 wakati wa mapambano na wanajeshi wa Russia, Kern alipigwa risasi ya kichwa iliyomsababishia majeraha hayo kiasi cha kutoweza tena kulala.

Baada ya kupelekwa hospitali ya Lemberg  kwa matibabu, baada ya vipimo daktari alieleza kwamba Kern anaweza kufariki ikiwa risasi itatolewa kwenye kichwa chake.

Kwa mujibu wa tovuti ya SOFREP, risasi hiyo iliingia kwenye fuvu la kichwa chake na kugusa sehemu ya ubongo iitwayo frontal lobe, ambayo huwa na kazi za hisia, kupanga na kutatua matatizo.

Kern alilazimika kurudi uraiani kutokana na tatizo hilo, lakini ajabu tangu wakati huo hakuwahi  kupata usingizi kwa miaka 40 hadi alipofariki dunia, licha ya kujilazimisha kufanya hivyo.

Kwa mujibu wanasayansi kutoka Marekani, muda mrefu ambao binadamu anaweza kukaa bila ya kulala ni saa 264 (sawa na siku 11), lakini kwa Kern inaonekana kuwa tofauti.

Mara nyingi ukikosa kulala unapata madhara mengi ikiwa pamoja na kupoteza kumbukumbu, kupata tabu ya kufikiria mambo, kuwa na kinga ndogo ya mwili, kuwa kwenye hatari ya kupata kisukari, shinikizo la damu na magonjwa ya moyo, lakini Kern hakuathirika kabisa na hili kiasi cha madaktari kueleza huenda alikuwa akilala bila ya yeye kujua.

Kwa mujibu wa tovuti ya Sofrep, baadhi ya madaktari walidai ni ngumu mtu kukaa muda wote huo bila ya kulala na kuna uwezekano Kern alikuwa akilala mchana bila hata ya yeye kujua kama amelala.

Madokta wengine walisema mwanajeshi huyu alikuwa anatunga tu maneno. Kern anadaiwa alitembelea hospitali zote za madaktari waliokuwa wakisema maneno hayo ili wamfanyie vipimo na baada ya hapo waligundua kuwa ni kweli Kern hakuwa na uwezo wa kulala.

Alifariki dunia mwaka 1955 akiwa na umri wa miaka 71, jambo ambalo pia lilishangaza wataalamu wengi wa masuala wa afya kwa sababu moja ya matokeo ya mtu kutolala kwa muda mrefu ni kufariki mapema.

Soma Zaidi; Tips au Dondoo za kukusaidia ulale vizuri

Chanzo cha kukosa Usingizi; Soma hapa Zaidi

Majeraha kichwani yasababisha tatizo la kukosa Usingizi kwa miaka 40
0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD