Tatizo la Afya ya Akili na Ugonjwa wa SononaAfyaclass Bongo Social •

Tatizo la Afya ya Akili na Ugonjwa wa Sonona
whatsapp sharing button
Afya ya Akili

Afya ya akili maana yake ni hali ya kuwa sawa kihisia, kisaikolojia na kijamii inayoambatana na kuwa na uwezo wa kutatua changamoto za kila siku. Ni hali ya kuwa na mawazo chanya, kuwa sawa kijamii na kisaikolojia na kuweza kuchangia katika utendaji wako na uwezo wa kuridhisha wa kimawazo na kitabia. Huhusisha uwezo wa mtu kumudu mfadhaiko wa kihisia kama vile wasiwasi, upweke, hasira, huzuni; ikiwa na maana ya kuwa mstahimilivu na kuwa na mchango katika jamii inayomzunguka.

Afya ya akili inaathiri jinsi tunavyofikiri, kuhisi, na kutenda. Pia husaidia kuamua jinsi tunavyokabiliana na mafadhaiko, kuhusiana na wengine, na kufanya maamuzi yanayofaa. Afya ya akili ni muhimu katika kila hatua ya maisha, kuanzia utotoni na ujana hadi utu uzima. Kumekuwa na tafsiri ambayo si sahihi katika jamii yetu ya kuwa afya ya akili ni hali ya kutokuwa sawa, afya ya akili ni tatizo, afya ya akili ni ugonjwa wa akili, afya ya akili ni upungufu wa akili. Tafsiri hizi zote hazipo sawa. Ukweli ni kwamba afya ya akili ni afya; hakuna afya pasipo afya ya akili. Afya ya akili sio ugonjwa wa akili na hakuna kitu kinachoitwa ugonjwa wa afya ya akili. Kuna umuhimu wa kujifunza maneno haya ili kupunguza unyanyapaa wa afya ya akili katika jamii zetu.

Ugonjwa wa Akili

Ugonjwa wa akili ni hali ya kutokuwa sawa inayoathiri utendaji kazi wa mtu na madiliko huweza kuonekana katika hisia, fikra na matendo tofauti na yale yanayotarajiwa na jamii na hivyo kushindwa kukabiliana na changamoto za maisha. Kuna zaidi ya magonjwa 200 ya akili, ikiwa ni pamoja na sonona, uraibu, wasiwasi uliopitiliza, skizofrenia, baipolar (mawazo mseto).

Ugonjwa wa Sonona

Sonona ni ugonjwa wa akili unaohusisha hali endelevu ya huzuni au kukosa shauku au raha inayoambatana na mabadiliko mbalimbali ya kimwili, kihisia na kiakili pia. Sonona ni hali inayoathiri utendaji kazi mzima wa mtu. Kuna utofauti mkubwa kati ya sonona na msongo wa mawazo. Aidha, msongo wa mawazo uliokithiri huweza kusababisha sonona.

Ugonjwa huu unatokana na namna tunavyotatua changamoto tunazokutana nazo katika maisha yetu ya kila siku. Sonona ni mrejesho wa hisia tulizozibeba ndani yetu kutokana na nyakati mbalimbali tunazozipitia. Hii inaweza kuwa kwa kupanga kutokana na utofauti katika utatuzi wa changamoto zetu. Kushindwa kukabiliana na changamoto za maisha ndio mwanzo wa kupata sonona. Sonona ni moja kati ya magonjwa ya afya ya akili ulimwenguni ikiwa na zaidi ya watu milioni 264 kwa mwaka wanaoathirika na changamoto hii. Hii ni hali inayoongoza kwa kuleta mzigo mkubwa kwa wagonjwa wengi duniani na katika hali iliyokithiri inaweza kusababisha mtu kuondoa uhai wake.

Watu wengi hupata msongo wa mawazo, ikiwa ni changamoto ya afya ya akili na ni hali ya kawaida kukutana nayo katika maisha. Msongo wa mawazo ukikithiri hupelekea sonona. Sonona pia ikikithiri hupelekea tatizo liitwalo Sonona Kubwa (Major Depressive Disorder, MDD). Sonona Kubwa ni kiwango cha juu cha tatizo ambacho kinahitaji matibabu ya haraka na kitaalamu zaidi.

Takwimu zinaonesha kuwa takriban watu milioni 350 wameathirika na magonjwa ya akili na zaidi ya watu 800,000 kila mwaka hufariki kwa kuondoa uhai wao wenyewe na hii hutokea sana kwa vijana kuanzia umri wa miaka 15 hadi 29. Ongezeko la changamoto za afya ya akili linakuja kwa kasi ulimwenguni kote ikiwemo Tanzania.

Kutokana na malengo ya maendeleo endelevu (SDG) yaliyooanzishwa mwaka 2015 na Baraza la Umoja wa Mataifa likiwa na malengo ya kufikiwa mwaka 2030, mkusanyiko huo wa malengo 17 yaliyopangiliwa kwa faida ya watu wote; lengo namba tatu ambalo ni “Afya Njema na Ustawi” linahakikisha kila mtu anapata huduma za afya bora. Sonona ni moja kati ya vipaumbele vya Shirika la Afya Duniani kupitia mpango mkakati uitwao WHO’s Mental Health Gap Action Programme (mhGAP) ikilenga kusaidia nchi mbalimbali, haswa kwa nchi za kipato cha chini na kati kuongeza utoaji huduma juu ya afya ya akili na magonjwa mbalimbali ya mfumo wa fahamu.

Kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa na Lancet Global Health, zinaonesha kuwa kuna uhaba wa takwimu juu ya afya ya akili barani Afrika hali ambayo inaonesha ni jinsi gani bado huduma hizi ni duni barani. Changamoto za afya ya akili zimekuwa zikiongezeka kwa kiasi kikubwa barani Afrika, kitu ambacho kinahitaji kuwekewa mkazo wa hali ya juu. Idadi ya watu barani Afrika inasadikika kuongezeka mara mbili katika miongo mitatu ijayo. Ongezeko la watu linaenda sambamba na ongezeko la changamoto za afya ya akili. Watu wengi hasa vijana wako katika hatari ya kuathirika na changamoto hizi, hii ikitokana na misukumo mbalimbali katika jamii na utumiaji wa dawa za kulevya ukiongezeka ikiwa kama njia kuu ya wahanga hawa kutumia kuepukana na changamoto hizo.

Je, Utajuaje Kama Una Sonona?

Ubaya ni pale ambapo mgonjwa wa sonona hajijui kama anasonona. Hii inapelekea kuongezeka kwa idadi kubwa ya waathirika na kukithiri kwa tatizo. Sonona ni ugonjwa usiofichika. Kupitia muongozo wa magonjwa mbalimbali ya akili (DSM V) pamoja na toleo la Kiswahili – Tiba Baina ya Watu (TBW) kwa International Rescue Committee (IRC) kutoka kwa Shirika la Afya Duniani tunaweza kuona vitu mbalimbali vinavyoweza kuashiria kuwa wewe ni muathirika wa ugonjwa wa akili, sonona. Dalili za sonona hujumuisha:

  • Mabadiliko ya usingizi aidha kulala sana ama kukosa usingizi kabisa.
  • Mabadiliko katika kula, aidha kukosa kabisa hamu ya kula ama kula sana.
  • Hisia za kujiona mwenye hatia au hufai.
  • Hisia za uchovu na umakini hafifu kazini.
  • Kukosa utulivu wa mwili na kihisia pia.
  • Ugumu katika kufanya maamuzi.
  • Kupungua uzito bila kutarajia, takribani 5% kwa mwezi ama kuongezeka uzito.
  • Kusononeka kila wakati, huzuni endelevu.
  • Kujitenga mbali na watu na kupendelea kukaa peke yako muda mwingi.
  • Kukosa matumaini kabisa.
  • Kupoteza msisimko wa kihisia na kukosa hamu ya tendo la ndoa.
  • Kuwa mvivu hata kwenye shughuli za kawaida.
  • Kupata maumivu ya mwili kama vile kichwa kuuma mara kwa mara, vidonda vya tumbo, kujihisi mchovu mara kwa mara, kushindwa kuzungumza, kushindwa kutembea.
  • Kuwa na hasira mara kwa mara hata sehemu zinazohitaji utulivu.
  • Kujawa na chuki juu ya wengine na kutoelewana na watu wanakuzunguka.
  • Kutamani kujidhuru na hatimaye kuondoa uhai wa mtu binafsi au pamoja na wale wanaomtegemea.
  • ubadilika katika siku za hedhi au kukosa kabisa.
  • Uraibu hasa wa pombe.
  • Kusahau na kukosa uwezo wa kufikiri vema.

Sababu za Ugonjwa wa Sonona

Visababishi vya ugonjwa wa sonona vinaweza kuwa katika makundi makuu matatu: kibailojia, kisaikolojia na kijamii.

1. Sababu za Kibailojia

  • Kurithi kwa vinasaba vya ugonjwa wa sonona. Uwepo wa historia ya ugonjwa huu katika familia huongeza uwezekano wa mtu kupata tatizo hili. Hii inamaanisha ugonjwa huu unaweza ukawa ni wa kurithi kutoka kizazi hadi kizazi, japokuwa kutokuwepo kwa historia ya ugonjwa huu katika familia haina maana ya kuwa hakuna uwezekano wa kupata.
  • Magonjwa ya mwili. Magonjwa ya mwili aidha ya muda mfupi kama vile malaria kali ama magonjwa sugu yaani ya muda mrefu kama vile kisukari, homa ya ini, saratani, UKIMWI, figo kushindwa kufanya kazi, nk.

2. Sababu za Kisaikolojia

  • Malezi. Watu wengi wanaopata ugonjwa huu wa sonona huwa wanahistoria ya kupata changamoto katika malezi yao walipokuwa watoto. Malezi kwa mtoto yanamchango mkubwa sana katika kujenga ama kuharibu afya ya akili ya mtoto.
  • Matukio ya kuhuzun

3. Kijamii

  • Matukio kama vile kukosa ajira, matatizo sehemu za kazi, kufukuzwa kazi/chuo, migogoro kazini au kustaafu kazi, kukosa mtoto, kuhamishwa mahali pa kazi, kuoa ama kuolewa.
  • Majanga kama vile kimbunga, mafuriko, tetemeko la ardhi, n.k.
  • Changamoto za kila siku za maisha kama vile talaka, mimba kuharibika, kutoa mimba, kutengana, kufungwa, kuuguza au kuugua muda mrefu, n.k.
  • Madeni, upweke, kukataliwa, kujuta vinaweza kusababisha ugonjwa wa sonona.

Matibabu ya Ugonjwa wa Sonona

Sonona ni ugonjwa unaotibika. Ni muhimu sana kuwahi hospitali au kuonana na mtaalamu husika katika hatua za awali kabisa ili kuzuia kukithiri kwa tatizo. Matibabu ya ugonjwa wa sonona yanagawanyika katika sehemu kuu mbili; ambazo ni:

1. Tiba ya Mazungumzo (Non-Pharmacological)

Mazungumzo na mtaalamu wa afya ya akili ni mojawapo ya tiba madhubuti kwa wagonjwa wa sonona. Njia hii haihusishi dawa ikiwa na maana ya vidonge wala sindano. Hii ni tiba ya kisaikolojia ikiwa na lengo la kubadilisha mtazamo wa muathirika.

2. Tiba ya Kutumia Dawa (Pharmacological)

Hii ni njia inayohusisha utumiaji wa vidonge kama vile amitriptyline, fluoxetine, lorazepam, n.k. Dawa hizi zinafanya kazi katika ubongo kwenye sehemu inayohusika na kupandisha ama kushusha kemikali katika mwili ili kuleta mabadiliko ya kihisia na kitabia kwa mgonjwa husika. Njia hizi zinaweza kutumika zote kwa pamoja kwa mgonjwa mmoja pia.

Njia ya Kuzuia Ugonjwa wa Sonona

Sonona Kazini – Hiki ni kitabu kilichoandikwa katika lugha ya Kiswahili nyepesi na yenye kueleweka na kinachoakisi uhalisia kwa lengo la kujifunza kwa undani zaidi juu ya ugonjwa huu wa sonona na namna gani unaweza kuepuka katika maisha yetu ya kila siku. Kitabu hiki ni kwa ajili ya kila mtu mwenye utashi wa kutambua changamoto anazopitia, aidha akiwa jinsia ya kike au ya kiume.

Credits: Dr. Grace Mapunda

Tatizo la Afya ya Akili na Ugonjwa wa Sonona
0 Comment

Homa ya Ini janga kwa Dunia,Takwimu mpya ZaonyeshaAfyaclass Bongo Social •

TAKWIMU za homa ya ini duniani zinaonesha zaidi ya watu milioni 240 huugua. Tanzania, watu watano hadi wanane kati ya 100 wanaugua ugonjwa huo, hususan aina ya B na C.

Bingwa wa Magonjwa ya Ini na Mfumo wa Chakula kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)-Mloganzila, Dk. Tuzo Lyuu, amebainisha hayo jana, jijini Dar es Salaam, katika maadhimisho ya Siku ya Homa ya Ini Duniani, ambayo huadhimishwa Julai 28, kila mwaka.

Tovuti ya Umoja wa Mataifa (UN), kwenye maadhimisho hayo jana, imebainisha kwamba homa ya ini inaua takribani watu 3,500 kila siku licha ya kuwapo kinga na tiba, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

WHO inasema kiungo hicho kina shughuli zaidi ya 500 kila siku, kuhakikisha binadamu anaendelea kuishi, likisisitiza umuhimu wa kuchunguza, kutibu na kuzuia virusi vya homa ya ini.

Akifafanua kuhusu ugonjwa huo, Dk. Lyuu alisema kwa kawaida mwili hupambana na ugonjwa huo, iwapo ni homa ya ini aina ya A na E.

“Kuna aina ya homa ya ini katika makundi haya; virusi vya hepatitis A na E na hepatitis B na C. Ugonjwa huu maambukizi yake aidha ni kwa njia ya kujamiiana bila kinga, kuongeza damu ya mwenye homa hii au kwa njia ya mdomo yaani chakula.

Hata hivyo, maambukizi yanaweza kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa ujauzito. Homa ya ini aina ya A na E huwa haiwi ‘chronic’ (sugu) na haikai muda mrefu mwili hupambana wenyewe ila wapo ambao hushindwa kupambana,” alisema bingwa huyo.

Alisema kuwa homa ya ini ya hepatitis B na C ndiyo hatari na maambukizi hukaa muda mrefu mwilini na yenye kuambukiza zaidi na kwamba duniani takribani watu 650,000 hupoteza maisha kutokana na homa hiyo.

Dalili za homa hii ni kutapika, macho kuwa ya njano, tumbo kuvimba. Madhara yake ni uvimbe katika ini au kupata saratani. Mabadiliko ya ini kusinyaa na kushindwa kufanya kazi,” alisema bingwa huyo.

Kuhusu tiba bingwa huyo alisema anayeugua homa aina C, inashauriwa aanze tiba ambayo kwa asilimia zaidi ya 95 ya wanaotumia dawa wanapona.

WHO

WHO inasema chanjo wakati wa utotoni, hupunguza kwa kiasi kikubwa maambukizi sugu na visa vya saratani ya ini na cirrhosis katika utu uzima.

“Ni wakati wa kuchukua hatua, kila sekunde 30 mtu mmoja anafariki dunia kutokana na ugonjwa unaohusiana na homa ya ini.

Lazima kuchagiza hatua bora za kinga, uchunguzi na tiba ili kuokoa maisha na kupata matokeo bora ya afya.”

WHO, kimataifa kuna aina tano za Homa ya Ini za virusi vinavyosababisha homa ya ini A, B, C, D na E. Kwa ujumla, maambukizi ya homa ya ini aina ya B na C ndio yamesambaa zaidi na husababisha vifo vya watu milioni 1.3 kila mwaka na maambukizi mapya kwa watu milioni 2.2 kila mwaka.

Licha ya kuwapo kwa mbinu bora za uchunguzi na matibabu na kupungua kwa gharama za huduma hizo, viwango vya uchunguzi na matibabu vimedorora, linasema WHO.

Shirika hilo linaona dunia ina nafasi ya kufikia viwango vya kutokomeza ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030, iwapo hatua zitachukuliwa mapema hivi sasa.

“Watu 6,000 huambukizwa homa ya ini B na C kila siku. Vifo vinavyosababishwa na virusi vya homa ya ini vinaongezeka. Mwaka 2022 homa ya ini aina B na C vilisababisha vifo vya watu milioni 1.3.”

Serikali yataka wazazi kuzingatia chanjo kwa watoto

UMUHIMU CHANJO

Serikali imewataka wazazi kuwapa chanjo watoto wao wanapozaliwa ili kuwakinga na maradhi ya kuambukiza ikiwamo homa ya ini.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dk. Grace Magembe, aliyasema hayo jana katika maadhimisho ya Siku ya Homa ya Ini kitaifa yaliyofanyika mkoani Dar es Salaam yakiwa na lengo la kuongeza uelewa wa tatizo hilo.

Aliwakumbusha wazazi hao kutotoka hospitali bila watoto wao kupatiwa chanjo, akieleza kwenye chanjo hizo ipo ya homa ya ini na inamkinga na maambukizi ya ugonjwa huo.

Aidha, serikali ilijumuisha chanjo hiyo tangu mwaka 2002 kwenye chanjo inayojulikana kitaalam kama ‘pentavalent vaccine’ wanayopatiwa watoto chini ya miaka mitano kuwaweka salama dhidi ya virusi hivyo.

Aliwapongeza Watanzania wanaojitokeza kuchangia damu na kuwahamasisha wengine kuunga mkono kwa kuwa inasaidia kuokoa maisha ya wagonjwa wanayoihitaji ikiwamo homa ya ini, Ukimwi, saratani na waliopata ajali.

Alisema uchangiaji damu pia husaidia serikali kuitambua hali ya maambukizi ya magonjwa hayo kwa kuwa inakwenda kupimwa kuangaliwa usalama kabla ya kuwekewa mgonjwa.

Alisema utekelezaji wa utoaji chanjo ya homa ya ini inatokana na Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi na Magonjwa ya Ngono na Homa ya Ini (NASHCoP), uliozinduliwa na wizara ya afya Novemba, mwaka jana.

Alisema magonjwa mengi yanaweza kuzuilika iwapo Watanzania watapata taarifa sahihi wanapokwenda kufuata huduma.

Watanzania pia wamekumbushwa kuzingatia matumizi sahihi ya dawa na kula milo sahihi kwa kuwa magonjwa mengine ya ini yanatokana na matumizi mabaya ya vitu hiyo pamoja na kemikali.

Mkuu wa Programu wa Wizara ya Afya, Dk. Catherine Joachim, alisema kwa mara ya kwanza nchi hiyo inafanya maadhimisho ya kitaifa ya ugonjwa huo toka mpango wa NashCop ulipazinduliwa Novemba 24, 2023.

Alisema tangu walipoanza kutoa huduma ya kupima ugonjwa huo Julai 25, mwaka huu, idadi ya waliojitokeza kupima hadi kufikia juzi ni 524, kati ya hao 15 sawa na asilimia 2.8 waligundulika kuwa na maambukizi, ambao ipo chini ya kiwango cha ushamiri cha kimataifa ambao ni asilimia tatu.

Watu 429 walipokea chanjo ya kwanza na kuunganishwa na vituo vingine ili wapate chanjo mbili zilizobakia, jumla ya chupa 26 za damu zilikusanywa kutoka kwa wachangiaji na watu 275 walipatiwa huduma ya ukatili wa kijinsia na 114 walipata huduma ya macho.

Homa ya Ini janga kwa Dunia,Takwimu mpya Zaonyesha
0 Comment

Madhara ya Kupumua kwa Kutumia Mdomo badala ya PuaAfyaclass Bongo Social •

Madhara ya Kupumua kwa Kutumia Mdomo badala ya Pua

Mara nyingi watu wengi wakipata Shida ya kupumua kwa sababu ya pua kuziba hutumia Mdomo kupumua, Pua huweza kuziba kwa Sababu mbali mbali ikiwemo Mafua n.k

je, ni Sahihi Mtu kupumua kwa kupitia mdomo? Yapi ni madhara ya kufanya hivo? Soma hapa Makala hii Mpaka Mwisho kujua…

Fahamu tafiti mbali mbali zinaonyesha Kwa wastani mtu hupumua lita 10,000 hadi 12,000 za hewa kwa siku. Hewa hii pia inaweza kuwa na mchanganyiko wa vitu vingine mbali mbali ikiwemo; vumbi, bakteria, virusi na kuvu au Fangasi. Vyote hivi huweza kusafiri kwenye njia ya upumuaji na kufika hadi kwenye mapafu.

Bahati Nzuri ni kwamba, Mfumo wa Upumuaji huweza kusafisha uchafu wote huu na kukuweka katika hali ya Usalama Zaidi,

Kupitia mfumo wa upumuaji, ni chembe chembe ndogo tu chini ya mikroni tatu ambazo zinaweza kuingia kwenye mapafu.

Jinsi ambavyo Mfumo wa Upumuaji huchuja Uchafu Huu

Kwenye njia ya Upumuaji kuna Maelfu ya nywele nyembamba sana kuliko ncha ya Sindano,nywele hizi hufahamika kama Cilia. Kati ya 25 hadi 35 ya cilia hizi hupatikana kwenye kila seli ndani ya pua. Zina urefu wa mikroni tano hadi saba kila moja.

Zinapatikana kwenye seli, na huonekana kama brashi. Kazi yao ni kuzuia kupenya kwa viumbe vidogo ambavyo ni chini ya 0.5 mm kwa upana.

Matokeo yake, huchuja viini vidogo vidogo na kuvitoa kupitia pua.

Vichujio katika pua

Kwa upande mwingine, tishu kwenye pua pia hutumika kuchuja vijidudu vya hewa. Kamasi iliyopo pia inaruhusu baadhi ya viini kuingia mwilini. Kimsingi huruhusu vijidudu visivyo na madhara ndani ya mwili wetu.

KingaMwili

Pia fahamu kwamba Mfumo wetu wa kingamwili unaweza kupambana na kuzuia viini hatari vinavyovuka kupitia kamasi na kuingia mwilini.

Madhara ya Kupumua kwa Kutumia Mdomo badala ya Pua

Unachotakiwa kujua ni kwamba;Kazi kubwa ya Mdomo ni kula chakula,Hakuna nywele ndogo au cilia zinazoonekana mdomoni ili kuchuja hewa.

Na mfumo wa chakula hupambana na kuzuia vijidudu vinavyoingia kwa njia ya chakula ambavyo huweza kuathiri mwili wetu.

Ndiyo sababu hatupaswi kula chakula kupitia pua zetu. Hivyo basi, usivute hewa kupitia mdomo.

Hii ina maana pia ni rahisi wewe kuvuta na kuingiza ndani kwenye mwili wako vimelea vya magonjwa ambavyo huja kwa njia ya Hewa.

Nini hufanyika unapopumua kwa mdomo kwa muda mrefu?

Baadhi ya watu hupumua kupitia kinywa kutokana na mabadiliko fulani ya kijeni pamoja na matatizo ya njia ya hewa kwenye pua.

Kupumua kwa kinywa husababisha matatizo ya usingizi.

Hata hivyo, utafiti uligundua kuwa mifupa usoni mwa watoto ambao walipumua kwa muda mrefu kupitia midomo yao iliathirika.

Imedaiwa katika utafiti kwamba husababisha matatizo katika ukuwaji wa mifupa na meno.

Kwa watu wazima, hata hivyo, kupumua kwa kutumia kinywa kunaweza kusababisha maumivu ya misuli ya uso na shingo pamoja na maumivu ya kichwa.

Mwaka 2020 utafiti ulifanywa na Baraza Kuu la Vyuo vya Madaktari wa Meno na Stomatologists nchini Uhispania juu ya upumuaji wa kutumia mdomo.

Utafiti huo ulibaini kuwa nusu ya watoto wenye umri wa miaka 12 waliohusika walikuwa na matatizo ya meno.

Utafiti huo huo pia uligundua kuwa miongoni mwa watu wazima, shingo zinaweza kulazimika kuinama mbele kidogo ili kupumua, na kusababisha mshtuko wa misuli.

Ikiwa una shaka yoyote juu ya faida za kupumua kwa pua, jaribu kupumua kwa mdomo.

Ikiwa kupumua kwa pua ni suala la kawaida, kupumua kwa mdomo husababisha shinikizo au athari fulani mwilini.

Hata hivyo, wataalam wanapendekeza kwamba unaweza kupumua kwa mdomo tu katika hali ya dharura.

Editor:Afyaclass

Source:Bbc

Madhara ya Kupumua kwa Kutumia Mdomo badala ya Pua
0 Comment

ACHENI KUWATOZA WAGONJWA POSHO ZA DEREVA KWENYE 'AMBULANCE'Afyaclass Bongo Social •

ACHENI KUWATOZA WAGONJWA POSHO ZA DEREVA KWENYE ‘AMBULANCE’

Na WAF – Tanga

Waziri wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini Mhe. Ummy Mwalimu amekemea vikali na kuwaonya viongozi wa Hospitali zote nchini zenye magari ya kubeba wagonjwa (Ambulance) waache tabia ya kuwatoza wagonjwa au ndugu zao malipo ya posho ya Dereva na mtaalam anaesindikiza mgonjwa kwenye rufani.

Waziri @ummymwalimu amesema hayo Julai 28, 2024 jijini Tanga wakati akikabidhi gari la kubeba wagonjwa (Ambulance) kwa uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga – Bombo ambalo ni sehemu ya magari 736 yaliyonunuliwa na Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Ni marufuku kwa Hospitali zote nchini kuwatoza wananchi pesa ya posho ya Dereva wala Muuguzi anayemsindikiza Mgonjwa na badala yake Mwananchi anapaswa kuchangia gharama za mafuta tu na sio vinginevyo.” Amesisitiza Waziri Ummy

Aidha, Waziri Ummy amesisitiza matumizi sahihi ya magari hayo ambapo amekataza yasitumike kinyume na shughuli za wagonjwa pale inapohitajika ili yaendelee kudumu na kutoa huduma kwa Watanzania kwa kuimarisha huduma za rufani na dharura kwa ngazi zote.

“Magari haya yamenunuliwa kwa gharama kubwa sana, yatunzwe kwa kutenga fedha za matengenezo ya kawaida (Service) pamoja na kuyakatia Bima kwakuwa yamekuwa yakipata ajali mara kwa mara.” Amesema Waziri Ummy

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt. Imani Clemency amesema, kufuatia uwepo wa huduma hii kwa kila Halmashauri, wamejipanga kuimarisha huduma za rufaa hususani kwa akina mama wajawazito ambapo wameanzisha huduma ya simu ya dharura ya bila malipo namba 115, mwananchi atapiga na kupatiwa huduma haraka.

Via Link;WizaraafyaTz

ACHENI KUWATOZA WAGONJWA POSHO ZA DEREVA KWENYE 'AMBULANCE'
0 Comment

Homa ya ini yaua watu 3,500 kila siku licha ya kuweko kinga na tiba- WHOAfyaclass Bongo Social •

Homa ya ini yaua watu 3,500 kila siku licha ya kuweko kinga na tiba- WHO

Kuzuia maambukizi ya homa ya ini kwa njia ya chanjo za utotoni hupunguza kwa kiasi kikubwa maambukizo sugu na visa vya saratani ya ini na cirrhosis katika utu uzima.

Leo Julai 28 ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu homa ya ini au Hepatitis, ambapo ini linavimba na kusababisha ugonjwa mkali wa ini na saratani.

Ni wakati wa kuchukua hatua, ndio ujumbe mahsusi wa siku hii ya leo kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO kwani shirika hilo linasema kila sekunde 30 mtu mmoja anafariki dunia kutokana na ugonjwa unaohusiana na homa ya ini.

Hivyo WHO inasema lazima kuchagiza hatua bora za kinga, uchunguzi na tiba ili kuokoa maisha na kupata matokeo bora ya afya.

Aina 5 za Homa ya Ini

Kuna aina 5 za virusi vinavyosababisha homa y aini – A, B, C, D na E. Kwa ujumla, maambukizi ya homa ya ini aina ya B na C ndio yamesambaa zaidi na husababisha vifo vya watu milioni 1.3 kila mwaka na maambukizi mapya kwa watu milioni 2.2 kila mwaka.

Licha ya kuweko kwa mbinu bora za uchunguzi na matibabu na kupungua kwa gharama za huduma hizo, viwango vya uchunguzi na matibabu vimedorora, inasema WHO.

Ingawa hivyo bado shirika hilo linaona dunia ina nafasi ya kufikia viwango vya kutokomeza ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030, iwapo hatua zitachukuliwa mapema hivi sasa.

Ujumbe muhimu mwaka 2024

Majukumu ya ini kila siku ya ini

Ini lina shughuli zaidi ya 500 kila siku za kuhakikisha binadamu anaendelea kuishi, na ndio maana WHO inasisitiza umuhimu wa kuchunguza, kutibu na kuzuia virusi vya homa ya ini.

Watu 6,000 huambukizwa homa ya ini B na C kila siku

Vifo vinavyosababishwa na virusi vya homa ya ini vinaongezeka. Mwaka 2022 homa ya ini aina B na C vilisababisha vifo vya watu milioni 1.3. Takribani watu milioni 304 wanaishi na maambukizi sugu ya homa ya ini. Watu 3,500 wanakufa kutokana na homa ya ini aina ya B na C kila siku, sawa na mtu mmoja kila baada ya sekunde 30. Na kwa maambukizi, zaidi ya watu 6,000 wanaambukizwa virusi vya homa ya ini kila siku.

Kuna idadi kubwa ya wagonjwa wa homa ya ini wasiojitambua

WHO inasema duniani kote takribani watu milioni 220 wana homa ya ini aina ya B lakini hawajui, ilihali kwa aina ya C watu milioni 36 wameambukizwa virusi lakini hawajui.

Dalili nyingi hutokea pale ambapo ugonjwa uko hatua za mwisho, hasa pale mtu ameshapata ugonjwa wa ini au saratani.

Hata baada ya mgonjwa kubainika na homa ya ini, kiwango cha matibabu na huduma bado ni kidogo.

Kati ya watu milioni 304 wenye homa ya ini aina ya B na C, ni milioni 7 tu wanatibiwa aina ya B na milioni 12.5 aina ya C.

Maambukizi na vifo vinaweza kuzuiwa

Ili kutokomeza homa ya ini na kufikia lengo la WHO mwaka 2030, hatua rahisi za huduma kudhibiti ugonjwa huo ni pamoja na; wajawazito wote wanaoishi na homa ya ini sugu aina ya B wapatiwe tiba na watoto wao wapatiwe chanjo dhidi ya ugonjwa huo ili kuzuia maambukizi.

Halikadhalika asilimia 90 ya watu wenye maambukizi ya homa ya ini B na C wapatiwe matibabu.

Kufahamu zaidi kuhusu homa ya ini (Hepatitis) na dalili zake bofya hapa.

Homa ya ini yaua watu 3,500 kila siku licha ya kuweko kinga na tiba- WHO
0 Comment

Changamoto za kutokomeza Ukimwi ifikapo mwaka 2030Afyaclass Bongo Social •

Changamoto za kutokomeza Ukimwi ifikapo mwaka 2030 

Umoja wa Mataifa umesema maamuzi ya kisiasa yatakayochukuliwa mwaka huu, yataamua ikiwa lengo la kutokomeza kabisa ugonjwa wa UKIMWI ifikapo mwaka 2030 linaweza kufikiwa.

Kauli hiyo ya Umoja wa Mataifa imetolewa kwenye mkutano wa 25 wa Kimataifa wa kujadili gonjwa la UKIMWI uliofunguliwa rasmi siku ya Jumatatu mjini Munich, Ujerumani.

Takwimu za mwaka 2023 zinaonyesha kupungua kwa idadi ya vifo na maambukizi mapya pamoja na uboreshaji wa upatikanaji wa matibabu kwa wagonjwa walio na Virusi Vya Ukimwi (VVU). Lakini wakati takwimu hizo zikionekana kuwa chanya, shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS limeonya kuwa maendeleo jumla bado si ya kuridhisha sana.

Ripoti ya shirika hilo imebainisha kuwa maamuzi yatakayochukuliwa na viongozi mwaka huu yataamua iwapo nchi zinaweza kufikia lengo la kuufanya UKIMWI kutokuwa tena tishio la afya ya umma ifikapo mwaka 2030 na kuhakikisha maendeleo zaidi katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Katika kipindi cha zaidi ya miongo minne tangu kuibuka kwa janga hilo duniani kote, UKIMWI tayari umeua zaidi ya watu milioni 42. Licha ya idadi ya vifo kupungua kutoka watu 670,000 mwaka 2022 hadi 630,000 mwaka jana, idadi hiyo hata hivyo bado ni kubwa mno.

UNAIDS yahimiza kuchukuliwa kwa hatua zaidi

Mkuu wa shirika la UNAIDS Winnie Byanyima amesema katika ripoti hiyo kwamba kila dakika, mtu mmoja hufa kutokana na magonjwa yanayohusiana au kusababishwa na UKIMWI, huku akionya kwamba dunia inasuasua kufikia malengo makubwa ya kutokomeza  UKIMWI ifikapo mwaka 2030. Aidha Bi Byanyima amelitaka shirika linalotengeneza dawa za kupunguza makali ya VVU la Gilead kuzalisha zaidi dawa yake aina ya Lenacapavir ambayo inonyesha matokeo bora zaidi:

” Nadhani Gilead inayo fursa ya kutusaidia pakubwa kukomesha UKIMWI kama tishio la afya ya umma. Wanaweza kuweka historia kwa hilo, si tu kwa kuisambaza kote ulimwenguni kama dawa ya kuzuia maambukizi, lakini kwa kuruhusu matumizi yake kwa kila mtu na si tu kwa ajili ya kuzuia bali pia itumiwe kwa matibabu.”

Mwenye VVU atahitaji sindano mbili tu kwa mwaka za dawa hiyo mpya ya Lenacapavir.

Mkuu huyo wa UNAIDS amesisitiza kuwa ukosefu wa usawa katika mapambano dhidi ya VVU haushughulikiwi vya kutosha, hasa ikizingatiwa kuwa dawa zenye ufanisi mkubwa zimekuwa zikiuzwa kwa bei kubwa.

Inakadiriwa kuwa takriban watu milioni 40 wanaishi na VVU , virusi ambavyo vinaweza kusababisha ugonjwa wa UKIMWI. Takriban maambukizi mapya milioni 1.3 yalirekodiwa mwaka jana. Upatikanaji wa dawa za kupunguza makali ya VVU pia umeboreshwa, lakini bado ni suala tete.

Mwaka jana, watu milioni 30.7 walipata matibabu hayo ikilinganishwa na milioni 7.7 tu mwaka 2010. Lakini bado kuna changamoto nyingi ili kufikia lengo la kutokomeza kabisa UKIMWI ifikapo mwaka 2030.

Mashariki na kusini mwa Afrika yanasalia kuwa maeneo yaliyoathirika zaidi, kwa kujumuisha vifo 260,000,  watu milioni 20.8 wakiwa wanaishi na VVU, na pia watu 450,000 wakiwa waliambukizwa virusi hivyo mwaka jana.

(Chanzo: AFP)

Changamoto za kutokomeza Ukimwi ifikapo mwaka 2030
0 Comment

Madhara baada ya kutumia p2,Fahamu hapaAfyaclass Bongo Social •

Madhara baada ya kutumia p2,Fahamu hapa

Fahamu P2 ni dawa ya dharura yaani kwa kitaalam hujulikana kama emergency contraceptive pill, dawa hii inazuia mtu asipate Mimba kwenye mazingira ambayo umefanya mapenzi pasipo kupanga na upo siku za hatari,au umelazimishwa kufanya mapenzi au umebakwa,ili kuzuia mimba zisizotarajiwa unalazima Kunywa hizi dawa.

Ukweli ni kwamba dose ya hormones ndani ya p2 ni kubwa kuliko vidonge vya kawaida vya Uzazi(birth control pills) kitu ambacho kinaifanya isifae kwa Matumizi ya kila siku,

Hii husababisha madhara Zaidi kwa Mtu mwenye mazoea ya kuzitumia mara kwa mara. Na moja ya madhara ni mzunguko wako wa hedhi kuathiriwa sana – Periods yako inaweza isitoke kama kawaida, inaweza kuwa nyingi,zito sana,isiyoeleweka(Irregular bleeding) n.k.

Pia baadhi ya Wanawake huongezeka uzito, Hivo basi P2 haishauriwi kabsa kwa matumizi ya kila siku au kutumia kama njia ya uzazi wa mpango ya muda mrefu.

Madhara baada ya kutumia p2,

Haya ni baadhi ya Madhara au matokeo baada ya kutumia p2(emergency contraceptive pills):

  • Kupata kichefuchefu
  • Kutapika
  • Mwili kuchoka Sana
  • Kupata kizunguzungu
  • Kupata maumivu ya kichwa
  • Kupata maunivu ya tumbo
  • Maziwa kuuma au kuvuta zaidi
  • Kubadilika kwa hedhi yako ya kawaida,ikiwemo kuvuja damu nyingi au kwa muda mrefu,au kuvuja katikati ya mzunguko n.k

Kutokwa na Vitone vya damu mara kwa mara(spotting) – Unaweza kupata vitone vya damu ndani ya wiki ijayo baada ya kumeza kidonge cha dharura cha kuzuia mimba yaani P2,

Pia, hedhi yako inayofuata inaweza kuwa nyepesi au nzito, ikawahi kutoka mapema au kuchelewa kuliko kawaida. Hakikisha unapata Msaada wa Tiba ikiwa unakutana na changamoto hizi.

Mzunguko wa hedhi usio wa kawaida(Irregular menstrual cycle) – Kwa sababu ya tembe za dharura za kuzuia mimba(p2), kipindi chako cha hedhi kinaweza kufika mapema au kuchelewa, jambo ambalo hutokea sana kwa wanawake wanaotumia vidonge hivi. Hata hivyo, unapaswa kufanya kipimo cha ujauzito ikiwa hupati kipindi chako cha hedhi ndani ya wiki mbili za tarehe inayotarajiwa.

MADHARA YA KUTUMIA P2

P2 Ni Dawa iliyotengenezwa kutumiwa mara chache tu,inapokulazimu.Sio dawa unayotakiwa kutumia kama njia ya uzazi wa mpango ya muda mrefu. Kuna wanawake humeza p2 kila mwezi,hii haitakiwi. Katika mazingira ya kawaida,haipaswi kumezwa zaidi ya mara 3 kwa mwaka. Kuendekeza kila mwezi kunywa hizi p2 sio sahihi,Unatakiwa ende hospitali ili upate njia sahihi ya uzazi wa mpango ya muda mrefu.

Baadhi ya Side effects/madhara ni ya matumizi holela ya dawa hizi ni

1.Unaweza kujisikia kichefuchefu au kutapika baada ya kumeza,

2.Maumivu ya tumbo

3.Matiti kuuma na kujaa

4.Pia hedhi zako zinazofuata zinaweza zikawahi au zikachelewa au zikatoka nyingi sana( ukiona zimezidi siku 8 fika muone daktari) au ukawa unapata hedhi nyepesi sana,au pia haupati hedhi kabisa (amenorhoea)

5.Kichwa kuuma na kizunguzungu

6.Mabadiliko ya Ute ukeni (change in cervical secretion,hapa unakuta Ute wa ovulation mtu hapati).

7.Kupata maambukizi ukeni,vaginal infections

8.Hatari ya kupata PID

9.Maumivu wakati wa sex(dyspareunia)

10.Mama anakuwa hatarini kutungisha mimba nje ya kizazi yaani ectopic pregnancy.

11.Lakini pia kuna wanawake hupata Ovarian cyst,vivimbe kwenye mfuko wa mayai.

Kuna sababu hapo juu kama PID,kutopata UTE,infections kwenye uke hizi zinakuja athiri mwanamke anakuwa anapata taabu kwenye Kupata mimba

Kama hujapanga kupata mimba,tafadhari fuata njia ya uzazi wa mpango ya muda mrefu inayokufaa,achana na kumeza p2 kila mwezi.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Chanjo ya kuzuia VVU yashindwa kupunguza maambukiziAfyaclass Bongo Social •

Chanjo ya kuzuia VVU yashindwa kupunguza maambukizi

Majaribio ya chanjo hiyo yalisitishwa Novemba, 2023 na baadaye kutangazwa hadharani Desemba mwaka huo.

Baada ya majaribio ya chanjo ya sindano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) ‘PrEPVacc’ yaliyofanyika kwa miaka minne Mashariki na Kusini mwa Afrika, imebainika haijafanikiwa kupunguza maambukizi ya virusi hivyo miongoni mwa waliofanyiwa utafiti.

Majaribio ya chanjo hiyo yalisitishwa Novemba, 2023 na baadaye kutangazwa hadharani Desemba mwaka huo.

Tanzania ni miongoni mwa nchi tatu zilizoshiriki majaribio hayo kuanzia mwaka 2020 hadi 2024 katika mikoa ya Mbeya na Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kiongozi wa mawasiliano wa mradi wa majaribio ya chanjo hiyo, Tom Miller, inaeleza maeneo mengine yaliyoshiriki majaribio hayo ni Masaka, nchini Uganda na Durban, Afrika Kusini.

Utafiti wa PrEPVacc, uliongozwa na watafiti kutoka Afrika kwa msaada wa wenzao wa Ulaya ukihusisha majaribio matatu.

Matokeo ya majaribio hayo yametangazwa leo Julai 23, 2024 katika mkutano kuhusu masuala ya Ukimwi uliofanyika Munich, Ujerumani.

Imeelezwa hakuna kati ya aina mbili za majaribio ya chanjo hiyo iliyofanikiwa kupunguza maambukizi ya VVU.

Mkuu wa mradi huo nchini, Dk Lucas Maganga kutoka Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (Nimr-Mbeya) hakupatikana kuzungumzia majaribio ya chanjo hiyo.

Kwa zaidi ya miaka mitano Tanzania imekuwa ikitumia dawa kinga aina ya PrEP, iliyo katika mfumo wa vidonge.

Mradi wa majaribio ya PrEPVacc ulishirikisha watu 1,512 wenye afya njema wa umri wa miaka 18 hadi 40, ambao wanajihusisha na tabia hatarishi zinazoweza kusababisha maambukizi ya VVU.

Idadi ya washiriki ilijumuisha asilimia 87 ya wanawake na asilimia 13 wanaume.

Kwa Tanzania walioshiriki ni wanawake pekee, huku maeneo mengine yalijumuisha wanaume na wanawake.

Mtafiti Mkuu wa mradi wa majaribio ya chanjo ya PrEPVacc, Profesa Pontiano Kaleebu amesema maswali ya chanjo yaliyoulizwa katika majaribio yamejibiwa na kilicho wazi ni kwamba haitaendelezwa.

“Matokeo yamekuwa ya kushangaza na yamekuwa ya kukatisha tamaa. Lakini hiyo ni sayansi. Umekuwa utafiti mzuri, unaofuata viwango vya juu vya kimataifa.”

“Lazima tusonge mbele kwa sababu dunia inahitaji kuwa na chaguo katika kisanduku chake cha zana za kuzuia maambukizi ya VVU. Chanjo dhidi ya VVU inasalia kuwa sehemu inayotafutwa na muhimu katika kisanduku hicho cha zana,” amesema Profesa Kaleebu.

Mkurugenzi wa mradi huo wa majaribio ya PrEPVacc, Dk Eugene Ruzagira akiwasilisha matokeo ya chanjo hiyo kwenye mkutano wa Ukimwi 2024, amesema ilisitishwa Novemba, 2023 baada ya kuonekana haizuii maambukizi.

Kiongozi wa mradi huo aliye katika kitengo cha majaribio ya kimatibabu cha Baraza la Utafiti wa Kitiba katika Chuo Kikuu cha London, Profesa Sheena McCormack amesema:

“Hatuwezi kuondoa uwezekano wa matokeo, hivyo ni wazi tunahitaji kuendelea kuwaunga mkono washiriki na kupima VVU ili kufuatilia mwenendo.”

“Jumla ya idadi ya maambukizi katika majaribio ilikuwa ndogo zaidi kuliko tulivyotarajia, ambayo ni habari njema na ninatumaini hii inaonyesha kile kinachotokea katika jamii pana,” amesema.

Chanjo ya kuzuia VVU yashindwa kupunguza maambukizi
0 Comment

Idadi ya vifo maporomoko mawili ya udongo kusini mwa Ethiopia yafika 157Afyaclass Bongo Social •

Idadi ya vifo maporomoko mawili ya udongo kusini mwa Ethiopia yafika 157

Idadi ya vifo kutokana na maporomoko mawili ya udongo kusini mwa Ethiopia imeongezeka kwa kasi hadi 157 na idadi hiyo inaweza kuongezeka zaidi, afisa wa serikali alisema Jumanne.

Maporomoko ya udongo yalizikwa katika eneo la Gofa katika jimbo la Kusini mwa Ethiopia, kisha ya pili yakawakumba wengine waliokuwa wamekusanyika kusaidia Jumatatu asubuhi, maafisa walisema.

“Utafutaji bado unaendelea na kuna miili ambayo bado haijapatikana. Eneo hilo lina changamoto nyingi,” Markos Melese, mkuu wa wakala wa Kitaifa wa Kukabiliana na Majanga katika Gof a Zone, aliiambia Reuters kwa njia ya simu.

“Hadi sasa tumeshapata miili 157 kutoka katika vijiji viwili… Tunaamini idadi itaongezeka.”

Idadi ya vifo maporomoko mawili ya udongo kusini mwa Ethiopia yafika 157
0 Comment

Chanjo ya Kifua Kikuu yatolewa KenyaAfyaclass Bongo Social •

Chanjo ya Kifua Kikuu yatolewa Kenya

Kundi la kwanza la Wakenya limepokea chanjo inayoelekea kuwa ya kwanza ya kifua kikuu (TB) katika kipindi cha takriban miaka 100.

Chanjo hiyo ilitolewa tarehe 12 Julai katika miji ya Kisumu, Kilifi, Machakos na Nairobi. Hata hivyo, chanjo bado inafanyiwa majaribio na huenda isipatikane kwa wingi kwa umma kabla ya mwaka 2030.

Hivi sasa, chanjo pekee ya TB inayopatikana ni BCG kwa watoto waliotengenezwa mnamo 1921.

BCG huwalinda watoto wachanga na watoto wadogo dhidi ya aina kali za kifua kikuu, lakini inatoa ulinzi duni kwa vijana na watu wazima dhidi ya aina ya ugonjwa wa mapafu, husababisha maambukizi ya bakteria wanaoeneza gonjwa wa kifua kikuu.

Chanjo ya Kifua Kikuu yatolewa Kenya
0 Comment

Tiba ya Mtoto aliyekatwa koo na mfanyakazi wa ndani (house girl)Afyaclass Bongo Social •

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema atalipia gharama za matibabu ya mtoto Maliki Hashimu (5), mkazi wa Goba, mkoani Dar es Salaam, anayedaiwa kujeruhiwa koo na mfanyakazi wa ndani (house girl).

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu aliyasema hayo jana baada ya kutembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), jijini Dar es Salaam ambako mtoto huyo yuko chini ya uangalizi maalum.

Tukio la kujeruhiwa mtoto huyo kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, lilitokea usiku wa Julai 15 mwaka huu na kuripotiwa siku iliyofuata.

Kutokana na majeraha makubwa aliyopata baada ya kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni kilichotenganisha njia ya hewa chini ya sanduku la sauti, mtoto huyo alifikishwa MNH – Mloganzila.

Baadaye mtoto huyo alihamishiwa MNH – Upanga kwa ajili ya matibabu zaidi kwa kuwa baada ya kujeruhiwa kulisababisha ashindwe kupumua, kuongea na kupata maumivu na kupoteza kiwango kikubwa cha damu.

MNH kupitia wataalamu wake tayari wamemfanyia upasuaji mkubwa mtoto huyo, ukichukua saa nne kurekebisha njia ya hewa, sanduku la sauti, matezi yaliyojeruhiwa na kutibu jeraha la nyuma ya shingo.

Wataalamu hao walibaini jeraha la mbele ya shingo liliharibu tezi la mbele (thyroid gland) kwa kulikata katikati na kusababisha mtoto huyo kuvuja damu kwa wingi, kupata maumivu makali kutokana na kukatwa sehemu iitwayo (trachea) ambako hewa hupita inapotoka katika mapafu.

Tangu Jumatatu iliyopita, mtoto huyo yuko chini ya uangalizi maalum akiendelea kupata matibabu kutoka kwa madaktari bingwa wa hospitali hiyo.

Tiba ya Mtoto aliyekatwa koo na mfanyakazi wa ndani (house girl)
0 Comment

Mwanafunzi wa shule ya sekondari ajinyonga baada ya mpenzi kukataa ujauzitoAfyaclass Bongo Social •

Mwanafunzi wa shule ya sekondari ajinyonga baada ya mpenzi wake kukataa ujauzito

Tukio la kusikitisha limetokea katika shule ya upili ya Nleta huko Bulawayo, Zimbabwe, ambapo mwanafunzi wa kidato cha nne alijinyonga baada ya kukabiliwa na kukataliwa na mpenzi wake kuhusu ujauzito wake.

Mwanafunzi huyo aliyekuwa anachumbiana na mwanafunzi Upper-sita katika shule moja, aliripotiwa kutafuta uungwaji mkono kutoka kwa mpenzi wake baada ya kugundua kuwa ana mimba.

Kukataa kwa mpenzi kuhusu ujauzito huo kulisababisha shida yake kubwa ya kihemko, na kuchangia uamuzi wake wa kuondoa maisha yake.

Mnamo Julai 12, msichana huyo alitembelea nyumba ya mpenzi wake lakini baadaye akakutana na shangazi yake na kurudishwa katika makazi yao. Inaaminiwa kwamba alikuwa amejaribu kuzungumza tena na rafiki yake wa kiume, ili tu apate Muafaka tena. Hilo lilizidisha kukata tamaa kwake.

Licha ya juhudi za shangazi yake kumuunga mkono, mwanafunzi huyo aliamua kumaliza maisha yake.

Inspekta msaidizi Nomamalanga Msebele alithibitisha tukio hilo, ingawa ripoti za awali za polisi hazikutaja mimba hiyo.

Kulingana na polisi, msichana huyo alikuwa ameondoka nyumbani akiwa hajahudhuria masomo ya ziada na baadaye alionekana akiingia kwenye makao ya rafiki yake mvulana. Kwa wasiwasi juu ya kutokuwepo kwake, shangazi yake aligundua kuna kitu hakipo Sawa.

Mwanafunzi wa shule ya sekondari ajinyonga baada ya mpenzi kukataa
ujauzito
0 Comment

Boni Mwaitege kufariki dunia,akanusha Taarifa hizi VIDEOAfyaclass Bongo Social •

Baada ya kuzuka kwa Taarifa zinazohusishwa na kifo cha Mwimbaji wa Nyimbo za Injili; Boni Mwaitege

Yeye mwenyewe kajitokeza na kukanusha Taarifa hizi zilizosababisha Taharuki kubwa miongoni mwa Watu.

Tazama hapa;

0 Comment

Mgonjwa wa Saba Apona Ugonjwa wa UkimwiAfyaclass Bongo Social •

Mgonjwa wa Saba Apona Ugonjwa wa Ukimwi

Mwanaume mmoja wa Ujerumani aliye na umri wa miaka 60, huenda akawa Mtu wa saba kupona Virusi vya Ukimwi baada ya kupandikizwa Uloto ambapo Mjerumani huyo ambaye ametaka kutotajwa jina, amepachikwa jina la “mgonjwa anayefuata wa Berlin”.

Mtandao wa DW Kiswahili umeripoti kuwa Daktari Mtafiti katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Charite cha Berlin Christian Gaebler, amesema Timu yao haiwezi kuthibitisha kwa uhakika ikiwa virusi vya VVU vimetokomezwa kabisa kwa Mgonjwa huyo.

Mgonjwa wa awali wa Berlin, Timothy Ray Brown, alikuwa Mtu wa kwanza kutangazwa kuponywa VVU mnamo mwaka 2008, hata hivyo, Brown alifariki kutokana na saratani mwaka 2020.

Mwanaume huyo anayetajwa kuwa wa saba kupona VVU aligunduliwa mara ya kwanza kuwa na maambukizi ya VVU mwaka 2009.

Mafanikio ya upandikizaji Seli Shina kwa Watu wenye VVU, yametangazwa kabla ya kufanyika kwa mkutano wa 25 wa kimataifa wa UKIMWI katika Mji wa Munich mapema wiki ijayo.

Mgonjwa wa Saba Apona Ugonjwa wa Ukimwi
0 Comment

Dawa muwasho sehemu za siri,chanzo cha muwasho sehemu za SiriAfyaclass Bongo Social •

Dawa muwasho sehemu za siri,chanzo cha muwasho sehemu za Siri

Nini dawa ya muwasho sugu sehemu za siri?

Haya ni baadhi ya Maswali kati ya Maswali mengi ambayo tunayapata Kila siku,

Tatizo la Muwasho Sehemu za Siri

Kwanza,Kabla ya kutafuta Dawa ni lazima ufahamu chanzo cha muwasho ni nini?

