Ticker

6/recent/ticker-posts

Zaidi ya watoto 160,000 wachanjwa Gaza



Zaidi ya watoto 160,000 wachanjwa, lengo ni watoto 640,000

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti leo Jumanne Septemba 3 kwamba watoto 161,030 walio na umri wa chini ya miaka kumi wamechanjwa katikati mwa Gaza wakati wa siku mbili za kwanza za kampeni ya chanjo inayoongozwa na Umoja wa Mataifa, hivyo kuvuka lengo la awali la watoto 156,000.

Idadi hii inawakilisha takriban robo ya jumla ya watu watakaofikiwa, watoto 640,000.
 
Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa X akisema, “timu zetu zimejizatiti kuhakikisha hakuna mtoto anayekosa (kuchanjwa), licha ya ufurushaji unaoendelea.”
Tweet URL

Saa za kutoshambuliana

Hata hivyo, mwakilishi wa WHO kwa Maeneo ya Palestina Yanayokaliwa, Rik Peeperkorn, akizungumza kutoka Gaza leo amesema watahitaji siku moja zaidi ili kukamilisha uchanjaji kikamilifu eneo la kati la Gaza.
 
Amesema siku ya tatu ya uchanjaji imeendelea wakati wa mapumziko ya kutoshambuliaana kila siku kwa saa nane ziliyokubaliwa na jeshi la Israel na wapiganaji wa Hamas (saa kumi na mbili asubuhi hadi saa tisaa alasiri).

Eneo la kusini

Peeperkon ameeleza kuwa timu za chanjo zitahamia eneo kubwa la kusini siku ya Alhamisi kwa siku nyingine tatu na kuna uwezekano mkubwa wa siku ya nne, kabla ya kuelekea ukanda wa kaskazini.
"Wiki nne baadaye, mchakato huo utarudiwa kwa awamu ya pili ya chanjo." ameongeza.
 
Kufikia sehemu ya kaskazini mwa Ukanda huo bado kunatia wasiwasi, kwani WHO imejaribu kutuma watu wake kaskazini katika wiki mbili zilizopita ili kuzipatia hospitali vifaa muhimu vya matibabu.
 
"Kati ya makundi nane au tisa yaliyopangwa, ni matatu au manne tu ndio yaliweza," anasema, akiongeza kwamba walituma timu ya matibabu ya dharura katika hospitali ya Indonesian na daktari wa watoto katika hospitali ya Kamal Adwan, pamoja na dawa na vifaa vingine.
 
"Kati ya makundi nane au tisa yaliyopangwa, ni matatu au manne tu ndio yaliweza," anasema.
Safari ya kurudi kwenye kituo ilihusisha kusubiri ruhusa kwa saa saba ili kuendelea hadi kufika mahali pa kupumika, na saa 2.5 za ziada kufikia kituo cha ukaguzi.
 

Asilimia 90

 
Kwa mujibu wa WHO, angalau asilimia 90 ya watoto wa Kipalestina wanahitaji kupewa chanjo ili kampeni hiyo iwe na ufanisi na kuzuia kuenea kwa polio ndani ya Gaza na duniani kote.
 
Ukanda wa Gaza ulikuwa na kiwango cha juu cha chanjo kwa watu wote kabla ya mzozo kuanza Oktoba 2023.
 
Kutokana na athari za vita, uchanjaji wa kawaida ulishuka kutoka asilimia 99 mwaka 2022 hadi chini ya asilimia 90 katika robo ya kwanza ya mwaka 2024, na kuongeza hatari ya magonjwa yanayoweza kuzuilika kwa watoto, ikiwa ni pamoja na polio.
 
Alipoulizwa kama itawezekana kutathmini masuala mengine makubwa ya kiafya, kama vile utapiamlo wa watoto, wakati timu za chanjo zikifanya kazi, Peeperkorn amesema hakuna uwezo wa kufanya hivyo.
 

Watoto waliochanjwa wanarudi kwenye eneo la vita

 
Wakati mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa yakikaribisha usitishaji mapigano katika maeneo maalum ili kuruhusu kampeni kubwa ya chanjo ya polio, yanasisitiza haja ya dharura ya kuachiliwa mara moja kwa mateka wote waliosalia na kusitishwa kwa mapigano katika Ukanda wa Gaza.
 
"Watoto hawa wakishachanjwa, watarejea katika maeneo ambayo tunafikiri yatapigwa mabomu tena wiki ijayo," anaonya James Elder, msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF).
 
"Hakuna kitu kuhusu hilo ambacho kinapaswa kukubaliwa kama hali ya kawaida," ameendelea. "Na nadhani kila mtu sasa anakubali kwamba mazungumzo ya kusitisha mapigano ni mazungumzo ya kutufanya tuendeleea.

Via:UN



Post a Comment

0 Comments