Ticker

6/recent/ticker-posts

Watoto chini ya miaka mitano waathiriwa Zaidi na Mpox nchini Burundi



Watoto chini ya miaka mitano waathiriwa Zaidi na Mpox nchini Burundi.

Vijana wameathiriwa zaidi na milipuko ya Mpox barani Afrika, huku watoto chini ya miaka mitano wakichangia karibu theluthi moja ya visa hivyo nchini Burundi, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto lilisema Ijumaa.

Burundi ni nchi ya pili barani humo kukumbwa na matatizo baada ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

“Watoto nchini Burundi wanabeba mzigo mkubwa wa mlipuko wa mpox, na viwango vya kutisha vya maambukizo na athari mbaya za kiafya,” Paul Ngwakum, Mshauri wa Afya wa UNICEF Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika alisema.

Ngwakum alisema theluthi mbili ya kesi nchini Burundi zilihusu watu wenye umri wa miaka 19 na chini.

“Kinachotia wasi wasi ni kuongezeka kwa ugonjwa wa mpox miongoni mwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano, ikiwa ni asilimia 30 ya kesi zilizoripotiwa,” aliwaambia waandishi wa habari mjini Geneva, akizungumza kupitia kiunga cha video kutoka Bujumbura.

Mpoksi, ambayo awali ilijulikana kama monkeypox, husababishwa na virusi vinavyopitishwa kwa wanadamu na wanyama walioambukizwa lakini pia inaweza kupitishwa kutoka kwa binadamu hadi kwa binadamu kwa kuwasiliana karibu kimwili.

Husababisha homa, maumivu ya misuli na vidonda vikubwa vya ngozi kama majipu, na wakati mwingine inaweza kuwa mbaya.

Ugonjwa Wa Homa ya Nyani,chanzo,dalili Na Tiba yake

Ugonjwa wa homa ya nyani au Mpox ni ugonjwa ambalo unasababishwa na virusi, Ugonjwa huu unasababishwa na virusi ambao hujulikana kwa jina la Mpox ambapo hapo awali vilijulikana kama MonkeyPox. Mpox Virus wapo kwenye kundi la Orthopoxvirus genus ndani ya familia ya Poxviridae.

Ugonjwa wa homa ya nyani kwa binadamu(Human Mpox),Mara ya kwanza kabsa uliripotiwa Mwaka 1970 nchini DRC(Democratic Republic of the Congo) kwa kijana mmoja wa Miaka 9 aliyekuwepo kwenye eneo ambalo ugonjwa wa Smallpox ulishaondolewa tangu mwaka 1968. Ndipo visa vingine vikaanza kuripotiwa na maeneo mengine, (Disease history Source:WHO)

Dalili za Ugonjwa wa Homa ya Nyani

DALILI ZA UGONJWA HUU WA Homa ya Nyani NI PAMOJA NA;

– Mtu kuwa na homa pamoja na mwili kutetemeka

– Kupata maumivu makali ya kichwa

– Mwili kuchoka kupita kawaida

– Mwili kukosa nguvu na kuwa dhaifu sana

– Lymph nodes kuanza kuvimba ambapo kwa lugha nyingine hujulikana kama lymphadenopathy

– Kupata maumivu ya viungo,joints pamoja na misuli ya mwili

– Kupata maumivu ya mgongo(back ache)

– Kutokewa na UPELE kwenye maeneo mbali mbali ya mwili wako kama vile; Usoni, kwenye mikono pamoja na viganja vya mikono,
miguuni,machoni,,mdomoni,sehemu za siri n.k

Upele huu unaweza kuwasha sana, na hata baadae huweza kutumbuka kabsa,

Mwili huweza kubaki na makovu au alama alama.

UGONJWA HUU WA HOMA YA NYANI(MPOX) husambaa kutokana na ukaribu(Close contact) kwa mtu,wanyama au vitu ambavyo tayari vina virusi hawa wa Mpox.

Unaweza kuupata kwa njia ya ya mgusano sehemu zenye majeraha, kupitia body fluids zote kama vile damu,mate,jasho n.k, kutoka kwa Mtu au wanyama wenye Virusi hawa(Mpox virus).