ZIPO SABABU MBALI MBALI AMBAZO HUWEZA KUSABABISHA TATIZO LA MUWASHO,

Unaweza kupata muwasho sehemu za Siri kwa Sababu mbali mbali ikiwemo;

– Maambukizi ya Fangasi Sehemu za siri, Hii ni miongoni mwa Sababu kubwa ya kuleta muwasho sehemu za Siri()

– Tatizo la allergies au Mzio

– Kuwa na Tatizo la Bacterial Vaginosis

– Maambukizi ya Magonjwa mbali mbali ya Zinaa(STIs) ikiwemo;

  •  Ugonjwa wa Chlamydia
  • Tatizo la Genital warts
  • Ugonjwa wa Kisonono(gonorrhea)
  • Tatizo la genital herpes
  •  Tatizo la Trichomoniasis n.k

– Matatizo mbali mbali ya ngozi ikiwemo;

  1.  Tatizo la skin irritation
  2.  Hali kama eczema,
  3.  Psoriasis n.k

– Tatizo la Saratani kama vile vulvar Cancer n.k()

MATIBABU

Matibabu ya tatizo hili hutegemea na chanzo chake,mfano kama shida ni Fangasi,basi utapata matibabu ya Fangasi N.K

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Rejea pia: Makala hii Kuhusu Muwasho sehemu za Siri. Soma hapa

Dawa muwasho sehemu za siri,chanzo cha muwasho sehemu za Siri
0 Comment

Nyama ya maabara sasa ruksaAfyaclass Bongo Social •

Nyama ya maabara sasa ruksa

Uingereza imekuwa Nchi ya kwanza Barani Ulaya kuidhinisha nyama iliyotengenezwa maabara na hivyo kufungua njia kwa kuku wa kukuzwa maabara kuanza kuuzwa katika maduka ya wanyama wa kufugwa mapema mwaka huu.

Uanzishaji wa kampuni inayozalisha nyama hizo ya “Meatly” Nchini Uingereza umeidhinishwa na Wadhibiti ubora wa Uingereza kwa nyama yake inayokuzwa kwenye maabara ili itumike katika chakula cha mifugo.

Uingereza sasa itakuwa Nchi ya kwanza ya Ulaya ambayo chakula cha wanyama kilichokuzwa kwenye maabara kinapatikana kwa Watu kununua, nyama hizo ni kwa ajili ya chakula cha wanyama kama vile mbwa, paka n.k.

Owen Ensor, Mtendaji Mkuu na Mwanzilishi mwenza wa Meatly, amesema hii imetokana na msukumo kutoka kwa Wadhibiti na Serikali kutetea uvumbuzi wa chakula na kuharakisha michakato ya kuidhinisha baada ya Brexit na Uingereza kuchukua “faida yake ni kubwa.”

Nyama ya maabara sasa ruksa
0 Comment

Madhara ya kuweka kope bandia,Fahamu hapaAfyaclass Bongo Social •

Madhara ya kuweka kope bandia,Fahamu hapa

Kope zetu za asili hufanya kazi muhimu, hulinda macho yetu kwa kuelekeza hewa mbali na mboni ya jicho, na kutufanya kupepesa, hatua ambayo pia huhakikisha kwamba macho yana majimaji vizuri.

Kope bandia hushikanishwa na kila kope asili, moja kwa moja.

Kope hizi huunganishwa na gundi ambayo inaweza kusababisha matatizo.

Wataalamu wengi wa vipodozi hufanya jaribio la awali la kiraka cha kope bandia kwenye eneo fulani la mwili, kwa kawaida kwenye mkono au nyuma ya sikio, ili kuangalia mizio ya gundi; hata hivyo, hata ikiwa hakuna athari ya mzio(Allergy), kemikali katika gundi inaweza kuwasha eneo la jicho na uzito wa gundi yenyewe inaweza kusababisha muwasho kwenye kope.

Matumizi sahihi ni muhimu. Kumekuwa na ripoti za watu ambao kope zao zimeshikamana kwasababu ya matumizi ya kope bandia.

Kwa mujibu wa utafiti mmoja, zaidi ya asilimia 60 ya wanawake waliripoti changamoto ya keratoconjunctivitis, hali ya jicho inayohusisha kuvimba kwa kornea na kiwambo cha jicho kwa wakati mmoja, baada ya gundi ya kope bandia kugusa macho yao.

Utafiti huo huo uligundua kuwa asilimia 40% ya wanawake walipata athari ya mzio kwasababu ya gundi.

Gundi inayosababisha saratani

Kumekuwa na nyakati ambapo gundi ya kucha, ambayo ina nguvu zaidi imeuzwa kama gundi ya kope.

Katika mojawapo ya matukio ya kushtua sana ya utumiaji usiofaa, kope za mwanamke ziliachwa zikiwa zimeshikamana pamoja baada ya kuweka kope bandia kwa kutumia gundi kali.

Gundi ya kope inaweza kusababisha hatari kadhaa za afya. Utafiti mmoja ulichanganua viambata 37 vya kibiashara na kitaalamu na kugundua uwepo wa formaldehyde, kemikali inayojulikana kusababisha saratani.

Uchambuzi huo uligundua kuwa asilimia 75 ya viambata 20 vya kitaalamu vilivyojaribiwa vilitoa formaldehyde, na gundi nne kati ya 17 za kibiashara pia zilikuwa na kemikali hiyo.

Madhara ya kuweka kope bandia,Fahamu hapa
0 Comment

Ugonjwa wa Typhoid,Chanzo,Dalili na Tiba yakeAfyaclass Bongo Social •

Ugonjwa wa Typhoid,Chanzo,Dalili na Tiba yake

Ugonjwa wa Typhoid ni Ugonjwa wa homa ya matumbo,hujulikana pia kama Typhoid fever au enteric fever, na chanzo chake ni maambukizi ya bacteria wanaojulikana kama salmonella bacteria. 

Maji kuchafuliwa pamoja na vyakula tunavyokula huweza kupelekea bacteria hawa kusambaa na kuingia kwenye miili yetu,kisha kupelekea ugonjwa wa typhoid au homa ya matumbo.

DALILI ZA UGONJWA WA TYPHOID

Dalili zinaweza kuanza polepole, mara nyingi huonekana wiki 1 hadi 3 baada ya kuathiriwa na bakteria kama salmonella bacteria. 

Dalili za Awali;

Dalili za awali ni pamoja na;

1. Mtu kuwa na Homa,

Homa ambayo huanza chini na kuongezeka siku nzima, ikiwezekana kufikia 104 degrees Fahrenheit (40 degrees Celsius).

2. Mwili kutetemeka

3. Kupata maumivu ya Kichwa

4. Mwili kuchoka sana na kuwa dhaifu

5. Kupata maumivu ya Misuli

6. Kupata Maumivu ya Tumbo

7. Kuharisha au kupata Choo kigumu(constipation).

8. Wengine hupata upele au Rashes kwenye ngozi.

9. Baadhi pia huweza kuwa na dalili zingine kama vile;

  • Kupata kikohozi
  • Kukosa Hamu ya kula
  • Kutoa Sana jasho n.k

Dalili za baadae;

Wiki chache baada ya dalili kuanza, ugonjwa unaweza kusababisha matatizo katika tumbo. Watu wanaweza kuwa na:

– Maumivu makali ya Tumbo

– Tumbo kuvimba Sana

Pia Maambukizi yanayosababishwa na bakteria hawa tumboni yanaweza kuenea katika mwili wote na kusababisha hali inayoitwa sepsis.

VIPIMO:

#SOMA Zaidi Hapa Kuhusu Vipimo cha Typhoid au homa ya matumbo

Chanzo cha Ugonjwa wa Typhoid

Aina ya bakteria inayoitwa Salmonella enterica serotype typhi ndyo husababisha homa ya matumbo au Ugonjwa wa Typhoid. Aina zingine za bakteria wa salmonella husababisha ugonjwa kama huo unaoitwa paratyphoid fever.

Watu hupata bakteria hawa kwa kiasi kikubwa katika maeneo ambayo milipuko ya Ugonjwa wa Typhoid hutokea mara nyingi. Bakteria hutoka nje ya mwili kwenye kinyesi na mkojo wa watu wanaobeba bakteria.

Bila kuosha mikono kwa uangalifu baada ya kwenda Chooni, bakteria wanaweza kupita kutoka kwenye mikono hadi kwa vitu vingine kama maji,chakula n.k au kwa watu wengine.

Bakteria pia wanaweza kuenea kutoka kwa mtu ambaye hubeba bakteria. Wanaweza kuenea kwenye chakula ambacho hakijapikwa, kama vile matunda mabichi ambayo hayana maganda.

Pia Katika maeneo ambayo maji hayatibiwi ili kuua vijidudu, unaweza kuchukua bakteria kutoka kwenye chanzo hicho. Hii inajumuisha maji ya kunywa, kutumia barafu iliyotengenezwa kwa maji ambayo hayajatibiwa, au kwa kunywa maziwa au juisi ambayo haijasafishwa(unpasteurized milk or juice). n.k

IKIWA UNA SHIDA HII KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Ugonjwa wa Typhoid,Chanzo,Dalili na Tiba yake
0 Comment

Mlipuko wa Ugonjwa wa Kipindupindu Morogoro,16 waathiriwaAfyaclass Bongo Social •

Wagonjwa 16 wenye viashiria vya maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu Morogoro

Wakazi wa Manispaa ya Morogoro wanahofia kukumbwa na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu huku wagonjwa 16 wanaodhaniwa kuwa na ugonjwa huo wakilazwa katika Kituo cha Afya cha Sabasaba.

Mganga Mkuu wa kituo hicho kilichopo Manispaa ya Morogoro ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake, amesema Julai 16 na 17, 2024, hospitali hiyo imepokea wagonjwa wa kuharisha na kutapika zaidi ya 15.

“Juzi na jana tulipokea wagonjwa wengi wa kutapika na walianza kuja watano lakini hadi jioni tulikua na wagonjwa 15 ambao walikuwa wakiharisha na kutapika, baada ya kuchukua sampuli na kuzipeleka maabara tuligundua wana viashiria vya maambukizi ya kipindupindu.

“Kwa hiyo, hadi leo Julai 18, 2024, tuna wagonjwa 16 ambao tunaendelea kuwahudumia kwenye hospitali yetu,” amesema.

Amesema tangu Januari 2024 wakati wa mvua za masika na maeneo mengi kukumbwa na mafuriko, kumekuwa na wagonjwa wa kuharisha na kutapika na kwa hali iliyopo, lazima jitihada za makusudi zifanyike ili kukabiliana na ugonjwa huo.

Meya wa Manispaa ya Morogoro, Pascal Kihanga amesema manispaa hiyo kupitia kwa Ofisa Afya wa Manispaa, wameagiza timu ya wataalamu kuchunguza kuhusu ugonjwa huo uliowakumba baadhi ya wananchi kwani hakuna kweli wowote kuwa ni kipindupindu.

“Jana, ofisa afya ametoa taarifa ya kuwa ule ugonjwa sio kipindupindu na ni vizuri kuheshimu taaluma yake maana yeye ndio mtaalamu wa hayo mambo na  kwa sasa bado wanafanya utafiti ili kugundua ni ugonjwa gani na chanzo chake ni nini,”  amesema.

Amesema kipindupindu kinaweza kutokea katika majira haya ya kiangazi, hivyo kinachofanyika kwa sasa kupitia wataalamu wa manispaa ni kungojea uchunguzi ili kujua ugonjwa huo ni wa aina gani na dalili zake ni zipi kwa kuwa maana umezuka ghafla,” amesema Kihanga.

Mkazi wa Kihonda, Deus Zephania amesema anaishi na ndugu yake ambaye naye siku mbili zilizopita alimpeleka hospitali akikabiliwa na changamoto ya kutapika na kuharisha, hata hivyo hakuwa anafahamu huo ni ugonjwa gani.

“Nimempeleka mdogo wangu Kituo cha Afya cha Sabasaba kupatiwa matibabu baada ya kuanza ghafla kuharisha na kutapika kwa pamoja. Ilitushtua lakini alipokwenda hospitali, alipewa matibabu na kwa sasa anaendelea vizuri, kwa maana hiyo tunawaomba Serikali watusaidie kuweka mazingira safi na salama ili tuepukane na haya magonjwa,” amesema Zephania.

VIA:Mwananchi.

#SOMA ZAIDI Hapa kuhusu Ugonjwa wa Kipindupindu

Mlipuko wa Ugonjwa wa Kipindupindu Morogoro,16 waathiriwa
0 Comment

NEW:Tetemeko la ardhi lazua taharuki MoshiAfyaclass Bongo Social •

NEW:Tetemeko la ardhi lazua taharuki Moshi

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa ‘Ritcher’ 4.6 lililopita usiku wa Julai 16, 2024, likitokea Nairobi, Kenya na kuzua taharuki kwa wakazi wa Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, halijasababisha madhara.

Moshi. Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa ‘Ritcher’ 4.6 lililopita usiku wa Julai 16, 2024, likitokea Nairobi, Kenya na kuzua taharuki kwa wakazi wa Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Hata hivyo inaelezwa kuwa mbali ya kuzua taharuki, tetemeko hilo halijasababisha madhara.

Kwa mujibu wa Mjiolojia Mwandamizi kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania, Gabriel Mbogoni, tetemeko hilo lilitokea saa 2:32 usiku jana likitokea nchi jirani ya Kenya.

Akizungumzia kutokea kwa tetemeko hilo, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Zephania Sumaye amesema hakuna madhara yaliyoripotiwa kuhusiana na tetemeko hilo.

“Mpaka sasa hakuna madhara yoyote ambayo yameripotiwa kuhusiana na tetemeko hilo la ardhi,” amesema Sumaye.

Wakizungumzia taharuki ya tetemeko hilo leo Jumatano Julai 17, 2024, baadhi ya wananchi wa Moshi wamesema walipata mshituko baada ya kuona viti walivyokuwa wamekalia vikisogea.

Jenrose Makashi, mmoja wa wakazi wa Kata ya Msaranga, wilayani Moshi, amesema alishangaa kuona mtikisiko mkubwa umepita kwenye nyumba yao huku baadhi ya vitu kama meza na viti vikisogea.

