Ugonjwa wa Amoeba: Sababu, Dalili na MatibabuAfyaclass Bongo Social •

Ugonjwa wa Amoeba: Sababu, Dalili na Matibabu

Ugonjwa wa amoeba ni ugonjwa hatari unaosababishwa na kimelea(parasite) kinachoitwa Entamoeba histolytica.

Entamoeba histolytica  ni kimelea kwenye kundi la anaerobic parasite na kwa mara ya kwanza hupatikana kwenye Utumbo mpana(colon);

Ingawa kutokana na Sababu zisizofahamika, kimelea hiki kina uwezo wa kutoka na kupita moja kwa moja mpaka kwenye Ini na kusababisha tatizo ambalo hujulikana kwa kitaalam kama amoebic liver abscesses."

Kimelea hiki kinaishi kwenye Utumbo wa binadamu na kinaweza kusababisha ugonjwa wa amoeba kwa mtu yeyote anayekula au kunywa kitu kilichoambukizwa na kimelea hiki.

Katika makala hii, tutajifunza kuhusu sababu, dalili na matibabu ya ugonjwa wa amoeba.

KUMBUKA; amoebiasis-Ndyo ugonjwa wenyewe ambao chanzo chake ni kimelea au parasite anayejulikana kama Entamoeba histolytica.

NANI YUPO KWENYE HATARI YA KUPATA UGONJWA WA AMOEBA(AMOEBIASIS)?

Ingawa mtu yoyote anaweza kuugua Ugonjwa wa amoeba, Tatizo hili huwapata sana watu ambao wanaishi kwenye mazingira machafu,

Lakini Pia baadhi ya Tafiti zinaonyesha Ugonjwa wa Amoeba(amoebiasis) huwapata sana Wanaume wanaoshiriki Mapenzi na wanaume wenzao

Sababu ya Ugonjwa wa Amoeba:

Ugonjwa wa amoeba husababishwa na kimelea kinachoitwa Entamoeba histolytica,

Kimelea hiki hupatikana kwenye kinyesi cha mtu aliyeambukizwa na kinaweza kuambukiza mtu mwingine kupitia chakula au maji yaliyoambukizwa.

Mbali na hilo, mtu anaweza kuambukizwa ugonjwa huu kwa kugusa vitu vilivyoambukizwa kwa mikono iliyochafuliwa na kimelea hiki.

Dalili za Ugonjwa wa Amoeba:

Baadhi ya dalili za ugonjwa wa amoeba ni pamoja na:

  1. Mtu Kuharisha mara kwa mara
  2. Mtu Kupata Maumivu ya tumbo
  3. Kupoteza hamu ya kula
  4. Kuhisi Kichefuchefu pamoja na Kutapika
  5. Kuhisi kizunguzungu n.k

Katika baadhi ya matukio, ugonjwa huu unaweza kusababisha matatizo makubwa zaidi ya kiafya kama vile;

  • kuvuja kwa damu kwenye utumbo
  • Pamoja na maambukizi kwenye ini.

Matibabu ya Ugonjwa wa Amoeba:

Matibabu ya ugonjwa wa amoeba hutegemea kiwango cha ugonjwa na dalili zinazojitokeza,

Dawa za kuuwa vimelea hivi vinavyosababisha Ugonjwa wa amoeba hutumiwa kutibu ugonjwa huu.

Matibabu ya maumivu ya tumbo pia yanaweza kutolewa kwa wagonjwa ambao wanapata maumivu makali.

Kwa kuongezea, lishe bora ni muhimu katika kusaidia kupona haraka kwa ugonjwa huu.

Kuzuia Ugonjwa wa Amoeba:

Kuzuia ugonjwa wa amoeba ni muhimu sana ili kuepuka madhara ya kiafya. Baadhi ya njia za kuzuia ugonjwa huu ni pamoja na:

✓ Kufuata kanuni zote za usafi wa mazingira

✓ Kunywa maji safi na salama

✓ Kula chakula kilichoandaliwa vizuri

✓ Nawa Mikono kwa Sabuni na Maji safi kabla ya kula au kunywa kitu chochote

#SOMA ZAIDI Hapa Ugonjwa wa Amiba

AMIBA

• • • • •

UGONJWA WA AMIBA(chanzo,dalili na Tiba yake)

Huu ni ugonjwa unaohusu utumbo mpana wa binadamu kushambuliwa na vimelea vya magonjwa ambavyo kwa kitaalam hujulikana kama Amoeba.

CHANZO CHA UGONJWA WA AMIBA

 Hivo basi, chanzo cha ugonjwa wa amiba ni mashambulizi ya vimelea vya amiba hasa hasa jamii ya Entamoeba histolytica.

Vimelea hivi huingia moja kwa moja kwenye mwili wa binadamu kwa kupitia mdomoni na kuenda moja kwa moja kwenye njia ya mfumo wa mmeng'enyo wa chakula mpaka kufika kwenye utumbo mkubwa.

DALILI ZA UGONJWA WA AMIBA NI PAMOJA NA;

- Mgonjwa kujisaidia kinyesi chenye vitu kama makamasi

- Mgonjwa kuanza kupata maumivu ya tumbo sana mithili ya tumbo kusokota

- Mgonjwa kuanza kujisaidia choo kilaini sana

- Mgonjwa kuharisha au kujisaidia haja kubwa ya maji maji sanaa

- Mgonjwa kujisaidia kinyesi ambacho kimechanganyika na damu

- Mgonjwa kutoa hewa kwa njia ya haja kubwa mara kwa mara(kujamba)

- Mgonjwa kupata maumivu ya tumbo,Kifua na viungo mbali mbali vya mwili

- Joto la mwili la mgonjwa kupanda au mgonjwa kuwa na Homa

- Mgonjwa kupatwa na tatizo la kupungukiwa na damu 

- Kupoteza appetite ya chakula kabsa

- Mgonjwa kupatwa na hali ya kichefu chefu pamoja na kutapika

- Mgonjwa kupungua uzito wa mwili na kukonda

KUMBUKA; Moja ya njia ya mtu kupata vimelea hivi vya amoeba ambavyo husababisha ugonjwa huu wa amiba ni pamoja na kunywa maji machafu sana.

Maji ambayo yamechanganyika ma kinyesi cha mtu ambaye alikuwa na vimelea hivi vya amoeba.

MATIBABU YA UGONJWA WA AMIBA

Zipo dawa mbali mbali ambazo hutumika kutibu ugonjwa huu wa amiba

Conclusion(Hitimisho):

Ugonjwa wa amoeba ni ugonjwa hatari unaosababishwa na kimelea kinachoitwa Entamoeba histolytica. Kimelea hiki kinaishi kwenye Utumbo wa binadamu na kinaweza kusababisha matatizo makubwa ya kiafya.

Ni muhimu kufuata kanuni zote za usafi wa mazingira na kula chakula kilichoandaliwa vizuri ili kuzuia ugonjwa huu. Kama unapata dalili za ugonjwa wa amoeba, ni muhimu kuwahi Hospital ili kupata matibabu sahihi.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Ugonjwa wa Gambiense Sleeping Sickness,African Trypanosomiasis,chanzo,dalili na Tiba yakeAfyaclass Bongo Social •

Ugonjwa wa Gambiense Sleeping Sickness,African Trypanosomiasis,chanzo,dalili na Tiba yake

Ugonjwa huu hujulikana kama African Trypanosomiasis au kwa Jina lingine “sleeping sickness”

Jina la African Trypanosomiasis ni kwa sababu ya Ugonjwa huu kuwepo Afrika Hasa sub-Saharan Africa,

CHANZO CHA UGONJWA HUU NI NINI?

Ugonjwa huu husababishwa na parasites wadogo sana kutoka kwenye jamii ya Trypanosoma brucei,

Kisha kusambazwa na tsetse fly (Glossina species),

Wanyama wa kufugwa na wanyama wa msituni huweza kuhifadhi Parasite hawa, wanyama hao ni kama Nguruwe, Mbwa,mbuzi, n.k

Na pia Binadamu anaweza kuwa Main reservoir wa Infection hii.

Kuna Species mbili za Trypanosoma brucei;

(1)Trypanosoma brucei-gambiense

(2) Trypanosoma brucei-rhodesiense

T. b. gambiense wanasababisha African trypanosomiasis hasa kwenye eneo la western na central Africa wakati T. b. rhodesiense husababisha African trypanosomiasis hasa hasa kwenye eneo la eastern na southern Africa.

DALILI ZA UGONJWA HUU WA SLEEPING SICKNESS

Ugonjwa huu umepewa jina la Sleeping sickness kwa Sababu Dalili zake huweza kujumuisha matatizo ya Usingizi,

- Baada ya Mtu kung'atwa na tsetse fly anaweza kupata maumivu kisha kuwa na kidonda chekundu(red sore) ambacho huitwa chancre.

- Mtu kupata homa

- Mtu kupata maumivu makali ya Kichwa

- Mwili kutokutulia(irritability)

- Mtu kupata uchovu usio wa kawaida

- Mara nyingi Mtu wenye Ugonjwa huu wa Sleeping sickness hupata maumivu ya Misuli Pamoja na Joints

- Baadhi ya watu hupata vipele kwenye ngozi au Skin rashes

- Mtu kuwa kama amechanganyikiwa

- Wagonjwa wachache huweza Kuvimba Uso

- Na kama mgonjwa hajapata Tiba maambukizi haya huweza kuwa makali zaidi na kusababisha Kifo

MATIBABU YA UGONJWA HUU WA SLEEPING SICKNESS

Matibabu ya Ugonjwa huu hutegemea na aina ya maambukizi(T. b. gambiense au T. b. rhodesiense) pamoja na hatua ya Ugonjwa ulipofikia.

Dawa kama Pentamidine,suramin, melarsoprol, eflornithine, nifurtimox huweza kutumika.

0 Comment

Ugonjwa wa kuota Nyama,Plexiform neurofibroma ni Ugonjwa wa Aina gani? Soma hapaAfyaclass Bongo Social •

 Ugonjwa wa kuota Nyama,Plexiform neurofibroma ni Ugonjwa wa Aina gani? Soma hapa

Plexiform neurofibromas ni aina ya Uvimbe ambao huota pembezoni mwa Neva, Na hii ndyo chanzo cha Jina Lake,

-"neuro" maana yake nerves, na "fibroma" ni aina ya Uvimbe(tumor).

Aina hii ya Uvimbe ambao hukua, huwa na Nerve tissue pamoja na aina mbali mbali nyingi za Seli ndani yake,

Na aina hii ya Uvimbe au Nyama huweza kutokea ndani ya Mwili au chini tu kwenye ngozi yako.

Plexiform neurofibromas ni aina ya benign tumors tu lakini wakati mwingine huweza kugeuka na kuwa Saratani/cancer,

Na wakati tumors hizi zikiwa Saratani hujulikana kama malignant peripheral nerve sheath tumors (MPNST).

UVIMBE HUU AU NYAMA HIZI HUWEZA KUOTA MAENEO YAPI?

Nyama hizi huweza kuota maeneo mbali mbali kama vile;

- Usoni, na mara nyingi huanzia kuzunguka eneo la macho

- Shingoni

- Kwenye Miguu na Mikono

- Maeneo ya Mgongoni na Kifuani

- Maeneo ya tumboni N.k

KUMBUKA; Tatizo la Kuota nyama au Plexiform neurofibromas huweza kuondolewa kwa Njia mbali mbali ikiwemo Upasuaji,

ila wakati mwingine nyama hizi huweza kurudi kuwa normal tissues kadri zinavyokuwa, hali ambayo huweza kupelekea kuwa vigumu hata kufanya Upasuaji.

0 Comment

Ugonjwa wa Sinonasal carcinoma,Chanzo,dalili,TibaAfyaclass Bongo Social •

Ugonjwa wa Sinonasal carcinoma,Chanzo,dalili,Tiba

Hii ni aina ya Saratani adimu kutokea na huathiri zaidi eneo la puani-nasal cavity au paranasal sinuses,

Aina hii ya Saratani(Kansa) huweza kumpata Mtu yoyote, kwenye eneo Lolote duniani,bila kujali jinsia yake wala umri wake,

Japo Inaonekana kuna uwezekano mkubwa kwa wanaume kuliko wanawake kupata ugonjwa huu.

DALILI ZA SINONASAL CARCINOMA

Dalili za Mwanzoni kabsa za Saratani hii ni Pamoja na;

- Mtu kutoa damu puani

- Mtu kupata maumivu ya Uso,

- Uso kuwa na ganzi,kuchoma choma n.k

- Pua kuvimba,maarufu kama Runny Nose

- Kuona marue rue,

- Kupata maumivu ya kichwa

- Kuwa na tatizo la Pua kuziba(Nasal obstruction)

- Uwepo wa Vivimbe(tumors) n.k

Vivimbe hivi kwa kawaida hutambuliwa kwa kutumia kipimo cha MRI au CT Scan ya ubongo na paranasal sinuses.

CHANZO CHA TATIZO HILI,

Hakuna Sababu ya Moja kwa moja ambayo inajulikana kama chanzo halisi cha tatizo hili, ila zipo baadhi ya Sababu zimeonekana kuwa na uhusiano wa karibu na tatizo hili,na Sababu hizo ni kama vile;

• Uvutaji wa sigara

• Mtu kuwa kwenye mazingira yenye Carcinogens,kama vile kwenye machimbo ya madini,

migodi ya makaa ya mawe na viwanda vya plating vya chrome,

wafanyakazi wa kusafisha nikeli n.k

Japo pia utafiti uliofanyika nchini Canada kwenye kiwanda Kimoja cha NIKELI,ulionyesha hata ambao sio wafanyakazi kwenye eneo la kusafishia Nikeli bado waliumwa na aina hii ya Saratani, Hivo bado chanzo halisi hakijulikani ni nini.

MATIBABU YA TATIZO HILI NI YAPI?

Zipo tiba mbali mbali kulingana na hatua ya Ugonjwa,Pamoja na Hali ya Mgonjwa,ikiwemo;

✓ Huduma ya UPASUAJI

✓ Huduma ya Mionzi(radiotherapy)

✓ Huduma ya chemotherapy kwa baadhi ya Cases n.k

#Saratani:MAGONJWA

#VIa:Afyaclass

0 Comment

Dalili za Ugonjwa wa lassa FeverAfyaclass Bongo Social •

Dalili za Ugonjwa wa lassa Fever

Dalili za Ugonjwa wa lassa Fever,Ugonjwa ambao unatokea Sana maeneo ya Afrika Magharibi

Ugonjwa huu hutokana na maambukizi ya virusi  ambayo huambatana na homa kali, unaotokea hasa Afrika Magharibi. Kawaida hupatikana kutoka kwa panya walioambukizwa.

UGONJWA WA LASSA FEVER,CHANZO,DALILI NA TIBA

Ugonjwa huu wa lassa Fever ni ugonjwa ambao husababishwa na Virusi au ni Viral haemorrhaigeic fever,

ambapo mwanzoni kabsa huweza kusambazwa kwa njia ya chakula,kinyesi au mkojo kutoka kwa panya maarufu kama Mastomy's Rats,

Lakini pia unaweza kuupata kutoka kwa mgonjwa kwa njia ya damu,maji maji ya mgonjwa n.k

Ugonjwa wa Lassa Fever umeathiri sana maeneo ya Afrika ya Magharibi(Western africa),

Hasa maeneo ya Sierra Leone,Guinea,Liberia na Nigeria.

DALILI ZA UGONJWA WA LASSA FEVER NI PAMOJA NA;

- Mtu kupata homa kali

- Maumivu makali ya kichwa

- Mwili kuchoka kupita kawaida

- Kupata vidonda kooni yaani Sore throat

- Maumivu makali ya misuli,mifupa,joint,kiuno n.k

- Kuhisi kichefuchefu na kutapika

- Mgonjwa kuharisha

- Mgonjwa kukohoa sana

- Mgonjwa kupata maumivu makali ya tumbo n.k

MATIBABU YA UGONJWA WA LASSA FEVER

Dawa ambayo ipo kwenye kundi la Antiviral Drug ijulikanayo kama RIBAVIRIN imeonyesha matokeo mazuri ugonjwa ukiwa kwenye stage za mwanzoni.

fanya vipimo na kuanza tiba mapema kama una dalili kama hizi

KWA USHAURI ZADI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

#Ugonjwa:Lassa fever

#Afrika Magharibi

0 Comment

Chanzo cha UGONJWA WA MAFUA YA AVIAN,Dalili na TibaAfyaclass Bongo Social •

Chanzo cha UGONJWA WA MAFUA YA AVIAN,Dalili na Tiba

Ugonjwa wa mafua ya avian ni ugonjwa wa mafua ambao husababishwa na virusi ambao hupatikana kwa ndege(Avian) na kwa kitaalam hujulikana kama Avian flu au Avian influenza.

Ugonjwa huu kwa asilimia kubwa hushambulia jamii ya ndege,kuku n.k japo kuna case chache pia ziliripotiwa kwamba ugonjwa huu huweza kushambulia hata binadamu pia.

DALILI ZA UGONJWA WA MAFUA YA AVIAN KWA BINADAMU

- Mgonjwa kupatwa na mafua makali

- Mgonjwa kupatwa na maumivu makali ya tumbo

- Mgonjwa kuvimba macho pamoja na macho kuwasha

- Joto la mwili la mgonjwa kuwa juu au mgonjwa kuwa na homa

- Mgonjwa kupata kikohozi

- Mgonjwa kupata maumivu ya misuli,viungo pamoja na joints

- Mgonjwa kuhisi kichefuchefu pamoja na kutapika

- Mgonjwa kukosa hamu ya kula pamoja na ladha ya chakula kupotea

- Mgonjwa kuanza kuharisha

- Mgonjwa kupata shida ya upumuaji

- Mgonjwa kukosa pumnzi ya kutosha

- Mwili wa mgonjwa kutetemeka au kutingishwa hali ambayo kwa kitaalam hujulikana kama fits au seizures.

- Mgonjwa kupata maumivu makali ya kichwa

- Mgonjwa kupatwa na hali ya kizunguzungu

N.k

MATIBABU YA UGONJWA WA MAFUA YA AVIAN

Kama ilivyo kwa matibabu ya magonjwa mengine mengi ambayo husababishwa na virusi, tiba huwa katika kudhibiti dalili za ugonjwa kama vile; mgonjwa kupewa dawa za kutuliza mafua,maumivu n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Ugonjwa wa Surua kwa Watoto: Sababu, Dalili, Matibabu na KingaAfyaclass Bongo Social •

Ugonjwa wa Surua kwa Watoto: Sababu, Dalili, Matibabu na Kinga

Ugonjwa wa Surua ni ugonjwa wa kuambukiza sana kwa watoto wadogo, na ni sababu kubwa ya vifo miongoni mwa watoto wachanga.

Ugonjwa huu husababishwa na virusi wa Surua wanaojulikana kama Paramyxovirus na hushambulia mfumo wa kinga ya mwili wa mtoto.

Ni muhimu kujifunza kuhusu ugonjwa huu ili kuchukua hatua za kinga na kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.

Makala hii itaelezea sababu za ugonjwa wa surua kwa watoto, dalili, matibabu na kinga dhidi ya ugonjwa huo.

Sababu za Ugonjwa wa Surua kwa Watoto,

Sababu kuu ya ugonjwa wa Surua kwa watoto ni virusi vya Surua wanaojulikana kama Paramyxovirus,

  • Watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa virusi hivyo.
  • Watoto walio na mfumo dhaifu wa kinga, kutokana na sababu kama upungufu wa lishe, magonjwa mengine au kukosa chanjo, wako katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa Surua.

Dalili za Ugonjwa wa Surua kwa Watoto

Dalili za ugonjwa wa Surua kwa watoto ni pamoja na:

  1. Homa
  2. Kikohozi
  3. hali ya kuziba kooni
  4. Kupiga chafya
  5. Jicho kutoa machozi
  6. Kuharisha
  7. Mafua
  8. Viashiria vya upele kuanza kutokea kwenye uso na kusambaa kwenye mwili mzima

Matibabu ya Ugonjwa wa Surua kwa Watoto,

Hakuna matibabu maalum ya ugonjwa wa Surua, lakini dalili zake zinaweza kutibiwa.

Watoto wanaopata ugonjwa wa Surua wanapaswa kupumzika na kunywa vinywaji vingi ikiwemo maji.

Dawa za kupunguza homa, kama vile Paracetamol, zinaweza kutumika kupunguza homa.

Ni muhimu pia kuzuia maambukizi ya bakteria kwa kutumia dawa za kupambana na maambukizi, kama vile antibiotics, ikiwa inahitajika.

Kinga dhidi ya Ugonjwa wa Surua

kwa Watoto, Chanjo ya Surua ni njia bora ya kinga dhidi ya ugonjwa huu.

Chanjo ya Surua inashauriwa kwa watoto wote wenye umri wa kuanzia miezi 9. Chanjo ya Surua ni ya kudumu, na inashauriwa kwa watoto wote ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu.

Watoto walio na umri wa chini ya miezi 9 hawapati chanjo, lakini wanapaswa kulindwa kwa kuhakikisha kuwa watu wote wanaowazunguka wamepata chanjo.

Faida za Chanjo ya Surua,

Chanjo ya Surua inaweza kuokoa maisha ya watoto wengi.

Inapendekezwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kama njia bora ya kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa Surua.

Watoto wanaopata chanjo ya Surua wana kinga dhidi ya ugonjwa huu na hawataambukizwa virusi vya Surua.

Vigezo vya Kupata Chanjo ya Surua

- Watoto wote wanapaswa kupata chanjo ya Surua wakati wa miezi 9.

-Watoto wanaozaliwa na mama ambao wamepata chanjo ya Surua au wamepata ugonjwa wa Surua hapo awali hawapaswi kupata chanjo.

- Watoto wanaosumbuliwa na magonjwa mengine wakati wa kupata chanjo wanapaswa kuahirisha kupata chanjo mpaka wawe wamepona kabisa.

FAQs:

Hitimisho

Ugonjwa wa Surua ni hatari kwa watoto wadogo, lakini unaweza kuepukwa kwa kuchukua hatua za kinga kama vile kupata chanjo ya Surua,

Kwa kuzingatia kanuni za usafi na kuweka mazingira safi, tuna uwezo wa kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu.

Ni muhimu kuwa na ufahamu juu ya ugonjwa wa Surua, kuhakikisha kuwa watoto wetu wamepata chanjo ya Surua na kuchukua hatua za kinga ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu.

Ugonjwa wa surua kwa watoto

Ugonjwa huu huhusisha Mfumo wa hewa na husababishwa na virusi aina ya Paramyxovirus na pia uenezwaji wa virusi hawa ni kwa njia ya mtu kupumua, kupiga chafya, kukohoa au wakati mwingine mtu akiongea.

Licha ya chanjo ambazo watoto hupewa kliniki lakini bado Ugonjwa huu wa Surua huendelea kusababisha Vifo kwa watoto wengi wenye umri wa chini ya Miaka 5.

FAHAMU KWAMBA:Licha ya kwamba viwango vya Vifo kutokana na Ugonjwa wa Surua vinapungua Duniani kote kadri watoto wengi wanavyopata chanjo ya Kuzuia ugonjwa huu wa Surua- measles vaccine,

Ugonjwa huu bado unasababisha Vifo vya Watu zaidi ya 200,000 kwa Mwaka,wengi wao wakiwa Watoto.

DALILI ZA UGONJWA WA SURUA NI ZIPI?;

Dalili za ugonjwa wa Surua huweza kuchukua Muda wa Siku 10 mpaka 14 kuanza kuonekana toka kushambuliwa na Virusi hawa, Na dalili hizo ni Pamoja na;

  •  Kuwa na mapele katika sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo Usoni
  •  Mgojwa kupatwa na hali ya kukohoa
  • Mgonjwa Kupatwa na mafua mepesi
  •  Joto la mwili la Mgonjwa kupanda
  •  Mgonjwa kubadilika rangi ya macho na kuwa mekundu  n.k

VITU HIVI HUONGEZA HATARI YA WEWE KUPATA SURUA

- Kutopata chanjo ya Kuzuia Ugonjwa wa Surua

- Kusafiri maeneo ambapo ugonjwa wa Surua upo kwa kiwango kikubwa

- Kuwa na Upungufu mkubwa wa Vitamin A.