Virusi vya MPox vinaweza kuingia mwilini kupitia kwenye ngozi iliyo na jeraha au michubuko yoyote, au kwa njia nyingine kama vile njia ya upumuaji au kupitia macho, pua pamoja na mdomo.

Pia Uenezwaji wake unaweza kuwa  kwa kugusana na wanyama walioambukizwa kama vile nyani, panya na kindi ,kupitia vitu kama vile matandiko au nguo za mgonjwa mwenye virusi hawa.

- Ugonjwa wa Homa ya Nyani unaweza kusambaa kutoka kwa mtu mwenye maambukizi kwenda kwa mwingine kwa njia zifuatazo; kupitia maji maji ya mwili ikiwemo mate, matapishi, jasho, mkojo, matone ya mfumo wa njia ya hewa na ngozi kupitia kugusana na kujamiana na mtu mwenye maambukizi ama kutumia vifaa, matandiko au kugusa sehemu zilizo na vimelea vya ugonjwa huu. Aidha, ugonjwa huu unaweza pia kuenezwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.

- Dalili kuu ya Homa ya Nyani ni upele, malengelenge au vidonda kwenye mwili hasa, mikono na miguu, kifuani, usoni na wakati mwingine sehemu za siri. Dalili nyingine ni homa, uchovu, maumivu ya kichwa, misuli, mgongo, uchovu na kuvimba mitoki.

- Ugonjwa huu wa homa ya nyani haujaingia nchini, hivyo, ni vyema tukashirikiana kuhakikisha nchi yetu inabaki kuwa salama. Wizara inatoa tahadhari kwa Wananchi wote kuchukua hatua za kujikinga na ugonjwa wa huu kwa kutekeleza yafuatayo;-

i. Kutoa taarifa kupitia namba 199 bila malipo endapo utamuona mtu mwenye dalili za Homa ya Nyani(Mpox).

ii. Kuepuka kugusa majimaji ya mwili au ngozi ya mtu mwenye dalili za ugonjwa wa Homa ya nyani(Mpox).

iii. Kuepuka kusalimiana kwa kupeana mikono, kukumbatiana na kubusiana mtu mwenye dalili za Ugonjwa wa homa ya nyani(Mpox).

iv. Kuepuka kugusana na mtu yeyote mwenye dalili za ugonjwa wa Homa ya Nyani(Mpox).

v. Kunawa mikono kila mara kwa maji tiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono.

vi. Epuka kula au kugusa mizoga au wanyama mfano nyani au swala wa msituni.

vii. Safisha na kutakasa vyombo vilivyotumika na mhisiwa au mgonjwa pamoja na maeneo yote yanayoguswa mara kwa mara.

viii. Kuvaa barakoa iwapo itabidi kukaa na kuongea kwa karibu na mtu mwenye dalili za Ugonjwa wa Homa ya Nyani(Mpox).

ix. Kuwahi katika vituo vya huduma za afya unapoona dalili za ugonjwa wa Homa ya Nyani(Mpox).

x. Watoa huduma za afya kuzingatia miongozo ya kuzuia kusambaa kwa maambukizi (IPC) wakati wote wanapowahudumia wagonjwa.

MATIBABU YA UGONJWA WA HOMA YA NYANI

Ugonjwa huu wa Homa ya Nyani hauna tiba(no cure),bali watalaam wa afya hudhibiti dalili zinazotokana na ugonjwa huu wa homa ya nyani.

Kwa Sasa Shirika la Afya Duniani(WHO) limeidhinisha Chanjo za Kutumika Kuzuia Ugonjwa huu wa Homa ya Nyani. #SOMA Zaidi hapa Kuhusu WHO na Chanjo hii ya Mpox

Hata hivo ugonjwa huu huisha wenyewe kwa kipindi flani baada ya kumpata mtu.

Fahamu pia,Maambukizi haya ya ugonjwa wa homa ya nyani(Mpox) huisha yenyewe na hudumu kati ya siku 14 na 21.

#Mpox #Hom ya Nyani