“Jana jioni tulikuwa tumekaa, tunakula chakula cha jioni nyumbani, tulishangaa ghafla kuona mtetemo mkubwa. Tulifikiri tunanyanyuliwa kwenye viti tulivyokuwa tumekaa. Tulipata mshituko tukafikiri nyumba inaanguka,” amesema Makashi.

Naye Joseph Matei, mmoja wa wananchi wanaoishi Moshi Mjini amesema wakati tetemeko hilo linapita alikuwa amelala akashituka baada ya kusikia kishindo kikubwa kwenye nyumba yao, hali ambayo iliwapa hofu yeye na familia yake.

“Nilikuwa nimelala ghafla nikasikia kama kitanda kinatikiswa, sikujua ni nini. Baadaye nikasikia wenzangu wakisema ilikuwa ni tetemeko la ardhi,” amesema Matei.

Akinukuliwa siku za hivi karibuni, Mjiolojia Mbogoni alisema matetemeko hayo ya ardhi ambayo hujitokeza mara kwa mara maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro huwa yanapita kutokea  maeneo ambayo yako ukanda wa bonde la ufa na kwa kuwa Mkoa wa Kilimanjaro ni miongoni mwa maeneo hayo, ndiyo maana hupita mara kwa mara.

Amesema chanzo chake kinatokana na nguvu za asili ambazo zimejikusanya kwa miaka mingi na  Kilimanjaro iko jirani na mlima wa Oldonyo Lengai ambao huwa unalipuka mara kwa mara.

“Kipande hiki cha ardhi kinajaribu kujigawa kutoka bara la Afrika kuingia baharini, kwa hiyo nguvu ambazo ziligawanya mabara saba duniani, ndiyo yanayoendelea hadi sasa, ndiyo maana Afrika kuna ukanda wa bonde la ufa la Afrika Mashariki ambalo kwa sasa linataka kutenga hiki kipande cha Afrika kiingie baharini,” amesema Mbogoni.

Via:Mwananchi.

 

NEW:Tetemeko la ardhi lazua taharuki Moshi
0 Comment

NEW:Tetemeko la ardhi lazua taharuki MoshiAfyaclass Bongo Social •

 NEW:Tetemeko la ardhi lazua taharuki Moshi

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 'Ritcher' 4.6 lililopita usiku wa Julai 16, 2024, likitokea Nairobi, Kenya na kuzua taharuki kwa wakazi wa Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, halijasababisha madhara.

Moshi. Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 'Ritcher' 4.6 lililopita usiku wa Julai 16, 2024, likitokea Nairobi, Kenya na kuzua taharuki kwa wakazi wa Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Hata hivyo inaelezwa kuwa mbali ya kuzua taharuki, tetemeko hilo halijasababisha madhara.

Kwa mujibu wa Mjiolojia Mwandamizi kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania, Gabriel Mbogoni, tetemeko hilo lilitokea saa 2:32 usiku jana likitokea nchi jirani ya Kenya.

Akizungumzia kutokea kwa tetemeko hilo, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Zephania Sumaye amesema hakuna madhara yaliyoripotiwa kuhusiana na tetemeko hilo.

"Mpaka sasa hakuna madhara yoyote ambayo yameripotiwa kuhusiana na tetemeko hilo la ardhi," amesema Sumaye.

Wakizungumzia taharuki ya tetemeko hilo leo Jumatano Julai 17, 2024, baadhi ya wananchi wa Moshi wamesema walipata mshituko baada ya kuona viti walivyokuwa wamekalia vikisogea.

Jenrose Makashi, mmoja wa wakazi wa Kata ya Msaranga, wilayani Moshi, amesema alishangaa kuona mtikisiko mkubwa umepita kwenye nyumba yao huku baadhi ya vitu kama meza na viti vikisogea.

"Jana jioni tulikuwa tumekaa, tunakula chakula cha jioni nyumbani, tulishangaa ghafla kuona mtetemo mkubwa. Tulifikiri tunanyanyuliwa kwenye viti tulivyokuwa tumekaa. Tulipata mshituko tukafikiri nyumba inaanguka," amesema Makashi.

Naye Joseph Matei, mmoja wa wananchi wanaoishi Moshi Mjini amesema wakati tetemeko hilo linapita alikuwa amelala akashituka baada ya kusikia kishindo kikubwa kwenye nyumba yao, hali ambayo iliwapa hofu yeye na familia yake.

"Nilikuwa nimelala ghafla nikasikia kama kitanda kinatikiswa, sikujua ni nini. Baadaye nikasikia wenzangu wakisema ilikuwa ni tetemeko la ardhi," amesema Matei.

Akinukuliwa siku za hivi karibuni, Mjiolojia Mbogoni alisema matetemeko hayo ya ardhi ambayo hujitokeza mara kwa mara maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro huwa yanapita kutokea  maeneo ambayo yako ukanda wa bonde la ufa na kwa kuwa Mkoa wa Kilimanjaro ni miongoni mwa maeneo hayo, ndiyo maana hupita mara kwa mara.

Amesema chanzo chake kinatokana na nguvu za asili ambazo zimejikusanya kwa miaka mingi na  Kilimanjaro iko jirani na mlima wa Oldonyo Lengai ambao huwa unalipuka mara kwa mara.

"Kipande hiki cha ardhi kinajaribu kujigawa kutoka bara la Afrika kuingia baharini, kwa hiyo nguvu ambazo ziligawanya mabara saba duniani, ndiyo yanayoendelea hadi sasa, ndiyo maana Afrika kuna ukanda wa bonde la ufa la Afrika Mashariki ambalo kwa sasa linataka kutenga hiki kipande cha Afrika kiingie baharini,” amesema Mbogoni.

Via:Mwananchi.


0 Comment

watu walio na afya bora ya utumbo wanaonekana kuwa na mifumo ya kinga inayostahimili magonjwa zaidiAfyaclass Bongo Social •

Fahamu hapa Jinsi ya kuboresha Afya ya utumbo

Si rahisi kutambua utumbo wenye afya kutokana na muundo wake ukilinganisha na viungo vingine, na hakuna chombo kimoja ambacho kinaweza kutumika kupima afya ya utumbo.

Utumbo wetu umejaa vijidudu. Kulingana na wataalamu vijidudu hivyo vikiwekwa pamoja, vinaweza kuwa na uzito wa zaidi ya kilo 1.8.

Kuna bakteria bilioni 100 katika kila gramu ya yaliyomo kwenye matumbo.

Kwa nini ni muhimu kuwa na utumbo wenye afya?

Utumbo unaweza kuathiri “karibu kila kiungo mwilini”, anasema Dk Johnson.

Ubongo na utumbo vina mfumo Thabiti wa mawasiliano unaojulikana kama mhimili wa utumbo na ubongo.

Viungo hivi vinategemeana na kila Kimoja ni muhimu kwa kingine -

Utumbo wakati mwingine huitwa ubongo wa pili kwa sababu bakteria wanaweza kuathiri mienendo yetu kupitia Neurons milioni 100 kwenye utumbo.

Neurons ni seli zinazopatikana katika ubongo wetu na mfumo mkuu wa neva ambao huelekeza mwili wetu jinsi ya kuishi.

Utumbo wa nje unaweza hata kudhibiti hali yetu kwa kutoa vipitishio vya mawasiliano vinavyopatikana kwenye ubongo, kama vile serotonin.

Jukumu linalojulikana zaidi la utumbo ni kufyonza virutubisho kutoka kwa chakula.

"Hatuwezi kuwa tunapoteza maji na madini kwenye kinyesi," anaelezea Dk Venkatraman Krishna, daktari wa magonjwa ya tumbo nchini India.

Dk Megan Rossi, anayejulikana pia kama Daktari wa Afya wa Utumbo nchini Uingereza, anasema kukosekana kwa vijidudu vya utumbo sasa kumehusishwa na zaidi ya hali 70 tofauti za kiafya - kutoka magonjwa ya moyo, mishipa ya kupumua hadi magonjwa ya kinga ya mwili kama ugonjwa wa arheumatoid arthritis.

Takribani 70% ya seli zetu za kinga huishi kwenye sehemu ya utumbo, na "huwasiliana mara kwa mara" na mfumo wa kinga, anasema Dk Rossi.

Hii ndiyo sababu "watu walio na afya bora ya utumbo wanaonekana kuwa na mifumo ya kinga inayostahimili magonjwa zaidi", anaongeza.

Unawezaje kuimarisha afya ya utumbo?

Kufuatia utafiti uliofanywa na Mradi wa American Gut 2018, wataalamu walianza kuwashauri watu kula walau aina 30 ya lishe inayotokana na mimea kila wiki ili kukuza bakteria wanopatikana kwenye utumbo.

Hii sio tu ni pamoja na matunda na mboga, lakini pia vitu kama mbegu, viungo na karanga.

Dk Rossi anashauri watu kuongeza matunda katika lishe ili kuimarisha afya ya utumbo.

Lishe yenye nyuzinyuzi nyingi hutusaidia kujisikia kamili, husaidia usagaji chakula na kuzuia kuvimbiwa, kulingana na Huduma ya Kitaifa ya Afya ya Uingereza, ambayo inapendekeza watu wazima kula gramu 30 ya nyuzi kwa siku.

Kuchagua mikate ya unga au punje badala ya nyeupe, na kuchagua wali wa kahawia au pasta ya ngano, kunaweza kuongeza ulaji wako wa nyuzi.

Chanzo kingine cha nyuzinyuzi ni pamoja na viazi ambavyoo havijamenywa (kama vile viazi vilivyookwa) na kunde kama maharagwe, dengu au mbaazi, ambazo zinaweza kuongezwa kwenye kitoweo, kari na saladi.

Vyakula vya prebiotic (aina fulani za nyuzi na wanga) vimepatikana ili kuhimiza ukuaji wa bakteria rafiki kwenye utumbo.

Baadhi ya vyakula hivyo ni ndizi, vitunguu, kabichi, nafaka, na zabibu.

Dk Hanisha Khemani, mtaalam wa magonjwa ya tumbo nchini Pakistan, anasema kuanzisha "mlo uliosawazishwa, na wenye virutubisho" katika miaka yetu ya 20 ni "muhimu kwa afya ya muda mrefu".

Ni vyakula gani Vibaya kwa utumbo

Matumizi ya vyakula vilivyochakatwa sana, pombe na tumbaku si mazuri kwa utumbo wako, aeleza Dk Krishna.

Chakula kilichochakatwa sana kina viambato ambavyo ama hukandamiza bakteria 'nzuri' au kuongeza bakteria 'mbaya'.

Kwa kuzingatia mahali ulipo ulimwenguni, huenda ukalazimika kuacha kununua vyakula kutoka kwa wachuuzi wa mitaani wasiozingatia usafi hasa wa kuosha matunda na mboga ili kujikinga dhidi ya virusi au bakteria hatari, Dk Krishna anaongeza.

Anasisitiza uchafua matumbo yetu, na inaweza kuongeza asidi na vidonda vya tumbo.

Dkt Johnson anasema watu walio na mfadhaiko zaidi huwa na vijidudu vidogo vya aina mbalimbali.

Maelezo|Source:Via Bbc



0 Comment

Mazoezi hunufaisha sana afya ya ubongo, na kuboresha utambuzi,Afyaclass Bongo Social •


Mazoezi hunufaisha sana afya ya ubongo, na kuboresha utambuzi, 

Mazoezi hunufaisha sana afya ya ubongo, kuboresha utambuzi, hisia na kupunguza hatari ya magonjwa ya mfumo wa neva. 

Tafiti nyingi mpya zimeonyesha athari kubwa ya mazoezi kwenye mifumo mbalimbali ya kibaolojia, ikieleza zaidi uwezo wake wa kuimarisha afya na kupambana na magonjwa.  Katika Kipengele hiki Maalum, tunachunguza utafiti wa hivi majuzi zaidi kuhusu jinsi mazoezi yanaweza kulinda afya ya ubongo tunapozeeka.

 Tafiti za hivi karibuni huchunguza njia ambazo mazoezi husaidia kuongeza muda wa afya, na kudumisha afya ya ubongo na umri. 

 Mazoezi yanahusishwa na kuongezeka kwa nguvu za misuli, uboreshaji wa afya ya moyo, sukari kuwa kwa kiwango cha chini kwenye damu na faida zingine nyingi za kiafya.

 Mazoezi kama vile kukimbia, kuendesha baiskeli juu ya mlima na mwinuko, kunyanyua vyuma au kuchukua matembezi ya haraka wakati wa chakula cha mchana hutoa faida mbalimbali zinazopita zaidi ya kuimarisha mwonekano wa kimwili au stamina.

 Ushahidi kutoka kwa tafiti unaonyesha kuwa mazoezi ya kawaida ya mwili yanaweza kuongeza hisia, kupunguza mfadhaiko, na kunoa utendakazi wa utambuzi, ikisisitiza uhusiano wa kina kati ya mwili na akili.

 Hata hivyo, watu tofauti wanaweza kuitikia kwa njia tofauti kabisa kwa aina mbalimbali za mazoezi, kama vile mazoezi ya aerobiki au mafunzo ya nguvu.

 Ingawa inajulikana kuwa mazoezi ya kawaida ni muhimu kwa maisha yenye afya, utafiti fulani wa zamani umependekeza kuwa mazoezi makali yanaweza kuwa na athari mbaya.

 Utafiti wa hivi majuzi zaidi, hata hivyo, ulionyesha kuwa wanariadha mashuhuri walipata matarajio ya maisha yaliyoongezwa kidogo kwa miongo kadhaa.