MADHARA YA UGONJWA WA SURUA NI PAMOJA NA;

  1. Mgonjwa kupatwa na tatizo la masikio
  2. Kuathiriwa utoaji wa sauti kwa Mgonjwa kwani ugonjwa huu huhusisha mfumo mzima wa hewa
  3. Athari katika ubongo wa binadamu
  4. Kuchangia tatizo la Pneumonia au Homa ya mapafu
  5. Kuchangia kuwepo kwa matatizo ya moyo
  6. Huathiri utengenezaji wa seli za Damu

MATIBABU YA UGONJWA WA SURUA

Hakuna tiba au dawa ya moja kwa moja mpaka sasa kwa ajili ya kutibu surua, Japo mgonjwa atashauriwa kupata mda wa kutosha kupumzika,kupata hewa ya kutosha na kunywa maji kwa kiasi kikubwa.

Hivo basi matibabu ya surua yataangalia sana dalili za Mgonjwa na singinevyo.

Hitimisho(Conclusion):

Hakikisha Mtoto wako anapata chanjo ya Surua ili kumkinga na Ugonjwa huu hatari wa SURUA.

0 Comment

Dalili za Ugonjwa wa Kaswende kwa MwanaumeAfyaclass Bongo Social •

Dalili za Ugonjwa wa Kaswende kwa Mwanaume: Jinsi ya Kujikinga na Kupata Matibabu

Ugonjwa wa kaswende ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na bakteria aina ya Treponema pallidum.

Ugonjwa huu unaweza kuambukizwa kupitia ngono, kugusana na vidonda vya mtu aliyeathirika, au kupitia damu.

Kwa wanaume, dalili za ugonjwa wa kaswende zinaweza kuwa tofauti na za wanawake. Katika makala haya, tutazungumzia dalili za ugonjwa wa kaswende kwa mwanaume na jinsi ya kujikinga na ugonjwa huu.

Dalili za Ugonjwa wa Kaswende kwa Mwanaume

1. Kujitokeza Kwa Vidonda au Michubuko kwenye sehemu za siri,
Mwanaume anaweza kuwa na vidonda au michubuko kwenye uume, korodani, au eneo la njia ya haja kubwa.

Vidonda hivi huweza kuonekana kama vipele vidogo, lakini huwa haviumi. Pia, vidonda hivi vinaweza kuambatana na maumivu ya tumbo na kuumwa na kichwa.

2. Kutokea Kwa Upele Mdogo kwenye Ngozi,

Kupata vipele vidogo au visivyotambulika kwa haraka kwenye ngozi ni dalili nyingine ya ugonjwa wa kaswende kwa mwanaume.

Upele huu huwa na ukubwa wa milimita chache na huwa hautambuliki kwa haraka sana.

3. Kutokwa Kwa Uchafu Mwepesi Kwenye Sehemu za Siri

Mwanaume anaweza kutokwa na uchafu mwepesi kwenye sehemu za siri. Uchafu huu huwa wa rangi nyeupe au kijivu na huwa na harufu kali.

4. Maumivu ya Kichwa, Uchovu na Homa

Mwanaume anaweza kuwa na dalili kama maumivu ya kichwa, uchovu, na homa. Dalili hizi hutokea katika hatua ya kwanza ya ugonjwa wa kaswende.

5. Michubuko kwenye Sehemu za Siri

Mwanaume anaweza kuwa na michubuko kwenye sehemu za siri, hasa baada ya kukojoa. Michubuko hii huweza kuambatana na maumivu.

6. Kufa Ganzi Kwenye Maeneo ya Mwili

Mwanaume anaweza kupata ganzi kwenye maeneo mbali mbali ya mwili

7. Kuvimba Kwa Tezi za Lymph

Mwanaume anaweza kuvimba tezi za lymph kwenye eneo la paji la uso, shingoni, au sehemu nyingine za mwili. Hii ni dalili ya hatua ya mwanzo ya ugonjwa wa kaswende.

Jinsi ya Kujikinga na Ugonjwa wa Kaswende kwa Mwanaume

- Tumia Kinga au Condom

Njia bora ya kujikinga na ugonjwa wa kaswende ni kwa kutumia kinga kila unapofanya ngono. Kinga zinaweza kujumuisha kondomu za kiume au kondomu ya kike.

- Kufanya Uchunguzi Mara kwa mara

Ni muhimu kufanya uchunguzi wa mara kwa mara ili kugundua ugonjwa wa kaswende mapema. Unaweza kufanya uchunguzi huu kwa kuchukua sampuli ya damu au kutumia kipimo cha haraka.

- Kuepuka Ngono Zisizo Salama

Epuka ngono zisizo salama na watu usiowafahamu. Hii inaweza kusaidia kupunguza hatari ya kuambukizwa ugonjwa wa kaswende.

- Kutumia Dawa kama Kinga

Ikiwa una hatari ya kuambukizwa ugonjwa wa kaswende, unaweza kutumia dawa za kinga kama vile antibiotic ya Penicillin.

Matibabu ya Ugonjwa wa Kaswende kwa Mwanaume

Ikiwa umeambukizwa ugonjwa wa kaswende, unaweza kutibiwa kwa kutumia antibiotic ya Penicillin. Antibiotic hii hutumiwa kwa muda wa wiki mbili hadi nne kulingana na hatua ya ugonjwa.

FAQs

Je, Ugonjwa wa kaswende ni Ugonjwa gani?

Ugonjwa wa kaswende ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na bakteria aina ya Treponema pallidum.

HITIMISHO

Ugonjwa wa kaswende ni hatari na unaweza kusababisha madhara makubwa ikiwa hautatibiwa mapema. Kujikinga na ugonjwa huu ni rahisi kwa kutumia kinga kila unapofanya ngono, kufanya uchunguzi wa mara kwa mara, na kuepuka ngono zisizo salama.

Ikiwa umeshukiwa kuwa umeambukizwa ugonjwa wa kaswende, unapaswa kutafuta matibabu haraka ili kusaidia kuzuia madhara makubwa kwa afya yako na kwa afya ya watu wanaokuzunguka.

Ni muhimu pia kujua dalili za ugonjwa wa kaswende ili uweze kugundua ugonjwa mapema na kutibiwa haraka. Kumbuka, kinga ni bora kuliko tiba!

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Fahamu Virusi vinavyojificha ndani ya Utumbo wakoAfyaclass Bongo Social •

Fahamu Virusi vinavyojificha ndani ya Utumbo wako

Microbiome - ni makundi ya bakteria na aina nyingine ndogo ndogo ya vidudu ambavyo huishi katika matumbo yetu. Imebainika kuwa bakteria hao wana virusi ambavyo vipo ndani na nje yao - na vina faida kwao na kwetu sisi.

Kuna mabilioni, labda hata trilioni za virusi hivi, vinavyojulikana kama bacteriophages au kwa jina jingine phages, ndani ya mfumo wa usagaji chakula wa binadamu.

Breck Duerkop, mtaalamu wa bakteria katika Chuo Kikuu cha Colorado Anschutz, anasema watafiti wanaamini ikiwa madaktari wanaweza kuvipata virusi sahihi, vinaweza kuboresha afya ya binadamu.

"Kutakuwa na virusi vizuri na virusi vibaya," anasema Paul Bollyky, daktari wa magonjwa ya kuambukiza na mtafiti katika taasisi ya Stanford Medicine.

Lakini kwa sasa, bado haijabainika ni virusi vingapi hukaa kwenye tumbo. Vilevile, kuna virusi vingine bado havijatambulika. Sehemu kubwa ya utafiti wa sasa wa virusi ni kutambua virusi hivi na bakteria wanaoishi nao.

“Aina zao ni za kushangaza," anasema Colin Hill, mwanabiolojia katika Chuo Kikuu cha Cork huko Ireland. Wanasayansi hupata virusi kutoka katika sampuli za kinyesi cha binadamu.

Virusi hutofautiana sana kutoka kwa mtu mmoja hadi mtu mwingine. Pia hubadilika kulingana na umri, jinsia, chakula na mtindo wa maisha, kama Hill na wafanyakazi wenzake walivyoeleza katika utafiti wa mwaka 2023.

Ingawa virusi huambukiza bakteria na wakati mwingine huwaua, uhusiano wa bakteria na virusi bado ni mgumu kuuelewa.

"Tulikuwa tukifikiri kwamba virusi na bakteria wanapigana," anasema Hill, "lakini sasa tunajua kwamba wanaishi pamoja na ni washirika."

Manufaa ya virusi

Fahamu kwamba; Kila mmoja wetu ana virusi vya kipekee vinavyoingiliana kila mara na bakteria wa utumbo

Virusi vinaweza kutoa manufaa kwa bakteria kwa kuleta jeni mpya. Wakati chembe za virusi zinapokusanyika ndani ya bakteria, kirusi huyo anaweza kuingiza jeni za bakteria kwenye ganda lake la protini pamoja na jeni zake mwenyewe.

“Baadaye, huzifanya jeni hizo kuwa jeni mpya, ni jeni zilizohamishwa kwa bahati mbaya na zinaweza kusaidia,” anasema Duerkop.

Virusi huwaweka bakteria katika hali nzuri, anasema Hill. Bakteria wanaweza kuwa na hadi aina kumi na mbili za kinga. Kinga tofauti zina faida tofauti; kuepuka mfumo wa kinga mwili au kukaa kona tofauti ya mfumo wa utumbo.

Hill anasema, bakeria lazima kila wakati wabadilishe kinga zao ili kukwepa virusi vinavyotambua kinga moja tu. Matokeo yake, wanakuwa na uwezo wa kushughulikia changamoto mpya.

Virusi pia huzuia idadi ya bakteria wasizidi kupita kiasi. Utumbo ni mfumo wa ikolojia, kama misitu, na virusi ni wawindaji wa bakteria, kama mbwa mwitu na wawindaji wengine.

Utumbo unahitaji virusi kama vile msitu unavyohitaji mbwa mwitu. Wakati mahusiano hayo yanapobadilika, ugonjwa unaweza kutokea.

Watafiti wameona mabadiliko ya virusi kwa watu wenye ugonjwa wa matumbo (IBS), kama ugonjwa wa kuharisha na saratani ya utumbo mkubwa - mfumo wa ikolojia wa mtu aliye na shida hizo mara nyingi huwa tofauti.

Hill anasema, wanasayansi wanatafuta virusi ambavyo vinaweza kutumiwa kimatibabu dhidi ya bakteria wanaosababisha vidonda vya tumbo.

“Nadhani, tunapaswa kushukuru kwa matrilioni ya virusi vinavyosimamia mfumo wa ikolojia ya utumbo. Bila wao, aina fulani ya bakteria zinaweza kutawala haraka - na uwezekano wa kushindwa kusaga baadhi ya vyakula na kukabiliwa na gesi, hutokea,” anasema Hill.

0 Comment

Uhusiano wa Usugu wa dawa na magonjwa ya figo,Prof. Jeremiah aelezaAfyaclass Bongo Social •

Uhusiano wa Usugu wa dawa na magonjwa ya figo,Prof. Jeremiah aeleza

#Picha:Prof. Jeremiah Seni, Profesa Mshiriki wa Vimelea vya Magonjwa katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Sayansi za Afya Bugando, Mwanza Tanzania.

Viongozi wa Umoja wa Mataifa wakutana jijini New York, Marekani kujadili hatua za kudhibiti hatari itokanayo na usugu wa vimelea dhidi ya dawa, UVIDA au kwa kiingereza AMR, nchini Tanzania mtaalamu wa suala hilo amedadavua uhusiano kati ya usugu wa dawa na magonjwa kama vile figo na maambukizi katika njia ya mkojo, UTI.

Katika mahojiano na Jeremiah Seni, Profesa Mshiriki wa Vimelea vya Magonjwa katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Sayansi za Afya Bugando, Bosco Cosmas wa Idhaa ya  Umoja wa Mataifa alimuuliza hasa chanzo na madhara ya usugu wa dawa hizo.

Usugu dhidi ya vimelea vya magonjwa ni hali ambayo vimelea wanaosababisha magonjwa mbalimbali, wanafanya mabadiliko na hivyo kukinzana na dawa ambazo awali zilikuwa zinatumika kuwatibu, na vimelea hawa tunawagawa katika makundi Matano ambayo tuna bakteria, virusi, fangasi, minyoo na jamii zingine za parasaiti kama wale wanaosababisha malaria.

UTI isipotibika inaposababisha magonjwa ya figo

Ingawa watu wengi wameishi na tatizo hili la usugu bila kufahamu, lakini athari zake ziko wazi kwa afya ya umma, nikamuuliza Prof. Seni kuwa usugu unawezaje kuathiri afya ya umma? Profesa Seni akachambua zaidi akisema, “tukiachana na haya magonjwa ambayo serikali yamejiwekea mpango mkakati wa kupambana nayo kama UKIMWI, kifua kikuu na malaria mgonjwa anapopata maambukizi maana yake ule ugonjwa utakaa muda mrefu zaidi kwa hiyo inawezekana mtu alikuja na maambukizi tu kwenye njia ya mkojo (UTI) ni kawaida lakini kama ana usugu maana yake anaweza akachelewa kupona na pia kusababisha mgonjwa kupoteza maisha na kuongezeka kwa gharama za matibabu.”

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, UVIDA husababisha vifo vya watu 700,000 kwa mwaka, lakini wanatabiri kuwa hadi ifikapo mwaka 2030, linaweza kusababisha vifo vya takribani watu milioni 10. Nikamuuliza nini kifanyike tatizo hili lisiwe na madhara zaidi kwa watu ulimwenguni?

Ukiangalia takwimu ni kweli kabisa mwaka 2014 utafiti mkubwa kabisa uliosimamiwa na Shirika la Afya Ulimwenguni ambao uliangalia zaidi vifo vinavyotokana na UVIDA na walifanya makisio ya wale watu takribani 700,000 wamepoteza maisha kutokana na UVIDA na mbaya zaidi robo tatu ya vifo hivyo ni kutoka bara la Afrika na Kusini mashariki mwa bara la Asia kwahia vifo hivyo ni kutoka bara la Afrika na Kusini mashariki mwa bara la Asia kwahiyo ni vyema  kwa serikali kuona ukubwa wa tatizo hili na kuwekea mkazo katika mapambano kama walivyoweka kwa magonjwa mengine makubwa.”

Wafamasia wanachukua hatua gani kudhibiti UVIDA?

Moja kati ya sehemu muhimu ambayo inaweza kusaidia kupunguza ama kumaliza tatizo hili ni katika maduka ya dawa ambapo mara nyingi wagonjwa huwa wanaenda kununua dawa bila kufuata taratibu za vipimo. Clinius Amani Caroly, Mteknolojia dawa katika hospitali ya Mwananchi iliyopo mkoani Mwanza, anaeleza hatua wanazochukua katika utoaji wad awa kwa mgonjwa.

Sasa kwa utoaji wa dawa kwa mgonjwa ambaye hana karatasi ya daktari, kuna makundi mawili, kwanza kwa kitaalamu kuna kitu kinaitwa over the counter medicine, ambazo ni dawa zinazoweza kutolewa kwa mgonjwa bila karatasi ya daktari lakini pia kuna prescription medicine ambazo mgonjwa akija bila karatasi ya daktari hatuwezi kumpatia. Mgonjwa anapokuja bila karatasi ya daktari kwanza tunajiridhisha kama kweli dawa anayotaka inaendana na ugonjwa wake na tunawapa ushauri wa Kwenda kumuone daktari.

Muathirika wa UVIDA na hatua alizochukua sasa

Je, wahanga wana uelewa kuhusu namna sahihi ya kukabiliana na usugu? Neema Gervas, muhanga wa tatizo hili anaeleza nini anafanya anapogundua amepata usugu.

“Kwa upande wangu suala la usugu wa dawa limenitesa kwa muda mrefu sana kwasababu hapo awali  nilikuwa natumia hizi dawa za kutuliza maumivu hasa ninapohisi maumivu ya kichwa lakini kwa sasa nikitumia haisaidii kupata unafuu. Nilienda phamasi nikawaambia dawa ambazo huwa ninatumia hazinisaidii kwahiyo wananishauri kubadilisha daw ana nikawa napata nafuu.” Via;UN

0 Comment

Ugonjwa wa CHLAMYDIA,chanzo,dalili na Tiba yakeAfyaclass Bongo Social •

Ugonjwa wa CHLAMYDIA,chanzo,dalili na Tiba yake

Chlamydia ni ugonjwa unaowapata watu wengi na unaenezwa kwa ngono,Hivo chlamydia ni miongoni mwa magonjwa ya Zinaa. Ni ugonjwa unaoshambulia jinsia zote na mara nyingi hauonyeshi dalili zozote. Dalili zikionekana, ni baada ya wiki kadhaa kutoka siku ya mambukizi.

#SOMA hapa Lists Mpya ya Magonjwa ya Zinaa kwa Sasa

Chanzo cha Ugonjwa wa Chlamydia

Chlamydia husababishwa na kuenezwa na bakteria aitwaye Chlamydia trachomatis. Bakteria huyu hupatikana kwenye shingo ya kizazi (cervix), mrija wa mkojo, uke na/au sehem ya haja kubwa.. Bakteria pia huishi ndani ya koo. Namna yo yote ya kujamiiana inaweza kumweneza bakteria huyu.

Bakteria wa Chlamydia trachomatis mara nyingi huenezwa kupitia kufanya mapenzi kwa njia ya uke, mdomo na haja kubwa(vaginal, oral and anal sex),

Pia inawezekana, kwa bakteria hawa kuenea kipindi cha ujauzito, wakati wa kuzaa mtoto n.k. Ugonjwa wa chlamydia unaweza kusababisha nimonia au maambukizi makubwa ya macho kwa mtoto mchanga.

Vitu ambavyo huongeza hatari ya kupata Ugonjwa wa Chlamydia

Tafiti zinaonyesha:Watu ambao huanza kufanya mapenzi kabla ya umri wa miaka 25 wapo kwenye hatari kubwa Zaidi ya kupata ugonjwa wa chlamydia kuliko wenye umri mkubwa Zaidi.

Vitu hivi huongeza hatari Zaidi ya kupata Ugonjwa wa Chlamydia;

– Kutokutumia kinga kama Condomu wakati wa tendo

– Matumizi yasio sahihi ya Condomu wakati wa Tendo,

#Soma hapa Matumizi Sahihi ya Condomu

– Kuwa na mpenzi mpya ambaye hujui hali yake au kuwa na wapenzi wengi

– Kutokufanya vipimo mara kwa mara

– Kutokujikinga na magonjwa ya Zinaa au kutokutibu magonjwa ya Zinaa n.k

Dalili za Chlamydia;

Katika hatua za awali maambukizi ya Chlamydia trachomatis huweza kusababisha dalili chache Zaidi na ambazo sio kali, hali ambayo hufanya baadhi ya watu kutokugundua mapema kwamba tayari wana maambukizi haya.

Hii ndyo maana,kufanya screening mara kwa mara ni muhimu Zaidi ili kukuweka Salama mapema Zaidi.

Dalili za maambukizi ya Chlamydia trachomatis ni pamoja na:

  • Kupata maumivu wakati wa kukojoa
  • Kutokwa na Uchafu ukeni
  • Kutokwa na Uchafu kwenye Uume
  • Kupata maumivu ukeni wakati wa tendo
  • Kuvuja damu ukeni katikati ya mzunguko wa hedhi
  • Kuvuja damu ukeni baada ya tendo
  • Kupata maumivu ya Korodani n.k

DALILI ZA CHLAMYDIA

Dalili za chlamydia zinaweza kuwa:

. Maumivu ya sehemu ya chini ya tumbo

. Maumivu wakati wa kukojoa

. Maumivu wakati wa tendo la ndoa

. Maumivu ya nyonga

. Usaha au uchafu kutoka kwenye uume

. Kutoka damu kwenye mkundu

. Uchafu kutoka kwenye mkundu

. Maumivu kwenye mkundu

. Maumivu kwenye korodani

. Kukojoa mara kwa mara

. Uchafu kutoka ukeni

. Maumivu ukeni

. Kutokwa damu katikati ya hedhi na baada ya tendo la ndoa kwa wanawake

Madhara ya Ugonjwa wa Chlamydia(Complications)

Maambukizi ya Chlamydia trachomatis huweza kuhusishwa na:

• Kupata tatizo la maambukizi ya bacteria kwenye via vya uzazi vya Mwanamke yaani Pelvic inflammatory disease(PID).

• Kupata maambukizi karibu na Korodani.

Maambukizi ya klamidia yanaweza kuleta athari kwenye mirija iliyojikunja iliyo karibu na kila korodani, inayoitwa epididymis. Maambukizi haya yanaweza kusababisha homa, maumivu ya scrotal na uvimbe.

• Maambukizi kwenye Tezi Dume(Prostate gland infection).

Mara chache, bakteria wa chlamydia wanaweza kuenea kwenye tezi ya prostate na kusababisha tatizo la kuvimba kwa tezi hili yaani Prostatitis,Hii inaweza kusababisha maumivu wakati au baada ya kufanya Mapenzi, homa,kuhisi baridi, maumivu wakati wa kukojoa, na maumivu sehemu ya chini ya mgongo au maumivu ya kiuno.

• Maambukizi kwa Mtoto mchanga.

Maambukizi ya klamidia yanaweza kupita kutoka kwenye mfereji wa uke hadi kwa mtoto wako wakati wa kujifungua, na kusababisha nimonia au maambukizi makubwa ya macho.

• Tatizo la mimba kutunga nje ya kizazi(Ectopic pregnancy).

Hii hutokea wakati yai lililorutubishwa hupandikizwa na kukua nje ya uterasi, kwa kawaida kwenye mrija wa fallopian. Yai hili linahitaji kuondolewa ili kuzuia matatizo ya kutishia maisha, kama vile kupasuka kwa mrija wa fallopian n.k. Maambukizi ya chlamydia huongeza hatari hii.

• Tatizo la Mwanamke kushindwa kubeba mimba(Infertility).

Maambukizi ya Klamidia yanaweza kusababisha kovu na kuziba kwa mirija ya uzazi, jambo ambalo linaweza kusababisha utasa.

• Kupata tatizo la Reactive arthritis.

Watu wenye maambukizi ya Chlamydia trachomatis wapo kwenye hatari Zaidi ya kupata tatizo la reactive arthritis, au pia hujulikana kama Reiter syndrome.

Hii ni hali ambayo huathiri mifupa,macho au urethra — mrija unaosafirisha mkojo kutoka kwenye kibofu hadi nje ya mwili wako.

Hayo ndiyo baadhi ya madhara yanayotokana na Ugonjwa wa Chlamydia, Ikiwa una tatizo hili hakikisha unapata Tiba mapema au;

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Ugonjwa wa Asthma kwa Mama MjamzitoAfyaclass Bongo Social •

Ugonjwa wa Asthma kwa Mama Mjamzito

Jinsi ya Kudhibiti Ugonjwa wa Asthma ukiwa Mjamzito

Katika Makala hii tumechambua baadhi ya tips za Jinsi ya Kudhibiti tatizo la Asthma(Ugonjwa wa Asthma) ukiwa Mjamzito;

Jinsi mimba inavyoathiri mtu mwenye ugonjwa wa Asthma

Ikiwa una tatizo la asthma, ni vigumu kutabiri kama dalili za ugonjwa wa Asthma zitakuwa tofauti wakati wa ujauzito. Dalili zako zinaweza zikawa za kawaida, zikae sawa au kuwa mbaya zaidi.

Pia Watu wenye Ugonjwa wa Asthma wakati wa ujauzito huweza kukumbwa zaidi na tatizo la Acid reflux,

Tatizo ambalo huhusisha asidi ya tumbo kurudi juu kuelekea kooni – ukiwa mjamzito, jambo ambalo linaweza kufanya tatizo la Asthma kuwa baya zaidi.

Matibabu ya Ugonjwa wa Asthma kipindi cha Ujauzito

Usiache kutumia dawa zako za Asthma - zungumza na daktari, muuguzi,mkunga au mtaalamu wa afya kwanza.

Dawa nyingi za Ugonjwa wa Asthma ni salama kutumia wakati wa ujauzito na, ikiwa pumu(asthma) yako imedhibitiwa vyema, hakuna hatari yoyote kwako au kwa mtoto wako.

Unapaswa kuendelea na matibabu yako ya ugonjwa wa Asthma katika kipindi chote cha ujauzito. Matibabu yako yanaweza kubaki sawa kabisa na hapo awali, Isipokuwa tu pale Ugonjwa wa Asthma(pumu) unazidi kuwa mbaya zaidi kwako au kusababisha madhara kwa ujauzito wako.

Dalili zinaweza kuwa mbaya zaidi ikiwa utaacha kutumia dawa zako za Asthma. Hii inaweza kusababisha hatari kwa afya yako mwenyewe na kuongeza hatari ya mtoto wako kuwa na tatizo la uzito mdogo wakati wa kuzaliwa(Low-birth weight).

Matibabu ya Ugonjwa wa Asthma Wakati Unanyonyesha

Ni salama kuendelea na matibabu yoyote ya Ugonjwa wa Asthma wakati unanyonyesha. Hata unapokuwa na shughuli nyingi na mtoto wako mpya, ni muhimu kutopuuza afya yako mwenyewe na kudhibiti pumu(Asthma) yako kadri uwezavyo.

Jinsi ya Kudhibiti Ugonjwa wa Asthma Kwa Mjamzito

Kuna mambo unaweza kufanya ili kusaidia kudhibiti hali yako wakati wa ujauzito,

Zingatia mambo haya ikiwa wewe ni Mjamzito halafu una ugonjwa wa Asthma;

✓ Hakikisha unaendelea na matibabu yako ya Asthma kama kawaida baada ya kuongea na wataalam wa afya

✓ Tumia dawa yako ya preventer inhaler (steroids) unapopata kikohozi au mafua - zungumza na daktari kuhusu kutumia dawa kama hizi wakati wa ujauzito.

✓ Epuka kuvuta sigara - pata vidokezo kuhusu kuacha kuvuta sigara wakati wa ujauzito

✓ Epuka vitu vyote ambavyo huweza kuchochea tatizo la Allergies pamoja na athari zaidi za mzio(Allergies) kwako - kwa mfano,vumbi, baadhi ya perfumes,mafuta,sabuni za kuogea,baadhi ya vyakula n.k

✓ Kama una Homa, hakikisha unaidhibiti kwa kutumia dawa- zungumza na daktari,Mkunga au mfamasia kuhusu ni dawa zipi ni salama kumeza wakati wa ujauzito.

✓ Endelea na Mazoezi ambayo ni salama wakati wa Ujauzito

✓ Hakikisha unakula mlo kamili na salama(healthy diet) n.k

Ugonjwa wa Asthma wakati wa Kujifungua

Ni mara chache sana kupata zile dalili za Asthma wakati unajifungua(asthma attack during labour),

Na endapo hali hii ikajitokeza wakati wa kujifungua,ni salama kabsa kutumia dawa yako ya Inhaler kama kawaida.

Hakikisha unamwambia mkunga wako na wahudumu wa hospitali kuhusu vitu vyote ambavyo una Allergi navyo.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Ugonjwa Wa Asthma(Pumu),Chanzo,Dalili Na Tiba

UGONJWA WA ASTHMA(PUMU) NI NINI?

Pumu au kwa Kitaalam Asthma ni ugonjwa ambao hushambulia njia za hewa ndani ya mapafu, na kusababisha tishu ndani ya njia za hewa kuvimba.  

Ugonjwa wa Asthma au Pumu pia husababisha bendi za misuli kuzunguka njia za hewa kuwa nyembamba.  Hii inafanya kuwa ngumu kwa hewa ya kutosha kupita na kwa mtu kupumua kawaida,

Tatizo hili humfanya mtu apumue kwa shida au apate shida ya kupumua.

Ugonjwa wa Asthma pia husababisha seli za kutengeneza kamasi(mucus cells) ndani ya njia za hewa kutengeneza kamasi zaidi kuliko kawaida.  

Hali Hii inazuia njia za hewa, ambazo tayari ni nyembamba sana wakati wa shambulio la pumu au Asthma, na inafanya kuwa ngumu zaidi kupumua.

Mtu anayesumbuliwa na Ugonjwa wa Asthma mara nyingi hutoa sauti wakati anajaribu kupumua, sauti hii hujulikana kama wheezing Sound

Hii ni sauti ya hewa inayojaribu kupita kwenye njia nyembamba sana ya hewa. Pia Mtu mwenye Ugonjwa wa Asthma hupumua kwa shida, hupatwa na hali ya kubanwa na kifua, kukohoa sana.n.k

Mashambulizi ya Asthma au pumu yanaweza kuwa dharura ya kiafya kwa sababu yanaweza kusababisha kifo, 

Na kwa bahati mbaya mpaka sasa Hakuna tiba ya kuondoa kabsa Ugonjwa wa Asthma, ila Kuna matibabu kama aina tofauti za dawa kwa ajili ya kusaidia kudhibiti dalili kwa watu wenye Asthma au pumu.  

Pia kuna mambo ambayo watu walio na Ugonjwa wa Asthma wanaweza kufanya ili kusaidia hali isizidi kuwa mbaya.

CHANZO NA SABABU ZA KUPATA UGONJWA WA PUMU(ASTHMA)

 Kuna vitu hatarishi vinaweza kusababisha mtu kupata Ugonjwa wa Asthma lakini Sababu halisi au za moja kwa moja,mtu kupata Asthma au pumu hazijulikani bado. Baadhi ya sababu hatarishi za Mtu kupata Pumu au Ugonjwa wa Asthma ni pamoja na;

1.Sababu za kimaumbile;

Mtu hurithi mabadiliko ya maumbile kutoka kwa mzazi mmoja au wazazi wote wawili ambayo yanaweza kuongeza nafasi ya kupata Ugonjwa wa Asthma. 

Epigenetics, ambayo ni mabadiliko katika njia ya jeni, yanaweza pia kuongeza nafasi ya mtu kupata Ugonjwa wa Asthma.  

Mabadiliko haya ya epigenetic pia yanaweza kurithiwa

Hivo kwa Lugha rahisi,Ugonjwa wa Asthma ni miongoni mwa magonjwa ya kurithi.

Mabadiliko haya huweza kutokea wakati mtoto bado akiwa ndani ya tumbo la mama yake, au wakati wa utoto.

Mabadiliko ya Epigenetiki au marekebisho husababisha mabadiliko anuwai ambayo yanaathiri jinsi jeni za mtu zinavyofanya kazi au 'kujieleza' kwa njia tatu tofauti (zinazoitwa mifumo ya epigenetic), lakini haibadilishi jeni kwenye DNA. 

Mabadiliko haya ya epigenetic yanaweza kurithiwa, au yanaweza kutokea kwenye uterus ambayo ni wakati mtoto bado yuko ndani ya mama yake. 

Yanaweza pia kutokea utotoni, kwa sababu ya sababu tofauti, kama 

  • Maambukizi ya njia ya kupumua
  • kuambukizwa na kemikali au dawa za kulevya
  •  lishe n.k.

Mabadiliko haya yanaweza kupitishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine lakini sio ya kudumu na yanaweza kupitishwa kwa kizazi kimoja au  vizazi viwili.  


Ingawa mabadiliko ya epigenetic yanaathiri jinsi jeni za mtu zinavyofanya kazi hayabadilishi kabisa jeni za mtu.  

Inaaminika mabadiliko haya ya epigenetic ndyo yanayoweza kumfanya mtu kuwa kwenye hatari zaidi ya kupata magonjwa kama pumu au Asthma.

2. Hali ya Kiuchumi;

Hali ya uchumi wa jamii pia inaaminika kuchangia mtu kupata Ugonjwa wa Asthma.  

Hali ya uchumi wa mtu inategemea vitu kama vile pesa ambazo familia hupata,wapi anaishi, na kiwango chake cha elimu. 

 Pia inahusiana na upatikanaji wa huduma ya matibabu, imani za kibinafsi, na Swala la lishe yake ya kila siku.  

Tafiti zinaonyesha; Watu wa hali ya chini kiuchumi wanakabiliwa na viwango vya juu vya pumu(Asthma),pia wana viwango vya juu vya vifo vinavyohusiana na pumu kuliko watu wa hali ya juu ya uchumi.

3. Sababu za mazingira ni vitu vinavyoathiri mtu;

 Sababu mbaya za mazingira ni vitu kama kuishi katika eneo ambalo kuna uchafuzi mwingi wa hewa au kuwa karibu na moshi wa sigara.n.k,

Vyote hivi huweza kuongeza hatari ya mtu kupata Ugonjwa wa Asthma.

DALILI ZA UGONJWA WA ASTHMA AU PUMU

Ishara na dalili za mapema za Ugonjwa wa pumu (Asthma) zinaweza kujumuisha:

  1. Kukohoa sana, haswa usiku
  2. Kukosa hewa kwa urahisi
  3. Kubwa sana kifua
  4. Kupumua kwa shida,wakati huu mtu hawezi kuvuta pumzi ndefu ambayo inamaanisha kuwa hawezi kujaza mapafu kwa njia yote na hewa.  
  5. Kupata uchovu kwa urahisi wakati wa mazoezi na kuhisi dhaifu na kupumua au kukohoa baada ya mazoezi
  6. Kuhisi dalili za homa au mzio unaokuja kama kupiga chafya, kukohoa, na maumivu ya kichwa n.k

VIPIMO Kwa Ugonjwa wa Asthma

- Kusikika kwa sauti zisizo za kawaida kwenye mapafu zinazojulikana kama "high-pitched wheezing Sounds"  

Baada ya kusikiliza kwa kutumia kifaaa kinaitwa stethoscope.Hii husaidia sana katika kugundua ugonjwa huu pamoja na vipimo vingine.

- Kipimo cha Chest X-ray n.k

MATIBABU ya Ugonjwa wa Asthma

kama una dalili zozote za Ugonjwa wa asthma, hakikisha unapata vipimo sahihi na kuanza tiba sahihi kulingana na Chanzo cha Tatizo lako.

KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584

Karibu Sana..!!

0 Comment

Mgonjwa atolewa Ini badala ya bandama kisha kupoteza maishaAfyaclass Bongo Social •

Mgonjwa atolewa Ini badala ya bandama kisha kupoteza maisha

Serikali ya Jimbo la Florida huko Marekani imemfungia Leseni ya Udaktari na kuagiza kusimamishwa kazi Daktari aitwae Thomas Shaknovsky baada ya kutuhumiwa kutoa ini la Mgonjwa badala ya Bandama wakati wa upasuaji na kusababisha Mgonjwa huyo kuvuja Damu nyingi hadi kupelekea kifo chake.

Kupitia taarifa ya dharura iliyotolewa na Idara ya Afya ya Jimbo la Florida, imesema kuwa Dkt. Thomas Shaknovsky wa Hospitali ya Ascension Sacred Heart Emerald Coast iliyopo Miramar Beach, Florida aliondoa ini la Mkazi wa Alabama, Bill Bryan (70) badala ya bandama na kusababisha hatari kubwa kwa Mgonjwa huyo ambaye alifariki dunia baada ya upasuaji huo.

Imeelezwa kuwa Daktari huyo baada ya kutambua kosa lake alijaribu kuficha taarifa za upasuaji kwa kutengeneza rekodi za matibabu zenye kudanganya juu ya kile kilichotokea na kuwashinikiza Manesi waliokua wakimsaidia katika upasuaji huo kusema uwongo na sasa Familia ya Marehemu imefungulia kesi kwa kusababisha kifo kwa uzembe.

“Mume wangu alifariki akiwa hoi kwenye meza ya chumba cha upasuaji na Dkt. Shaknovsky, sitaki Mtu mwingine yeyote afe kutokana na uzembe wake katika Hospitali ambayo alipaswa kujua hapo awali alifanya makosa makubwa ya upasuaji” - amesema Mjane wa Marehemu.


0 Comment

Suluhu ya Janga la Usugu wa vimelea dhidi ya dawa duniani yatafutwaAfyaclass Bongo Social •

Suluhu ya Janga la Usugu wa vimelea dhidi ya dawa duniani yatafutwa

Usugu wa dawa hutokea pale ambapo vimelea vya magonjwa kama vile bakteria,virusi n.k vinapokuwa vimebadilika katika kipindi fulani na hivyo haviwezi tena kutibika kwa kutumia dawa zilizopo.

Viongozi wa dunia na wataalamu wa afya leo wamekusanyika kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani wakitafta suluhu ya janga la usugu wa vimelea dhidi ya dawa, UVIDA au AMR kwa lugha ya kiingereza, na hatimaye kupitisha azimio la kisiasa la kukabiliana na tishio hilo la kiafya linalozidi kukua kila uchao.

Akizungumza na waandishi wahabari wakati wa Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus, amegusia ukubwa wa suala hilo, akisema UVIDA au AMR husababisha vifo vya zaidi ya watu milioni 1 kila mwaka.

“Azimio hili ni ishara thabiti kutoka kwa nchi kwamba wameazimia kutatua kitisho hiki cha kimataifa,” amesema Dkt. Tedros akiongeza kuwa “leo hii UVIDA ni moja ya vitisho vikubwa zaidi vya afya duniani. UVIDA inaweza kurudisha nyuma kwa miaka 100 maendeleo ya kiafya yaliyopatikana duniani, kwa kufanya maambukizi yanayoweza kutibika haraka, kuwa chanzo kikubwa cha Vifo.

Lengo la azimio ni kupunguza vifo kwa asilimia 10 ifikapo 2030

Pia amesisitiza kuwa hakuna taifa lililo na kinga dhidi ya kitisho hicho, ijapokuwa nchi za kipato cha chini na kati zinabeba mzigo mkubwa zaidi.

Ameeleza kwamba lengo la azimio hilo ni kupunguza vifo vihusianavyo na UVIDA kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030.

“Kufikia lengo hilo la kwenye azimio, kunahitaji kuchukua hatua sio kwenye sekta ya afya ya binadamu pekee, bali pia sekta ya afya ya wanyama na mazingira,” ametanabaisha.

Dkt. Tedros amesema kwamba WHO pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa, lile la Afya na Chakula, FAO, afya ya Wanyama, WOAH, na lile la mazingira, UNEP yanashirikiana chini ya mpango mmoja wa AFYA MOJA ili kutatua suala hilo.

Wengi wetu hatumalizi dozi ya dawa - Mottley

Akizungumza kwenye mkutano huo na waandishi wa habari ni Waziri Mkuu wa Barbados, Mia Mottley ambaye ameelezea UVIDA kama  janga linalokua kimya kimya.

Ametaja matumizi holela au matumizi ya kupita kiasi ya dawa za kuua vimelea vya magonjwa kuwa kichochea kikubwa cha usugu.

Mottley amesema wengi wetu tunapata dawa za kuua vimelea vya magonjwa Tunatumia kwa siku chache. Hatumalizi dozi kama tulivyoelekezwa na daktari.

Amesema “lazima tubadili tabia hii katika ngazi ya mtu mmoja mmoja na hilo ndilo lengo la msingi kwanza kabisa, katika mkutano huu wa ngazi ya juu wa viongozi na azimio la kisiasa ili kuanza kuleta mabadiliko.”

“Hebu fikiria unapata maambukizi kwa kwenda bustanini au kujifungua mtoto au unapokwenda kwa daktari wa meno. Vitu hivi vinawea kumaliza maisha yako ndani ya saa 48 au 72 iwapo dawa mahsusi ya kuua vimelea vya magonjwa husika itashindwa kufanya kazi,” amesema Bi.Mottley.

UNEP, WOAH, FAO nao wazungumza

Kwa Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira, UNEP, usugu huo hatari wa vimelea dhidi ya dawa unaweza kusababisha vifo vya watu milioni 40 na watu wengine milioni 160 kufa kwa magonjwa yahusianayo na UVIDA kati yam waka 2025 na 2050 iwapo hatua haitachukuliwa.

Mkurugenzi wa WOAH, Emmanuelle Soubeyran amekaribisha azimio hilo la kisiasa linalotilia mkazo kinga, hasa kwenye afya ya Wanyama na matumizi ya chanjo. Amesema chanjo zinaweza kusadia kuzuia magonjwa ambayo yanaweza kusababisha matumizi ya dawa za kuua vimelea mbali mbali.

Naye Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa FAO, Thanawat Tiensin, ametaka kuweko kwa hatua za pamoja ili kupunguza matumizi ya dawa za kuua vimelea kwenye sekta ya kilimo. “Na tunatarajia kuwa ifikapo mwaka 2030 tutaweza kupunguza matumizi duniani ya dawa za kuua vimelea kwenye mfumo mzima wa mazao ya kilimo na chakula, lakini tunahitaji msaada wenu.”

0 Comment

Mabaki ya watu 42 yarejeshwa Afrika KusiniAfyaclass Bongo Social •

Mabaki ya watu 42 yarejeshwa Afrika Kusini

Mabaki ya watu 42 waliopigania uhuru wa Afrika Kusini na waliofariki wakiwa uhamishoni katika mataifa ya Zimbabwe na Zambia yamerejeshwa nchini humo.

Mabaki hayo yalipokelewa na maafisa wa serikali na wanafamilia katika Kituo cha Jeshi la anga la Waterkloof katika mji mkuu Pretoria baada ya kufukuliwa nchini Zambia na Zimbabwe kwa ajili ya kuzikwa upya katika nchi walikozaliwa.

Hii ilikuwa ni sehemu ya mpango wa serikali wa kuzisaidia familia kuwa karibu na mabaki ya wapendwa wao waliokufa wakikipambania chama cha African National Congress ANC na kile cha Pan Africanist Congress PAC.

Kabla ya utawala wa kibaguzi wa wazungu walio wachache kuhitimishwa mwaka 1994, wanaharakati wengi waliondoka Afrika Kusini wakihofia kukamatwa lakini wengine waliondoka ili kupata mafunzo ya kijeshi katika mataifa mengine, kwa lengo la kurejea nyumbani kufanya mapambano ya kutumia silaha.


0 Comment

Upungufu wa nguvu za kiume,chanzo,Dalili na Tiba yakeAfyaclass Bongo Social •

Upungufu wa nguvu za kiume,chanzo,Dalili na Tiba yake

TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME,CHANZO,DALILI NA TIBA

Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume huweza kuhusisha; Uume kushindwa kabsa kusimama, uume kutokusimama kwa muda mrefu, Kukosa nguvu ya kuanza au kuendelea na tendo n.k

hali ambazo hupelekea mwanaume kushindwa kumridhisha mwenza wake ambaye anashiriki naye tendo la ndoa kwa wakati huo.

CHANZO CHA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Zipo sababu nyingi sana ambazo huchangia wanaume kuwa na tatizo hili la Kukosa nguvu za kiume, na baadhi ya sababu hizo ni pamoja na;

- Mtindo mzima wa maisha kwa mwanaume ikiwemo ulaji wake wa kila siku

- Mwanaume kuwa na magonjwa ya moyo ambayo huweza kuathiri usafirishaji wa damu mwilini

- Uwepo wa kiwango kikubwa cha lehemu yaani High cholesterol unaweza kusababisha tatizo la uume kushindwa kusimama vizuri(erectile dysfunction)

- Tatizo la kuwa na kiwango kidogo cha hormones za kiume yaani Low testosterone Level

- Tatizo la Clogged blood vessels (atherosclerosis)

- Ugonjwa wa presha ya kupanda yaani High blood pressure huweza kuleta effect mpaka kwenye mfumo wa uzazi

- Ugonjwa wa kisukari(Diabetes),huweza kuathiri uwezo wa mwanaume kufanya tendo la ndoa ikiwemo tatizo hili la uume kushindwa kusimama vizuri yaani erectile dysfunction

- Tatizo la Uzito kuwa mkubwa yaani Overweight/Obesity, Mwanaume mwenye uzito mkubwa sana,Bonge n.k anaweza kushindwa kufanya vizuri hata kwenye tendo la ndoa.

Hivo unashauriwa kuhakikisha unazuia tatizo hili la uzito kuwa mkubwa/kupita kiasi.

- Tatizo la Metabolic syndrome, ambalo huhisisha vitu hivi kwa ujumla wake; Presha kuwa kubwa zaidi,Level ya Insulin kuwa kubwa sana,Mafuta ya mwili(Body fat) kuzidi pamoja na kiwango cha cholestrol kuwa kikubwa zaidi.

- Matatizo mengine kama vile;Parkinson's disease,Multiple sclerosis n.k pia huweza kuleta athari kwenye mfumo wa uzazi

- Uvutaji wa Sigara ikiwemo matumizi ya Tumbaku(Tobacco)

- Matumizi ya baadhi ya Dawa kama vile dawa jamii ya antidepressants, antihistamines,dawa za kutibu presha(high blood pressure), maumivu au matatizo ya tezi dume

- Unywaji wa Pombe kupita kiasi pamoja na aina nyingine za ulevi au madawa ya kulevyia

- Ugonjwa wa Peyronie's disease, ugonjwa huu huhusisha kutokea na kuendelea kwa kovu(Scar tissues) ndani ya Uume

- Tatizo la kukua kwa tezi dume(enlarged prostate),kansa/Saratani ya Tezi Dume(prostate cancer) pamoja na Matibabu yake

- Mwanaume kuumia au kupata majeraha kwenye maeneo ya via vyake vya uzazi ikiwemo kwenye nyonga pamoja na uti wa mgongo

- Mwanaume kufanyiwa upasuaji kwenye eneo la nyonga(Pelvic) au uti wa mgongo(Spinal cord)

- Tatizo la msongo wa mawazo,hofu,wasi wasi pamoja na matatizo mengine ambayo huhusisha afya ya akili(mental health problems),Vitu hivi huweza kuleta athari mpaka kwenye uwezo wako wa kufanya tendo la ndoa.

- Migogoro ya kila mara kwenye mahusiano yako ambayo pia huweza kuleta tatizo la msongo wa mawazo au stress,wasi wasi,hofu n.k

- Pia tafiti zinaonyesha kadri Mwanaume anavyokuwa na umri mkubwa(mzee) ndivo na nguvu zake za Kiume huendelea kupungua sana ikiwemo uwezo wa uume kusimama vizuri na kwa muda mrefu.

- Baadhi ya matatibu kama vile;Upasuaji wa Tezi Dume(prostate surgery) au huduma ya mionzi(radiation treatment) kwa wagonjwa wa kansa pia huweza kuathiri uwezo wa tendo kwa mwanaume

- Pamoja na Sababu zingine...

Dalili za Tatizo la Upungufu wa Nguvu za Kiume

DALILI ZA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NI PAMOJA NA;

• Uume kushindwa kusimama kabsa

• Uume kutokusimama vizuri

• Uume kusimama ila sio kwa muda mrefu

• Mwanaume kushindwa kurudia tendo, goli moja chali hawezi tena kurudia tendo

• Mwanaume kuwahi kufika kileleni na kushindwa kabsa kuendelea

• Kukosa kabsa hisia au hamu ya kufanya tendo la ndoa n.k

Madhara ya Tatizo la Upungufu wa Nguvu za Kiume

MADHARA YA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NI PAMOJA NA;

✓ Mwanaume kushindwa kumridhisha mwenza wake wakati wa tendo la ndoa

✓ Kuongeza wasi wasi,woga na hofu kubwa ya kufanya mapenzi kwa Mwanaume

✓ Mwanaume kutokujiamini tena

✓ Mwanaume kukosa kabsa hamu ya kufanya tendo la ndoa

✓ Kuanza migogoro kwenye mahusiano au ndoa,kusalitiana n.k

ERECTILE DYSFUNCTION

Shida Ya Uume Kushindwa Kusimama Na Kufanya Kazi Vizuri Wakati Wa Tendo La Ndoa.

Kutokana na Mfumo wa maisha yetu,kazi tunazofanya,vyakula tunavyokula au mtindo wa maisha kwa ujumla, tunajikuta kupata madhara mbali mbali katika miili yetu pasipo kujua sababu hasa ni ipi.

Tatizo hili la uume kushindwa kusimama na kufanya kazi vizuri,huwatokea wanaume wengi kwa hivi sasa, na kusababisha madhara makubwa yakiwemo ya mahusiano au Ndoa kuvunjika.

Chanzo cha tatizo la Erectile dysfunction

JE SABABU ZA TATIZO HILI NI ZIPI?

Zipo Sababu mbali mbali ambazo huweza kuchangia hali hii ikiwemo;

✓ Uchovu wa mwili kupita kiasi kutokana na shughuli nyingi za Siku nzima

✓ Kuwa na shida ya msongo wa mawazo au Stress huweza kusababisha hali hii

✓ Kutawaliwa na wasiwasi pamoja na hofu kubwa wakati wa tendo la Ndoa

✓ Matumizi ya dawa za kulevya pamoja na Uvutaji wa Sigara

✓ Kuwa na umri mkubwa

✓ Ukiwa unatumia baadhi ya Dawa flani

✓ Kuwa na shida ya uzito kupita kiasi au Unene huweza pia kuchangia hali hii

✓ Kuwa na historia ya kupata tatizo katika sehemu za siri siku za nyuma

✓ Kuwa magonjwa mbali mbali kama magonjwa ya moyo, presha au kisukari

✓Kujihusisha na tabia ya kufanya Punyeto au masterbution n.k

DALILI ZA TATIZO HILI LA ERECTILE DYSFUNCTION

- Hamu ya tendo la Ndoa kupote kabsa au kukosa hisia za kufanya mapenzi

- Kupata wasiwasi kabla ya kuanza kufanya mapenzi kuhusu kumridhisha mwenza wako

- Hali ya uume kusinyaa mapema

- Hali ya uume kushindwa kusimama kabsa

- Uume kunyong'onyea wakati wa tendo la ndoa n.k

TIBA YA TATIZO HILI LA ERECTILE DYSFUNCTION

Mgonjwa atatibiwa baada ya chanzo cha tatizo kujulikana hivo matibabu yake yatahusu chanzo cha tatizo lake,ambapo kwa ujumla wake, 

Mgonjwa anaweza kupewa ushauri wa kumsaidia kukaa sawa, mtindo wa maisha kuubadilisha ikiwemo vyakula,kazi n.k Pamoja na Dawa ikiwa shida hii itahitaji matibabu ya Dawa.

  • Dawa
  • Upasuaji
  • Kubadilisha Mtindo wa Maisha

Zingatia Vitu hivi Muhimu kwako kama ni Mwanaume ili kuwa na Afya bora ya Uzazi;

- Epuka matumizi ya Pombe

- Epuka Uvutaji wa Sigara, au matumizi ya Ugoro,tumbaku n.k

- Epuka matumizi ya dawa zozote za kulevyia

- Hakikisha Unadhibiti Uzito mkubwa wa mwili

- Fanya Mazoezi ya mwili mara kwa mara,angalau kwa dakika 30 kila siku

- Epuka tabia ya kufanya Punyeto

- Epuka matumizi ya vyakula vya mafuta mengi sana au chumvi nyingi

- Endapo una magonjwa kama haya hakikisha unapata Tiba mapema;

  • Magonjwa ya Moyo
  • Ugonjwa wa kisukari
  • Ugonjwa wa Presha
  • Magonjwa ya Zinaa kama kaswende,kisonono,chlamydia n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Afariki akifanyiwa Upasuaji wa Kuongeza MakalioAfyaclass Bongo Social •

Afariki akifanyiwa Upasuaji wa Kuongeza Makalio

Mama wa Watoto watano aitwae Alice Delsie Preete Webb (33), amefariki dunia baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuongeza makalio Nchini Uingereza ikielezwa kuwa alifanyiwa upasuaji huo na Mtu asiyekuwa na mafunzo rasmi ya kitiba.

Maafisa wa Polisi wameanzisha uchunguzi juu ya kifo chake na tayari Watu wawili wamekamatwa na kuachiliwa kwa dhamana wakikabiliwa na tuhuma za mauaji ya Alice ambapo imeandika kuwa huduma hiyo hugharimu pound 2,500 ( zaidi ya milioni 9 Tsh. ) na hufanyika ndani ya dakika 60 tu.

Alice ambaye anatajwa kuwa Muingereza wa kwanza kufariki kutokana na upasuaji wa aina hiyo, ameacha Mume na Watoto wao watano ambao ni Delsie (15), Preete (13), Gracie (12), Nylie (10) na Clarie (7).

0 Comment

Njia ya Vipandikizi yatumika zaidi miongoni mwa wanawakeAfyaclass Bongo Social •

Njia ya Vipandikizi yatumika zaidi miongoni mwa wanawake.

Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria Tanzania (TDHS) ya mwaka 2022 unaonyesha asilimia 45 ya wanawake wenye uwezo wa kufanya tendo la ndoa wanaotumia njia za uzazi wa mpango, asilimia 36 wanatumia njia za kisasa na asilimia nane wanatumia za asili.

Hata hivyo, njia ya vipandikizi ndiyo inayotajwa kutumika zaidi miongoni mwa wanawake kwa asilimia 14 ikifuatiwa na njia ya sindano kwa asilimia tisa.

Hayo yamebainishwa na Mhariri wa Afya wa Mwananchi, Herieth Makwetta Siku ya Jumatano, Septemba 25, 2024 wakati akichokoza mada kwenye mjadala wa Mwananchi Space, ulioandaliwa na Mwananchi Communications Limited (MCL) kwa kushirikiana na Marie Stopes Tanzania @mariestopestz isemayo ‘Uhuru wa Kuamua: Namna upatikanaji wa haki muhimu za afya ya uzazi unavyochangia maendeleo Tanzania’. 

Amesema takwimu zinaonyesha mwaka 2022 vifo vitokanavyo na uzazi vilikuwa 104 kwa kila vizazi hai 100,000. Hata hivyo, lengo la Serikali ni kupunguza vifo kutoka 104 katika kila vizazi hai 100,000 hadi 70 kufikia mwaka 2025.

“Uzazi wa mpango ni muhimu kwa maendeleo ya Tanzania, kwani huokoa maisha kwa kusaidia kupunguza magonjwa ya kina mama na vifo, na kuongeza viwango vya kuishi kwa watoto wachanga,” amesema. 

Amefafanua kuwa uzazi wa mpango ni sehemu ya kuboresha afya ya mama na mtoto lakini pia kujenga uchumi wa familia na Taifa kwa ujumla. 

Amesema kwamba upatikanaji wa uzazi wa mpango wa hiari na huduma ya afya ya uzazi kwa wanandoa na watu binafsi ni muhimu katika kuhakikisha uzazi salama, familia zenye afya na jamii zinazostawi.

(Imeandikwa na Sute Kamwelwe)

Via; mwananchiupdates

0 Comment

Madakati bingwa wa Tanzania waitwa Zambia kufanya Upasuaji wa moyoAfyaclass Bongo Social •

Madakati bingwa kutoka Tanzania waitwa nchini Zambia kufanya Upasuaji wa moyo

Madakati bingwa wanne wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete JKCI wako nchini Zambia wakiendelea kufanya upasuaji wa moyo.

Timu hiyo ya madakari hao itashirikiana na wenzao wa Hospitali ya Taifa ya Moyo ya Zambia na watafanyakazi upasuaji wa moyo kwa muda wa wiki moja .

Mkuu wa ujumbe huo, Dk Viviane Mlawi wa (JKCI), ambaye ni daktari bingwa wa moyo kwa watoto, alisema ujumbe huo pia umeambatana na mtaalam mbobezi wa chumba cha upasuaji na mtaalamu wa usingizi katika upasuaji Moyo.

Alisema wameambatana pia na mbobezi katika kuhudumia wagonjwa wa nje wanaokuja kupata matibabu Tanzania, Dk. Maiyer Msengi na wauguzi wawili ambao ni wabobezi wa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).

Dk Mlawi alisema malengo makubwa ya safari hiyo ni matano ambayo ni kufanya upasuaji wa moyo kwa wahitaji ambao ni wengi nchini Zambia na kuwajengea uwezo madaktari wa Zambia mbinu za upasuaji ambazo bado hawajawa nazo na kubadilishana ujuzi.

Alitaja lengo lingine kuwa ni kukagua kwa pamoja na kubainisha maeneo ambayo Tanzania inaweza kushirikia na Zambia katika kuwasaidia wazambia matibabu ya kibingwa kwa wepesi na gharama nafuu.

Dk. Mlawi alisema madaktari hao watakagua na kubainisha vifaa tiba ambavyo vipo na vile ambavyo havipo ili kuweka mikakati ya jinsi gani wanaweza kushirikiana kuvipata ili kuboresha huduma zao.

Alitaja lengo lingine kuwa ni kuona maeneo mbalimbali ya ushirikiano katika tafiti, teknolojia na mambo ya msingi ambayo Tanzania iko mbele sana katika eneo hilo kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.

Naye Dk. Maiyer ambaye ni mtaalam wa usimamizi wa wagonjwa kutoka nje ya nchi, alisema yapo mambo mengi ambayo JKCI na Hospitali ya Taifa ya Moyo Zambia wanaweza kuyafanya kwa kushirikiana kwaajili ya maendeleo ya nchi hizo mbili.

Alitaja masuala hayo kuwa ni kuhakikisha wanarahisisha utoaji wa vibali vya kuingia kwenye nchi hizo (visa), malazi kwa wanaotembelea nchi hizo na usajili wa mawasiliano ya namba za simu na vibali vya kwenda kupata matibabu.

Alisema kwa upande wa Tanzania watahakikisha kunakuwa na uhakika wa miadi ya kukutana na madaktari bingwa na kupata huduma kwa wakati ili kupunguza gharama za kuishi nchini kwa muda mrefu .

Alisema watahakikisha kunakuwa na huduma bora wakati na baada ya upasuaji wa wagonjwa wa moyo na kufanya JKCI iendelee kuwa kimbilio kwa mataifa mengi ya Afrika na kwingineko.

Alisema jambo lingine la msingi ambalo watahakikisha linazingatiwa ipasavyo ni uhakika wa gharama sahihi za vipimo na matibabu na usalama wa mgonjwa kwa kulinda haki zake zote akiwa anapata matibabu.

Alisema kuna umuhimu wa kuendelea kuboresha uhusiano baina ya mataifa hayo mawili katika utoaji wa taarifa ubalozini hasa kwa kuzingatia kuwa kuna mahitaji makubwa ya watu kuja nchini kupata matibabu ya moyo.

Msemaji wa Hospitali ya Moyo ya Taifa ya Zambia, Dk. Chabwela Shumba alisema wamekutana na madaktari wa Tanzania na baada ya kufanya uchambuzi wa uwekezaji ambao serikali imefanya kwa JKCI wameona kwamba watanufaika kwa kiwango kikubwa kama watashirikiana na Tanzania.

“Tumeshangaa sana kuona uwekezaji mkubwa uliofanywa katika vifaa vya kisasa kama MRI, CT SCAN, rasilimali watu, teknolojia na kiwango kikubwa cha wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa moyo kwa mafanikio makubwa,” alisema Shumba.

Alisema wamebaini kuwa JKCI inateklojia ile ile inayotumiwa na mataifa yaliyoendelea hivyo hakuna haja ya kuwapeleka wagonjwa wao kwenye nchi hizo kwani wanaweza kupata huduma kama hizo taasisi ya JKCI.

0 Comment

Maumivu ya chini ya kitovu kwa mjamzitoAfyaclass Bongo Social •

Maumivu ya chini ya kitovu kwa mjamzito

Nini Husababisha Maumivu ya Chini ya Kitovu au tumbo Wakati wa Ujauzito?

Hili ni Swali ambayo wanawake wengi wajawazito hujiuliza,baada ya kuona shida hii, Leo tumekuchambulia kila kitu ili uweze kujua.

Wakati wa ujauzito,hali ya maumivu chini ya kitovu au tumbo inaweza kutokea kwa sababu ya maumivu ya misuli, gesi, kuvimbiwa,kukosa choo au kupata choo kigumu tatizo ambalo hujulikana kama Constipation, au sababu mbaya zaidi ya Kiafya kama vile maambukizi au leba kutokea kabla ya wakati(hapa tunazungumzia preterm labor).

Kuanzia siku ya kwanza ya kupata dalili za mimba(ulipotambua kuwa ulikuwa mjamzito) hadi kuanza kupata maumivu ya kiuno unayohisi sasa,kadri ukuaji wa mtoto wako unapoongezeka, kila siku ya ujauzito unaweza kuona mabadiliko mbali mbali mwilini mwako ambayo huja na aina fulani ya usumbufu,

Pengine Inaweza kuwa ni Ujauzito wako wa kwanza kwahiyo huna Uzoefu wa aina yoyote, Maumivu ya chini ya kitovu kwa mjamzito ni miongoni mwa hali ambazo huwasumbua wanawake wengi pindi wakiwa wajawazito.

Swali moja ambalo unaweza kuhangaika nalo linahusu; Ni wakati gani wa kumjulisha Mtoa huduma wako wa afya ikiwa unahisi maumivu chini ya kitovu na wewe ni mjamzito?.  Kwani hutaki chochote kiende vibaya kwako na kwa mtoto wako anayekua.

Ili kukusaidia kujua sababu hasa za maumivu hayo ya chini ya kitovu au tumbo, tumejumuisha orodha ya sababu zinazoweza kusababisha maumivu hayo pamoja na baadhi ya ishara za onyo zinazomaanisha kuwa ni wakati wa kumjulisha mtoa huduma wako wa Afya Mapema.

Chanzo cha Maumivu ya chini ya kitovu kwa mjamzito

Ni sababu gani zinazopelekea maumivu ya chini ya kitovu au tumbo wakati wa ujauzito?

 Baadhi ya sababu kubwa za maumivu ya chini ya kitovu au tumbo wakati wa ujauzito ni pamoja na:

1. Maumivu kutokana na ligaments;

Ligament ni mkusanyiko wa tishu( a band of connective tissue) ambazo huunganisha mifupa, joints or Au viungo mbali mbali vya mwili.

Ligaments kwenye fupanyonga(pelvis) zinazoshikilia uterasi yako hunyooshwa Zaidi wakati tumbo lako likikua na kupanuka, Na Kwa sababu mimba huweka mkazo zaidi kwenye mishipa hii, ligaments zinaweza kuwa na mkazo na kutanuka kupita kiasi, Hali hii huweza kupelekea wewe kupata maumivu ya chini ya kitovu.  

Hii hutokea Zaidi kwenye kipindi cha second na third trimesters kwenye Ujauzito wako,ambapo unahisi maumivu na usumbufu hasa ukitembea haraka.

Trimesters; Tunazungumzia kipindi cha miezi mitatu mitatu(3) ya Ujazito, mfano tukisema first trimester tunamaanisha miezi 3 ya mwanzo ya Ujauzito n.k.(kumbuka vizuri maana ya neno hili Trimester maana tutalitumia sana kwenye mada hii).

Unachotakiwa kufahamu pia; Aina ya maumivu haya ambayo chanzo chake ni Ligaments sio Maumivu ya kudumu, hutokea kwa muda mfupi kisha kupotea.

2. Tatizo la Gas;

Tatizo la Gas kujaa tumboni huweza kutokea wakati wowote wa Ujauzito, na hali hii huchangiwa zaidi na;

  • Kutanuliwa kwa misuli ya utumbo kwa sababu ya kiwango kikubwa cha hormones aina ya progesterone kipindi cha Ujauzito. 
  • Pia kuongezeka zaidi kwa ukubwa wa Uterus wakati mtoto anakua,hali ambayo huweka mgandamizo zaidi kwenye viungo vyako na kupunguza umeng'enyaji wa chakula(slowing digestion).

Hali hii ya kujaa gesi tumboni huweza kupelekea tatizo la maumivu ya chini ya kitovu ukiwa mjamzito, Ikiwa unapata maumivu kutokana na kuwa na gesi tumboni, unaweza kula kidogo kidogo ila mara kwa mara.  Unaweza pia kujaribu mazoezi yatakayokusaidia usagaji wa haraka wa chakula, lakini pia tambua na kisha uepuke vyakula vinavyosababisha gesi zaidi kwako. 

3. Tatizo la kukosa choo au kupata choo kigumu(Constipation);

Takriban robo ya wanawake wajawazito wanapatwa na tatizo hili la kukosa choo na kupata choo kigumu wakati fulani wa ujauzito.  Lishe isiyo na nyuzinyuzi(fibers),kutokunywa vimiminika vya kutosha kama maji, matumizi ya virutubishi vya madini ya chuma, na kubadilika-badilika kwa homoni ni baadhi tu ya sababu zinazoweza kuchangia tatizo hili kujitokeza.

Hali hii Pia huongeza hatari ya mama mjamzito kupata maumivu ya chini ya kitovu.

Iwapo unapata tatizo hili la constipation, unaweza kujaribu kunywa maji zaidi, kula milo midogo mara kwa mara, kuongeza kiasi cha nyuzinyuzi katika milo hiyo na kufanya mazoezi.  Ikiwa unajitahidi kufanya hivo lakini tatizo la kupata choo kigumu au kukosa choo kabsa lipo pale pale ongea na wataalam wa afya wanaweza kukuagiza dawa za kulainisha kinyesi chako na kukusaidia upate choo vizuri. au kwa Ushauri Zaidi na Tiba juu ya tatizo lolote Tuwasiliane hapa hapa ndani ya afyaclass kupitia namba +255758286584.

4. Hali ya Braxton-Hicks contractions;

Hii ni aina ya mikazo ambayo mara nyingi hutokea kwenye kipindi cha third trimester, mikazo hii imepewa jina la Braxton-Hicks contractions, Na wakati inatokea husaidia kulainisha mlango wa uzazi( Tunasema it helps to soften the cervix). Hapa unaweza kupata maumivu ya Chini ya Kitovu.

Kumbuka; Ukiwa katika hali hii,kunywa maji mengi zaidi,badilisha mkao na usilale kifudifudi ila lala ubavu hasa ubavu wako wa kushoto, na Pia unashauriwa kupata muda wa kupumzika.

5. Mimba kukua(Pregnancy growth);

Mtoto anapokua mkubwa katika trimester ya pili na ya tatu, unaweza kupata maumivu zaidi katika eneo la chini la tumbo,kitovu na kibofu.  Unaweza kuhisi hali ya ngozi yako kunyooshwa na kupata shinikizo zaidi kutoka kwa uzito ulioongezwa. 

Hivo kadri mtoto anavyokuwa,uzito zaidi huongezeka eneo hili, tumbo kuongezeka ukubwa, misuli,ligaments na ngozi kwa ujumla huvutwa zaidi, na mgandamizo kuongezeka zaidi eneo hili, Hivi vyote huweza kupelekea maumivu ya chini ya kitovu,kibofu,maumivu ya kiuno pamoja na mgongo.

Hizo ni baadhi ya Sababu za kawaida za Mjamzito kupata maumivu chini ya kitovu, lakini je unafahamu zipo Sababu za hatari ambazo huweza kupelekea maumivu ya chini ya kitovu kwa mjamzito? Tuzitazame Sababu hizo;

Sababu za hatari zinazopelekea maumivu ya chini ya kitovu kwa mjamzito

Kama nilivyosema,Sababu nyingi tulizokwisha kuzitaja hapo ni za kawaida kwa Mjamzito,lakini zipo Sababu za maumivu ya chini ya kitovu au tumbo ambazo sio za kawaida kwa Mjamzito au kwa lugha nyingine hizi ni Sababu ambazo huashiria tatizo la kiafya na zinaonyesha kwamba kuna kitu hakipo Sawa.

Hizi hapa ni baadhi ya Sababu za hatari zinazoweza kusababisha maumivu ya Chini ya kitovu kwa Mjamzito;

1. Maambukizi au magonjwa mbali mbali(Infections or diseases)

Hapa nazungumzia maambukizi na magonjwa kama vile;

  • Ugonjwa wa UTI;Urinary tract infection
  • Tatizo la mawe kwenye Figo;kidney stones
  • Tatizo la mawe kwenye kifuko cha nyongo;gallstones
  • Tatizo la kuvimba kwa bandama
  • Tatizo la Appendix
  • Kuwa na Vidonda vya Tumbo
  • Tatizo la Mzio dhidi ya  vyakula mbali mbali
  • Tatizo la maambukizi ya bacteria kwenye via vya uzazi;PID
  • Maambukizi ya magonjwa ya Zinaa n.k

2. Kuwa na Uvimbe kwenye Kizazi

Wakati mwingine hali ya maumivu makali ya tumbo au chini ya kitovu huweza kusababishwa na Kuwepo kwa Uvimbe kwenye kizazi.

3. Tatizo la Mimba kutishia kutoka au Mimba kutoka(miscarriage)

Unaweza kuwa kwenye hatari ya mimba kutoka au kutishia kutoka, na hapa ndipo dalili mbali mbali huweza kujitokeza ikiwemo;

  • Kuvuja damu nyingi ukeni
  • Kupata maumivu makali ya tumbo au chini ya kitovu
  • Kupata maumivu makali ya mgongo n.k

4. Tatizo la mimba kutunga nje ya kizazi(Ectopic pregnancy)

Baadhi ya Tafiti zinaonyesha;Takriban mimba 1 kati ya kila mimba 50 hutunga nje ya kizazi.  Huu ndio wakati yai lililorutubishwa linaposhikamana au kujishikiza sehemu ya nje na uterasi. 

 Ikiwa tatizo la mimba kutunga nje ya Kizazi limetokea,baadhi ya dalili mbali mbali na Ishara huweza kujitokeza,hii ni pamoja na;

  • Kupata maumivu makali sana ya tumbo,chini ya kitovu,kiuno au nyonga,mgongo n.k
  • Pia baadhi ya wanawake maumivu haya huweza kufika mpaka kwenye mabega na shingoni
  • Kuvuja damu Ukeni
  • Kupata hali ya kizunguzungu au kuzimia n.k

5. Kupata Uchungu kabla ya wakati wake(Preterm labor)

Takriban robo moja ya  leba zote za kabla ya wakati (zinazotokea kabla ya wiki 37) hutokea zenyewe.  Na Baadhi ya sababu za leba kuanza kabla ya wakati ni pamoja na:

  • Mlango wa uzazi kuwa dhaifu( weakeness in cervix)
  • Chupa kupasuka mapema
  • Kupata shinikizo la juu la Damu
  • Kuvuja damu wakati wa Ujauzito n.k

Hali hii huweza kusababisha mama mjamzito kuanza kupata maumivu ya chini ya kitovu au maumivu ya tumbo.

6. Tatizo la kifafa cha mimba Preeclampsia and eclampsia

Tatizo hili huhusisha shinikizo la damu kuwa juu pamoja na uwepo wa proteins kwenye mkojo. Mwanamke Mjamzito yupo kwenye hatari ya kupata kifafa cha mimba ikiwa;

  • Ana shida ya shinikizo la juu la damu(High blood pressure)
  • Ana ugonjwa wa kisukari
  • Mnene kupita kiasi
  • Kabeba mimba kwenye umri mdogo sana au kabeba mimba kwenye umri mkubwa zaidi n.k

Moja ya Dalili ambazo huweza kujitokeza ikiwa una tatizo hili ni pamoja na;

- Kupata maumivu makali ya kichwa

- Kuona marue rue

- Kupata maumivu ya tumbo

- Kuvimba sana miguu,uso,mikono n.k

7. Tatizo la Placental abruption

Tatizo hili huhusisha kondo la nyuma au placenta kuachia sehemu lilipojishikiza, na hapa dalili mbali mbali huweza kujitokeza ikiwemo;

  • Mama mjamzito Kuanza kupata maumivu makali ya tumbo,chini ya kitovu na mgongo ghafla
  • Kuanza kutokwa na damu nyeusi ukeni n.k

Kumbuka; Hakikisha unaongea na Wataalam wa afya ikiwa una Dalili zozote ambazo huzielewi wakati wa Ujauzito wako, ikiwemo;

✓ Kuvuja damu Ukeni

✓ Unapata Homa

✓ Unahisi maumivu wakati wa kukojoa

✓ Unapata maumivu makali sana ya tumbo au chini ya kitovu

✓ Unatokwa na Uchafu wenye rangi na harufu mbaya

✓ Unapata maumivu makali ya kichwa,kuona marue rue,kuvimba sana miguu,mikono,uso n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD