MATIBABU YA BRUCELLA NA NAMNA YA KUJIKINGA
MATIBABU YA BRUCELLA.
Matibabu ya brusela yapo na yanategemea na stage au hali ya ugonjwa umefikia wapi. Ugonjwa huu unatibika kabsa na mgonjwa anapewa dawa shida inaisha kabsa.
Kulingana na stage ya ugonjwa, wakati mwingine Matibabu ya brusela ni lazima utumie dawa mbili za kumeza kila siku kwa muda usiopungua wiki 6 au zaidi.
Watu Wa rika zote,wajawazito wanatibiwa kwa mfumo huo huo. Cha msingi kama unapata dalili hizo basi muone Dr akupime na kama una brusela basi utatibiwa..
UGONJWA WA BRUCELLA(chanzo,dalili na tiba)
Huu ni ugonjwa ambao kwa kitaalam hujulikana kama brucellosis,
na chanzo chake ni bacteria wanaojulikana kwa jina la Brucella,
bacteria hawa hutokea kwa wanyama, hivo ugonjwa huu huambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.
CHANZO CHA UGONJWA WA BRUCELLA
Hivo chanzo cha ugonjwa wa brucellosis ni bacteria wanaojulikana kwa jina la brucella, ambao husambaa kutoka kwa wanyama mbalimbali kama vile Ng'ombe na kwenda kwa binadamu
•Soma: Ugonjwa wa Wengu,Chanzo,Dalili pamoja na Matibabu yake
DALILI ZA UGONJWA WA BRUCELLA NI PAMOJA NA;
- Joto la mwili la mgonjwa kupanda au mgonjwa kuwa na homa
- Mgonjwa kupata maumivu makali ya mgongo
- Mgonjwa kuhisi vitu vinatembea mwilini,na wakati mwingine kwenye njia ya haja kubwa mithili ya mtu mwenye minyoo
- Mgonjwa kuhisi hali ya kichefuchefu pamoja na kutapika
- Kupata maumivu ya joint,misuli pamoja na viungo vya mwili
- Mgonjwa kuhisi uchovu wa mwili usio wa kawaida
- Uzito wa mwili kupungua kwa mgonjwa
- Mgonjwa kupata maumivu makali ya kichwa
- Mgonjwa kupatwa na hali ya kutoa jasho jingi mwilini wakati wa usku
- Mgonjwa kukosa kabsa hamu ya chakula
- Mgonjwa kupatwa na kikohozi cha mara kwa mara
- Mgonjwa kuumwa na tumbo
- Mgonjwa kupata rashes kwenye ngozi yake ya mwili
- Mwili kuwa dhaifu sana pamoja na kukosa nguvu
VIPIMO VYA UGONJWA WA BRUCELLA
Kulingana na hali ya mgonjwa pamoja na dalili ambazo zinajitokeza kwake,
Mambo mbali mbali huweza kufanyika kama hatua ya kwanza kabsa ili kufahamu chanzo halisi cha Ugonjwa wako,
mambo hayo ni Pamoja na;
- Mgonjwa kuelezea historia ya ugonjwa wake jinsi ulivyoanza(Patient history taking)
- Kufanya vipimo mbali mbali ikiwemo,
- Kipimo cha Damu(Blood tests)
- Kuchek Joto la Mwili
- Kupima presha(blood pressure)
- Uzito wa mgonjwa(body weight)
- Sukari n.k
MATIBABU YA UGONJWA WA BRUCELLA
Zipo dawa mbali mbali ambazo hutumika kutibu ugonjwa huu wa brucellosis,
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
NAMNA YA KUJIKINGA NA BRUCELLA
Mpaka sasa hakuna chanjo ya BRUCELLA ilopatikana na kwa maana hiyo ni lazima kujilinda kwa njia zingine mpaka pale chanjo itakapopatikana..
1) Epuka kunywa maziwa mabichi; maziwa yanatakiwa yachemshwe kikamilifu
2) Epuka migusano ya majimaji ya wanyama tajwa na wewe, majimaji kama mate,uharo,mkojo,kondo la nyuma,kamasi nk.
3) Kuwapatia chanjo wanyama wote wafugwao au wanaokua karibu na binadamu dhidi ya chanjo ya brusela
4) Kwa wale wachinjaji na wauza nyama mabuchani wazingatie utaratibu Wa kazi zao ili kujilinda na migusano ya damu au majimaji yeyote kutoka kwa mnyama husika.
5) kwa zile jamii zilizo kwenye hatari ni vyema mkawa na desturi ya kupima homa ya brusela kwani unaeza kuambukuzwa brusela mwezi Wa kwanza lakini ukaja kuona dalili mwezi Wa 12.
0 Comments