0 Comment

Dalili za magonjwa ya figo ambazo hakuna Mtu anazizungumziaAfyaclass Bongo Social •

Dalili za magonjwa ya figo ambazo hakuna Mtu anazizungumzia

Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni wa Shirika la India la Nephrology, watu milioni 84 duniani kote wanaugua magonjwa mbalimbali ya figo, yaani, mtu mmoja kati ya kila watu kumi duniani ana aina fulani ya ugonjwa wa figo.

Ikumbukwe kwamba kati ya sababu kumi za vifo duniani, ugonjwa wa figo uko katika nafasi ya saba.

Moja ya sababu za kuongezeka kwa magonjwa ya figo ni kwamba magonjwa haya hayazingatiwi kuwa mabaya katika hatua za mwanzo. Mara nyingi umakini huoneshwa kwa ugonjwa wa figo ugonjwa huo unapofikia hatua mbaya.

Kwa hiyo, ni muhimu kuelewa magonjwa ya figo na dalili zake na kumsaidia Mgonjwa katika hatua za mwanzo za ugonjwa huo.

Lakini kabla ya kuendelea na maelezo mengine, ni nini na jinsi gani figo hufanya kazi?

Je, kazi ya figo ni nini?

Figo ni moja ya viungo muhimu vya mwili wa binadamu, ambayo kazi yake kuu ni kuondoa taka kutoka mwilini kwa njia ya mkojo.

Kwa kusudi hili, figo hutenganisha vitu kutoka kwenye damu, ambavyo ni hatari kwa mwili wa binadamu, ikiwa ni pamoja na baadhi ya madini yasiyo ya lazima, na kisha damu safi huzunguka katika mwili.

Mtindo wa maisha, lishe, tabia, matatizo ya kijeni, dawa na matatizo mengine yanayohusiana na afya yanaweza kusababisha kushindwa kufanya kazi kwa figo.

Usumbufu katika utendaji wa kawaida wa figo husababishwa na magonjwa fulani. Hatari kubwa katika suala hili ni kwamba ugonjwa huo haujatambuliwa katika hatua za mwanzo na baadhi ya dalili zake hazionekani kabisa.

Fahamu kadiri ugonjwa unavyoendelea, dalili huonekana na unaweza kuelewa maendeleo haya kupitia uchunguzi na vipimo vya afya pekee.

Hebu sasa tuambie ni magonjwa gani ya kawaida ya figo na dalili zake.

#SOMA PIA Dalili za Ugonjwa wa Figo kwenye Makala Hii

Ugonjwa sugu wa figo

Aina hii ya ugonjwa wa figo hudumu kwa muda mrefu na mara nyingi huwapata watu wenye kisukari au shinikizo la damu.

Katika hatua za mwanzo za ugonjwa huu, hakuna dalili zinazoweza kuonekana, lakini jambo muhimu ni kwamba ugonjwa huu unaweza kuponywa kwa matibabu sahihi.

Dalili zake ni pamoja na:

  • kutapika,
  • kukosa hamu ya kula,
  • kuvimba miguu na viungo,
  • matatizo ya kupumua,
  • kukosa usingizi
  • Pamoja na kujisaidia haja ndogo kidogo.

Mawe kwenye figo

Mawe kwenye figo kimsingi ni madini ambayo hujilimbikiza kwenye figo na kuwa na muonekano wa mawe.

Kulingana na wataalamu wa matibabu, baada ya jiwe moja au mawili kuundwa, kwa mara ya kwanza hakuna dalili na mgonjwa hana matatizo yoyote makubwa.

Tatizo hili husababishwa na unywaji wa maji kidogo, unene kupita kiasi, lishe isiyofaa na mtindo wa maisha.

Watu wanaougua ugonjwa huu hupata shida kupata haja ndogo au kuwa na damu kwenye mkojo. Watu walioathirika wanalalamika kwa maumivu kwenye eneo la figo lenye jiwe.

#SOMA Zaidi hapa kuhusu Mawe kwenye figo

Ugonjwa wa figo kutokana na kisukari

Kwa mujibu wa utafiti, kila mtu wa tatu mwenye kisukari anaugua ugonjwa wa figo na figo zao kushindwa kufanya kazi.

Ugonjwa huu ni wa kawaida zaidi kwa watu ambao hawana udhibiti wa ugonjwa wa kisukari.

Dalili zake ni pamoja na;

  • maumivu ya miguu,
  • uchovu,
  • kupoteza uzito,
  • upele wa mwili,
  • na kutapika.

Ugumu wa figo na shinikizo la damu

Mbali na ugonjwa wa kisukari, ugonjwa unaoharibu figo ni shinikizo la damu, kutokana na mishipa ya damu kwenye figo kuharibika na kazi yake ya kawaida huathirika.

Kwa sababu hii, figo haiwezi kufanya kazi yake ya kusafisha vitu visivyohitajika kutoka kwenye damu na haiwezi kuondoa madini hatari kwenye mwili kutoka kwenye damu. Kwa hivyo, vitu visivyo vya lazima hujilimbikiza kwenye mishipa ya damu na shinikizo la damu huongezeka zaidi.

Dalili ni pamoja na;

  • kichefuchefu na kutapika,
  • udhaifu wa mwili,
  • maumivu ya kichwa na shingo.

Maambukizi katika njia ya mkojo(UTI)

ingawa maambukizi ya mfumo wa mkojo sio ugonjwa wa figo moja kwa moja, huathiri figo.

Ugonjwa huu unaweza kusababishwa na bakteria na iwapo bakteria hao hawatazuiliwa na kutibiwa haraka wanaweza kufika sehemu ya juu ya njia ya mkojo na kuharibu figo.

Dalili zake ni pamoja na;

  • maumivu ya mgongo,
  • homa,
  • kuumia wakati wa kukojoa,
  • maumivu ya tumbo,
  • Kutoka damu kwenye mkojo,
  • kuumwa miguu na kutapika.

#SOMA ZAIDI Kuhusu Ugonjwa wa UTI pamoja na Dalili Zake

Ugonjwa wa figo wa polycystic

Ugonjwa huu husababishwa na uvimbe kwenye kibofu ambao hukua kwa muda na kusababisha figo kushindwa kufanya kazi. Jeni pia inaweza kuwa sababu.

Dalili za ugonjwa huu ni pamoja na;

  • maumivu katika sehemu ya juu ya tumbo,
  • maumivu upande mmoja wa tumbo,
  • damu kwenye mkojo n.k.

AJ Nephropathy

Ugonjwa wa figo kwa kawaida huanza utotoni na wakati wa ujana.

katika ugonjwa huu, Unaweza kuona damu kwenye mkojo. Ugonjwa huu unaweza kutambuliwa kupitia vipimo.

Figo kushindwa kufanya kazi

Katika kushindwa, figo huacha kufanya kazi, kwa sababu mara nyingi, dalili huonekana kwa watu wenye ugonjwa huu, wakati ugonjwa huo unaendelea sana.

Kuna hatua tano za ugonjwa huu na dalili hazionekani hadi hatua ya nne.

Dalili za ugonjwa huu huonekana tu wakati figo zinaacha kufanya kazi kabisa.

Dalili zinazoonekana kwa wakati huu ni pamoja na kupoteza hamu ya kula, kutapika, udhaifu mkubwa wa kimwili, uvimbe wa sehemu za mwili na usingizi.



0 Comment

Madhara ya acid tumboni,Fahamu hapaAfyaclass Bongo Social •

Madhara ya acid tumboni,Fahamu hapa

Asidi ya tumbo ni muhimu kwa usagaji wa chakula, lakini wakati mwingine seli zinazozalisha asidi katika mfumo wako wa usagaji chakula husukuma asidi nyingi kupita kiasi.

Asidi inapokuwa nyingi tumboni ndipo madhara huanza kuonekana Zaidi,Dalili za asidi kuwa nyingi tumboni zinaweza kujumuisha maumivu ya tumbo, kiungulia.n.k.

#SOMA Pia kuhusu Tatizo la Acid Reflux,chanzo,dalili na Tiba

Kuna baadhi ya sababu za uzalishaji wa asidi kuzidi tumboni ikiwa ni pamoja na maambukizi ya bakteria, Stress, na athari za baadhi ya dawa.

Makala hii itajadili Sababu zinazohusishwa na kuzidi kwa asidi tumboni, ishara na dalili zake, Pamoja na njia za kupunguza dalili zinazotokea kama matokeo.

Dalili za Asidi kuzidi Tumboni

Dalili za asidi kuzidi tumboni zinaweza kujumuisha:

  • Kiungulia
  • Kuhisi Ladha ya Chachu kinywani mwako(Sour taste)
  • Kuwa na Kikohozi cha mara kwa mara au kwikwi
  • Sauti kubadilika
  • Tumbo Kujaa
  • Kichefuchefu
  • Kuharisha n.k

Chanzo cha Acid kuwa nyingi Tumboni

Zipo Sababu mbali mbali zinazopelekea kuzalishwa kwa kiwango kikubwa cha Acid Tumboni, Sababu hizo ni pamoja na;

1. Maambukizi ya bacteria kama vile Helicobacter pylori (H. pylori)

Helicobacter pylori (H. pylori) ni bacteria ambaye huharibu tissues ndani ya tumbo lako pamoja na Sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo ambayo hujulikana kama duodenum.

#Mfahamu Zaidi bacteria huyu wa Helicobacter pylori (H. pylori) 

Ukiwa na maambukizi makali ya bacteria wa H.pylori tumboni huweza kupelekea kuongezeka kwa kiwango cha Acid Tumboni, Ingawa pia maambukizi haya yakiwa ya Muda Mrefu(chronic infection) huweza kupunguza uzalishaji wa gastric acid.

2. Kuwa na Stress

Fahamu kwamba,Stress au Msongo wa Mawazo huhusishwa na kuchelewa kwa Acid kutoka tumboni yaani delayed gastric emptying of acid.

Tafiti zinaonyesha kuwa msongo wa mawazo wa muda mrefu unaweza pia kumaliza prostaglandini, ambayo hulinda utando wa tumbo kutokana na asidi, na kuongeza hatari ya kupata vidonda vya Tumbo.

#Soma Zaidi kuhusu Madhara ya Stress na Njia za kukabiliana na Stress kwa binadamu

3. Matumizi ya baadhi ya Dawa,

Zipo baadhi ya dawa ambazo huweza kusababisha Ongezeko la Acid tumboni mwako.

4. Matatizo Mengine kama vile Zollinger-Ellison syndrome (ZES)

ni hali ya nadra ya usagaji chakula ambapo uvimbe wa neuroendocrine unaoitwa gastrinomas husababisha tumbo lako kutoa asidi nyingi. Tumors hizi huzalisha gastrin, homoni ambayo huchochea uzalishaji wa asidi. ZES wakati mwingine iko kwa wale ambao wana hali adimu za kijeni kama vile aina nyingi za endokrini neoplasia 1 (MEN1)

Madhara ya acid tumboni

Acid ikizidi Tumboni huweza kuleta Madhara mbali mbali kama vile;

– Kupata Vidonda vya Tumbo,Peptic ulcers:

Vidonda hivi ni matokeo ya Acid kula ukuta wa tumbo au sehemu ya kwanza ya Utumbo mdogo yaani duodenum lining.

– Kuwa na tatizo la Gastroesophageal reflux disease (GERD):

Tatizo hili hujulikana pia kama Acid reflux, na huhusisha acid kutoka Tumboni kupanda juu kwenye njia ya chakula–umio au esophagus.

#SOMA Pia kuhusu Tatizo la Acid Reflux,chanzo,dalili na Tiba

– Kupata tatizo la Gastrointestinal (GI) bleeding:

Tatizo hili huhusisha kuvuja damu kwenye tumbo na Utumbo,kutokana na acid kuharibu au kula kuta za tumbo na utumbo,kisha kupelekea majeraha yanayohusisha mishipa ya damu kwenye eneo hili.

Hayo ni baadhi ya Madhara ya Acidi Tumboni. Ikiwa Una Tatizo hili hakikisha Unapata Tiba Mapema na;

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comment

Faida Za Nanasi Mwilini mwako,Soma hapa kufahamuAfyaclass Bongo Social •

Nanasi ni tunda la kitropiki ambalo huchukua miaka mitatu kukomaa. Nanasi ni tamu, huongeza vitamini na virutubisho mbalimbali kwa afya ya mlaji. Pia hupambana na magonjwa.

Nanasi lina faida mbalimbali za afya, ikiwa ni pamoja na kuboresha usagaji wa chakula, kuondoa hatari ya saratani, na kuondoa maumivu.

Hata hivyo, wale walio na mzio wanapaswa kuepuka matunda haya na wale wanaotumia dawa za kupunguza damu wanapaswa kuwa waangalifu.

Kupambana na magonjwa

Tunda hili lina utajiri mkubwa wa vitamini C na magnishiamu. Vitamini C ni muhimu katika kusaidia kinga ya mwili.

Magnishiamu husaidia kupambana na seli zinazoweza kuleta madhara katika mwili, husaidia kuzuia uvimbe ambao unaweza kusababisha saratani na magonjwa mengine sugu.

Nanasi ni chanzo muhimu cha kupambana na magonjwa. Kutumia nanasi mara kwa mara kunaweza kukupunguzia hatari ya kupata ugonjwa wa moyo na kisukari.

Usagaji wa chakula

Tunda hili lina enzaimu wa kusaidia usagaji chakula waitwao bromelain, ambao husaidia kurahisisha usagaji wa chakula.

Bromelain huvunja molekuli za protini, ikimaanisha utumbo wako mdogo unaweza kuzifyonza kwa urahisi zaidi.

Hilo ni muhimu sana kwa watu walio na upungufu wa maji ya kongosho, hali inayoifanya kongosho kutotengeneza vimeng’enya vya kutosha vya kusaga chakula.

Kwa kuwa lina nyuzinyuzi nyingi, pia husaidia mfumo wa usagaji chakula na kuboresha afya ya vijidudu vyenye faida ambavyo hukaa kwenye utumbo wako.

Uponyaji baada ya kuumia

Tafiti kadhaa zinaonyesha kuwa bromelain ambayo pia inapatikana katika nanasi, husaidia kupunguza uvimbe na michubuko baada ya jeraha au upasuaji.

Nanasi linaweza kuwa muhimu ikiwa utakula kabla ya ung’oaji wa jino, husaidia kupunguza maumivu na kutoa ahueni kama vile dawa ya kuzuia maambukizi.

Utafiti wa taasisi ya Vitro (uliofanywa katika maabara), pia umeonyesha bromelain husaidia katika uponyaji wa jeraha.

Kupunguza maumivu ya viungo

Tatizo la maumivu ya viungo, ni ugonjwa unaohusisha viungo kuvimba, kuwa vyekundu na kuleta maumivu. Ugonjwa huu ni matokeo ya mfumo wa kinga kushambulia tishu zenye afya kimakosa.

Tafiti nyingi, zilizoanzia miaka ya 1960, zimeonyesha jinsi bromelaini inavyoweza kuwa muhimu katika kutuliza maumivu yanayohusiana na viungo.

Maumivu ya viungo huathiri zaidi ya watu wazima milioni 54 huko Marekani. Kuna aina nyingi za ugonjwa wa maumivu ya viungo, lakini mengi ya magonjwa hayo huhusisha kuvimba kwa viungo.

Virutubisho vya bromelaini, husaidia kuondoa maumivu katika sehemu ya chini ya mgongo kama sawa na matibabu ya maumivu.

Kusaidia kinga ya mwili

Utafiti wa wiki tisa wa watoto wa shule ambao walikula kiasi cha wastani cha mananasi kila siku, walikuwa na hatari ndogo sana ya kuambukizwa virusi au bakteria kuliko wale ambao hawakula.

Mbali na hayo, wale waliokula kiasi kikubwa walipata mara nne ya idadi ya seli nyeupe za kinga za kupambana na maambukizi.

Nanasi pia kusaidia kurekebisha mfumo wa kinga, na linaweza kuwa bora kwa wale walio na kinga dhaifu za mwili.

Kusaidia mfumo wa moyo

Kwa mara nyingine tena, ni bromelain ambayo inaonekana kuwa na umuhimu kwa moyo na mfumo wa mzunguko wa damu, kwa kuzuia au kupunguza ukali wa mshtuko wa moyo.

Uchunguzi kwa wanyama unaonyesha bromelain pia huzuia shinikizo la damu, kuganda kwa damu kwa kuzuia utengenezwaji wa protini inayoitwa fibrin ambayo inahusika katika kuganda kwa damu.

Kupunguza hatari ya pumu

Juisi ya nanasi pia inaweza kuwa na ufanisi katika kupunguza dalili zinazohusiana na pumu. Katika utafiti wa wanyama, watafiti waligundua kuwa bromelain zinaweza kuwa na faida kwa watu wanaoishi na pumu.

Zaidi ya hayo, nanasi lina vitamini C, ambavyo hulainisha mirija ya mapafu. Na katika matukio ya mashambulizi ya pumu kutokana na baridi, vitamini C vilikuwa ya manufaa

Nanasi ni salama kwa kila mtu?

Kama huna mzio na nanasi, kwa ujumla inatambulika kuwa nanasi ni salama kwa watu wengi na ni sehemu ya lishe bora.

Hata hivyo, kula au kunywa kiasi kikubwa kunaweza kusababisha shida ya usagaji chakula. Jambo jingine ni kujiepusha kula nanasi ambalo halijaiva kwa sababu, linaweza kusababisha kuhara na kuwasha koo.

Zaidi ya hayo, ikiwa unakabiliwa la asidi ya reflux, nanasi linaweza kuongeza dalili zako. Asidi hiyo inaweza kusababisha kiungulia.

Wale wanaotumia dawa za kupunguza damu wanapaswa kukumbuka kwamba bromelaini iliyo katika nanasi inaweza kuathiri uwezo wa damu kuganda na inapoliwa kwa wingi, na kwa kushirikiana na dawa za kupunguza damu, inaweza kuongeza hatari ya kutokwa na damu.

Licha ya faida zake, ni muhimu kukumbuka kuwa juisi ya mananasi ina nyuzinyuzi kidogo lakini ina sukari nyingi sana.

Hii inamaanisha haitakuwa na uwezo wa kukujaza tumbo lako kama kula nanasi la kawaida la kiwango hicho hicho, lakini inaweza kusababisha uzito kwa baadhi ya watu.

Via:Bbc



0 Comment

Muuguzi wa KCMC atoweka kwenye mazingira ya kutatanishaAfyaclass Bongo Social •

Muuguzi wa KCMC atoweka kwenye mazingira ya kutatanisha

Zikiwa zimepita siku sita tangu muuguzi wa Hospitali ya KCMC, idara ya masikio, pua na koo, Lenga Masunga, kutoweka katika mazingira ya kutatanisha, mwenye nyumba alikokuwa akiishi, Robert Mwakalinga, amesimulia namna alivyoamka asubuhi na kukuta mlango wa chumba alichokuwa amepanga ukiwa wazi.

Akizungumza nasi nyumbani hapo leo Jumatatu Julai 8, 2024, Mwakalinga, mkazi wa Mtaa wa Rau Pangaleni, Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, amesema Jumatano, Julai 3, 2024, alipoamka asubuhi alikuta chumba cha muuguzi huyo kikiwa wazi, huku ndani kukiwa hakuna mtu. Hali hiyo ilimlazimu kukifunga chumba hicho.

Mwakalinga anasema Jumatano Julai 2, muuguzi huyo alirudi nyumbani saa mbili usiku wakati yeye alikuwa analisha mifugo yake nje, alimsalimia na akaingia ndani kama ilivyokuwa kawaida yake.

“Huyu kijana ni mpangaji wangu. Alikuja siku ya Jumanne usiku, alinikuta nikilisha kuku wangu, alinisalimia, akaingia ndani. Baadaye alikaa kama dakika tano, akatoka nje kwenda msalani, akarudi. Alipoingia ndani hakutoka tena na muda huo ilikuwa imefika saa tatu na dakika kadhaa. Nami niliingia ndani na sikutoka tena nje mpaka asubuhi,” amesema Mwakalinga.

Hata hivyo, amesimulia kuwa asubuhi alivyotoka nje, alikuta mlango wa chumba cha muuguzi huyo uko wazi.

Amesema: “Nikaita nikaona kimya, nikajiuliza imekuwaje mlango uko wazi, nilipoingia ndani, niliona mabegi yake kama yamepekuliwa na moja likiwa karibu na mlango lakini hakukuwa na mtu ndani.” Mwenye nyumba huyo amesema tangu usiku ule walipoonana na muuguzi huyo, mpaka sasa hajui yuko wapi.

Akimwelezea muuguzi huyo, Mwakalinga amesema alikuwa sio mtu wa makundi na mara zote alikuwa akitoka kazini huingia ndani na kujifungia.

“Alikuwa sio mtu wa makundi wala kujichanganya na watu. Alikuwa akitoka kazini anaingia zake ndani na wakati mwingine akiwa ndani unaweza usijue kama yupo kama hujamwona wakati anaingia,” ameeleza.

Akimzungumzia muuguzi huyo, Mratibu wa idara ya masikio, pua na koo, Hospitali ya KCMC, Neema Masawe,  amesema  Julai 4, 2024, alipaswa kuwepo kazini lakini hakufika na hata alipotafutwa kupitia simu zake za mkononi hakupatikana.

“Julai 4, mwaka huu, alikuwa awe zamu ya asubuhi na kawaida yake huwa anawahi kufika hospitali mapema. Sasa ilipofika saa 1:30 asubuhi tukawa hatujamuona, tukasema labda yuko ibadani, ilipofika saa mbili asubuhi tukaona hajafika tukaanza kujiuliza kwa nini amechelewa kazini kwa kuwa si kawaida yake,” amesema Massawe.

Amesema waliamua kumtafuta anakoishi na walipofika hawakumkuta, bali walikutana na mwenye nyumba wake.

“Tukawatafuta marafiki zake wa karibu ili tujue taarifa zake, nao hawakujua wapi alipo. Baadaye tulitoa taarifa kwa uongozi wakatushauri tuendelee kumtafuta.

Tuliondoka kama watano, tulimtafuta kwa saa nane bila mafanikio, tukarudi nyumbani anakoishi tukamkuta mwenye nyumba aliyetuambia alipoamka asubuhi alikuta chumba chake kiko wazi na ndani hakukuwa na mtu,” amesema Massawe. Amesema baadaye waliamua kutoa taarifa Kituo cha Polisi cha Polisi Longuo na wakapatiwa RB namba LNG/RB/33/2024 na kisha kuandika maelezo.

Amesema mpaka sasa wanaendelea kumtafuta kupitia simu zao za mkononi lakini hawajafanikiwa kumpata.

Akizungumzia utendaji wake wa kazi, amesema tangu aajiriwe mwaka 2023, amekuwa ni mtu wa kujituma na mwenye upendo na kila mtu na  mara kadhaa amekuwa akipongezwa kwa utendaji mzuri wa kazi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi, uchunguzi  wa tukio hilo bado unaendelea.

Share this Kusaidia apatikane..!!!!

Muuguzi wa KCMC atoweka kwenye mazingira ya kutatanisha
0 Comment

Ripoti Mpya;Ongezeko la Joto Duniani lisilolakawaidaAfyaclass Bongo Social •

Kulingana na ripoti mpya iliyotolewa na Huduma ya Mabadiliko ya Tabia nchi ya Muungano wa Ulaya ya Copernicus, wastani wa hali joto duniani umekuwa juu ya nyuzi joto 1.5 za Selsiasi kwa miezi 12 mfululizo jambo ambalo si la kawaida na mara ya mwisho kushuhudia hali kama hii ilikuwa mwaka 2015/2018.

Data za Huduma ya Mabadiliko ya Tabia nchi ya Muungano wa Ulaya, Copernicus ERA5, zinaonesha kwamba mwezi juni ulikuwa na nyuzi joto 1.50 za Selsiasi juu ya makadirio ya awali ya Mwezi Juni kwa mwaka 1850 – 1900 wakati wa mapinduzi ya viwanda ikiwa huu ni mwezi wa 12 mfululizo hali joto kuvuka nyuzi joto 1.5.

“Takwimu hizi za hivi karibuni  kutoka kwa Huduma ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa ya Copernicus kwa bahati mbaya zinaangazia kwamba tutakuwa tukizidi kiwango cha nyuzijoto 1.5 za selsiasi kwa muda na kuongezeka kwa marudio, kila mwezi. Hata hivyo, ni muhimu kusisitiza kwamba ukiukaji wa muda mfupi haumaanishi kuwa lengo la 1.5 °C litapotea kabisa kwa sababu hii inahusu ongezeko la joto la muda mrefu kwa angalau miongo miwili,” Anasema Katibu Mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Celeste Saulo.

Katika mkataba wa Paris, nchi zilikubaliana kuweka wastani wa halijoto wa muda mrefu  kuwa ni chini ya nyuzi joto 2 kabla ya kuanza kwa viwanda na baadae wakaweka kikomo hadi nyuzi joto 1.5 kufikia mwisho wa karne hii, huku wanasayansi wameonya mara kwa mara kwamba ongezeko la joto la zaidi ya nyuzi joto 1.5 linasababisha athari mbaya zaidi za mabadiliko ya tabianchi.

Hata, Katika viwango vya sasa vya ongezeko la joto duniani, tayari kuna athari mbaya za hali ya hewa ambazo ni Pamoja na joto kali, mvua kali na ukame, barafu ya bahari, kuongeza kasi ya kupanda kwa kina cha bahari na joto la bahari.

“Juni ilishuhudiwa kuenea na kuongezeka kwa joto kwa muda mrefu katika nchi nyingi, na athari kubwa katika nyanja zote za maisha ya watu. Hii ilikuwa hata kabla ya kilele cha jadi cha majira ya joto ya kaskazini mwa ulimwengu, ambayo bila shaka itaona joto kali zaidi. Halijoto iliyorekodiwa kwenye uso wa bahari inatia wasiwasi mkubwa kwa mifumo ya ikolojia ya baharini na pia inatoa nishati kwa vimbunga vya kitropiki vinavyoshangaza zaidi – kama tulivyoona kwenye Kimbunga Beryl,” Amesema Celeste Saulo.

WMO hutumia hifadhi data sita za kimataifa, ikiwa ni pamoja na ERA5, kwa hali yake ya ufuatiliaji wa tabianchi. Ni muhimu kutambua kwamba hifadhi data nyingine huenda zisithibitishe mfululizo wa miezi 12 ulioangaziwa na Huduma ya Mabadiliko ya Tabianchi ya Copernicus, kutokana na ukingo mdogo zaidi ya nyuzi joto 1.5 ya viwango vya joto duniani ERA5 kwa Julai na Agosti 2023 na Mei na Juni 2024.

Mkurugenzi wa Huduma ya Mabadiliko ya Tabianchi ya Copernicus, Carlo Buontempo anatoa tahadhari kwamba hata kama hali hii ya kuongeza kwa hali joto itaisha kwa wakati Fulani, lakini kuna uwezekano mkubwa wa jambo hili kujirudia tena, hivyo dunia inapaswa kuangalia namna ya kuacha kuongeza hewa chafu kwenye ang ana bahari ili kuepukana na athari za baadae endapo jambo hili litajirudia tena.

Ripoti Mpya;Ongezeko la Joto Duniani lisilolakawaida
0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD